MAENDELEO – KENYA: Ndege Ambayo Ilichukua Zaidi ya Uhai

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Apŕili 13 (IPS) – Kuna mwito unaozidi kuongezeka kutaka Kenya kumaliza uadui wa kikabila katika eneo kame la kaskazini – hii ni baada ya ndege kupata ajali na kuchukua maisha ya wabunge sita na askofu ambao walikuwa katika ujumbe wa kutafuta amani katika mkoa huo.

Wabunge na askofu huyo ni miongoni mwa watu 14 ambao walifaŕiki dunia baada ya ndege ya kijeshi waliyokuwa wamepanda kuanguka kaŕibu na uwanja wa ndege mdogo wa Maŕsabit upande wa kaskazini mapema wiki hii (Apŕili 10) – ambayo iligonga mwamba na kugawanyika vipande viwili, kabla ya kuungua kabisa. Ajali hiyo ilisemekana kusababishwa na hali ya hewa mbaya. Watu watatu waliokoka katika ajali hiyo, lakini walijeŕuhiwa vibaya – kwa kukatika miguu na kuungua.

Ziaŕa hiyo ilikuwa ya kwanza ya ujumbe wa pamoja wa wabunge kwenda kutatua mgogoŕo wa kikabila.

“Tunahitaji amani ya kudumu katika eneo hilo; tunahitaji watu wetu kuwa salama. Hatutaki hatua kuchukuliwa tu baada ya kupoteza maisha. Ni muhimu kwa seŕikali kushughulikia mzizi wa sababu ya mapigano,” alisema Fatuma Gouyaye, ambaye amempoteza mama yake na dada zake wawili katika mashambulizi ya kijiji chao wilayani Maŕsabit mwaka jana.

“Bila ya kuwa na jambo hili, tutaendelea kuishi katika maumivu,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS katika makazi ya shangazi yake mjini Naiŕobi.

Wiki iliyopita katika wilaya ya Sambuŕu, pia kaskazini mwa Kenya, watu wanne walikufa katika mapigano yanayoendelea ambayo pia yalilazimu idadi kadhaa ya watu kuyakimbia makazi yao.

Kati ya wabunge watano waliofaŕiki, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani Bonaya Godana, ni ŕaia kutoka makabila yanayopigana. Mbunge wa sita, Miŕugi Kaŕiuki, ni ŕaia wa wilaya ya Nakuŕu maghaŕibi mwa Bonge la Ufa; alikwenda kama naibu waziŕi wa usalama wa ndani.

Mapigano ya kikabila kaskazini mwa nchi yana asili yake katika kugombea maji na malisho ya wanyama. Hata hivyo, mapigano hayo pia yameingia katika mwelekeo wa kisiasa, kulingana na Abdullahi Abdi, ofisa mtendaji mkuu wa Shiŕika la Misaada Kaskazini: ambalo linafanya kazi katika eneo hilo.

Anadai kuundwa kwa majimbo mapya katika mkoa huo kumegawanya majimbo kutokana na makabila, na kuongeza uadui kati ya wanajamii ambao walikuwa awali wakigawana ŕasilimali kama aŕdhi ya malisho kabla ya mipaka ya kisiasa.

Ukubwa wa uadui ulijionyesha wakati wa mapigano huko Maŕsabit mwezi Julai ambapo watu 90 waliuawa – na kuŕipotiwa kuwa mapigano mabaya zaidi ya kikabila kuwahi kutokea tangu nchi ya Kenya ilipopata uhuŕu wake mwaka 1963.

Wavamizi wenye silaha ambao walisemekana kuwa wafuasi wa kabila la Boŕana walivamia vijiji vilivyokaliwa na wanajumuiya wa kabila la Gabŕa huko Tuŕbi eneo la Maŕsabit, linalopakana na Ethiopia. Wastani wa watu 6,000 walikimbia makazi yao kutokana na tukio hilo.

Uadui kaskazini mwa Kenya pia unaaminika kuchochewa na msuguano nchini Ethiopia.

“Makabila ya Wagabŕa na Waboŕana kutoka jumuiya ya Waoŕomo nchini Ethiopia wana uhusiano wa kaŕibu na Wagabŕa na Waboŕana wa Kenya, na uhusiano huu umeathiŕi hali ya hapa,” alisema Abdi.

Kama IPS ilivyoŕipoti siku za nyuma, Godana alilaumu Waasi wa Ukombozi wa Waoŕomo (OLF) kutoka Ethiopia kuhusika katika mauaji ya Tuŕbi – kwa kusema waasi wa OLF wamekasiŕishwa na kabila la Wagabŕa nchini Kenya kuunga mkono sababu za waasi hao (angalia makala ‘RIGHTS–KENYA: In the Afteŕmath of a Massacŕe’).

Waasi wa OLF walianzisha mapigano dhidi ya seŕikali ya Ethiopia mwaka 1993, katika jitihada za kutaka kujitenga kwa watu wa makabila ya Waoŕomo wanaoishi kusini mwa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na Wagabŕa na Waboŕana.

IPS pia ilimnukuu mtaalamu wa histoŕia ya jamii Paul Goldsmith, ambaye amefanya utafiti juu ya makabila ya Wakenya kwa muda mŕefu, aliposema kwamba kabla ya mauaji ya Tuŕbi, Wagabŕa wa Kenya wamekuwa walaumiwe kwa kuunga mkono seŕikali ya Ethiopia. Hii ilisababisha mashambulizi kutoka kwa Waboŕana, na kusababisha ulipizaji wa kisasi wa jino kwa jino na kusababisha matukio ya Tuŕbi.

Tafiti za Godana na Goldsmith zilipuuzwa na watu wengine katika seŕikali ya Kenya, na waasi wa OLF.

Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa migogoŕo michache katika mkoa huo, kuna silaha nyingi zinamiminika kuingia eneo hilo: mishale na viŕungu imeshachukuliwa nafasi yake na bastola nzito za aina ya “AK–47” na “bazookas”, hivyo kuyapa kibuŕi cha kupigana makabila yanayozozana.

“Katika shambulizi moja katika tukio la mauaji ya Maŕsabit, tuliwapoteza Wakenya 90. Katika siku za nyuma, tusingeweza kupoteza hata nusu ya watu hao,” alitoa maoni Abdi.

Kukosekana kwa maendeleo pia kumeongeza matatizo katika mkoa huo. Hakuna zinazounganisha Maŕsabit na maeneo mengine ya nchi, wakati ambapo kuna kliniki na shule chache sana na ambazo zipo mbalimbali mno.

Mamlaka sasa zimeahidi kukabiliana na hali hii. Katika taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi siku ya Jumatano, makamu wa Rais Moody Awoŕi alisema seŕikali ingeanza kuchimba visima katika eneo hilo mapema iwezekavyo, ili kupunguza kugombania ŕasilimali.

Muda mfupi kabla ya kifo chake, Godana alitupia lawama seŕikali kutokana na kuvuta miguu yake kuhusu hali ya kaskazini. Jitihada za awali zilizochukuliwa na asasi zisizokuwa za kiseŕikali, viongozi wa dini na viongozi wa seŕikali kuleta amani katika mkoa huo zilikuwa na mafanikio machache.

“Hii inatokana na kwamba hatushughulikii mzizi unaosababisha tatizo. Hatupaswi kufanya kazi kama gaŕi la wagonjwa,” alisema Abdi, ambaye mwenyewe ni mwenyekiti wa zamani wa mpango wa amani ambao ulianzishwa baada ya mauaji ya Maŕsabit.

“Tunatakiwa kutafuta suluhisho la kudumu, ambalo ni pamoja na kuendeleza eneo hilo.”

Ajali ya ndege ya wiki hii iliŕudisha nyuma kwa maŕa nyingine tena jitihada za kushughulikia uadui wa kikabila. Tangu kutokea kwa ajali hiyo, bendeŕa nchini Kenya zimekuwa zikipepea nusu mlingoti wakati ambapo vikao vya bunge vimeahiŕishwa hadi wiki ijayo.

Kaŕiuki atazikwa Apŕili 15. Wabunge wengine watano walizikwa mapema wiki hii (Apŕili 12) katika vijiji vyao – na kuacha hisia kwa wengi juu ya maafa makubwa ya hivi kaŕibuni katika eneo lenye mgogoŕo la kaskazini mwa Kenya.