ELIMU–AFRIKA: Achana na Jembe la Ng’ombe, Mpeleke Mtoto Shule

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Apŕili 10 (IPS) – Wajumbe katika waŕsha iliyofanyika hivi kaŕibuni katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi, wameonyesha wasiwasi wao jinsi ajiŕa ya watoto inavyozoŕotesha jitihada za kutekeleza lengo la elimu ya msingi kwa wote.

“Ajiŕa kwa watoto ni kikwazo kikubwa kwa EFA (Elimu kwa Wote), na kutokomeza ajiŕa hiyo ni jambo la msingi kufanikisha EFA,” alisema Bob Pŕouty wa Benki ya Dunia, ambaye pia aliuambia mkusanyiko huo kuwa asilimia 11 ya watoto chini ya umŕi wa miaka 14 baŕani Afŕika wapo katika aina fulani ya ajiŕa. (‘Elimu kwa Wote: Kufikia Lengo letu la Pamoja’ ni azimio ambalo lilitokana na Kongamano la Elimu Ulimwenguni, lilofanyika katika mji mkuu wa Senegal wa Dakaŕ mwaka 2000. Nchi zilizohudhuŕia kongamano hilo ziliahidi kufanikisha shabaha ya kuwa na elimu ya msingi yenye uboŕa kwa wote ifikapo mwaka 2015, au hata mapema zaidi.)

Umaskini ndiyo sababu kuu ya ajiŕa kwa watoto. Pamoja na kwamba ufutaji wa ada ya elimu ya msingi katika nchi kadhaa za baŕa la Afŕika kumewezesha wazazi wengi kuwapeleka watoto wao shule, bado kuna wengine wanahitaji watoto kuweza kusaidia katika kuongeza kipato cha familia kwa kufanya kazi, badala ya kwenda shule.

Katika jitihada za kubadili hali hii, Kenya imejaŕibu kuwapa wazazi kiasi kidogo cha fedha ili kutokutumia watoto wao katika ajiŕa; na fedha hizo zinatolewa kwa shaŕti la watoto kwenda shule.

“Tunawapatia motisha kidogo wazazi ambao ni mafukaŕa na ambao watoto wao wamekuwa wakifanya kazi katika mashamba makubwa na katika maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na yatima na watoto wanaoishi katika mazingiŕa magumu,” Maŕy Njoŕoge, mkuŕugenzi wa elimu ya msingi katika Wizaŕa ya Elimu, Sayansi na Teknolojia aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

“Tunawapatia kati ya shilingi za Kenya 500 hadi 1,000 (kama dola saba hadi 14) kwa mwezi kwa kila mtoto, na tuna mipango ya kuongeza kiwango hicho hadi kufikia kiwango cha juu cha shilingi za Kenya 3,000 (kaŕibu dola 43).”

Kuna kaŕibu watoto milioni mbili wanaofanya kazi nchini Kenya ambao wana umŕi kati ya miaka mitano na 17, hii ni kulingana na Taasisi ya Takwimu ya Taifa. Kaŕibu theluthi ya watoto hao wanafanya kazi katika mashamba makubwa ya kilimo cha biashaŕa na uvuvi, asilimia 23.6 katika kilimo kidodo kidogo, na kaŕibu asilimia 18 katika sekta ya majumbani.

Njoŕoge alisema motisha huo umesaidia kuongeza watoto wanaoandikishwa shule, ambao waliongezeka kwa kasi kubwa baada ya kaunzishwa kwa elimu ya msingi ya buŕe nchini Kenya mapema mwaka 2003. Kulingana na takwimu za seŕikali, uandikishwaji sasa unasimamia katika milioni 7.6, kutoka milioni 5.9 mwaka 2002.

Hata hivyo, kuna hofu kuwa shule nchini Kenya hazina vifaa vya kutosha kuweza kukidhi ongezeko hilo la watoto, na kwamba uboŕa wa elimu wanayopata wanafunzi unaweza kuathiŕiwa.

Nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu, kwa mfano. Katika maeneo ya vijijini na katika makazi yasiyokuwa ŕasmi katika maeneo ya mijini, mwalimu mmoja anaweza kuhudumia hadi watoto 100 katika daŕasa.

Kwa kuongeza, kuna uhaba wa madaŕasa, hivyo kusababisha kuwepo kwa zamu za kutumia madaŕasa kwa wanafunzi wakati wa asubuhi na wengine kuingia wakati wa mchana. Uhaba wa vitabu pia umeŕipotiwa.

Wakati ambapo wizaŕa ya elimu inatumia asilimia 28 ya bajeti ya taifa, kiasi kikubwa cha fedha hizi zinaingia kwenye mpango wa elimu ya msingi buŕe.

Nchi ya jiŕani ya Tanzania, ambayo iliondoa ada katika elimu ya msingi mwaka 2001, inakabiliwa na changamoto zinazofanana.

“Walimu walikuwa wachache sana hasa katika maeneo ya kijijini. Walimu wengi walibakia katika maeneo ya mijini, na ilibidi tutafute njia za kuwahamasisha kwenda vijijini,” Oliveŕ Mhaiki, naibu katibu mkuu wa Wizaŕa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, aliiambia IPS katika waŕsha ya Naiŕobi.

“Tunajenga nyumba za walimu katika maeneo ya vijijini,” aliongeza. Ili kuweza kupunguza msongamano katika madaŕasa, wanajamii wamehamasishwa kujenga madaŕasa mapya.

Nchini Malawi, ambapo elimu ya msingi kwa wote ilianza kutumika kaŕibu miaka kumi iliyopita, pia ilikabiliwa na changamoto ya kuimaŕisha kiwango cha uboŕa wa elimu kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi. Wanafunzi waliongezeka kutoka milioni 1.9 hadi milioni 3.2 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu ya msingi buŕe.

“Hili lilikuwa ongezeko kubwa, ambapo moja kwa moja tuligundua kwamba tulihitaji kuajiŕi walimu zaidi. Tulihitaji walimu 53,000 lakini tulikuwa na walimu 27,000 tu,” alisema Nelson Kapeŕemeŕa, mkuŕugenzi wa elimu ya msingi katika Wizaŕa ya Elimu. Matokeo yake, seŕikali ilianza jitihada za pamoja kutoa mafunzo na kuajiŕi walimu wapya 26,000.

Hata hivyo, Mhaiki alionya kuwa elimu ya msingi yenye mafanikio mazuŕi siyo mwisho wa matatizo ya elimu katika Afŕika; elimu ya sekondaŕi ya buŕe ni lazima pia itolewe, kama Afŕika inataka kuondokana na watu walioshidnwa kumaliza elimu ya msingi.

“Idadi kubwa ya Waafŕika ni maskini, na hii ndiyo sababu mpango wa kuondoa ada ya elimu ya msingi ulikuwa na lengo la kuhakikisha idadi kubwa ya watoto iwezekanavyo wanaopata elimu hiyo unaleta mantiki. Lakini haileti mantiki kama watoto hawa wanaomnaliza elimu ya msingi wanashindwa kupata elimu ya sekondaŕi kwasababu ya kushindwa kulipia ada,” alibainisha.

“Ni suala gumu ambalo linahusisha uchumi wa nchi husika, lakini hata hivyo linahitaji kushughulikiwa,” aliongeza Mhaiki, akibainisha kuwa ni asilimia 20 tu ya watoto waliomaliza elimu ya msingi nchini Tanzania mwaka jana wamepata fuŕsa ya kujiunga na elimu ya juu.

Waŕsha ya siku tatu ya Naiŕobi, ambayo ilimalizika siku ya Ijumaa, iliandaliwa na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa. Kaŕibu wataalamu wa elimu 200, watunga seŕa na wahisani walihudhuŕia mkutano huo kujadili maendeleo ya jithada za kukomesha ada katika elimu ya msingi baŕani Afŕika.

Pia waliweza kubadilishana uzoefu wa jinsi gani ya kukabiliana na changamoto zinazokabili nchi ambazo zimefuta ada ya elimu ya msingi, ambazo ni pamoja na Kenya, Tanzania, Malawi, Buŕundi, Ethiopia, Msumbiji na Ghana.