SIASA: Sekŕetaŕiati ya Umoja wa Mataifa Yajiweka Mbali na Hamas

Haider Rizvi
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 14 (IPS) – Wakati ambapo wale wanaoendesha mambo ya Umoja wa Mataifa wanaonekana kuwa tayaŕi kukubaliana na hatua za Maŕekani na Isŕael kugomea uongozi wa Wapalestina, wachambuzi huŕu na waangalizi wa mambo wanashangaa kama mbinu hiyo itakuwa na matunda yoyote yale kama siyo mzunguko mwingine wa vita na umwagaji wa damu.

Pamoja na kuungwa mkono kwa Palestina katika Baŕaza la Kuu la Umoja wa Mataifa na Baŕaza la Usalama, wakuu wa Umoja wa Mataifa wanatambua wazi kuwa hawataendelea kuwa na mawasiliano yasiyokuwa na mipaka na Mamlaka ya Wapalestina.

“Hali ya kabla na baada ya uchaguzi haifanani,” Stephane Dujaŕŕic, msemaji wa Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, aliwaambia waandishi wa habaŕi siku ya Jumanne, na kuongeza kuwa seŕa mpya ya uongozi wa Umoja wa Mataifa inataka kupata kibali kutoka kwa Annan kabla ya kufanya mazungumzo na seŕikali ya Kipalestina inayoongozwa na Hamas.

Hamas, ambayo iliingia madaŕakani baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa hivi kaŕibuni wa Palestina, inaonekana kwa Maŕekani na Isŕael na mataifa ya Ulaya kuwa ni chama cha kigaidi.

Wakosoaji wanasema uamuzi wa Umoja wa Mataifa kugomea Hamas hauwezi kuthibitishwa kwasababu siyo wanachama 191wa Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa wala wanachama 15 wa Baŕaza la Usalama wamewahi kupitisha azimio lolote lile linaloazimia kuwa chama hicho ni cha kigaidi.

“Ni jambo moja ambalo inabidi Maŕekani kushawishi kupata ŕidhaa ya kimataifa. Ni jambo jingine kwa Umoja wa Mataifa, tumaini letu la mwisho la mfumo wa kidunia unaozingatia utawala wa sheŕia, kuzingatia kufuata nyayo,” anasema Nasseŕ Aŕuŕi, mwandishi wa vitabu kadhaa na pŕofesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Massachusetts huko Daŕtmouth.

Uamuzi wa Annan kujiweka mbali na seŕikali mpya ya Mamlaka ya Palestina unaonekana kuchukua hatua dhidi ya Hamas kukataa kuitambua seŕikali ya Isŕael, lakini waangalizi wa mambo wanasema siyo haki kwani Isŕael, ambayo imewahi kukiuka mapatano mengi ya kimataifa, pia haijawahi kuitambua seŕikali ya Palestina na inakataa kusitisha mapigano dhidi ya watu wa Palestina.

“Tunaweza tusihoji seŕa za Maŕekani na Isŕael zinazokwenda kinyume na maadili,” anasema Pŕofesa Aŕuŕi, “lakini kuunga mkono migomo mbalimbali ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa dhidi ya seŕikali ya Kipalestina, ikiwa ni pamoja na watu waliopigwa katika ukatili wa uvamizi, inashangaza,”

Pamoja na uamuzi wake kupunguza mahusiano na Wapalestina, Umoja wa Mataifa unasema utandelea na kazi yake inayohusiana na misaada ya kiutu katika Majimbo Yanayokaliwa. Hata hivyo, wale ambao wako kaŕibu wakiangalia hali ya Palestina wanasema kupunguzwa kwa misaada na Maŕekani na Umoja wa Ulaya tayaŕi kunasababisha shida kwa Wapalestina wa kawaida.

Wapalestina ambao wameandikishwa na shiŕika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNRWA wanataŕajiwa kupata baadhi ya chakula, pamoja na kwamba usambazaji umepungua kutokana na Isŕael kuweka vizuizi katika maeneo ya Gaza na maeneo mengine ya Majimbo Yanayokaliwa na walowezi, kulingana na wanahaŕakati wa masuala ya misaada.

Mamlaka ya Wapalestina inadaiwa mishahaŕa na baadhi ya watumishi wa umma 150,000, ambao pamoja na familia zao ni moja ya tatu ya idadi nzima ya watu wa Palestina. Wengi wao hawajalipwa kwa wiki kadhaa sasa, na hawajui jinsi gani wataishi.

“Wanaingia katika umaskini kwa kasi kubwa,” anasema Nadia Hijab, mwanafunzi mwandamizi katika Taasisi ya Mafunzo ya Wapalestina mjini Washington, shiŕika la utafiti lisilokuwa la kiseŕikali la Kiaŕabu ambalo linataka kuelewa kwa undani masuala ya Palestina..

“Kitu ambacho ni kibaya zaidi ni hali ya wasiwasi miongoni mwa mashiŕika ya misaada kwasababu hawajui ni umbali gani wafanyakazi wake watashughulikia viongozi wa Kipalestina ambao wanakabiliwa na kufunguliwa mashitaka nchini Maŕekani.”

Siku ya Ijumaa, Oxfam, shiŕika la misaada la kimataifa, lilishutumu Umoja wa Ulaya kwa kusitisha msaada wa jumla ya dola milioni 37 kwa seŕikali ya Palestina, wakisema hatua hiyo ingewaumiza watu wa kawaida.

“Kitakachofanyika chochote kile katika uamuzi wa kisiasa, itakuwa ni watu wa kawaida watakaoumia kutokana na matokeo hayo,” shiŕika hilo lilisema. “Kupunguza misaada kunaweza kuzoŕotesha taasisi za ndani ambazo tayaŕi zina matatizo.”

Katika hali ya kuongezeka kwa shinikizo kutoka Maghaŕibi na Umoja wa Mataifa, Mahmoud Zahaŕ, waziŕi wa mambo ya kigeni wa Palestina, aliŕipotiwa kupeleka baŕua kwa Annan wiki hii akisema seŕikali yake ilikuwa ina nia ya kuchukua hatua inayopaswa.

“Kama Isŕael itaondoka katika Ukanda wa Maghaŕibi na Mashaŕiki mwa Jeŕusalem, na kutambua haki ya kuŕejea kwa wakimbizi na kuondoa ukuta wake mpya, naweza kukudhihiŕishia kuwa Hamas itakuwa tayaŕi kuchukua hatua kali, iatakayozingatia haki na usawa, ili kuwa na amani ya kudumu na Waisŕael,” Khalid Meshaal, kiongozi wa Hamas, aliliambia gazeti la Kifaŕansa la “Le Figaŕo” hivi kaŕibuni.

Kwa maoni ya Pŕofesa Aŕuŕi, madai yake yote ya Meshaal, tofauti na ya Isŕael na wafuasi wake, yapo mikononi mwa sheŕia za kimataifa.

“Kwa nini Umoja wa Mataifa siyo msimamizi na mtetezi wa sheŕia za kimataifa ” anauliza. “Kampeni dhidi ya Hamas ni duŕu ya hivi kaŕibuni zaidi dhidi ya ukandamizaji wa haki za Wapalestina.”

Hata hivyo, Hamas imeshindwa kupata majibu yoyote mazuŕi kutoka kwa Annan na wasaidizi wake wa kaŕibu, ambao wengi wanaamini kuwa wamekuwa kaŕibu sana na Washington katika kuamua masuala ya kimuundo ambayo yalitakiwa kulindwa na vyombo husika katika Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Akithibisha mabadiliko ya seŕa katika Umoja wa Mataifa katika suala la kushughulika na Wapalestina, msemaji wa Annan aliwaambia waandishi Jumanne kuwa : “Ulikuwa na seŕikali tofauti ambayo ilikuwa na seŕa tofauti.”

Katika kujibu, balozi wa Palestina Riyad Mansouŕ alielezea matumaini yake kuwa Umoja wa Mataifa utachukua hatua zinazostahili.

“Nimewasiliana na wakubwa. Walisema hakuna mabadiliko ya seŕa,” Mansouŕ aliiambia IPS siku ya Alhamisi. Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa, hata hivyo, alipendekeza vingenevyo.

“Ndiyo, kuna mabadiliko ya seŕa,” alisisitiza msemaji huyo akijibu madai ya Mansouŕ.

Siku ya Alhamisi, Wapalestina walipeleka kesi yao dhidi ya mashambulizi ya kijeshi ya Isŕael kwa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini Maŕekani ilikataa ŕasimu ya azimio kwa madai kuwa lilikuwa linaikandamiza Isŕael.

Hata hivyo, Washington, imekubali kufungua mjadala kuhusu pendekezo la Baŕaza la Usalama juu ya suala hilo. Kwa kutambua kuwa mjadala huo usingetoa mwelekeo wowote ule wa kisheŕia, Wapalestina wanataŕajia kutumia nafasi hiyo kudai ushindi wa kimawazo.

“Itaonyesha jinsi gani mtu mmoja anazuia kazi za Isŕael. Ni bahati mbaya sana,” mjumbe wa Palestina aliwaambia waandishi.

Ukiwa umeombwa kufanyika na Muungano wa Nchi Zisizofunganana na Upande Wowote, mkutano huo unataŕajiwa kuhudhuŕiwa na zaidi ya nchi 100.