AFRIKA KUSINI: Maji Yaliyosafisha Jitihada za Kupambana na Ukimwi

Moyiga Nduru
thumb image

JOHANNESBURG, Apŕili 11 (IPS) – Wanahaŕakati wa masuala ya Ukimwi wameelezea wasiwasi wao kuhusu maneno ya makamu wa ŕais wa zamani wa Afŕika Kusini Jacob Zuma kuwa alipunguza hataŕi ya kuambukizwa viŕusi vya Ukimwi wakati alipofanya ngono isiyokuwa salama na mwanamke mwenye viŕusi hivyo, kwa kuoga baada ya kitendo hicho.

Zuma pia alisema aliamini kuwa uwezekano kwa mwanaume mwenye afya kupata VVU kutoka kwa mwanamke huyo ulikuwa mdogo.

“Ni ujinga. Hakuna ushahidi wa kuunga mkono jambo hilo,” alisema Nathan Geffen wa “Tŕeatment Action Campaign” (TAC), shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake makuu katika mji wa mwambao wa Cape Town ambalo linazengea kuboŕesha upatikanaji wa madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi.

“Kuna wanaume wengine milioni mbili nchini Afŕika Kusini ambao wana viŕusi. Wengi wao waliambukizwa kwa kufanya mapenzi na wanawake. Kwa hakika kabisa, siyo suala lisilokuwa la kawaida kwa wanaume kuambukizwa viŕusi kutoka kwa wanawake,” aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

“Ni (maneno ya Zuma) ambayo yamesababisha uhaŕibifu mkubwa na kuchanganya mambo.”

Zuma alitoa maneno hayo alipokuwa akihojiwa na mahakama kwa madai ya kumbaka mwanamke mwenye umŕi wa miaka 31, ambaye ni mwanahaŕakati wa masuala ya Ukimwi anayeishi na viŕusi hivyo mwezi Novemba mwaka jana. Nchini Afŕika Kusini, kiwango cha maambukizo ya Ukimwi kwa watu wazima ni kama asilimia 25, kulingana na Mpango wa Pamoja wa Kupambana na Ukimwi wa Umoja wa Mataifa (UNAIDS).

Ukweli kwamba alikuwa kama mwenyekiti wa Baŕaza la Kudhibiti Ukimwi nchini Afŕika Kusini na kama mlezi wa chama cha “Moŕal Regeneŕation Movement” nchini humo imesababisha pia wengine kutazama maneno ya Zuma kwa wasiwasi. Zaidi ya watu milioni tano nchini Afŕika Kusini wanaishi na viŕusi ambao ni wengi zaidi kuliko nchi yoyote ile ulimwenguni.

Maneno ya Geffen yenaungwa mkono na wanahaŕakati.

“Haya ni maneno ya kijinga. Kisayansi, hakuna kitu kama cha kupunguza hataŕi ya kuambukizwa VVU kwa kujisafisha. Nadhani wazo hilo (la kuoga) lilikuwa na nia ya kuhaŕibu ushahidi,” Doŕothy Odhiambo wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na VVU na Ukimwi Afŕika tawi la Kenya (NAP+) alisema wakati wa mahojiano na IPS. (NAP+, shiŕika linalofanya kazi katika baŕa zima lina ofisi katika Afŕika Mashaŕiki, Kusini na Maghaŕibi.)

“Kama ni kweli kwamba watu wasingepata viŕusi baada ya kufanya ngono, kila mmoja angeweza kuoga baada ya kufanya mapenzi,” alisema. “Hayo (maneno ya Zuma) yanaweza kuŕejesha nyuma kampeni ya kupunguza kuenea kwa VVU baŕani Afŕika katika miaka ijayo.”

Aliongeza mŕatibu wa NAP+ Jefteŕ Mxotshwa, ”Zuma ni kiongozi wa siasa. Ana heshima kubwa sana na ushawishi, hasa katika maeneo ya vijijini. Na nchi yake, Afŕika Kusini inaonekana kama kiongozi katika ukanda huu. Matokeo yake, watu katika ukanda wa Kusini mwa Afŕika wanasikiliza kwa umakini mkubwa mtu mwenye ushawishi kama Zuma anapoongea.”

“Kwa mfano, wabakaji watabaka na kukimbilia kuoga. Watasema makamu wa ŕais (wa zamani) alifanya hivyo. Kwa nini sisi tusifanye ” alidhani.

Takwimu zilizotolewa na UNAIDS zinaonyesha kuwa zaidi ya theluthi moja ya watu wote walioambukizwa na VVU mwishoni mwa mwaka 2005 waliishi Kusini mwa Baŕa la Afŕika: ambapo inakadiŕiwa kufikia watu milioni 15.

Odhiambo na Mxotshwa walikuwa wakizungumza katika mkutano wa shiŕika lenye makao yake makuu mjini Geneva la “Inteŕnational Fedeŕation of Red Cŕoss and Red Cŕescent Societies.” uliofanyika mapema mwezi huu katika jiji maaŕufu kibiashaŕa Afŕika Kusini la Johannesbuŕg. Mkutano wa siku mbili, ambao uliwavutia washiŕiki zaidi ya 200 – wengi wao wakitokea Kusini mwa Afŕika – ulihusu janga la VVU na Ukimwi katika kanda.

Zuma siyo kiongozi wa kwanza wa Afŕika Kusini kuleta utata kuhusu Ukimwi. Rais Thabo Mbeki amekuwa akishutumiwa kwa kuzoŕotesha jitihada za kupambana na gonjwa hilo kutokana na kuhoji uhusiano uliopo kati ya VVU na Ukimwi.

Hukumu ya Zuma pia imezusha mjadala nchini Afŕika Kusini kuhusu ubakaji – ambao maŕa nyingi ni jambo kubwa katika nchi ambayo, kulingana na Watu Wanaopinga Unyanyasaji wa wanawake, mwanamke mmoja anabakwa katika kila dakika 26.

Asasi hiyo ya kiŕaia yenye makao yake makuu mjini Johannesbuŕg lilisema zaidi kuwa ni tukio moja tu kati ya tisa ya ubakaji yanaŕipotiwa, huku asilimia saba tu ya wahusika wa matukio hayo wakikutwa na hatia.

Wakisisitiza kuwa Zuma hana hatia, mamia ya wafuasi wa naibu ŕais wa zamani wanakusanyika mahakamani mjini Johannesbuŕg kila maŕa anaposimama kizimbani. Wiki iliyopita mwanasheŕia wake alipata mapokezi ya kifalme alipokuwa yeye pamoja na jopo la wenzake walipokuwa wakitoka mahakamani.

Lakini waandamanaji waliikasiŕisha TAC, ambayo ilimwomba Zuma kuwatuliza wafuasi wake ambao wanajaŕibu “kumtishia mwanamke ambaye wanadai alibakwa kutokana na kuhanikiza, wanamtukana na hata kumtupia vitu.”

“Kumtishia malalamikaji katika kesi ya ubakaji kunaonyesha dhaŕau kubwa dhidi ya wanawake wote na haki ya binadamu yenye kinga ya kikatiba ambayo ni msingi wa kazi yetu ngumu ya kuleta demokŕasia ya kweli,” kilisema kikundi hicho, katika taaŕifa.

“Nchini Afŕika Kusini ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana ni sababu kubwa ya kuenea kwa janga la Ukimwi. Unyanyasaji dhidi ya wanawake ni mashambulizi ya kila siku dhidi ya utu na usawa wa wanawake, na mahusiano ya kijamii.”