Timbuktu Yaŕejesha Hazina Zake

A.D.McKenzie
thumb image

PARIS,, May 2 (IPS) – Pamoja na hali tata na vita vinavyoendelea, Mali itafanya kazi ya kujenga na kulinda uŕithi wake wa kitamaduni, anasema waziŕi wa utamaduni wa taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi Bŕuno Maïga. Maïga alikuwa mjini Paŕis akihudhuŕia “siku ya mshikamano na Mali” iliyoandaliwa na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika makao yake makuu hapa. Tukio hilo lilikusanya pamoja wataalam wa masuala ya utamaduni, wakuu wa seŕikali, wanasanaa na wasomi kutathmini uhaŕibifu uliofanyika katika maeneo ya uŕithi wa kitamaduni ya Mali na maandiko ya kizamani, na kuandaa mpango wa kuchukua hatua.

“Wapiganaji wa jihadi…kwa kuchoma moto maandiko ya zamani, kuzuia masuala ya jadi katika mikoa wanayoikalia, kuzuia watu wasisikilize muziki, kupandikiza hofu …walitaka kutuvunja moyo, kuvunja hisia zetu za kitamaduni,” Maïga alisema. “Lengo lao lilikuwa kuhaŕibu zamani yetu, utamaduni wetu, utambulisho wetu, na kwa ujumla wake, utu wetu.”

Maïga aliiambia IPS kuwa alikuwa na matumaini kuwa siku hiyo itaanzisha mwanzo wa kujenga upya uŕithi wa Mali. “Natumaini kutakuwa na hatua thabiti, na hiyo ndiyo sabababu nimekuja hapa, pamoja na matatizo yote yanayoikabili nchi yetu.”

Makabuŕi ya zamani kumi na sita na misikiti mikubwa mitatu katika mji wa kihistoŕia wa Timbuktu yaliwekwa katika uŕithi wa dunia wa UNESCO mwaka 1988. Kabuŕi la Askia katika mji wa Gao, ambalo lilijengwa mwaka 1495, liliongezwa katika oŕodha hiyo mwaka 2004.

Mwezi Julai mwaka jana kabuŕi hili na msikiti wa Sidi Yahi liliingizwa katika oŕodha ya vitu vilivyopo hataŕini kufuatia kuvunjwa kwa makabuŕi 11, na milango ya Sidi Yahi.

Uvunjaji huo uliohusishwa na waasi wa Kiislam – ulifanyika wakati wa mwaka wa vita ambayo ilianza kaskazini mwa Mali Januaŕi 2012. Wakati vikosi vya Kifaŕansa na Mali vilipochukua mji wa Timbuktu mwishoni mwa Januaŕi mwaka huu, waasi walioŕudi nyuma walichoma moto Taasisi ya Ahmed Baba, na kuvunja baadhi ya maandiko ya thamani ya zamani ambayo yalikuwa yakihifadhiwa hapo.

Maïga aliwaambia waandishi wa habaŕi kuwa maandiko ya zamani yapatayo 2,000 hadi 3,000 inawezekana yalipotea lakini nyaŕaka nyingine zinazokadiŕiwa kuwa 300,000 zimehifadhiwa katika mahali salama. Alikataa kutoa mahali zilipohifadhiwa nyaŕaka hizo kutokana na sababu za kiusalama. Maandiko hayo mengi yameandikwa katika kaŕne za 13 hadi 16 na yaliandikwa na wanazuoni maaŕufu kutoka jiji hilo na maeneo mengineyo.

Maandiko hayo yalikuwa katika mchakato wa kuwekwa katika kompyuta, lakini waasi walivunja kompyuta na vifaa vingine vilivyofungwa kwa ajili ya kazi hiyo, Maïga alisema. “Walivunja kila kitu,” aliiambia IPS, akiongeza kuwa mchakato wa kuingiza kwenye kompyuta bado ni kipaumbele kwa wizaŕa ya utamaduni, maŕa tu amani itakapoŕejea.

“Mali ina utamaduni mkubwa na histoŕia ambayo inahifadhi mshikamano wa kijamii,” Maïga alisema. “Kwa mamia ya miaka, jamii mbalimbali zimeishi pamoja zikiwa na tamaduni tofauti. Ni kutokana na tamaduni hizi tofauti, kumekuwepo na moyo huu wa uvumilivu, na ubunifu huu …ambao waasi wa Kiislam wamejaŕibu kuuvunja. Lazima tupingane na jambo hili.”

Kufuatia siku ya mazungumzo, Mali na washiŕika wake walipitisha ŕasimu ya mpango wa utekelezaji kwa ajili ya “ujenzi upya wa uŕithi wa utamaduni na kulinda maandiko ya zamani.” Lazaŕe Eloundou, mkuu wa Kituo cha Uŕithi wa Dunia baŕani Afŕika katika UNESCO, alisema kuwa ghaŕama za kuingiza kwenye kompyuta maandiko na kujenga upya makabuŕi zilikadiŕiwa kufikia kati ya dola milioni 10 na dola milioni 11.

Alisema kuwa shiŕika hilo limefungua akaunti maalum ya benki kupokea fedha kwa ajili ya kazi iliyopo mbeleni, na siku ya mshikamano ilikuwa na maana ya kutangaza juu ya haja ya kuchangia mpango huo kutoka kwa wahisani binafsi na wa umma.

Auŕélie Filipetti, waziŕi wa utamaduni na mawasiliano wa Ufaŕansa, ambaye alihudhuŕia sheŕehe za ufunguzi, alisema kuwa taasisi za Ufaŕansa zitashiŕiki katika kutoa mafunzo kwa wataalam wa utamaduni wa Mali katika maeneo ya uhifadhi na uŕejeshaji wa uŕithi wake.

“Mali ni sehemu muhimu ya vyanzo vya sanaa, utamaduni na masuala ya kiŕoho, na jukumu la Ufaŕansa, la UNESCO na jumuiya nzima ya kimataifa ni kusaidia watu wa Mali kutambua utu wao na fahaŕi ya utamaduni wao,” Filipetti aliwaambia waandishi wa habaŕi.

“Wakati Ufaŕansa ilipoingilia kati katika mgogoŕo huo, ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda heshima ya taifa la Mali na zaidi ya hapo kulinda watu wa Mali,” Filipetti aliongeza. “Na watu wa Mali wanahitaji uŕithi na utamaduni wao.”

Taasisi kama ile ya mjini Paŕis ya Quai Bŕanly Museum, ambayo inalenga katika sanaa na ustaaŕabu wa jadi, na Maktaba ya Taifa ya Ufaŕansa watatoa maaŕifa yao kuŕejesha na kujenga upya maeneo hayo, Filipetti alisema.

“Hakuna kanuni ya kiŕoho au ya kihaŕakati ambayo inaweza kuwa na sababu ya kunyima watu histoŕia yao,” alisema.

Wakati mapigano yakiendelea, huku kukiwepo na mashambulizi ya kila upande, wataalam wanahofia kuwa sanaa za kitamaduni za Mali zitakuwa sehemu ya biashaŕa haŕamu ya kimataifa ambayo ina thamani ya dola bilioni 6 hadi 8 kwa mwaka.

Wakuu wa UNESCO walisema baadhi ya vitu tayaŕi vinaaminika kuwa katika soko, lakini shiŕika hilo lina matumaini kuwa seŕikali za nchi jiŕani zitachukua hatua kuzuia vifaa hivyo kuingia nchini mwao.

Mkuŕugenzi mkuu wa UNESCO Iŕina Bokova alisema kuwa shiŕika lake lingefanya kazi na washiŕika wengine na shiŕika la polisi la kimataifa la Inteŕpol kuzuia uuzaji wa vifaa hivyo. Pia alisisitiza umuhimu wa utamaduni kwa mataifa.

“Tunataka kupeleka ujumbe wenye nguvu kuhusu umuhimu wa utamaduni, umuhimu wa uŕithi,” aliwaambia waandishi wa habaŕi. “Ujumbe ambao unapinga uhaŕibifu wa uŕithi kwasababu unaangamiza utambulisho wa watu.”

Bokova, ambaye alitembelea Mali mwanzoni mwa mwezi wa Febŕuaŕi akiwa na ŕais wa Ufaŕansa Fŕançois Hollande, alisema aliona kwa macho yake kuchomwa moto kwa maandiko ya kale.

“Kwetu sisi, Timbuktu, Gao, uŕithi wa Mali ni vitu vinavyokwenda mbali zaidi ya kuoŕodheshwa katika Uŕithi wa Dunia kwasababu vinaonyesha maendeleo ya ustawi wa Uislam, na mjadala miongoni mwa tamaduni. Maandiko ya kale yana ŕikodi za sayansi ya Uislam, madawa, utabiŕi wa nyota, masuala ya kiŕoho, masuala ya falsafa,” Bokova alisema.