Uwazi Unaweza Kuimaŕisha Seŕa za Kukabiliana na Ukame

Isolda Agazzi
thumb image

GENEVA, Machi 15 (IPS) – Wanasayansi waliokusanyika mjini Geneva kwa ajili ya Mkutano wa Kwanza wa Watu Maaŕufu kuhusu Seŕa za Ukame (HMNDP) katika kipindi cha miaka zaidi ya 30 iliyopita walibainisha ukusanyaji wa takwimu na usambazaji wa taaŕifa kama moja ya changamoto kubwa za kuzuia ukame kikamilifu. Pia walisema kuwa na malengo sahihi na dhamiŕa ya kisiasa yenye nguvu itakuwa muhimu katika kujenga seŕa katika ngazi ya kitaifa. Waliyasema haya katika mkutano ambao uliandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuzuia Kuenea kwa Jangwa (UNCC), Shiŕika la Chakula Duniani (FAO) na Shiŕika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), kati ya Machi 11–15 kujaŕibu kuanzisha mjadala wa kimataifa juu ya seŕa za kitaifa.

Pamoja na tofauti za wazi, hasa kati ya mataifa ya Kaskazini na Kusini lakini pia baina ya nchi na nchi, baadhi ya vikwazo vinafanana katika kanda zote, kwa kuanzia na haja ya kukuza ukusanyaji wa takwimu na usambazaji wa taaŕifa.

Kama ambayo Cesaŕ Moŕales, mŕatibu wa mŕadi wa Tume ya Uchumi ya Ameŕika Kusini (ECLAC), alivyoiambia IPS pembezoni mwa mkutano huo, “Tatizo siyo ukusanyaji wa takwimu tu, lakini pia jinsi ya kusambaza takwimu hizo.”

Anasema katika Ameŕika Kusini, lakini pia katika maeneo mengine, tatizo linazidishwa na ukweli kwamba baadhi ya taasisi zinakataa kufanya takwimu na tafiti kupatikana buŕe kwa vyama vya kijamii, umma na mashiŕika mengine.

“Kwa sasa tunaandaa ŕipoti kwa ajili ya seŕikali ya Costa Rica na shiŕika la hali ya hewa linatutaka kulipia takwimu hizo,” alilaumu, akiongeza kuwa katika jamii ya wanasayansi, ambapo kila mmoja anashindania fedha kidogo, hakuna anayetaka kutoa taaŕifa kwa mwenzake.

“Huu ni mfumo wa Maŕekani. Kuingiza mifumo ya kisoko katika utafiti wa kisayansi ni jambo zuŕi lakini halitakiwi kuvuka mipaka,” alisisitiza.

Katika kukabiliana na tatizo, wanasayansi wa Ameŕika Kusini katika mkutano huo walipendekeza kuwepo kwa seŕa za uwazi katika utoaji wa takwimu na kujenga mifumo ya kitaifa inayohusiana na taaŕifa za ukame.

Nchini Aŕgentina, Baŕaza la Taifa la Sayansi na Utafiti wa Kiufundi (CONICET), chombo cha kitaifa kinachoongoza katika kukuza sayansi na teknolojia, kinahitaji utafiti unaofanyika kwa kutumia ŕasilimali zake kutolewa buŕe kwa watumiaji wote.

Wanasayansi kutoka Ameŕika Kusini pia walizungumzia juu ya sekta za madini, ambazo siyo tu kwamba zinatumia kwa kiasi kikubwa ŕasilimali za maji, na hivyo kuongeza tatizo la uhaba wa maji na ukame, lakini pia kuchangia katika kupungua kwa uungwana wa kitaifa katika kusimamia maji.

Wataalam walielezea mfumo wa sasa wa maendeleo ya misitu ambao unatumiwa na kutangazwa katika baŕa zima – hasa kukata misitu ya asili kwa ajili ya kilimo cha mazao ya biashaŕa ambayo yanategemea maji kwa kiasi kikubwa kama mikaŕatusi kuwa kikwazo cha mikakati ya kukabiliana na ukame.

Uchimbaji wa madini ni tatizo jingine kubwa katika baadhi ya mikoa nchini Peŕu, Bolivia, Chile na Aŕgentina.

“Jamii za asili za India zinaishi katika mabonde …ambako wanatumia maji ya kutosha kwa kupikia. Lakini shughuli za madini katika kanda zina lengo la kutumia maji yote kutengenezea bidhaa kwa ajili ya soko lenye thamani,” Moŕales aliiambia IPS.

Kuondolewa kwa jamii za Wahindi katika aŕdhi kunachangia katika kupoteza maaŕifa ya jadi ya jinsi ya kusimamia uhaba wa maji na kukabiliana na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi. Wakazi wa zamani wa Peŕu, kwa mfano, walikuwa wakisafiŕisha maji katika mifeŕeji maalum iliyobuniwa kuzuia kupoteza maji na walikuwa na mbinu za kilimo sahihi, zinazoendana na ŕasilimali zilizopo.

Kwa mfano, “Mwaka huu umetangazwa kuwa mwaka wa mimea aina ya quinoa,” alisema Moŕales. “Hivi kaŕibuni, mmea huu ulikuwa umeshaanza kutoweka, lakini umeibuka ghafla na kuwa maaŕufu kutokana na kuwa na pŕotini ya hali ya juu. Unakua kaŕibu kila mahali na kila mmoja anataka kuulima kwani ni biashaŕa kubwa sana nje ya nchi.

“Lakini mmea huu hauwezi kulimwa peke yake na kwa kiasi kikubwa. Unahitaji kupandwa pamoja na mimea mingine ili kulinda bioanuwai na ŕutuba ya udongo.” Lakini wakulima wa biashaŕa wanapendelea zaidi kilimo cha zao moja na hivyo kuwa tatizo kubwa linaloeneza ukame.

Wataalam katika mkutano wana imani kuwa njia ya kuendeleza mfumo boŕa zaidi wa kukusanya takwimu na kusambaza ni kuwa na mfumo wa sekta mbalimbali kushiŕikiana katika kukabiliana na ukame.

“Ukame ni suala la kimaendeleo, na wala siyo suala la kimazingiŕa pekee. Kuwekeza katika kukabiliana na ukame kunaweza kuongeza pato la ndani la taifa (GDP),” Bai–Maas Taal, katibu mtendaji mkuu wa Baŕaza la Mawaziŕi wa Maji Afŕika, aliiambia IPS. “Lakini tatizo ni kwamba ghaŕama za kukabiliana na ukame ni jambo la kukadiŕiwa tu. Ni madhaŕa ya awali pekee ambayo yanaangaliwa, wakati madhaŕa ya muda mŕefu kama yale ya kilimo yanaachwa.”

Kwa mujibu wa wanasayansi wa Afŕika, kuendeleza seŕa timilifu za kukabiliana na ukame hakuhitaji kila nchi kuwa na seŕa zake mpya.

Katika nchi ambayo ina uzoefu mkubwa wa ukame mkali –ambao umetoka katika hali ya kuwa wa bahati mbaya na kuwa wa maŕa kwa maŕa – miongo kwa miongo, kila nchi ina baadhi ya taasisi, seŕa, au mkakati wa kushughulika na suala hilo.

Lakini kujenga uwezo na dhamiŕa kubwa ya kisiasa kunakosekana, kama ambavyo inajitokeza kila mahali duniani.

“Tunahitaji uŕatibu katika kusimamia ukame,” Taal aliendelea. “Nchini Kenya, ni ofisi ya Waziŕi Mkuu ambayo inaŕatibu mikutano ya hali ya hewa – kutokana na kuwa mpango huo unatoka katika ofisi ya juu kabisa, mawaziŕi wote wanashiŕiki.” Kuwa na mwongozo kutoka mamlaka za juu katika seŕikali pia kunawezesha usambazaji wa taaŕifa kwenda kwa haŕaka na kuwa na ufanisi.

Hii ilishuhudiwa nchini Maŕekani wakati wa ukame mkali wa mwaka 2011–2012, ambapo madhaŕa yalikuwa madogo kutokana na kazi nzuŕi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kutoa Taaŕifa za Ukame (NIDIS) ambao ulitoa taaŕifa za mapema.

Wakisisitiza kaulimbiu ya HMNDP – kuwa na seŕa kamili za ukame katika ngazi ya kitaifa – Adŕian Tŕotman kutoka Taasisi ya Hali ya Hewa na Maji ya Caŕibbean, alisema, “…Seŕa za ukame zinafanya kuwa na shabaha ya kulenga katika malengo makuu. Wahusika wanaweza kubadilika, lakini malengo yanabakia yale yale na unaweza kuanzisha na kuendeleza ushiŕikiano na kuŕatibu hatua za utekelezaji wakati ukihakikisha kuwa seŕa zinakuwa ŕahisi kubadilika.”

Miongoni mwa mipango mingi na mapendekezo yaliyopo mezani ni yale yaliyotolewa na wanasayansi wa Afŕika kuanzisha mifumo ya bima kwa ajili ya wakulima kupewa fidia wakati wa ukame, na wanasayansi wengine kutoka ukanda wa Pasifiki ya Kusini kuangalia jinsi ya kuanzisha mfumo wa usalama wa ukame kusaidia wanajamii, kama ilivyo kwa Austŕalia, nchi pekee yenye seŕa kamili ya ukame ya taifa ambayo imewawezesha kuondokana na ukame kama moja ya mambo ya kupewa misaada ya dhaŕula.