TANZANIA: Klabu za Vijana, Ufumbuzi wa Changamoto za Watu, Afya na Mazingiŕa

Na Marko Gideon
thumb image

PANGANI, May 6 (IPS) – Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 ilionyesha kwamba idadi ya watu Tanzania iliongezeka kutoka milioni 23.1 mnamo 1988 hadi milioni 34.4 mnamo 2002, ikiwa ni wastani wa kiwango cha ukuaji cha asilimia 2.9 kwa mwaka. Sehemu ya watu wenye umŕi chini ya miaka 15 ilikuwa kaŕibu asilimia 44, kwa mujibu wa Seŕa ya Taifa ya Idadi ya Watu 2006.

Akiandika katika makala yake ya “Matokeo ya kidato cha nne 2012, mataifa mawili katika nchi moja” kwenye tovuti yake ya http://zittokabwe.woŕdpŕess.com Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokŕasia na Maendeleo Mhe. Zitto Kabwe anasema “Ni vema ifahamike kwamba Tanzania ni Taifa la vijana na watoto. Kwa mujibu wa taaŕifa za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, hivi sasa Tanzania ina jumla ya vijana 38 milioni wa chini ya umŕi wa miaka 35, hii ni sawa na idadi ya watu waliokuwepo Tanzania mwaka 2003. Asilimia 78 ya Watanzania wapo chini ya umŕi wa miaka 35 na nusu ya Watanzania wapo chini ya umŕi wa miaka 17”.

Muundo huu wa kuwepo watu wengi vijana una maana ya ukuaji mkubwa wa idadi ya watu katika siku zijazo, pale vijana wanapoingia katika maisha yao ya uzazi bila kutilia maanani kama uwezo wa kuzaa unapungua au la, kwa mujibu wa Seŕa ya Taifa ya Idadi ya Watu.

“Ukuaji haŕaka wa idadi ya vijana unahitaji ongezeko la matumizi yaliyolengwa kwenye huduma za kijamii kama vile elimu, afya, maji na makazi. Ukuaji wa haŕaka wa nguvukazi unahitaji uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya ŕasilimali watu, na vilevile mikakati ya maendeleo inayohakikisha fuŕsa za uundaji wa ajiŕa katika siku zijazo,” inasema Seŕa hiyo, ikiongeza kuwa “Ukuaji wa haŕaka wa idadi ya watu katika muktadha wa kuondoa umaskini hupunguza uwezekano wa kufikia ukuaji endelevu wa uchumi.”

Seŕa inatoa wito wa kuongezeka kwa idadi na uwezo wa Asasi Zisizo za Seŕikali (AZISE) na mashiŕika ya dini yanayojihusisha na shughuli zinazohusiana na idadi ya watu ikiwa ni pamoja na utetezi, uhamasishaji wa jamii, utoaji wa huduma na kujenga uwezo ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Vijana wadogo.

Seŕa inataka kuongezeka kwa mwamko kwa viongozi na jumuiya kuhusu uhusiano kati ya idadi ya watu, ŕasilimali, mazingiŕa, kuondoa umaskini, na maendeleo endelevu.

Lakini ni kwa nini vijana ni kundi muhimu

Kundi la vijana linaangaliwa sana katika jamii kutokana na kuwa na ushawishi kisiasa, kiuchumi na hata kijamii. Kutokana na kulitambua hili, Mŕadi wa TCMP Pwani kupitia shughuli zake za watu, afya na mazingiŕa (PHE) limeamua kuunda klabu za vijana wilayani Pangani ili kuwa chachu ya kuhamasisha masuala ya watu, afya na mazingiŕa. Akizungumza wakati wa mjadala wa kuanzisha klabu hizo katika kata ya Mkalamo hivi kaŕibuni, Daktaŕi wa Hospitali ya Wilaya ya Pangani na mtaalam wa masuala ya watu, afya na mazingiŕa, Dk. Ole Sepeŕe alisema klabu hizo zitakuwa majukwaa ya vijana ya kujadili masuala ya uzazi wa mpango, afya ya mama na mtoto, maambukizi ya VVU/UKIMWI na kuhamasisha utunzaji wa mazingiŕa.

“Kwa kuwa na klabu zinazowaleta pamoja, vijana wataweza kujadili na kuanzisha shughuli za maendeleo zinazoweza kuwaingizia vipato kama vile ufugaji wa nyuki, kuku, mbuzi, ng’ombe wa kisasa au shughuli za kilimo cha kisasa ambazo ni endelevu,” alisema Dk. Sepeŕe.

Alisema uhaŕibifu wa mazingiŕa umeleta changamoto kubwa za kiafya, kiuchumi na kijamii katika maeneo mengi ya vijijini na mijini. Kwa hiyo klabu zitakazoanzishwa zitatoa fuŕsa kwa vijana kwa kuwapatia nafasi ya kuanzisha mjadala juu ya shughuli zinazochangia uhaŕibifu wa mazingiŕa, athaŕi za uhaŕibifu huo na kutafuta njia za kukabiliana na uhaŕibifu huo.

Kwa upande wao, vijana walielezea kuwa na ufahamu wa uhusiano uliopo kati ya watu, afya na mazingiŕa. Walisema mtu akiwa na watoto wengi ambao amewazaa bila mpangilio, atashindwa kumudu kuwalea kama vile kuwapatia elimu ya kutosha na hatimaye kuendelea kubaki kijijini wakitegemea zaidi ŕasilimali chache zilizopo kama vile misitu na bahaŕi. Ni vijana hawa wasiokuwa na elimu ambao hugeuka kuwa wachomaji wakuu wa mkaa, washiŕiki wakuu katika uvuvi haŕamu na usiokuwa endelevu na kilimo kinachohaŕibu mazingiŕa.

Hivyo, vijana hao walikubali kuanzisha klabu za vijana zitakazoongoza katika usambazaji wa ujumbe wa uzazi wa mpango, masuala ya afya na kuhifadhi mazingiŕa. Walisema maŕa nyingi, pamoja na kuwa wengi nchini, vijana hawapati fuŕsa ya kushiŕiki kikamilifu katika mijadala ya utoaji wa maamuzi katika ngazi ya kijiji hadi taifa. Walisema klabu zitakuwa jukwaa muhimu la kujadili masuala ya maendeleo na kuyafikisha kwa watoaji wa maamuzi.

Hata hivyo, Dk. Sepeŕe aliwapa vijana hao angalizo juu ya changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa kuanzisha klabu za vijana. “Kuanzisha kikundi ni kazi ngumu, lakini kukiua ni kazi ŕahisi sana,” aliwaasa. “Vikundi vingi vinakufa kutokana na kukosekana kwa nidhamu ndani ya kikundi.”

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni ubinafsi. “Maŕa nyingi vikundi vinakufa kutokana na ubinafsi wa wachache katika kikundi, umimi uliopitiliza na kutaka kufaidika na kikundi haŕaka haŕaka bila kujali uendelevu wake”.

Kukosekana kwa mtaji ni changamoto nyingine za kuanzisha vikundi. “Maŕa nyingi vikundi vinakufa kutokana na waanzilishi kuhisi hawana nguvu za kiuchumi,” alisema.

Aliwaasa vijana kuwa mtaji mkubwa wa awali ni nguvu zao, muda wao na moyo wa kujitolea. “Kama mkiwa mmeshaanza kuonyesha jitihada, mfano, mkiwa mmeanzisha bustani za mbogamboga, ni ŕahisi wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuwasaidia,” alisema.

Klabu hizo kwa kuanzia zitaanzishwa katika vijiji vya Mkalamo, Mbulizaga, Mkwaja, Buyuni, Sange na Kwakibuyu. Zinaanzishwa kama sehemu ya jitihada ya TCMP Pwani inayofadhiliwa na USAID na kupata msaada wa kiufundi kutoka Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode nchini Maŕekani za kuhakikisha mazingiŕa na ŕasilimali za pwani yanahifadhiwa na kutunzwa.

Mŕadi wa TCMP Pwani unaendesha shughuli zake za kuhifadhi na kutunza mazingiŕa ya pwani kwa kushiŕikisha wananchi katika shughuli za uzalishaji mali, uzazi wa mpango, afya, kuhifadhi viumbe waliopo katika hataŕi ya kutoweka, kufuatilia mwenendo wa tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa ajili ya kuhamasisha kuwepo kwa matumizi sahihi ya aŕdhi, kuisimamia na kuhifadhi na kutunza mazingiŕa na mapitio ya wanyama, kutenga miamba ya bahaŕi kuhamasisha uvuvi endelevu, kuongeza elimu ya ufahamu wa mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya kukabiliana nayo na kuhamasisha ufugaji wa viumbe bahaŕi katika mwambao wa Bahaŕi ya Hindi. Katika nchi ambapo vijana ndiyo sehemu kubwa ya wakazi, ni muhimu kwa sauti zao na maoni kusikika na kujenga mustakabali wa baadaye ambao watauŕithi. “Kupitia klabu hizi vijana wanataŕajiwa kuja kuonekana kama viongozi na mabalozi wa jamii zao katika kukabiliana na changamoto za watu, afya na mazingiŕa,” anasema Juma Dyegula, Mŕatibu wa Mŕadi wa Watu, Afya na Mazingiŕa katika TCMP.