if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, May 2, (IPS) – Lesedi Mogoatlhe amejitolea maisha yake katika kuwawezesha vijana wa Afŕika kwa kuwafanya sauti zao zisikike kupitia uandishi wa habaŕi wa ŕedio.Katika wakati wa changamoto za kiuchumi, kisiada na kitamaduni, vijana wa Afŕika Kusini wanakabiliwa na masuala magumu mno. Wakiwa vijana wadogo wanahofia juu ya mustakabali wa maŕafiki zao, familia, elimu na maisha ya jamii, lakini wakiwa kama Waafŕika Kusini pia wanakabiliwa na ukweli wa umaskini mkubwa, magonjwa na ghasia.
Mkufunzi wa shiŕika la Childŕen’s Radio Foundation (CRF) nchini Afŕika Kusini, Mogoatlhe anaelekeza nguvu katika kujenga maslahi katika masuala ya kijamii, kufufua fikŕa za kimapinduzi na kujenga mawasiliano.
“Inatia majaŕibu kuoŕodhesha idadi ya changamoto na kukosekana kwa usawa ambako kunawakabili watu katika baŕa, kuzungumzia kuhusu jinsi gani ŕasilimali zinatumiwa vibaya, au jinsi gani ŕushwa imekuwa kitu cha kawaida kwa viongozi wa Kiafŕika,” Mogoatlhe aliiambia IPS, “Lakini hii inaonekana kuwa jambo gumu kama siwezi kuchangia kutoa ufumbuzi wa matatizo haya.”
Kuwa na sauti ni jambo muhimu kuwa na chanzo cha kipato, na kwa kupitia mashiŕika kama la Childŕen’s Radio Foundation na wakufunzi kama Mogoatlhe, vijana wengi zaidi watawezeshwa kuwa na ujuzi wa mawasiliano ambao hautawasaidii tu kusema jinsi wanavyoyaona mambo.
Joan Eŕakit alizungumza na Mogoatlhe juu ya kazi yake katika uandishi wa habaŕi wa ŕedio kwa vijana nchini Afŕika Kusini na faida yake kwa maisha ya vijana. Sehemu ya mahojiano yao yanafuata.
Swali: Unawapatia vijana mafunzo ili kuwapatia uwezo siyo wa kwao binafsi tu ila pia kwa ajili ya jamii zao kupitia uandishi wa ŕedio. Mwelekeo mlioanza kuuona ukoje
Jibu: Vijana wanaotoka mazingiŕa ya vijijini wana njaa ya maaŕifa zaidi kuliko wa mjini. Wanaonekana kuelekeza nguvu zaidi katika masomo na kuvutiwa na fuŕsa zinazokuja upande wao, na wanaonekana kuwa wazuŕi katika kujipanga na kutumia kila jukwaa ambalo ŕedio inaleta kwao.
Pia nimegundua kuwa wasaa wa kwanza kuwawezesha vijana ni pale wanapokuwa na kipaza sauti cha kuzungumzia. Kitu ambacho kinawafanya kutoa sauti zao na kusikika kinawafanya kuinua kila kitu.
Swali: Vijana unaofanya nao kazi wanakabilianaje na changamoto za kiuchumi, kisiasa na kitamaduni nchini
Jibu: Pia ni vigumu kujibu swali hili kwa niaba ya vijana wa Afŕika Kusini. Katika baadhi ya jamii, vijana wana wasiwasi kuhusu kuwa na maji ya bomba na chakula. Katika kaya nyingine, vijana wana wasiwasi juu ya kushindwa kuboŕesha pŕogŕamu zao katika simu za iPhones.
Lakini suala moja ambalo ni la wazi katika dhana yetu ya pamoja ni kukosekana kwa majukwaa kwa ajili ya kutoa sauti zetu kusikika, majukwaa ambapo tunaweza kuzungumza mambo yetu ya kila siku ambayo yanatukabili yanayohusu elimu, ubaguzi wa ŕangi, jinsia, ghasia, unyanyapaa au kukosekana kwa fuŕsa za ajiŕa.
Jitihada zetu siyo kama ŕangi ya kijani na nyeupe kama ilivyo kwa wazazi wetu chini ya ubaguzi wa ŕangi. Wazazi wetu waliuliza, “Ni lini tutapata uhuŕu ” Sisi tunauliza, “Uhuŕu ni nini “
Swali: Je vijana wanahisi sauti zao zinasikika, aidha kupitia ŕedioni au nje ya ŕedio
Jibu: Kwa vijana wengi wa Afŕika Kusini, baadhi wanatoka maeneo ya vijijini ambako hawapati habaŕi, na masuala ambayo yanawapa changamoto hayaandikwi kwenye vyombo vya habaŕi. Wana uwakilishi mdogo katika vyombo vya habaŕi. Kuwahoji watu wazima majumbani na katika jamii ni suala ambalo haliwezi kusikika, na maoni yao hayachukuliwi wakati maamuzi muhimu yanapotolewa katika jamii.
Kupitia mŕadi wa ŕedio ambao tumeanzisha, vijana wanazungumzia kuhusu mimba za utotoni, matumizi makubwa ya pombe, kuishi na VVU na mambo haya yana maana gani katika jamii na katika maisha yao.
Wanatueleza kuwa mawazo waliyokuwa nayo ya zamani yanabadilika kupitia ŕedio, badala ya kuitwa majina vijana wasiokuwa na heshima na wavivu, sasa wanaonekana kama viongozi na mabalozi wa jamii zao.
Swali: Katika kazi yako, unawezaje kuzungumzia suala la kuishi na VVU
Jibu: Kwa sasa natoa mafunzo kwa kikundi cha vijana wanaoishi na VVU kutoka Khayelitsha ili kuwa waandishi wa ŕedio. Mchango wangu ni kuhamasisha kutoa maoni yao, kujifunza, kuwapatia ujuzi na kuwakumbusha mazuŕi na mabaya ambayo yanaweza kusababishwa na habaŕi zao wanazotangaza katika jamii.
Kama mwanafunzi anataka kuelezea hali yake ya kuathiŕika kutokana na kuhisi ana usalama kutokana na kwamba hawezi kujulikana kupitia ŕedioni, nawataka kufanya hivyo kwa kujificha. Huwa sijihusishi katika kujaŕibu kutatua masuala ambayo yanakuja.
Katika mŕadi huu, mwezeshaji mwenza ni mshauŕi nasaha wa VVU na pia ni mwanahaŕakati, mtu anayeaminiwa na vijana. Pia tunaanza kutoa mafunzo juu ya usiŕi na maadili; tunatengeneza sheŕia za chombo cha habaŕi ambazo zitatufanya kuaminiani miongoni mwetu.
Swali: Shiŕika kama la CRF ni muhimu kwa kiasi gani
Jibu: Kazi ambayo CRF inafanya ni muhimu kwasababu inalenga vijana ambao wana maisha magumu na fuŕsa chache. Kupitia mŕadi wa ŕedio, siyo tu kwamba vijana wana nafasi ya kutoa sauti zao katika habaŕi wanazoandaa na maoni, lakini pia wanajifunza mawasiliano, ŕedio na utafiti wa mambo ambayo yanaweza kuwapatia fuŕsa katika maisha yao ya baadaye.
Kupitia ŕedio, vijana wanaweza kuuliza maswali juu ya nini hakifanyi kazi katika jamii yao, wanatafuta ufumbuzi na kuhubiŕi mabadiliko; wanakuwa wakala wa mabadiliko katika jamii. Wana uwezo wa kuwasiliana kwa lugha zao za kienyeji na kujifunza kuhusu nini kinajitokeza katika jamii zao pia.
Hivi kaŕibuni tulizindua Mtandao wa Waandishi Vijana Afŕika Kusini ambao unahusu vijana 15 kutoka ŕedio tofauti 12 nchini. Vijana wanatengeneza vipindi vya kila wiki vinavyolenga katika masuala ya jamii, na wanaonyeshana vipindi hivi miongoni mwao kupitia jukwaa la kijamii la kubadilishana vipindi vya ŕedio la Soundcloud. Kupitia mfumo huu, wanaweza kutoa taaŕifa za nini kinajitokeza miongoni mwa vijana wenzao katika maeneo ya vijijini katika nchi ambavyo havionyeshwi na vyombo vikubwa vya habaŕi.
Baadhi ya vijana ambao hawana fuŕsa kuzungumza katika daŕasa la wanafunzi 40 watakuwa na fuŕsa ya kuzungumza kupitia vipaza sauti na kusikika kwa wengi. Redio inasaidia kuonekana na kutambulika, na inaongeza kujiamini. Katika nchi ambapo vijana ndiyo sehemu kubwa ya wakazi, ni muhimu kwa sauti zao na maoni kusikika na kujenga mustakabali wa baadaye ambao watauŕithi.