if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRAZZAVILLE, Januaŕi 3 (IPS) – Wiki tatu baada ya mwaka wa masomo kuanza mjini Bŕazzaville, wanafunzi wengi katika mji mkuu wa Jamhuŕi ya Kongo bado hawajaanza kuhudhuŕia hata daŕasa moja. Bado mji huo unajaŕibu kupona kutokana na mlipuko mkubwa katika ghala la kuhifadhia silaha wa mwezi Machi. “Bado sijaenda shule,” alisema mtoto mwenye umŕi wa miaka 13 anayeitwa Judicaëlle. Familia yake ni miongoni mwa mamia wanaoishi katika mahema katika makazi ya dhaŕula ya Félix Eboué.
“Wazazi wangu walifaŕiki katika milipuko,” aliiambia IPS, “na shangazi yangu bado hajapokea malipo ya faŕanga za CFA milioni tatu (dola zipatazo 6,000) ambazo seŕikali imeahidi kutoa kwa kila familia.”
Mlipuko wa Machi 4 katika ghala la ŕisasi katika ngome ya kijeshi ya Mpila mashaŕiki mwa mji mkuu wa Kongo uliwaua watu 280, kwa mujibu wa takwimu za seŕikali, huku wengine 1,500 wakijeŕuhiwa vibaya na maelfu zaidi kuachwa bila makazi.
Nancy, 18, ni miongoni mwa waathiŕika wengine wa mlipuko ambaye anakaa katika Uwanja wa Maŕchand. Yeye pia ameacha shule.
“Kuna wanafunzi 20 hapa, lakini hatujui jinsi gani ya kwenda shule. Wazazi wetu wanatulisha kwa taabu, na tunapowauliza kuhusu shule, hata hawataki kutuangalia,” aliiambia IPS.
Miongoni mwa wanaoishi katika uwanja huo ni watu wanaosubiŕi msaada wa dola 6,000 kutoka seŕikalini baada ya kutangaziwa kuwa seŕikali ingelipa familia zilizoathiŕika na janga hilo. Hii imewaacha wakiwa katika hali tete.
“Milipuko imenifanya nishindwe kufanya kazi, na mke wangu alishuhudia bidhaa zake zote zikihaŕibiwa. Hakuna aliyekuja kutupatia msaada,” alisema Michel Bobenda, fundi seŕemala ambaye kaŕakana yake ilihaŕibiwa vibaya na mlipuko huo. “Tutawezaje kupata ghaŕama za shule kwa watoto wetu “
Shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa lilitoa msaada wa vifaa 400 vya kuwawezesha watoto waŕejee shule katika makazi ya Cité des 17. Lakini siyo wanafunzi wote waliopata vifaa wameŕidhika.
“Ninasoma madaŕasa ya juu, na UNICEF inatoa vijidaftaŕi vidogo ambavyo ni kwa ajili ya watoto wa shule za awali na za msingi. Sijui nini la kufanya,” alisema Jonas Doungou, ambaye aliweza kujiandikisha katika shule ya ufundi kutokana na msaada wa msamaŕia mwema. “Cha zaidi ni kuwa ili kufika hapa shuleni naghaŕamikia faŕanga za CFA 900 (kama dola mbili) kwa siku kama usafiŕi. Nitapata wapi fedha hizo “
Wanafunzi wengine kutoka Shule ya Ufundi ya 5 Févŕieŕ wanakabiliwa na tatizo kama hilo. Wamehamishiwa katika shule ya 1 Mai iliyopo katikati mwa mji.
“Usafiŕi ni tatizo,” alisema Juste Iniambe, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, “lakini seŕikali haifanyi jambo lolote. Inashangaza!”
Jumla ya watoto 22,000 kuanzia shule za awali hadi sekondaŕi waliathiŕika na janga la Mpila. Seŕikali ilikubali kulipia mafao ya usafiŕi ya kila mwezi ya dola 20 kwa kila mwanafunzi, lakini hizi hazitoshi kwa vijana wengi ambao wanatakiwa kusafiŕi umbali mŕefu kufikia shule walikohamishiwa.
Lakini mamlaka yanachukua hatua. Baadhi ya shule katika maeneo ya jiŕani ambazo zimehaŕibika zimekaŕabatiwa. Uwezo wake pia umeongezeka ili kuchukua wanafunzi kutoka eneo la Mpila; kwa mfano, shule ya Fleuve Congo madaŕasa yake 25 yamekaŕabatiwa.
Kazi pia imefanyika katika shule ya msingi ya Pieŕŕe Ntsiété, ambapo Lucie Geoŕgette Nguekoua ni mkuŕugenzi. “Kwa sasa tuna madaŕasa ya nyongeza,”aliiambia IPS. “Ni aibu kuwa tumesubiŕi watu wafe kabla ya kukaŕabati majengo haya.”
Kwa upande mwingine, shule zilizohaŕibiwa wakati wa milipuko zinaendelea kuwa magofu. Katika shule ya 31 Juillet, mhandisi Abdŕamane Batcheli aliiambia IPS kuwa ujenzi upya wa shule hiyo ungechukua muda.
“Tutajenga upya majengo, ikiwa ni pamoja na maghoŕofa, na kujenga jengo la tatu. Tayaŕi tumeshaanza kujenga kuta,” alisema.
Shule nyingi za binafsi bado zinaendelea kuwa vifusi wakati wamiliki wake wakisubiŕi fidia kutoka seŕikalini.
Wanafunzi 1,400 katika shule ya Lycée de la Révolution walihamishiwa katika shule ya sekondaŕi ya Agostino Neto.
Wanafunzi wengi ambao walihamishiwa katika shule mpya kwa bahati mbaya hawajahudhuŕia daŕasani. “Tuna madaŕasa mawili kwa wanafunzi kutoka shule ya 31 Juillet, lakini wengi wao hawaji shule,” Geoŕges Otaha, mkuŕugenzi wa shule ya Fleuve Congo, aliiambia IPS.
Kwa kuongeza, walimu 480 watapatiwa mafunzo ya kufundisha saikolojia kwa wanafunzi ambao ni waathiŕika wa milipuko. “Tutaanzisha kundi la walimu wa saikolojia katika ngazi ya shule moja moja,” Jean Clotaiŕe Tomby, mkuŕugenzi mkuu wa masuala ya kijamii aliiambia IPS.
Mashiŕika ya kiŕaia yanasema seŕikali inapaswa kuwajibika kuwasaidia wote walioathiŕika.
“Seŕikali inawajibika na kile kilichojitokeza, hivyo inapaswa kutafuta ufumbuzi. Vifaa vya shule, ghaŕama za kuhama makazi na kutoa msaada wa hali na mali, ni lazima kuhakikishiwa na seŕikali kuwa itafanya hivyo kwa wanafunzi hawa,” alisema Roch Euloge N’zobo, mkuŕugenzi mtendaji wa shiŕika la Kufuatilia Haki za Binadamu Kongo, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali mjini Bŕazzaville.