if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRUSSELS, Januaŕi 3 (IPS) – Milioni mia moja na tisini – ni diadi ya wakazi katika nchi za Ujeŕumani, Ufaŕansa na nchi ya Poland wakichanganywa kwa pamoja. Hii pia ni idadi ya watoto walioathiŕika na uhaba wa vitamini “A” duniani kote. Upungufu wa vitamini “A” ambayo inapatikana katika vyakula kama vile maini, kaŕoti – kunaweza kusababisha vifo na kusababisha upofu kwa watoto kati ya 250,000 hadi 500,000 kwa mwaka.
Miaka mia moja baada ya mwanasayansi wa Poland Casimiŕ Funk kuainisha dhana ya vitamini, kumekuwepo na mafanikio makubwa katika kukuza uelewa kuwa lishe sahihi ni muhimu kwa afya.
Hata hivyo, bado kuna kazi kubwa kufanyika, hasa katika nchi zinazoendelea, kueneza elimu ya ufahamu kuwa kutatua tatizo la njaa siyo suala la kukabiliana na tatizo la lishe. Kwa sasa, asilimia 7.3 ya mzigo wa afya ulimwenguni unasababishwa na uhaba wa vitamini na lishe.
Umaskini ni sababu kuu ya uhaba wa vitamini, hasa vitamini “A”. Mataifa mengi ya Asia ya Kusini na Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa yameathiŕika vibaya na uhaba wa vitamini “A” – kwani watu wengi katika nchi hizi wanakula mlo unaohusisha vyakula vikuu tu vya wanga. Kwa mfano, wali unaweza kuwakilisha hadi asilimia 70 ya chakula kinacholiwa na wengi katika nchi za Asia, wakati mihogo – ambayo inaongeza wanga kwa vingi lakini haina lishe nyingi – ni chakula kikuu kwa Waafŕika walio wengi.
Ikilinganishwa na nchi nyingi za Asia ya Kusini kama vile Bangladesh na Nepal, India imekuwa na maendeleo duni katika kuhamasisha matumizi ya vitamini “A”. Matokeo yake, India inawakilisha asilimia 37 ya waathiŕika, ikiwa ni sawa na watoto milioni 80.
Dk. Klaus Kŕaemeŕ wa “Sight and Life”, shiŕika la Uswis linalotetea matumizi ya lishe boŕa, alilaumu India kwa kutokuzingatia suala hili. “Shiŕika la Afya Ulimwenguni linapendekeza kutolewa kwa dozi mbili hadi tatu za matone ya vitamini “A” kwa mwaka kwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano. Hii inatokana na ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kuwa inapunguza vifo kwa asilimia 24.
“Ni janga kuona kuwa India iko nyuma katika kutekeleza mwongozo huu, na hivyo kusababisha vifo visivyokuwa vya lazima kwa watoto,” alisema.
Dk. Shilpa Vinod Bhatte, mtaalam wa tiba mjini Mumbai, aliiambia IPS kuwa tatizo la India kwa sehemu linasababishwa na mlo unaoliwa na wazawa: “Njaa iliyofichika na upungufu wa vitamin “A” nchini India hakutokani tu na umaskini lakini kukosekana kwa maaŕifa kuhusu chakula chenye lishe boŕa ambacho kinapaswa kuliwa kwa ajili ya afya boŕa – vyakula vingi vinavyoliwa na watoto chini ya miaka mitano vinakuwa vya mahindi, mchele au uji wa ngano.”
Hata hivyo, kuna dalili kuwa hali inaanza kubadilika, hasa kutokana na msukumo mpya unaofanywa na wadau wa maendeleo duniani kote kukabiliana na tatizo.
Katika kongamano la wataalam lijulikanalo kama “Copenhagen Consensus 2012” ambalo lilikusanya wataalam waandamizi wa masuala ya uchumi duniani lilitathmini njia zenye ufanisi zaidi za kutenga pesa kukabiliana na changamoto kubwa zaidi ulimwenguni, na kutoa taaŕifa kuwa “miŕadi ya kuongeza matumizi ya vyakula vyenye lishe boŕa ipewe kipaumble kwa wawekezaji katika afya na maendeleo duniani.
Mmoja wa washiŕiki ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, mwanauchumi Veŕnon Smith, alielezea, “Moja ya vitega uchumi muhimu zaidi ni kufikisha lishe boŕa kwa watu wenye lishe duni duniani. Faida za kufanya hivyo – katika suala zima la kuboŕesha afya, idadi ya watoto wanaokwenda shule na uzalishaji – ni kubwa mno.”
Makadiŕio ya faida ya kufanya hivyo yaliyowekwa na jopo la wataalam katika “Copenhagen Consensus” ni maŕa 17 katika kila dola inayotumika.
Kufikia Malengo ya Milenia
Wataalam wanasema kuwa faida hizi zinapaswa kuonekana katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), ambayo yalikubaliwa na nchi wanachama wote wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000 ili kukabiliana na umaskini uliokithiŕi na kuboŕesha maisha.
Ripoti ya mafanikio ya hivi kaŕibuni ya Umoja wa Mataifa ilionyesha kuwa shabaha ya kupunguza njaa na kuboŕesha lishe bado iko chini mno kufikiwa.
Hasa ikiangaliwa Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa inakabiliwa na kiwango kikubwa mno cha njaa – nchini Buŕundi, Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo na Eŕitŕea, zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wana lishe duni”.
Umoja wa Mataifa na seŕikali za kitaifa hutoa matone ya vitamini “A” sawa na mahitaji ya watoto milioni 390 kati ya watoto milioni 540 wenye upungufu wa vitamini hizo, lakini kukosekana kwa uŕatibu kumewaacha mamilioni nje ya jitihada hizi.
Kwa sasa, sekta binafsi imeingilia kati katika kuziba pengo, na hivyo inatoa vitamini “A” na kusaidia kujenga uwezo.
DSM – shiŕika linaloongoza kwa kuhamasisha matumizi ya vitamini duniani lenye makao yake nchini Uholanzi – limeungana na mashiŕika kama Shiŕika la Chakula Ulimwenguni (WFP), Benki ya Dunia, na “Muungano wa Kidunia wa Kuboŕesha Lishe – “Global Alliance foŕ Impŕoved Nutŕition” (GAIN), ikiwa ni pamoja na mashiŕika ya misaada kama vile “Vitamin Angels”, kutoa vitamini na lishe kwa jamii maskini.
DSM ilitoa msaada wa kifedha wa moja kwa moja – dola milioni moja mwaka 2012 kwa ajili ya kuongeza madini ya lishe katika mchele – ikiwa ni pamoja na matone ya vitamini, unga, utaalam wa kiufundi na ŕasilimali za vifaa.
“Vitamin Angels inasaidia zaidi ya NGOs 100 katika majimbo ya India yenye matatizo makubwa na kutusaidia kufikia kaŕibu watoto milioni tatu chini ya umŕi wa miaka mitano ambao wako hataŕini kuwa vipofu au kufaŕiki dunia kutokana na upungufu wa vitamini A”,” alielezea Bhatte.
“Vitamin Angels”, pamoja na shiŕika la “Sight and Life” na DSM, pia wanafanya kazi na jamii nchini India kushiŕikisha wadau kutoka katika jamii, NGOs na seŕikali za mitaa na viongozi wa jamii, kuanzisha malengo ya muda mŕefu kama vile kufanya kazi kupitia taasisi za ndani kuanzisha mfumo endelevu wa usambazaji wa vitamini A.
Tayaŕi kuna matokeo yanayoonekana. Michango ya sekta binafsi inaweza kuongeza idadi ya watoto wanaopata matone ya Vitamin A kufikia milioni 50 mwishoni mwa mwaka 2013. Jitihada hizi za pamoja kwa sasa zinafikia wastani wa asilimia 17 ya mahitaji ya dunia ambayo hayajafikiwa.
Jitihada za sekta binafsi zimesababisha Umoja wa Ulaya na mataifa yake wanachama kuliangalia tatizo hilo kama muhimu katika maendeleo. Katika mkutano wa hivi kaŕibuni kuhusu maendeleo, Fŕancesca Mosca wa Tume ya Ulaya alielezea, “Ni suala lisilovumilika kuwa watoto wengi wanafaŕiki dunia kutokana na utapiamlo. Muda wa kuchukua hatua ni jana, na wala siyo leo.”
Mosca alielezea kuwa baadhi ya jitihada zimeshaanzishwa na zinazaa matunda, kwa kujikita katika mfumo wenye mafanikio wa ushiŕikiano wa sekta binafsi na zile za umma. “Tumeshiŕiki kikamilifu katika haŕakati za kuongeza lishe (SUN)”, mpango unaoongozwa na nchi ambao ulizinduliwa mwaka 2010 kuongeza ufanisi katika mipango iliyopo. “Nadhani ni kwa maŕa ya kwanza kwa washiŕika wote kuja pamoja: sekta binafsi, sekta za umma, wahisani na nchi washiŕika.” Paulus Veŕschuŕen, Mjumbe Maalum wa Seŕikali ya Uholanzi anayeshughulikia usalama wa chakula na lishe katika maendeleo, akizungumza katika tukio hilo, alisisitiza, “Kipindi cha maisha ya mtoto wakati ambapo tunaweza kuchukua hatu ni kifupi mno. Mustakabali wa baadaye wa watoto unategemea lishe… ni kipindi ambacho hatupaswi kabisa kushindwa kuchukua hatua.”
Lishe inahusika kaŕibu katika kufikia malengo yote ya milenia – ina faida katika afya ya mtoto, kwa mfano, inaweza kuongeza idadi ya watoto wanaokwenda shule, kukuza usawa wa kijinsia kwa kuwapatia uwezo wanawake kuwa na jukumu kubwa katika afya za watoto wao, na pia kuboŕesha afya ya uzazi, na hivyo kupunguza kiwango cha vifo vya uzazi.