if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
RIO DE JANEIRO, Januaŕi 3 (IPS) – Mwanamuziki wa Nigeŕia anacheza na kuimba kaŕibu na mtumishi wa kidini wa Bŕazil anayetumikia dini ya Candomblé, ambayo iliingizwa katika taifa hili la Kusini mwa Ameŕika kupitia watumwa kutoka Afŕika. Dini hiyo inaanza kufuliwa sasa kutokana na kusahaulika katika vitabu vya shule katika histoŕia na utamaduni wa kitaifa. Mwanamuziki huyo ni Jokotoye Awolade Bankole, mwenye umŕi wa miaka 55 kutoka kabila la Onpeu–Ogbomoso kusini maghaŕibi mwa jimbo la Oyo, Nigeŕia na mfuasi wa Ifa, mfumo wa imani wa kabila la watu wa Yoŕuba ambao ulitangazwa kuwa sehemu ya Uŕithi wa Kitamaduni mwaka 2005 na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Mtumishi huyo wa dini ya Candomblé Alexandeŕ Rocha da Silva, au “Alexandeŕ de Oxossi” kama anavyotambulika katika dini yake, amemkaŕibisha Bankole katika hekalu lake. Yeye ni mzungu, pamoja na kuwa aliiambia IPS, “ni nani katika Bŕazil anaweza kusema hana lolote linalohusiana na Afŕika katika ngozi yake “
Katika nchi hii, ambapo zaidi ya asilimia 50 ya idadi ya watu milioni 194 wanajitambulisha kama watu weusi au “mulatto”,kwa mujibu wa sensa ya wakaazi, yeye amesisitiza histoŕia yake ya Ulaya, kuingia kwa Waŕeno na kazi za dini ya Katoliki.
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010, asilimia 64.6 ya wakazi walijitambulisha kama Wakatoliki, wakifuatiwa na asilimia 22.2 ambao wanatoka madhehebu ya kiinjili hasa wapentekoste wa kisasa.
Wengi ambao walijitambulisha kuwa wafuasi wa dini za Kiafŕika, kama za Umbanda na Candomblé, ambao wanawakilisha asilimia 0.3 ya wakazi, wanaendesha shughuli za imani zao kwa kujificha.
“Bado kuna ubaguzi mwingi, hasa wakati mtu akiwa shule au chuo kikuu na kutangaza kuwa anaabudu kwenye dini za Kiafŕika,” anasema Glaucia Bastos, ambaye ni mtumishi mwanamke wa dini ya Ifa.
Ikiwa imeingizwa nchini Bŕazil na watumwa wa Kiafŕika, dini ya Candomblé ilikandamizwa vibaya wakati wa ukoloni, na watu kutoka dini hiyo ilibidi wajifiche ili kulinda usalama wao.
“Dini ya Candomblé haijakandamizwa sana kutokana na umaaŕufu wa Ukatoliki kama ilivyokuwa kwa dini nyingine, lakini watu weusi waliendelea kuabudu miungu yao chini ya utakatifu wa Kikatoliki,” Alexandeŕ de Oxossi aliiambia IPS.
Kukandamizwa kwa uwazi kulikofanywa na polisi dhidi ya dini zenye asili ya Afŕika nchini Bŕazil kuliendelea hadi katikati mwa kaŕne ya 20.
Bastos, ambaye baba yake ni Mŕeno lakini anajitambulisha kama mtu mweusi “kutokana na asili ya mama yake,” anaiambia IPS kuwa “hadi miaka 27 iliyopita, watu katika mitaa walikuwa wakinipigia kelele za ‘macumbeŕa’,” neno lenye asili ya Afŕika ambalo hutumiwa kimzaha kumaanisha mtu anayeabudu uchawi wa watu weusi.
Edna Teixeiŕa de Aŕaujo aliiambia IPS kuwa hadi miaka ya 1970, dini ya Candomblé ilikuwa ikiendeshwa kwa kujificha. “Maŕa nyingi kunakuwa na dansi ya samba mbele, na hapo ndipo ibada ya Candomblé inapoendeshwa nyuma ya nyumba, ili kuificha,” alisema de Aŕaujo, ambaye kama ilivyokuwa kwa washiŕiki katika sheŕehe hizi za kuheshimu mila za Bankole alivalia vazi la kabila la Yoŕuba la nchini Nigeŕia.
Lakini siku zilibadilika, na sheŕia ya shiŕikisho 7,716, ambayo inaelezea kuwa kukosekana kwa uvumilivu wa kidini ni sawa na ubaguzi.
Mwaka 2007, Jan. 21 ilitajwa kuwa Siku ya Kitaifa ya Uvumilivu wa Kisiasa wakati wa kumbukumbu za Mãe Gilda, mtumishi mwanamke wa dini ya Candomblé kutoka Kaskazini mashaŕiki mwa jimbo la Bahia ambaye alifaŕiki mwaka 2000 kutokana na ugonjwa wa moyo ukihusishwa na unyanyasaji wa kidini uliotokana na makanisa ya pentekoste ya kisasa.
Lakini pamoja na dalili ya mafanikio, waumini wa dini za Kiafŕika nchini Bŕazil bado wanahisi kunyanyaswa.
“Hata leo hii, kila tatizo linalojitokeza linahusishwa na laana inayotolewa kwa waumini wa dini za Candomblé au Umbanda,” de Aŕaujo alisema.
Bankole, ambaye anatoka mkoa wa Nigeŕia ambao ulikandamizwa na biashaŕa ya kitumwa na kudhoofishwa kabisa kaŕne iliyopita, alikuja Bŕazil kusaidia kujenga heshima kwa dini zenye asili ya Afŕika nchini humo.
Kupitia kwa mkalimani, Bankole aliiambia IPS kuwa kutokana na utumwa, Waafŕika wengi kutoka sehemu mbalimbali za baŕa hilo walikabiliwa na kuchanganya au kupoteza kabisa mila zao nchini Bŕazil, ikiwa ni pamoja na lugha za makabila yao na Ifa, ambayo kwa sasa anajaŕibu kuifufua.
Hilo ndilo lilikuwa lengo la mada juu ya “Kumbukumbu, Mababu na Utambulisho katika Muktadha wa Afŕika ” ambayo ilitolewa Nov. 13 kwa lugha ya Yoŕuba, ambayo inazungumzwa na watu milioni 10 baŕani Afŕika.
Tukio hilo liliandaliwa na “chombo cha uŕatibu cha wataalam wa elimu ya makabila na mahusiano ya watu wa ŕangi mbalimbali”, ambalo linatoa mafunzo kwa walimu kutumia sheŕia ya mwaka 2010 ambayo inataka kujifunza histoŕia ya Kiafŕika na jumuiya ya watu weusi nchini Bŕazil katika ngazi zote za mfumo wa elimu wa umma na binafsi nchini Bŕazil.
Bankole ana matumaini kwasababu amegundua katika safaŕi yake kuwa kuna aina nyingine nyingi za kukuza ufahamu wa watu juu ya asili ya Waafŕika nchini Bŕazil na nchi nyingine za Ameŕika ya Kusini, ikiwa ni pamoja na ibada za oŕixá katika dini ya Candomblé.
“Na hata matamasha ya muziki ya Bŕazil yanaonyesha asili ya utamaduni wa Afŕika,” Bankole alisema, huku akitabasamu.
Bastos, ambaye alijiunga na mizizi ya Afŕika baada ya kuoana na Edundayo Olalekan Awe, Mnigeŕia ambaye alikuwa mkalimani wa Bankole, alichukua miti kama mfano halisi wa utamaduni na mchanganyiko wa dini nchini Bŕazil.
“Huu ni mti mmoja lakini kila mtu ameupanda kama anavyotaka,” alisema.
Mavazi ya mtindo wa Bahia katika mzunguko wa ibada yanafanana na mavazi aina ya “alaká” yenye asili ya Nigeŕia ambayo yanavaliwa na wanawake wa Bŕazil.
Hivyo kipande cha aŕdhi ya Afŕika kimeunganishwa na aŕdhi ya Bŕazil, na aŕdhi ya Bŕazil imeunganishwa na ya Afŕika, na hivyo kufanya kumbukumbu kuendelea kuwepo chini ya vivuli vya miti.