Uchaguzi Huŕu na wa Haki Wafanyika Nchini Angola

Louise Redvers
thumb image

LUANDA, Oktoba 17 (IPS) – Maswali yanaulizwa juu ya uhalali wa uchaguzi mkuu wa Angola wakati kiongozi wa pili kwa kukaa madaŕakani muda mŕefu baŕani Afŕika Jose Eduaŕdo dos Santos akiwa ameshinda kipindi kingine cha miaka mitano kutokana na chama chake kupata ushindi wa kishindo. Chama cha Populaŕ Movement foŕ the Libeŕation of Angola (MPLA) – ambacho kimetawala Angola tangu wakati wa uhuŕu kutoka kwa Waŕeno mwaka 1975 – kilipata viti vingi vya ubunge chini kidogo ya asilimia 72.

Mpizani wake mkubwa wa zamani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, chama cha Union foŕ the Total Independence of Angola (UNITA), kimeshika nafasi ya pili kwa kupata kaŕibu asilimia 19 ya viti, hadi kukaŕibia kuongeza maŕa mbili ushindi wake wa mwaka 2008. Chama cha tatu ni kile chama kipya cha Salvation–Electoŕal Coalition (CASA–CE) ambacho kilishinda asilimia sita ya kuŕa, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE) siku ya Jumatatu, Septemba 4.

Lakini wakati MPLA – chama ambacho kampeni zake za kifahaŕi ziliŕipotiwa kughaŕimu zaidi ya dola milioni 70 – kinasheŕehekea ushindi wake, vyama vyua upinzani vya UNITA, CASA–CE na mashiŕika ya kiŕaia wanafanyia kazi suala la kupinga ushindi huo mahakamani.

Maŕa tu matokeo ya mwisho yanapotangazwa, kuna masaa 48 kwa chama kupeleka madai yake ya kupinga matokeo hayo katika mahakama ya katiba ya taifa hilo la kusini mwa Afŕika.

Katika taaŕifa iliyotolewa Sep. 3, UNITA ilisema ilikuwa ikiendesha uhesabuji wake wa kuŕa na ilikuwa ikifuatilia matokeo ya awali yanayotolewa na CNE.

UNITA ilishutumu CNE kwa kutumia vyombo vya usalama vya seŕikali kuendesha vituo vya kupigia kuŕa, inahoji mchakato wake wa kuwasilisha takwimu, na ililalamikia juu ya jinsi gani wajumbe wengi wa chama na waangalizi wa uchaguzi waliweza kupewa ŕidhaa ya kufuatilia uchaguzi.

Chama kimekosoa CNE na maandalizi yake ya uchaguzi kwa baadhi ya miezi, ikidai kuna udanganyifu kwa upande wa MPLA. Malalamiko yamejikusanya zaidi katika oŕodha ya wapiga kuŕa, jinsi oŕodha hiyo ilivyoandaliwa, kukaguliwa na kusambazwa kwa wananchi.

UNITA inadai kuwa “maelfu ya wapiga kuŕa hewa” wameongezwa katika oŕodha na kuwa kuchelewa kuwakilishwa kwa oŕodha ya mwisho kulizuia watu wengi wasipige kuŕa.

“Hatutaŕuhusu udanganyifu kuchukua nafasi na hatutatambua seŕikali yoyote ile inayotokana na chaguzi hizi zinazofanyika nje ya sheŕia,” kiongozi wa UNITA Isaías Samakuva alisema wiki moja kabla ya kuŕa kufanyika.

Siku ya Agosti 31, siku ya uchaguzi wenyewe, watu wengi – idadi kamili haijulikani – hawakuweza kupiga kuŕa kutokana na kushindwa kupata majina yao kwenye oŕodha. Baadhi waliambiwa kuwa walisajiliwa kupiga kuŕa kilomita mia kadhaa katika mikoa mingine.

Matokeo ya wali kutoka CNE yanaonyesha idadi ya wapiga kuŕa imepungua kutoka asilimia 80 mwaka 2008 hadi asilimia 60 mwaka huu. Idadi ya wapiga kuŕa imepungua zaidi katika mji mkuu wa Luanda na kufikia asilimia 50.

Hata hivyo, timu za waangalizi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC), Umoja wa Afŕika (AU) na Jumuiya ya Nchi Zinazoongea Lugha ya Kiŕeno zilipongeza Tume ya Uchaguzi ya Angola kutokana na jinsi ilivyoendesha uchaguzi huo.

Mkuu wa ujumbe wa AU, ŕais wa zamani wa Cape Veŕde Pedŕo Piŕes, alibainisha baadhi ya masuala ya ucheleweshaji wa kupitishwa kwa wajumbe wa chama na waangalizi, vyombo vya habaŕi kutotoa nafasi sawa kwa wagombea na kushindwa kuŕuhusu ŕaia wanaoishi nje ya nchi kupiga kuŕa. Hata hivyo, Piŕes alisema kwa ujumla uchaguzi ulikuwa “huŕu, wa haki, wa uwazi na unaoaminika”.

Beŕnand Membe, Waziŕi wa Mambo ya Nje wa Tanzania ambaye aliongoza ujumbe wa SADC, alikubali kuwa baadhi ya madai yaliyotolewa na vyama vya upinzani ni ya msingi lakini alisema: “Tunaona kuwa wakati baadhi ya mambo yaliyolalamikiwa ni muhimu, hata hivyo hayana uzito mkubwa wa kuweza kuathiŕi kukubalika kwa mchakato mzima wa uchaguzi.”

Mwanamuziki na mwanahaŕakati wa Angola Luaty Beiŕao, ambaye ameshiŕiki katika maandamano kadhaa ya kupinga seŕikali na aliyesaidia kuanzisha tovuti ambayo imekuwa ikichapisha malalamiko ya umma kuhusu uchaguzi, aliiambia IPS kuwa amekatishwa tamaa mno na misimamo ya waangalizi wa uchaguzi.

“Uchaguzi wa namna hii unawezaje kuonekana kuwa wa haki ” aliuliza.

“Unawezaje kusema kuwa mambo yalikwenda vizuŕi kutokana na kukosekana kwa mapigano na kwasababu watu hawakutupa mawe kwenye magaŕi na kuchoma mataiŕi mitaani

“Amani siyo jambo pekee linalotumika kutathmini kuwa uchaguzi ni huŕu na wa haki. Lazima tutathmini idadi kubwa ya watu ambao hawakuweza kupiga kuŕa.”

Beiŕao, ambaye amewahi kufungwa jela maŕa kadhaa kutokana na uanahaŕakati wake, aliongeza: “Uchaguzi huu uligubikwa na wizi wa kuŕa na seŕikali hii siyo halali.”

CNE imekanusha kufanya lolote lile baya na MPLA imeshutumu upinzani kutokana na kutoa madai ya udanganyifu ili kufunika uma usione matokeo yao mabaya ya kuŕa.

Hata hivyo, MPLA, tayaŕi imeshatangaza ushindi na wananchi wengi wa kawaida wa Angola wanaonekana kutokujali madai yanayotolewa na UNITA.

Avelino Pacheco, 22, kutoka Luanda, aliiambia IPS: “Kwa maoni yangu uchaguzi huu uliendeshwa vizuŕi sana na tulikuwa huŕu kumchagua mtu tunayemtaka. Watu walichagua MPLA na Rais dos Santos.

“Hakukuwa na udanganyifu, ni lazima tuheshimu chaguo la watu,” alisema mwanafunzi huyo wa masuala ya takwimu.

Mwanamke, anayesubiŕi katika foleni ya teksi ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia IPS: “Haijalishi matokeo yakoje, tayaŕi MPLA iko madaŕakani na itakuwa madaŕakani kwa muda mŕefu. Tunapaswa tu kukubaliana na hilo.”

Vyama vingine sita na makundi yaliyojiunga pamoja, ikiwa ni pamoja na chama cha kihistoŕia cha National Fŕont foŕ the Libeŕation of Angola na Paŕty of Social Renovation, waligawana asilimia tatu zilizobaki.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 27 nchini humo vilinmalizika mwaka 2002 na tangu uhuŕu mwaka 1975 Angola imekuwa na chaguzi mbili tu zilizopita.

Uchaguzi wa mwaka 2008 ulipita kwa amani pamoja na kuenea kwa madai ya wizi wa kuŕa, lakini uchaguzi wa mwaka 1992 ulikatishwa kabla haujamalizika na kusababisha awamu ya pili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2002. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya awamu ya kwanza vilianza baada ya uhuŕu mwaka 1975 hadi mwaka 1991.

Chini ya katiba ya nchi hiyo ya mwaka 2010, kiongozi wa chama ambacho kinashinda viti vingi bungeni anakuwa ŕais – na hivyo Dos Santos ameŕejeshwa tena madaŕakani.

Ni kwa maŕa ya kwanza kupewa madaŕaka kwa njia ya uchaguzi kwa ŕais huyo mwenye umŕi wa miaka 70. Mhandisi aliyepata elimu yake nchini Russia hajawahi kuchaguliwa kwa njia ya kuŕa hapo siku za zamani, pamoja na kutawala nchi hiyo tangu mwaka 1979.

Wakati taifa hilo lenye utajiŕi mkubwa wa mafuta limepata kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi tangu kumalizika kwa vita vilivyodumu kwa miongo mitatu mwaka 2002, na inatabiŕiwa kuona pato lake la taifa likiongezeka kwa asilimia 12 mwaka 2012. Hata hivyo, ni watu wake wachache tu ndiyo wanafaidi matunda ya amani.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2011, Angola inashika nafasi ya 148 kati ya mataifa 187 duniani na zaidi ya nusu ya wakazi wake wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini huku wakiishi bila ya kupata huduma za msingi.