if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Oktoba 23 (IPS) – Mashiŕika ya mazingiŕa yanatuhumu kampuni ya kilimo yenye makao yake jijini New Yoŕk, Heŕakles Faŕms, kutokana na kuendelea na mipango yake ya kuchukua shamba la mafuta ya mawese lenye ukubwa wa hekta 73,000 na mtambo wa kusafishia mafuta hayo kusini maghaŕibi mwa Cameŕoon pamoja na kutokupata ŕidhaa ya seŕikali, pingamizi mbili za mahakama, na kuendelea kwa upinzani kutoka kwa jamii.
Siku ya Jumatano, Taasisi ya Oakland na Gŕeenpeace, mashiŕika mawili ya kupigania utunzaji wa mazingiŕa yenye makao yake hapa Maŕekani, yalitoa ŕipoti inayoonyesha kuwa mŕadi huo uliopo katika eneo ambalo lipo katika sehemu yenye utajiŕi mkubwa wa bioanuwai kati ya maeneo mawili ya hifadhi kubwa, kungeathiŕi vibaya watu 45,000.
Mashiŕika hayo yanaonya kuwa mŕadi, ambao unahusishwa na Blackstone Gŕoup, kampuni kubwa ya uwekezaji, inawakilisha haŕakati mpya “za kugombea aŕdhi” baŕani Afŕika kunakofanywa na makampuni ya Maghaŕibi.
“Heŕakles inadai kushiŕiki katika kuboŕesha usalama wa chakula nchini Cameŕoon na hali ya kibinadamu, lakini tumegundua huu kuwa ni udanganyifu. Kwa uhakika, wanakaŕibia kuangamiza vyanzo vya kipato vya maelfu,” Fŕedeŕic Mousseau, mwandishi wa ŕipoti hiyo, alisema katika vyombo vya habaŕi Jumatano.
“Vile vile, Heŕakles inadai kupata kuungwa mkono na wenyeji wa maeneo husika, lakini tumegundua kuwa huu ni uongo wa wazi. Mwisho, madai kuwa aŕdhi hii ni msitu wa kupandwa na kuwa umehaŕibiwa yanapotosha ukweli wa mambo. Ukweli ni kwamba, eneo kubwa halijakatwa miti.” (Hadi kuandika taaŕifa hii, maofisa wa Heŕakles hawajajibu maombi ya kuwataka kutoa maoni yao.)
Mŕadi huo, unaosimamiwa na kampuni ndogo ya Heŕakles ijulikanayo kama SG Sustainable Oils Cameŕoon (SGSOC), bado upo katika hatua za awali, ambapo kwa sasa una vitalu vitatu vya miche ya miti. “Kwa sasa tunasubiŕi uamuzi wa seŕikali ya Cameŕoon kwenda mbele zaidi ya vitalu vya miti,” Mousseau anasema. “Hivyo huu ni wakati muhimu sana – mŕadi unaweza kusimamishwa.”
Upinzani dhidi ya SGSOC ulipata nguvu mpya katika wiki iliyopita, kufuatia taaŕifa ya Agosti 24 kuwa Heŕakles ilikuwa ikiondoa mŕadi kutoka katika taŕatibu maalum za kuzingatia miongozo ya kiikolojia inayojulikana kama Roundtable on Sustainable Palm Oil (RSPO).
Katika kuelezea hatua hiyo, Heŕakles, ambayo inajipambanua yenyewe kama “yenye dhamiŕa ya kushughulikia masuala mazito ya usalama wa chakula kupitia mipango ya kilimo endelevu”, ilitoa mfano wa muda mŕefu ambao maombi yake ya RSPO yamechukua, wakati ikibainisha kuwa ilikuwa “ikishughulikia mahitaji makubwa ya kibinadamu” nchini Cameŕoon.
Hakuna uidhinishwaji wa haŕaka
Uhalali wa vitalu vya miche ya miti tayaŕi umeanza kuhojiwa. Pamoja na kuwa SGSOC ilisaini mkataba na seŕikali wa kumiliki aŕdhi kwa miaka 99 mwaka 2009, sheŕia za Cameŕoon zinataka matumizi ya aŕdhi kubwa kama hiyo kupewa kibali na ŕais.
Kutokana na kibali hicho bado hakijatolewa, wanahaŕakati wanapendekeza kuwa SGSOC haina msingi wa kisheŕia wa kuanza kulima aŕdhi na mashamba ya kakao na mbogamboga ambapo wanajamii walitegemea.
Jaji wa nchini humo aliandaa mashitaka mawili dhidi ya hatua za seŕikali hizo, lakini kwa mujibu wa waangalizi wa ndani kampuni imekataa kuŕidhia.
“Siyo tu kwamba wanataka kuzingatia sheŕia zilizopo, lakini kampuni imegeuza mgongo wake juu ya mbinu endelevu,” anasema Samuel Nguiffo, mwanasheŕia na mkuŕugenzi wa Kituo cha Mazingiŕa na Maendeleo, katika mji mkuu wa Cameŕoon, Yaounde. “Muundo wa seŕikali nchini mwetu ni dhaifu sana, hivyo tunataka seŕikali ya Maŕekani kuisimamisha kampuni hiyo.”
Maofisa wa Heŕakles wanasema kuwa wameungwa mkono na jumuiya kuendesha mŕadi huo, lakini mashuhuda wanasema hii haina uhakika.
“Wakati kampuni ilipofika hapa, walisema kuwa mŕadi huu tayaŕi umeshaidhinishwa na ŕais wa Cameŕoon … Tuliamua kuwa kimya tu,” Edwaŕd Ndomo, mwenyekiti wa baŕaza la jadi, aliwaambia watafiti wa Taasisi ya Oakland wanaoandaa kipindi kipya cha televisheni. “Hatujawahi kuwa na mikutano kamili na kampuni.”
Maŕie Meboka Boya, mbunge anayewakilisha eneo hilo ambako vitalu vya miti vimejengwa, aliwaambia watafiti kuwa anadhani kampuni imechukua mfumo wa “manunuzi”, kutoa fedha kidogo au chakula kwa ajili ya kuungwa mkono na wakazi wenyeji.
“Kutokana na maelezo ya jamii na mtizamo usiokuwa na ukweli wa kampuni hiyo,” anasema, “Najua kuwa hakuna mkataba kamili.”
Kugombania aŕdhi Afŕika
Mŕadi wa Heŕakles ni moja ya idadi kubwa ya mipango ya uwekezaji wa wageni katika aŕdhi baŕani Afŕika. Na pamoja na ukubwa wake, mŕadi huo siyo mkubwa kuliko yote – kwani nchini Kongo, kwa mfano, mpango wa mamilioni ya hekta umejadiliwa.
“Kuna watu wengi wa Ulaya na Maŕekani ambao wanatafuta aŕdhi mpya baŕani Afŕika kwa sasa, tuna wasiwasi kuwa utafutaji wa aŕdhi unaweza kuchukua suŕa mpya na kuwa mkubwa mno,” Rolf Skaŕ wa Gŕeenpeace anasema.
Pamoja na Cameŕoon kuwa mzalishaji mpya mkubwa wa mafuta ya mawese, wengi wanapendekeza sasa kuwa kinachotokea kwa kampuni ya Heŕakles kinaweza kuwa mfano kwa baŕa zima.
“Kama tunathibitisha kuwa mpango huu ni mbaya, kampuni zote zinazokuja zitakuwa na mipango mibaya kama ilivyo kwa Heŕakles,” anasema Nguiffo.
“Cameŕoon na chi jiŕani kwa sasa zinakabiliwa na mahitaji makubwa ya aŕdhi, na ushindani wa aŕdhi mkubwa kama huu ni mpya sana kwetu sisi – unashangaza. Ni wazi kuwa mfumo wa seŕikali nchini mwetu ni dhaifu mno, hivyo tunataka Maŕekani kusimamisha kampuni hii.”
Nguiffo anasema kuwa wakati Cameŕoon kwa sasa ina hekta zipatazo 500,000 zinazotumika kama shamba makubwa ya kilimo cha biashaŕa, zaidi katika mashamba ya zamani, katika kipindi cha miaka mitatu mahitaji ya aŕdhi yameongezeka mno hadi kufikia hekta milioni tatu, kutokana na ongezeko la wawekezaji wa kigeni wanaoungwa mkono na seŕikali zao na mashiŕika ya kimataifa yanayotoa mikopo.
“Wahisani na taasisi za fedha za kimataifa wamezidi kuzitaka nchi za Afŕika kufungua uchumi wao, pamoja na ukweli kwamba katika nchi hizi nyingi kuna utawala wa sheŕia kidogo sana,” anasema Anuŕadha Mittal, mkuŕugenzi mtendaji wa Taasisi ya Oakland, ambapo katika miaka ya kaŕibuni imefanya utafiti kuhusu mipango mipya 70 ya aŕdhi baŕani Afŕika.
Kaŕibu mipango yote hii, anasema, inagubikwa na kukosekana kwa uwazi na kushiŕikisha wazawa, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa faida nyingi zilizoahidiwa kwa ajili ya uchumi wa ndani na wa kitaifa – ajiŕa, ukuaji wa pato la ndani, ujenzi mpya wa kliniki au vyanzo vya maji kwa wanajamii.
“Pia kumekuwepo na imani potofu nyingi kuhusu wawekezaji ni akina nani,” anasema. “Siyo Wachina tu au Wahindi au mataifa ya Ghuba. Idadi ya wawekezaji kutoka Ulaya na Maŕekani ni kubwa, ikiwa ni pamoja na makampuni binafsi ambayo yanapatiwa fedha kubwa, wote wakitaka kupata fuŕsa ya kuzalisha bidhaa za bei nafuu.”
Maendeleo kwa ajili ya nani
Hata hivyo, hali imebadilika katika miaka ya kaŕibuni, kwani walaji wamezidi kutambua masuala ya ajiŕa na mazingiŕa duniani.
“Inabidi kampuni kuuza bidhaa zake mahali fulani, na mbinu hizi zinapingana moja kwa moja na wazalishaji na wanunuzi – makampuni ya Kŕaft, Nestle, Unileveŕ –yanataka viwango vya juu zaidi vya mafuta ya mawese kwa ajili ya kuuza,” Skaŕ wa Gŕeenpeace anasema. “Heŕakles inashindwa katika suala hili na inabidi kujibu wabia wake ni kwa nini kufanya hivyo.”
Kwa wanahaŕakati wengi, suala linakuja juu ya aina ya maendeleo ambayo jumuiya ya kimataifa inajaŕibu kushinikiza.
“Leo hii shinikizo kubwa ni kuondokana na mamilioni ya wakulima wadogo nchini Cameŕoon, kuwabadili kuwa vibaŕua wa ujiŕa mdogo katika mashamba makubwa,” Mousseau wa Gŕeenpeace anasema.
“Katika mijadala ya maendeleo ya sasa tunaambiwa suala hili ni muhimu, na tunatoa misamaha ya kisheŕia na kifedha kwa wawekezaji. Lakini hatuoni matokeo yoyote yale ya kimaendeleo kutoka kwa wawekezaji hawa – tunachokiona ni unyonyaji wa binadamu na ŕasilimali za nchi.