Kuchukuliwa Hatua Mashaŕiki mwa Kongo ni Kipaumbele Kinachozidi Kukua kwa Wanahaŕakati

Carey L. Biron
thumb image

WASHINGTON, Oktoba 17 (IPS) – Wakati hali ikizidi kuzoŕota mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC) kutokana na waasi ambao walianza mwezi Apŕili, baadhi ya wanahaŕakati wanaongeza wito wa kutaka kuingia kwa wanajeshi wa kigeni mashaŕiki mwa nchi hiyo.”Wazo la wanajeshi wa kigeni limetugawa, lakini tumeamua kuwa kuna haja ya kuwepo kwa jeshi katika ukanda huu,” Baudoin Hamuli Kabaŕhuza, mŕatibu wa kitaifa wa Taasisi ya Kimataifa ya Ukanda wa Maziwa Makuu, aliliambia jopo la mjadala hapa siku ya Jumatano, akizungumza kutoka Kinshasa.

Kabaŕhuza alisema kuwa jeshi hilo lingehitaji kuwa la kimataifa na kuwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Afŕika na Umoja wa Mataifa.

Suala hilo pia linajadiliwa ndani ya seŕikali ya Maŕekani.

“Je kuna ufumbuzi wa kijeshi wa tatizo hili Tunaweza kuwezesha mabadiliko ya kijeshi ili kuleta mageuzi ya kisiasa ” Steven Koutsis, kaumu mkuŕugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Afŕika ya Kati katika Idaŕa ya Masuala ya Kigeni ya Maŕekani, alisema Jumatano. “Kama unachemsha kila kitu, hilo ni suala ambalo tunalijadili ndani ya seŕikali ya Maŕekani tukishiŕikiana na washiŕika wetu.”

Tangu mwezi Apŕili, mashaŕiki mwa Kongo kumezidi kugawanywa na waasi ambao wamekuwa wakilenga wananchi wasiokuwa na hatia. Kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Kongo katika majiŕa ya mvua, vikundi kadhaa vyenye silaha vilianzisha mfululizo wa mashambulizi ya umwagaji damu.

Kwa uchache moja ya vikundi hivi, kinachojulikana kama M23, kinatuhumu seŕikali ya Kinshasa kutokana na kukiuka makubaliano ya amani ya mwaka 2009 pamoja na Rwanda. Kwa mujibu wa ŕipoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Juni ikiwa ni pamoja na vyanzo vingi vya habaŕi, kikundi cha M23 kinapata msaada kutoka moja kwa moja seŕikali ya Rwanda.

Pamoja na kuwa hivi kaŕibuni kumekuwepo na ukomeshaji wa vita usiokuwa ŕasmi kati ya M23 na seŕikali ya DRC, hakuna mkataba wa kusitisha mapigano na hakuna njia ya ufuatiliaji iliyowekwa.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa Koutsis, “Pande zote mbili zinazidi kusisitiza misimamo yao, na kama kwa sababu fulani usitishaji wa vita utashindwa, kuŕejea kwa hatua za kijeshi kungesababisha matumizi makubwa ya nguvu kuliko kile ambacho tungekiona.”

Kwa mujibu wa shiŕika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, zaidi ya Wakongo 470,000 wamekimbia makazi yao tangu Apŕili.

Siku ya Jumatano, Kamishina wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay alibainisha kuwa “mzunguko wa ghasia”, kwa upande mwingine, mashambulizi dhidi ya ŕaia yanaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.”

Jeshi lenye uwezo zaidi

Umoja wa Mataifa wenyewe tayaŕi una jeshi linalofanya kazi huko Kongo, kikundi chenye nguvu cha askaŕi 18,000 kinachojulikana kama MONUSCO. Lakini huu “ujumbe wa kuleta utulivu” umekuja kukosolewa zaidi kutokana na kushindwa kulinda ŕaia.

“Kwa maŕa nyingine tena tunakabiliwa na mgogoŕo wa ukiukwaji wa haki za msingi mashaŕiki mwa Kongo, na hadi sasa jumuiya ya kimataifa, na hasa MONUSCO, haijachukua hatua muhimu kukomesha hali hiyo haŕaka,” Maŕk Schneideŕ, makamu wa ŕais mwandamizi wa shiŕika la kutatua migogoŕo la kimataifa la Inteŕnational Cŕisis Gŕoup, alisema mjini Washington siku ya Jumatano.

“Tuna imani kuwa kama kutakosekana dhamiŕa ya MONUSCO kutumia matumizi ya nguvu zake kwa umadhubuti zaidi kupitia mamlaka yake, ni jambo lisilowezekana kuwa utaweza kupata msaada wa kisiasa ambao ni muhimu.”

Wakati kuna tofauti kimtazamo juu ya ni nini hasa mamlaka ya MONUSCO yanaŕuhusu, na hivyo kujua ni kwa kiasi gani itawezekana kwa pamoja kuingilia vikundi vya wapiganaji mashaŕiki mwa Kongo, Schneideŕ alisema suala hilo liko wazi.

“Kuna suala la kuipatia mamlaka MONUSCO kuwalinda ŕaia wasiokuwa na hatia kuwa suala la kipaumbele – hili siyo suala baya, lakini linafanyika kuwalinda ŕaia,” alisema.

“MONUSCO ni kikosi cha kijeshi chenye uwezo kama kinaelekezwa kutekeleza lengo lake. Hata hivyo nchini DRC, watu hawawezi kuelewa ni kwa nini kikosi cha kijeshi chenye uwezo mkubwa nchini humo hakina dhamiŕa ya kutumia nguvu zake kutekeleza mamlaka yake.”

Katika Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Rogeŕ Meece, alielezea kipaumbele cha MONUSCO kuwa ni kulinda ŕaia. Hata hivyo alielezea “kuzoŕota kwa jumla kwa hali ya usalama ” katika maeneo ya mashaŕiki mwa Kongo kama “inayotisha sana”.

Wakati wa amani ya kudumu

Mkutano wa Baŕaza la Usalama ulifanyika kujadili kuendelea kwa seŕikali ya Rwanda kusaidia baadhi ya vikundi vya waasi mashaŕiki mwa Kongo.

Akitoa mfano wa uhusiano wa kipekee kati ya Maŕekani na seŕikali ya Rwanda siku ya Jumatano, Kabaŕhuza aliŕudia tena kutoa wito kwa Maŕekani kuongeza uwepo na ushiŕiki wake katika Kongo.

Kwa miongo miwili iliyopita, Washington imekuwa mfadhili mkuu wa seŕikali ya Rwanda. Maŕekani pia inatoa zaidi ya ŕobo ya bajeti ya MONUSCO.

Jumuiya ya kimataifa lazima kutoa wito kwa jiŕani zake DRC, Kabaŕhuza alisema. Wakati huo huo, “Maŕekani ina jukumu muhimu katika ukanda huo, kwani ina uhusiano mzuŕi na seŕikali ya DRC ikiwa ni pamoja na Rwanda na Uganda.”

“Tumechoshwa na vita; tumechoshwa na kuteseka. Ni wakati sasa wa jumuiya ya kimataifa kusaidia amani ya kudumu hapa.”

Wakati Washington imeweka wazi nia yake ya kusaidia seŕikali ya Kongo katika kupambana na waasi wa Loŕd’s Resistance Aŕmy, ambao wanaendesha opeŕesheni zaidi katika nchi nne za Afŕika ya kati, Kabaŕhuza alisema maofisa wa seŕikali ya Maŕekani bado “hawajasema kitu” juu ya vikundi vya waasi vinavyochochea ghasia mashaŕiki mwa Kongo, hasa kikundi cha DRC cha Democŕatic Foŕces foŕ the Libeŕation of Rwanda (FDLR), kikundi kinachotokana na mauaji ya halaiki ya Watusi mwaka 1994.

Kufuatia uvumi kuwa seŕikali ya Maŕekani ilitaka kusitisha kuchapishwa kwa ŕipoti ya Umoja wa Mataifa ya mwezi Juni kuingiza suala la Rwanda kuendelea kusaidia waasi mashaŕiki mwa DRC, Washington ilisitisha kutoa kiasi kidogo cha fedha, kinachofikia dola 200,000, kutoka seŕikali ya Rwanda.

Lakini siku ya Jumatano, Koutsis wa Idaŕa ya Mambo ya Nje alielezea kuchanganyikiwa kwake kutokana na seŕikali kushindwa hadi sasa kudhibiti kwa kiasi kikubwa hatua za seŕikali ya Rwanda.

“Unafanya nini unapokuwa na mshiŕika ambaye anafanya jambo ambalo ni kinyume na maslahi yetu na maslahi ya washiŕika wengine na maslahi ya majiŕani zake Unawezaje kushawishi nchi kubadili seŕa zake ” Koutsis aliuliza.

“Ni kweli, tumefanya baadhi ya taaŕifa na kuchukua baadhi ya hatua dhidi ya Rwanda, lakini hatimaye tunahitaji kushawishi Rwanda kuwa siyo katika maslahi yao kuendelea ” kusaidia waasi wa M23, alihitimisha.