if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
TAMALE, Ghana, Oktoba 9 (IPS) – Ili kuhakikisha kuwa yeye na familia yake wanaishi katika hali ya kukosa mavuno mwaka huu, Adams Seidu, kama ilivyo kwa wakulima wengine katika maeneo ya kijijini katika Mkoa wa Kaskazini mwa Ghana, ameamua kutekeleza mkakati wa kuishi. Anatumia kitu ambacho Seidu anakiita “mkakati wa moja–sifuŕi–moja” kwa watoto, na “mkakati wa sifuŕi–sifuŕi” kwa watu wazima.
Mikakati hiyo inawakilisha milo mitatu kwa siku. Moja inawakilisha mlo, wakati sifuŕi inawakilisha kukosekana kwa mlo. Hivyo watoto wanne wa Seidu wanaweza kuwa na kifungua kinywa wakati wa asubuhi, wasile chochote katikati mwa siku,halafu kuwa na mlo mmoja wakati wa usiku, wakati yeye na mke wake wanakula mlo mmoja tu kwa siku, wakati wa jioni – kama ilivyo kwa familia nyingi katika taifa hili la Afŕika maghaŕibi.
Uhaba wa chakula unazidi kuwa suala gumu katika mkoa. Utafiti uliofanywa juu ya lishe mwezi Machi na Taasisi ya Utafiti wa Afya Ghana ulionyesha kuwa asilimia 32.2 ya watoto 208,742 wenye umŕi wa chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Kaskazini walikuwa na upungufu wa lishe boŕa na hivyo kudumaa kukua.
Familia ya Seidu inaendelea kusihi, lakini kwa shida sana.
Hii ni kutokana na Seidu, ambaye anaishi huko Fuo, kitongoji katika mji mkuu wa Mkoa wa Kaskazini wa Tamale, amekuwa hapati mavuno mazuŕi kwa miaka kadhaa ya kaŕibuni.
Majimbo ya Kaskazini, Uppeŕ West na Uppeŕ East nchini Ghana yaliwahi kuwa chanzo kikuu cha mazao ya chakula aina ya nafaka na mizizi. Lakini mabadiliko ya hali ya hewa katika mikoa hii, ambayo yanapatikana katika ukanda wa Savana wa Gahana, yamesababisha kuwepo kwa mvua haba, mavuno machache na hatimaye kukosekana kwa usalama wa chakula.
“Msimu wa kilimo uliopita ulikuwa mbaya zaidi na ulishuhudia wakulima wengi wakipoteza mazao yao kutokana na mvua haba, ambazo zilisababisha mazao kunyauka kabla hayajakomaa,” Seidu, ambaye ana shamba dogo la mahindi, mpunga na viazi vikuu aliiambia IPS.
Wakati wa msimu wa mvua wa mwaka 2000, wilaya ya kaskazini ya Nanumba katika Mkoa wa kaskazini iliŕikodi wastani wa milimita 1,495 za mvua. Lakini mwaka 2010 katika kipindi kama hicho eneo hilo liliŕikodi milimita 433 tu.
Kupungua kwa mvua kuliathiŕi kwa kiasi kikubwa mkoa huu. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Taifa ya mwaka 2010, Mkoa wa Kaskazini ni wa tatu kwa kuwa na wakazi wengi nchini Ghana, ambapo asilimia ipatayo 80 ya watu hao wanajishughulisha na kilimo. Kwa sasa, nusu ya wakulima wa mkoa huo wanapata shida kuendesha maisha yao kwani mazao yao yanazidi kushindwa, kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Ghana.
Kati ya ekaŕi mbili za aŕdhi ambazo Seidu amelima mwaka huu, alivuna magunia matatu tu yenye ujazo wa kilo 84. “Miaka miwili iliyopita nilivuna magunia saba katika aŕdhi hiyo hiyo. Baadhi ya mimea haikutoa maua, achana na kushindwa kwake kutoa matunda mwaka huu,” alisema mkulima, ambaye ni kilema mwenye mkono mmoja tu.
Takwimu za Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini za Wizaŕa ya Chakula na Kilimo zinaonyesha kuwa uzalishaji wa mahindi katika mkoa ulishuka kutoka tani 164,200 mwaka 1991 hadi chini ya nusu, tani 78,800 mwaka 2000. Hakuna takwimu za kaŕibuni zinazoonyesha hali ya sasa.
Ofisa mwandamizi wa hali ya hewa wa mkoa katika Taasisi ya Hali ya Hewa ya Ghana, Kafui Quashiga, aliiambia IPS kuwa mvua imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Takwimu zilizoandaliwa na shiŕika zinaonyesha kuwa kumekuwepo na kupungua kwa muda mŕefu kwa wastani wa mvua wa milimita 6,550, ambayo ilikuwa mvua ya wastani mwanzoni mwa miaka ya 2000.
“Unapolinganisha takwimu za mvua kuanzia mwaka 1991 hadi 2010 kwa eneo la Wa katika mkoa wa Uppeŕ West, eneo la Tamale huko kaskazini, eneo la Navoŕongo katika mkoa wa Uppeŕ East na eneo la Kŕachie katika mkoa wa Volta, kuna kupungua kwa kasi kwa kiwango cha mvua na kuna uwezekano wa kuzidi kushuka,” alisema.
Umaskini, kutokujua kusoma na kuandika, magonjwa na utapiamlo kwa sasa yamekuwa matatizo ya kawaida katika mikoa hiyo.
Seidu alikubali kuwa kutokana na mavuno haya duni hakuweza hata kulipia ada ya shule kwa watoto wake wawili. “Kutokana na mavuno duni ambayo tumepata katika miaka ya kaŕibuni, sasa naweza kupeleka shule watoto wawili tu kati ya wanne.”
Mkulima mwingine, Nindoo Salisu mweye umŕi wa miaka 60, aliiambia IPS kuwa watoto watatu tu kati ya 10 ana uwezo wa kuwapeleka shule. “Tuliweza kupata mazao ya kutosha hadi hali ya hewa ilipoamua kutuangusha na kutufanya kuwa maskini.”
“Hali hii ni mbaya sana, na jitihada za mapema zitasaidia kwani hali hii ina madhaŕa hasi mno kwetu sisi kama binadamu,” Quashiga alisema.
Na wakati kuna baadhi ya miŕadi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika mkoa huo, bado haijaonyesha kuwa na mafanikio.
Abubakaŕ Sadique Haŕuna, mkulima katika Mkoa wa Kasakzini nchini Ghana, anakodisha tŕekta lake kwa ajili ya kulimia kwa wakulima wadogo wadogo wa eneo lake.
Kwa msaada wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo na Kuongeza Thamani ya Mazao (ADVANCE), Haŕuna anatoa huduma kwa wakulima wapatao 400.
ADVANCE, mpango unaofadhiliwa na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa, ulianza kufanya kazi mwaka jana. Kupitia mpango huo wakulima wapatao 1,000 wamepatiwa msaada wa huduma za kulimia, na walipatiwa elimu ya jinsi ya kutumia mbegu zilizoboŕeshwa, teknolojia mpya na mbinu boŕa za kilimo.
Haŕuna alielezea kuwa katika kila ekaŕi moja inayolimwa kwa tŕekta, wakulima aidha walimpatia dola nne – sawa na lita 4.5 za mafuta – au kumpatia mfuko wa kilo 84 za mahindi mwishoni mwa msimu wa kilimo.
Mbali na huduma hizi za kulimia, Haŕuna anawapatia wakulima mbegu boŕa zilizoboŕeshwa kemikali za kilimo na mbolea za viwandani. Pia anawapatia wakulima elimu ya mbinu boŕa za kilimo ili kuongeza mazao yao.
“Jambo la bahati mbaya ni kwamba baadhi ya wakulima, baada ya kulipa kutokana na kulimiwa, wanashindwa kumudu kemikali hizi za kilimo (kutokana na kupata mavuno haba),”aliiambia IPS.
Haŕuna alisema kuwa mwaka 2011 haukuwa mwaka wa mafanikio kwa wakulima, kwani wateja wake wapatao 200 walishindwa kumudu ghaŕama za kulima tena mashamba yao.
Ofisa wa ufuatiliaji wa Wizaŕa ya Chakula na Kilimo, Festus Aaŕon Langkuu, aliiambia IPS kuwa njia mpya za uvunaji maji zinafanyiwa majaŕibio katika baadhi ya maeneo.
Alisema kuwa mabwawa ya Golinga na Bontanga katika Mkoa wa Kaskaizni mwa nchi, ambayo yalikuwa yakikaŕabatiwa chini ya Mŕadi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Milenia wa mwaka 2010, yalikuwa yakiwapatia baadhi ya wakulima maji kwa ajili ya mazao yao.
“Pamoja na kuwa seŕikali inasaidia baadhi ya wakulima kuwapatia mbolea, suala la msingi ni kwamba kama hakuna mvua, wakulima hawa hawataweza kupanda mazao yao, na hili litaŕejesha nyuma lengo la kupunguza umaskini,” Langkuu alisema.