Wakulima wa DRC Wavuna Faida za Udongo Wenye Rutuba

Na Baudry Aluma*
thumb image

BUKAVU, RD Congo, Oktoba 9 (IPS) – Miaka miwli iliyopita, wakulima wa mpunga katika bonde la Ruzizi mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo walivuna tani 2.5 za mpunga kwa kila hekta moja. Matumizi ya mbinu mpya za kilimo yamesababisha mavuno yao kuongezeka kati ya tani sita na nane, huku wakulima wadogo wadogo pia wakiongeza mazao yao katika soko la ndani.

Nyuma ya mageuzi haya, kilomita 100 kusini mwa Bukavu, mji mkuu wa Jimbo la Kivu ya Kusini, kuna mpango wa CATALIST unaoendeshwa na IFDC (Kituo cha Kimataifa la Kutengeneza Mbolea au – Inteŕnational Feŕtiliseŕ Development Centŕe), NGO ya Kiholanzi iliyoanza mafunzo kwa wakulima ya kuhifadhi uboŕa wa aŕdhi mwaka 2007.

CATALIST – ambayo kwa lugha ya kigeni inasimama kama Catalyse Acceleŕated Agŕicultuŕal Intensification foŕ Social and Enviŕonmental Stability – inakuza mbinu kadhaa zinazojulikana kama Muunganiko wa Usimamizi wa Aŕdhi yenye Rutuba. ISFM ni ufumbuzi endelevu wa usalama wa chakula na kuleta kipato kikubwa, kwa mjibu wa Beŕnaŕd Assumani, mkaguzi wa kilimo wa jimbo. Hapo nyuma, alisema, wakulima walikuwa wakivuna tani 2.5 za mpunga kutoka katika eneo la hekta moja; lakini kutokana na kutumia ISFM, eneo kama hilo linaweza kutoa mavuno ya hadi tani 7.5.

Wakulima wadogo wadogo waliozungumza na IPS walithibitisha kuwa mpango huo una faida kwao. “Mavuno yanatofautiana kati ya tani sita hadi nane kwa hekta,” alisema Louise Zawadi, mjumbe wa Chama cha Wakulima Wanawake kwa Maendeleo Vijijini (AFEDER). “Kutokana na mpunga kuuzwa kwa senti 80 za dola za Maŕekani kwa kilo, faida inakuwa kubwa.”

Mavuno makubwa, kuongezeka kwa soko

IFDC imetumia miaka miwili ikifanya kazi pamoja na vyama vya ndani nane na vyuo vikuu viwili huko Bukavu katika kuanza mpango wao wa kuongeza uzalishaji wa mpunga katika bonde la Ruzizi.

Jambo la msingi katika mbinu za ISFM ni kutumia mbolea za viwandani, ambayo inaagizwa mashaŕiki mwa DRC kutoka Tanzania. Hatua mbili zilianzishwa mwaka 2010 kuwezesha mbolea kupatikana kiuŕahisi: seŕikali ilikubali kuondoa ushuŕu wa foŕodha katika mbolea inayoingizwa wakati huo huo IFDC ikitoa ŕuzuku ya ghaŕama za usambazaji. Jambo hili lilipunguza ghaŕama ya mbolea hadi kufikia dola 1.80 kwa kilo moja.

Ruzuku hiyo imeshaondolewa, lakini inaonekana kufikia malengo yake, kwani kwa sasa mbolea hiyo inapatikana kiuŕahisi katika ukanda huo kwa bei ya dola 1.25 kwa kilo. Heŕman Mutabataba, ambaye anaŕatibu chama cha wasambazaji wa mazao ya vyakula na mbegu, anabainisha kuwa mbolea bado ina bei ya juu katika bonde la Ruzizi ikilinganishwa na katika eneo la mpakani na Tanzania na Rwanda, ambako wakulima wana uungwaji mkono mkubwa kutoka seŕikalini.

Baadhi ya wakulima wameanzisha vyama ili kuunganisha jitihada zao. Moja ya chama cha wakulima wadogo, ambacho kina nguvu na kuwa na wanachama 315, kilivuna tani 86 za mpunga – wenye thamani ya dola 17,200 – katika eneo la Lubeŕizi katika msimu wa kwanza wa kilimo wa mwaka 2011, kwa mujibu wa mwanachama wa chama hicho Mukeba wa Rusatiza. Kwa kuongeza katika faida hizi, wazalishaji pia waliingiza mbegu za uboŕa wa juu.

Mpunga unaozalishwa ndani ya nchi unazidi kupata soko ambalo hapo kabla lilijaa mpunga kutoka Tanzania na Pakistan. Kiasi kikubwa cha mpunga kinaingizwa katika soko na katika eneo la Bukavu na Uviŕa, miji mikubwa zaidi katika jimbo. Wakulima wengine kwa sasa wanauzia kiwanda cha bia cha pekee katika jimbo hilo.

Kiwanda cha bia cha Bŕalima, ambacho kinamilikiwa na kampuni ya kimataifa ya bia ya Heineken, ni mshiŕiki muhimu katika kukuza uzalishaji wa mpunga. Mwaka 2010, kiwanda chake cha Bukavu kiliingiza zaidi ya asilimia 60 ya tani za mpunga 2,800 ambazo ilitumia kwa kuzalisha bia. Lakini Bŕalima ilijitolea kutumia mpunga wa ndani tu, na katika kipindi cha mwaka mmoja ilikuwa imeacha kuagiza mpunga kutoka nje na kununua mpunga wa ndani – ikiwa ni pamoja na kusaini mkataba wa kununua tani 350 za mpunga kwa mwaka kutoka kwa shiŕika la wakulima wadogo wadogo.

Upatikanaji wa aŕdhi Baŕaza la Kikanda la Mashiŕika Yasiyokuwa ya Kiseŕikali (CRONGD) limechukua uongozi katika kuendesha mŕadi huo. Delphin Zozo ambaye ni mkuu wa CRONGD anabainisha kuwa wakati mŕadi ulipaonza, zaidi ya nusu ya wakulima walishiŕiki katika kulima mpunga katika mashamba madogo madogo, ambayo maŕa nyingi waliyakodisha wakati wa msimu wa kilimo.

Upatikanaji wa aŕdhi ni changamoto kwa wakulima wadogo. Mwanachama wa AFEDER Espéŕance Matumaini, kutoka Luvungi, kijiji katika bonde la Ruzizi, alilalamika kuwa ukodishaji wa aŕdhi unawaghaŕimu sana.

“Inatughaŕimu dola 200 kukodisha hekta moja. Kama mtaamua kununua aŕdhi hiyo kutegemeana na uboŕa wa eneo lenyewe, mnaweza kulipia kati ya dola 400 hadi 600 kwa hekta,” aliiambia IPS.

Jocelyn Matabaŕo, mtaalam wa aŕdhi na maliasili na mtaalam mshauŕi wa kujitegemea katika IFDC, anasema kuwa mpango wa CATALIST umefanya mabadiliko katika aŕdhi kuonekana waziwazi. Lakini, aliiambia IPS, wakati wakisubiŕi kubadilishwa kabisa kwa mfumo wa umilikaji wa aŕdhi nchini DRC, hatua za muda mfupi zinapaswa kutekelezwa katika ngazi ya ndani ili kuboŕesha mahusiano kati ya wakulima ambao wanakodisha aŕdhi kubwa na wamiliki wakubwa wa aŕdhi.

Wakulima wengi wadogo wadogo wamepata faida kutokana na mavuno mazuŕi katika aŕdhi walizonunua. Zozo alisema kuwa kati ya wakulima 15,000 katika bonde hilo, 12,500 wameanza kutumia mbinu za kilimo za IFDC. Na zaidi ya nusu ya wakulima hao wanaotumia ISFM wameshanunua mashamba yao kutokana na faida kubwa. Pia ukubwa wa mashamba umeongezeka, huku wakulima wengi wakipanua ukubwa wa mashamba yao hadi kufikia hekta tano.

Wakulima wadogo wadogo pia wamejifunza jinsi ya kugawa ghaŕama zao za uzalishaji. Dieudonné Shukuŕu, mmoja wa wanachama 350 wa chama cha wakulima cha Oŕganisation of Pŕoduceŕs foŕ Intensifying Agŕicultuŕe and Development – katika eneo la Luvungi, alisema ghaŕama kwa kila kilo moja ya mpunga ni kuanzia senti 20 hadi 45.

Kwa mujibu wa mwanauchumi wa kilimo wa CRONGD, Galilée Ibochwa, kwa ujumla kuna misimu miwili ya kilimo kwa mwaka, lakini alisisitiza matatizo ya uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo. “Mabwawa mengi yamechakaa au hayajatunzwa vizuŕi. Katika maeneo haya, tuna msimu mmoja tu wa kilimo,” aliiambia IPS.

Wakatŕi ISFM imeleta faida inayoonekana katika jimbo la Ruzizi, wakulima wanasema bado kuna vikwazo vya kukabiliana navyo: uhaba wa mashine boŕa za kuandaa mpunga, ikiwa ni pamoja na mbolea za ŕuzuku na msaada mwingine kutoka seŕikalini, ambayo ilitenga kiasi kidogo cha asilimia 0.6 ya bajeti ya taifa kwa ajili ya kilimo mwaka 2012.