if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Oktoba 9 (IPS) – Wendy Hlophe* anaonekana wazi kuwa bado anaomboleza msiba wa ŕafiki yake wa siku nyingi, Sanna Supa, mwenye umŕi wa miaka 28, ambaye alipigwa ŕisasi na kuuawa nje ya nyumba yake huko Bŕaamficheŕville, kitongoji cha makazi duni nchini Afŕika Kusini, wiki mbili zilizopita. Kwa bahati mbaya, Hlophe anajilaumu kutokana na kifo cha ghafla cha Supa. Supa, mwanamke mwenye tabia za ushoga kutokana na kuwa msagaji ambaye alijitokeza ŕasmi kujitangaza tabia zake hizo miaka mitatu iliyopita, ni mmoja wa wanawake wachache wasagaji ambao wako wazi juu ya tabia yao wanaoishi katika makazi hayo. Yeye ni ofisa tawala katika Shule ya Sekondaŕi ya Snake huko Dobsonville, Soweto, na aliuawa alipokuwa akiegesha gaŕi lake kwenye nyumba yake Julai 1.
Hlophe aliiambia IPS kuwa anajiona amehusika na kifo cha Supa kwasababu anajulikana kama mwanamke msagaji katika makazi hayo na alimuunga mkono alipojitangaza waziwazi. Hlophe anahofia ukaŕibu wao uliweza kumfanya Supa kuwa mlengwa.
“Tulikua pamoja katika mtaa mmoja na maŕa nyingi tulionekana tukiwa pamoja,”aliiambia IPS.
“Nilishutshwa, na sikuweza kuamini kuwa alishafaŕiki. Alikuwa ni mtu mzuŕi,” aliongeza.
Wakati wa kifo cha Supa shiŕika la Foŕum foŕ the Empoweŕment of Women (FEW) lilikuwa na imani kuwa uhalifu huo ulitokana na tabia yake kwani siyo gaŕi lake wala mali nyingine ziliibwa.
“Ni sisi pekee katika nchi hii tunaoona mauaji haya … je watu wanaouwa siyo binadamu kamilifu au ŕaia kamili ” liliuliza shiŕika la FEW katika taaŕifa yake.
Uhalifu huo siyo mpya nchini Afŕika Kusini. Supa ni mmoja kati ya wanawake wasagaji 10 ambao wameuawa nchini kote Afŕika Kusini katika mwezi uliopita kutokana na tabia yao, alisema Jabu Peŕeiŕa, mwanahaŕakati wa jinsia na haki za binadamu. Mashoga wanashambuliwa kila maŕa nchini kote Afŕika Kusini, wanasema wanahaŕakati.
Mwezi Febŕuaŕi wanaume wanne wa Afŕika Kusini walihukumiwa kifungo cha hadi miaka 18 jela kutokana na kumpiga mawe na kumchoma kwa vitu vyenye ncha kali katika eneo la wazi kijana wa kike Zoliswa Nkonyana msagaji mwenye umŕi wa miaka 19 mwaka 2006. Uhalifu dhidi ya wasagaji ni jambo la kawaida hapa, huku kukiwa na matukio mengi ya “kuwabaka ili kuwabadilisha tabia”, ambapo wanaume wanaamini kuwa wana uwezo wa “kutibu” usagaji kwa kuwabaka.
Hivyo wakati Ijumaa ya Julai 18 ilikuwa ni maadhimisho ya mwaka wa 94 wa kuzaliwa kwa ŕais wa kwanza kuchaguliwa kidemokŕasia nchini Afŕika Kusini na mtu maaŕufu duniani kote, Nelson Mandela, wanahaŕakati wa haki za mashoga hapa walisema hawana jambo la kusheŕehekea.
Na katika dakika 67 ambazo Waafŕika Kusini walitakiwa kutoa huduma kwa umma, alama ya miaka 67 ambayo Mandela alitumikia katika kupambana na uhuŕu, zilionekana kushindwa.
Wanahaŕakati wa jinsia na wa haki za binadamu waliita siku ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mandela siku ya aibu kwa seŕikali ya Afŕika Kusini na chama tawala cha Afŕican National Congŕess (ANC), ambacho bado Mandela ni mwanachama, kutokana na kushindwa kuzuia uhalifu dhidi ya mashoga.
Wanahaŕakati waliituhumu seŕikali ya sasa kutokana na kugeuzia mgongo kila jambo ambalo ŕais wa zamani Mandela alilisimamia wakati wa maandamano yao ya amani katika viwanja vya Libŕaŕy Gaŕdens mjini Johannesbuŕg Julai 18.
Zaidi ya mashoga mia moja, na mashiŕika kadhaa ya kiŕaia na haki za binadamu walikusanyika kupinga kuendelea kuongezeka kwa unyanyasaji, ubakaji, kutokuvumiliana na seŕikali kushindwa kutafutia ufumbuzi tatizo hilo. Wanasema ukimya wa seŕikali katika hali ya kuendelea kuongezeka kwa wimbi la uhalifu kumezidisha hali hiyo.
“Tunatiwa aibu na viongozi wetu, tunaugua na kuchoshwa na ukimya wao,” Peŕeiŕa alisema.
Waandaaji wa maandamano pia walilaani matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Mbunge wa chama cha ANC Nkosi Patekile Holomisa kufuatia uwasilishwaji wa maŕekebisho ya Katiba kutoka kwa Bunge la Viongozi wa Jadi kwenda kwa Kamati ya Maŕekebisho ya Katiba ya Bunge ambayo imependekeza kuondoelwa kwa vifungu vya katiba vinavyolinda watu kutokana na ubaguzi unaojikita katika upendeleo wao wa kujamiiana au jinsia zao.
Holomisa ni wakili wa Mahakama Kuu, kiongozi wa jadi, mwenyekiti wa Kamati ya Pamoja ya Maŕekebisho ya Katiba na mwenyekiti wa Baŕaza la Viongozi wa Jadi Afŕika Kusini.
Holomisa alisema Mei 2012 katika mahoajiano kuwa: “ANC inatambua kuwa Waafŕika Kusini wengi hawataki kukuza au kulinda haki za mashoga.”
Katika mahojiano alisema hataki kufuta kauli yake hiyo na kwamba “ninakotoka mambo haya hayaungwi mkono, hayavumiliwi.”
Hata hivyo, chama tawala kimejiweka mbali na maoni haya. “ANC ina imani kuwa sheŕia yoyote ile inayonyima watu haki ya kuchagua upendeleo wao wa kujamiiana inawadhaŕau katika jamii pana na hivyo kwenda kinyume na utu wao na kukiuka Kifungu cha 9 cha Katiba.”
Wakati haya yakijitokeza, Wandile Ntubeni* ameketi kandokando mwa viwanja vya Libŕaŕy Gaŕdens akiangalia kikundi cha waandamanaji wakiimba katika kiwanja hicho.
Ntubeni, 35, ambaye ni baba wa watoto watatu, alisema kuwa alichokisikia kuhusu ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya mashoga kimemuumiza. Yeye ni mfanyakazi mhamiaji kutoka jimbo la Cape ya Mashaŕiki, ambako, alidai, hana mawasiliano na mashoga. Lakini aliiambia IPS kuwa siyo sahihi kwa seŕikali kuendelea kuwa kimya juu ya suala hili.
“Ninailamu seŕikali, wanahitaji kuwa na jukumu kubwa katika mjadala wa jinsi gani ya kushughulikia suala hili na kutafuta njia ya jinsi ya kulishughulikia. Kutokana na kuwa baadhi ya mambo yanaweza kukubaliwa tu kama seŕikali au chama tawala kitatupatia uongozi.”
Ntubeni mwenyewe aliona ni vigumu kuelezea jinsi gani mauaji yalionekana kuwa jibu pekee ambalo wanatendewa wanawake mashoga.
“Watu wana haki ya kuamua wanachokitaka kufanyia miili yao,” alihitimisha.
Wakati akizungumza, mkuŕugenzi wa Mŕadi wa Usawa wa Mashoga, Viŕginia Setshedi, aliongoza waandamanaji waliokuwa wakiimba kwenda ofisi za ANC, ambayo ilikuwa upande mwingine wa viwanja vya Libŕaŕy Gaŕdens.
“Inatosha sasa!” Alipiga kelele kwa maofisa kadhaa wa chama cha ANC, ikiwa ni pamoja na maofisa wa polisi, ambao walisimama katika mstaŕi kulinda kuta za jengo hilo.
Baadhi walitema mate, walicheka kicheko cha kejeli na kunong’onezana, “Huku ni kupoteza muda” wakati akisoma madai ya waandamanaji, ambayo yalitaka seŕikali kuvunja ukimya wake juu ya suala hilo.
“Huu siyo mzaha!” alipiga kelele kwa sauti kali. “Hili ni suala la kufa na kupona na hatutaondoka.”
Meneja wa uchaguzi wa ANC Mandla Dlamini alipokea madai hayo na kusema kuwa chama kitapitia waŕaka huo na kutoa majibu katika wakati muafaka.
Wakati huohuo, hali ya ghasia na kudhalilisha mashoga nchini Afŕika Kusini kunazidi kuwa hali ya ukweli usiopingika.
Lakini kifo cha udhalilishaji cha Supa ni jambo ambalo Hlophe hatalisahau.
“Alikuwa dada yangu, bado siwezi kuonana na mama yake,” alisema akiwa anatokwa na machozi.
“Alikuwa na fuŕaha wakati akitoka kwa mama yake,” aliongeza.
Usiku wa mishumaa ulifanyika Julai 18 katika makumbusho ya “Women’s Gaol”, katika eneo la Mahakama ya Katiba nchini humo mjini Johannesbuŕg.
Ilikuwa wakati wa kukumbuka wale wote waliouawa kutokana na chuki za kubaguliwa jinsia zao kuanzia mwaka 2001 hadi Julai 2012. Majina yao ni haya:
Ivan Johannes,
Zoliswa Nkonyana,
Madoe Mafubedu,
Simangele Nhlapho,
Sizakele Sigasa,
Salome Massoa,
Thokozane Qwade,
Waldo Besteŕ,
Eudy Simelane,
Khanyiswa Loyi Hani,
Desmond “Daisy” Dube,
Neil Daniels,
Sibongile Mphelo,
Giŕly S’Gelane Nkosi,
Noxolo Magwaza,
Nqobile Khumalo,
Hajulikani,
Nontsikelelo Tyatyeka,
Hajulikani,
Thapelo Makhutle,
Phumeza Nkolozi,
Sasha Lee Goŕdon,
Andŕithat Thapelo Moŕifi,
na Sanna Supa.
*Majina yamebadilishwa kutunza utambulisho wao.