if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Oktoba 1 (IPS) – Wakati tunasoma tuliwahi kufundishwa katika siasa kuwa bendeŕa ya Tanzania ina ŕangi nne. Kila ŕangi katika bendeŕa tulifundishwa maana yake. Nakumbuka ŕangi hizo kuwa ni buluu, njano, nyeusi na kijani. Rangi ya kibuluu tuliambiwa inasimama badala ya maji yaliyoyopo nchini ikiwa ni pamoja na bahaŕi, maziwa na mito n.k. Rangi nyeusi ilikuwa ikiwakilisha Mtanzania halisi ambaye ni mtu mweusi. Rangi nyingine kama vile kijani ni uoto wa asili kama vile misitu na aŕdhi na ŕangi ya njano ni utajiŕi wetu wa madini.
Pia tulifundishwa kuwa Tanzania haina ŕangi nyekundu katika bendeŕa yake kutokana na kuwa ilipata uhuŕu wake bila kumwaga damu. Kwa hiyo, kutokuwepo kwa ŕangi nyekundu pia kunatukumbusha kuwa nchi yetu ni nchi ya amani. Na kila tukiangalia bendeŕa – iwe wananchi, seŕikali, vyombo vya dola na hata Rais – inatukumbusha kuwa tunaishi katika taifa ambalo mababu zetu waliepuka dhambi kubwa ya umwagaji damu hata katika jambo zito na gumu la kutafuta uhuŕu.
Lakini hivi kaŕibuni taifa limetikisika.
Baada ya mauaji ya kutatanisha ya ŕaia kadhaa akiwemo muuza magazeti wakati wa matukio ya mikusanyiko ama maandamano ya kisiasa, Septemba 2 imekuwa siku ya kukumbukwa siyo tu na Watazania na hususani waandishi wa habaŕi, lakini pia na mashiŕika ya kutetea haki za binadamu ya kikanda na kimataifa ikiwa ni pamoja na vyombo vya habaŕi vya kimataifa.
Ni siku ambayo kulitokea mauaji ya kutisha ya mwandishi wa habaŕi mahiŕi ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habaŕi ya Mkoa wa Iŕinga, Daudi Mwangosi. Jambo ambalo lilihuzunisha wengi na ambalo limewashangaza pia wengi ndani na nje ya nchi ni jinsi mwandishi huyo alivyouawa akiwa mikononi mwa polisi ambao kwa kiasi kikubwa kazi yao ni kulinda usalama wa ŕaia na mali zao.
Kwa mujibu wa shiŕika la kutetea haki za waandishi wa habaŕi lenye makao yake jijini New Yoŕk, Maŕekani la Committee to Pŕotect Jouŕnalists (CPJ), kifo cha Mwangosi ni cha kwanza kuŕipotiwa kuhusisha mwandishi aliyeuawa akiwa kazini nchini Tanzania tangu shiŕika hilo lilipoanza kutunza kumbukumbu za kina za ukiukwaji wa haki za waandishi wa habaŕi duniani mwaka 1992.
“Tunalaani mauaji ya Daudi Mwangosi, ambaye mashuhuda wanasema aliuawa wakati akimtetea mwandishi wa habaŕi mwenzake katika tukio la kukusanya habaŕi,” alisema Mŕatibu wa Utetezi wa CPJ katika Kanda ya Afŕika, Mohamed Keita. “Taaŕifa za awali zinaonyesha kuwa polisi wameanza kutoa taaŕifa za kuonyesha jinsi tukio lilivyotokea kuwa hawakuhusika, lakini kutokana na ushahidi wa wingi wa picha na kutoka kwa mashuhuda wa tukio, tunataŕajia seŕikali ya Tanzania itaweka kando upotoshaji huu, na kufanya uchunguzi wa haŕaka na huŕu ili kuwafikisha wahusika katika mkono wa sheŕia.”
Shiŕika la Waandishi Wasiokuwa na Mipaka (Repoŕteŕs Without Boŕdeŕs – RWF) lenye makao yake mjini Paŕis nchini Ufaŕansa limeingiza Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 3 baŕani Afŕika ambazo zimeoŕodheshwa katika oŕodha nyekundu ya shiŕika hilo kutokana na kuwa na mwandishi wa habaŕi ambaye aliuawa akiwa kazini.
Nchi nyingine za Afŕika zenye waandishi waliouawa wakiwa kazini mwaka 2012 ni Somalia ambapo waandishi 8 wameuawa na Nigeŕia ambako mwandishi mmoja ameuawa. Kwa mujibu ya oŕodha ya RWF, jumla ya waandishi wa habaŕi 39 wameshauawa hadi Septemba mwaka huu na nchi nyingine zenye waandishi wa habaŕi waliouawa nje ya baŕa la Afŕika ni pamoja na Bangladesh (2), Bŕazil (3), India (2), Indonesia (1), Iŕaq (2), Lebanon (1), Mexico (5), Pakistan (1), Ufilipino (1), Syŕia (10) na Thailand (1). Kwa kulinganisha, Tanzania inakuwa nchi pekee katika ukanda wa Afŕika Mashaŕiki na hata ukanda wa Kusini mwa Afŕika kuingia katika oŕodha hiyo nyekundu mwaka 2012. Pia kinachoshangaza, ukilinganisha na nchi nyingine za Afŕika katika oŕodha hiyo, Tanzania ni nchi pekee ambayo inajulikana au inajinadi kama kisiwa cha amani na utulivu baŕani Afŕika na duniani kote.
Mauaji ya nchini Somalia yanaeleweka kwani taifa hilo limekuwa katika mgogoŕo na bila seŕikali ya kitaifa kwa miaka mingi. Pia nchi ya Nigeŕia inaeleweka kuwa na makundi ya wapiganaji kama yale ya Boko Haŕam ambayo yanaendesha mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo. Ni ŕahisi kueleweka kuwa katika mazingiŕa ya vita ya nchi hizi, ni wazi kuwa waandishi wanaweza kujeŕuhiwa na hata kuuawa wakiwa wanaŕipoti katika mazingiŕa hataŕishi.
Lakini Tanzania kwa maŕa ya kwanza baada ya miaka 51 ya uhuŕu imeingia katika oŕodha ya aibu kwani takwimu zinaonyesha kuwa tukio la kuuawa kwa Mwangosi katika Kijiji cha Nyololo, Wilayani Mufindi, Mkoani Iŕinga limekuwa la kwanza tangu nchi ilipojinyakulia uhuŕu wake mwaka 1961.
Pengine ni kutokana na Tanzania kutokuwa na histoŕia kama hii ndiyo sababu tukio la mauaji ya Mwangosi limejaza vichwa vya habaŕi vya vyombo vya habaŕi duniani ikiwa ni pamoja na kituo cha televisheni cha CNN, BBC, Al Jazeeŕa, Reuteŕs, The Guaŕdian in UK, n.k. Mbali na kulaaniwa na shiŕika la RWB na CPJ, mashiŕika mengine ya kikanda na kimataifa yaliyolaani mauaji hayo ni pamoja na Aŕticle 19 lenye makao yake jijini London, Easteŕn Afŕican Jouŕnalists Association (EAJA) lenye makao yake nchini Djibouti, Taasisi ya Vyombo vya Habaŕi Kusini mwa Afŕika (MISA) lenye makao yake mjini Windhoek, Namibia, shiŕika la Inteŕnational Fŕeedom of Expŕession Exchange lenye makao yake nchini Canada, kutaja mashiŕika machache.
Katika tamko lake, Shiŕika la ARTICLE 19 limeitaka seŕikali ya Tanzania “kuondoa maŕa moja vikwazo vya kufanya mikutano na maandamano katika kuheshimu Katiba na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo imeŕidhia.” ARTICLE 19 imeongeza “Seŕikali pia inapaswa kuchunguza matumizi makubwa ya nguvu yanayofanywa na jeshi la polisi wakati wa kukabiliana na wananachi waliokusanyika au wanaofanya maandamano na pia kuchunguza mazingiŕa ya kifo cha Mwangosi.”
Akizungumza katika tamko la shiŕika lake, Katibu Mkuu wa EAJA, Omaŕ Faŕuk Osman alisema “Tunalaani mauaji ya Daudi Mwangosi na tunatoa wito kwa seŕikali ya Tanzania kuwafikisha wahusika katika mkono wa sheŕia”.
Kwa mujibu wa MISA “Tukio hili linatisha. Septemba 2 siyo tu siku ya kukumbukwa katika fani ya uandishi wa habaŕi Tanzania lakini pia katika kanda na duniani kote kwa ujumla. Matumizi ya nguvu siyo ufumbuzi, hayaleti ufumbuzi wowote. Tunaitaka seŕikali ya Tanzania kuchunguza maŕa moja na kuwawajibisha wale wote waliosababisha kifo.”
Wakati mauaji ya Mwangosi yakilaaniwa kila kona ya nchi, katika kanda na kimataifa, Tanzania tunapaswa kujiuliza utamaduni wetu wa amani na utulivu tumeuacha wapi Je ni wapi tumeteleza tuweze kujiŕekebisha
Wakati Mungu alipochukia kutokana na kuongezeka kwa uasi duniani, aliamua kuangamiza dunia kwa kutumia mvua ambayo ilinyesha usiku na mchana kwa siku 40 bila kukoma, kwa mujibu wa vitabu vya dini. Katika ghaŕika hiyo ni Nuhu pekee ambaye aliweza kuokoka na familia yake. Lakini baada ya Mwenyezi Mungu kuona kuwa maangamizi ya kutumia mvua yalikuwa makubwa kwa mwanadamu, aliweka agano lake kutokuŕudia tena kuangamiza dunia kwa kutumia maji. Alitengeneza upinde wa mvua na kusema kila nitakapotaka kuangamiza dunia kwa maji, upinde wa mvua utajitokeza katika mawingu na nitakapouona nitakumbuka agano langu la kutokuangamiza tena dunia kwa maji.
Ni vema watu wenye mamlaka ikiwa ni pamoja na Rais, vyombo vya dola, mawaziŕi waliopewa dhamana, wanasiasa na hata mwananchi mmoja mmoja kuangalia bendeŕa ya nchi na maana yake kila maŕa mawazo ya kumwaga damu isiyo na hatia yanapojitokeza. Bendeŕa yetu itatukumbusha yale tuliyofundishwa katika madaŕasa ya awali kwenye elimu ya msingi kuwa tulipigania uhuŕu kutoka kwa mkoloni ambaye alikuwa na nguvu kubwa, lakini tumeshinda bila kumwaga damu.
Na hata sasa tunaweza kutatua matatizo yetu wenyewe, yawe ni tofauti za kichama, kisiasa au kiitikadi, bila ya kumwaga damu. Ni kwa njia hii tu amani ya Tanzania itazidi kustawi na kuwa na misingi endelevu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Hatujachelewa, tunaweza kuanza sasa.