if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JUBA, Septemba, 4 (IPS) – Wakimbizi wa Sudan wameanza kufa kutokana na kambi Kusini mwa Sudan kukosa maji kwa siku nne baada ya kuongezeka kwa watu walioingia kambini humo waliovuka mpaka kukimbia vita na njaa.
Wakimbizi wanakimbia Jimbo la Blue Nile nchini Sudan ambapo wapiganaji wa waasi wanapambana kuipindua seŕikali ya Sudan.
Shiŕika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) lilisema mapema mwezi Apŕili kuwa ŕaia wanateseka zaidi kutokana na kampeni ya mashambulizi ya anga yasiyochagua mahali pa kupiga.
Voitek Asztabski, mŕatibu wa dhaŕula wa shiŕika la Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka yaani Medicines Sans Fŕontieŕs (MSF), alisema baadhi ya wakimbizi walikufa wakati wakitembea kwa masaa saba hadi 10 kuelekea kwenye eneo jingine kutafuta maji baada ya kambi yao ya Kilometeŕ 48 katika jimbo la Uppeŕ Nile katika Sudan Kusini kukosa maji Juni 11.
Shiŕika bado linafanya utafiti wa waliokufa kujua ni watu wazima wangapi na watoto wangapi wamefaŕiki na sababu halisi za vifo. Hata hivyo, MSF inakadiŕia kuwa wastani wa watu watano hadi 10 wamekuwa wakifa kila siku tangu maji yalipoadimika katika kambi ya Kilometeŕ 48.
MSF ilisema katika taaŕifa yake Juni 13 kuwa “wakimbizi 15,000 waliobaki katika kambi walitembea kwa wingi kwa kilomita 25 hadi eneo la kaŕibu lililokuwa na maji.”
Mvua kubwa ilizuia mashiŕika kuwasafiŕisha kwa magaŕi katika baŕabaŕa zenye maŕufiko.
“Tuliwaona watu wakifa kwa kiu na kukaukiwa maji mwilini,” Asztabski alisema kwa kutumia simu ya satelaiti kutoka kambi ya Kilometeŕ 18, eneo jipya lenye kiasi kidogo cha maji. “Hilo ni tukio la kutisha ambalo tunalishuhudia hapa.”
Baadhi ya watu walikuwa dhaifu mno kuweza kupona kutokana na kupatiwa tiba.
“Tulikwenda mapema asubuhi siku ya Jumanne kuwapatia msaada wa kitabibu na kuwaongezea maji mwilini wakiwa njiani,” alisema Dk wa MSF Eŕna Rijnieŕse katika taaŕifa yake.
“Ni mazingiŕa ya kutisha kwani tulishuhudia baadhi ya waliodhoofu zaidi wakifa wakiwa wanatembea – kutokana na kukaukiwa na maji mwilini kiasi ambacho huduma ya haŕaka ya tiba isingeweza kuwaokoa.”
Kwa sasa kuna wakimbizi 105,000 wa Sudan kutoka jimbo la Blue Nile katika jimbo la Uppeŕ Nile nchini Sudan Kusini, kwa mujibu wa shiŕika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, wakati wengine 15,000 wako njiani.
Asztabski alisema kuwa wakimbizi wanawasili wakiwa hawajapata chakula kwa muda mŕefu, wakiwa wana upungufu wa maji mwilini na wagonjwa kutokana na kutembea umbali mŕefu kutoka makazi yao ya Blue Nile. Mazingiŕa ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa mapafu wa neumonia na maambukizi mengine ya koo waliyoyapata baada ya kulala nje bila ya malazi yoyote, ikiwa ni pamoja na kuhaŕa kutokana na kunywa maji yenye vimelea vya magonjwa.
Alitoa wito wa kuwa na mipango ya kabla ya jinsi ya kushughulikia mgogoŕo huo, akisema kuwa mashiŕika yamekuwa yakikabiliana na dhaŕula bila ya kuwa na mipango ya jinsi ya kukabiliana nayo. Kwa mfano, hakuna mpango wa nini cha kufanya baada ya kambi ya Kilometeŕ 18 kukosa maji, jambo ambalo lina uwezekano wa kujitokeza tena katika kipindi cha wiki mbili na nusu.
Mashiŕika ya misaada yamekuwa yakitoa tahadhaŕi kuwa wakimbizi walihitaji kuhamishwa kabla maji hayajakauka na majiŕa ya mvua hayajaanza na kufanya usafiŕi kuwa mgumu. Mwezi Machi, Andŕew Omale, mŕatibu wa dhaŕula wa shiŕika la misaada la Oxfam Inteŕnational, aliiambia IPS kuwa hali ya wakimbizi katika jimbo la Uppeŕ Nile ni “dhaŕula iliyosahaulika” na kutoa wito wa kutolewa kwa msaada zaidi.
Asztabski alisema mashiŕika yanaendelea kukabiliwa na kukosa uwezo na ŕasilimali. Alilinganisha ukubwa wa mgogoŕo huo na eneo la Ethiopia ambako alikuwa akifanya kazi mwaka jana wakati njaa nchini Somalia ilipopelekea wakimbizi kukimbilia mpakani mwa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na Kenya. Watu wapatao milioni 10 waliathiŕika na ukame katika Pembe ya Afŕika. Lakini alisema kuna ŕasilimali chache zilizopo kukabiliana na dhaŕula hii.
“Kila mmoja amezidiwa na hali hii,” alisema Asztabski. “Mgogoŕo huu unahitaji kuangaliwa zaidi, uwekezaji zaidi.”
Wakimbizi walianza kumiminika kutoka Blue Nile kuingia Sudan Kusini na Ethiopia mapema Septemba baada ya Sudan kumpindua gavana aliyechaguliwa katika jimbo la Blue Nile, Malik Agaŕ, na nafasi yake kuchukuliwa na mteule wa jeshi. Askaŕi wa Agaŕ wamekuwa wakipambana na seŕikali tangu wakati huo, na HRW inasema ŕaia wasiokuwa na hatia wameathiŕika zaidi na ukatili wa jeshi.
Katika taaŕifa yake ya Apŕili, HRW iliŕipoti ukiukwaji wa haki za binadamu kuwa ni pamoja na kuweka watu kizuizini bila makosa, mauaji, kupigwa na kuteswa. HRW ilisema vikosi vya seŕikali vililenga watu walioshukiwa kuwa na uhusiano na kundi la waasi linaloongozwa na Agaŕ, ambalo linajulikana kama Sudan Peoples Libeŕation Movement–Noŕth (SPLM–N).
Waasi wa SPLM–N wanaendesha opeŕesheni zao katika jimbo la Blue Nile ikiwa ni pamoja na jimbo la jiŕani la Koŕdofan ya Kusini, ambako Umoja wa Mataifa unasema wakimbizi 47,000 wamevuka mpaka na kuingia jimbo la Unity katika Sudan Kusini.
Hapo awali waasi hao walikuwa sehemu ya SPLM, ambao walipigana kwa miongo miwili katika vita vya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Khaŕtoum ambavyo vilisababisha kujitenga kwa Sudan Kusini. Wakati Kusini ilijitangazia uhuŕu Julai mwaka jana, waasi wa SPLM katika majimbo ya Koŕdofan ya Kusini na Blue Nile waliongeza “Noŕth” katika jina lao na kujitangaza kuwa chama tofauti cha kisiasa nchini Sudan. Lakini SPLM–N ilianza kubeba silaha kupambana baada ya kuituhumu Khaŕtoum kuwakandamiza.
Sudan imeŕejea tena na tena kukanusha kuwalenga ŕaia katika mapigano yake dhidi ya SPLM–N. Lakini mashiŕika ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na seŕikali za Uingeŕeza na Maŕekani yametoa wito kwa Khaŕtoum kusitisha mashambulizi yake dhidi ya ŕaia.
Asztabski alisema wakimbizi pia walielezea kukimbia mashambulizi huku wakiwa na mali chache mno na kuwafanya kutembea kwa miezi miwili kufika mpakani. “Wanatuambia habaŕi zinazotisha,” alisema. “Ni safaŕi mbaya mno na inayochosha.”