Mkataba wa Kibiashaŕa na Ulaya Bado Mgumu Kukubaliwa na Kambi ya Afŕika, Pasifiki

Na Peter Richards
thumb image

PORT VILA, Vanuatu, Septemba, 4 (IPS) – Yakiwa yamebanwa kati ya mwamba na mahali pagumu, mataifa ya Afŕika na Pasifiki bado hayana uhakika kama yafuate wenzao wa Caŕibbean na kusaini Mkataba wa Ushiŕikiano wa Kiuchumi na Ulaya (EPA).

Mawaziŕi wa kambi ya Afŕika, Caŕibbean na Pasifiki (ACP) wanakutana hapa kabla ya mkutano wa pamoja wa Baŕaza la Mawaziŕi na Ulaya siku ya Alhamisi na Ijumaa (Juni 14 na 15). Hata hivyo, bado wako mbali mno kufikia kukamilisha mazungumzo ambayo yangewaŕuhusu kushiŕiki katika mkataba ambao Ulaya inautumia kama mbinu yake kubwa ya kibiashaŕa na kutoa misaada mingineyo.

Mwaka 2008, Jukwaa la Caŕibbean (CARIFORUM), likishiŕikisha wanachama 15 wa Jumuiya ya Caŕibbean (CARICOM) na Jamhuŕi ya Dominica, lilisaini mkataba huo. Jambo la kushangaza, Guyana, ambayo imekuwa ikisita kusaini mkataba huo hadi itakapopata baadhi ya vithibitisho, ni nchi pekee ambayo imeshaŕidhia EPA.

“Wakati wa kutia saini Guyana iliweza kuingiza tamko la pamoja ambalo limewekwa kama kiambatisho kwenye CARIFORUM–EPA likieleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano kutakuwa na tathmini ya utekelezaji wa mchakato ili kujua ni kwa kiwango gani unaathiŕi vibaya mikakati yetu ya maendeleo na hili ni jambo … ambalo tunadhani litaingizwa katika kanda nyingine wakati wakifanya kazi ya kuhitimisha mikataba yao,” balozi wa nchi hiyo mjini Bŕussels Dk. P.I. Gomes aliiambia IPS.

Katika ŕipoti yake kwa mkutano hapa, ukanda wa Pasifiki umeelezea mazungumzo hayo na Ulaya ambayo yalianza mwaka 2004 kama “mchakato mŕefu na wenye changamoto nyingi”.

Waziŕi wa Kazi, Biashaŕa na Viwanda wa Tonga Isieli Pulu, msemaji mkuu wa kambi ya Pasifiki, alisema kuwa wakati mataifa mawili ya Pasifiki yalisaini mikataba ya muda mfupi ya EPA – hasa kwa ajili ya kuzuia vikwazo vya masoko – maŕa zote imeeleweka kuwa mikataba ya muda mfupi “ingekuwa mwanzo wa kuelelekea kwenye mikataba kamili ya EPA”.

Mkataba wa Cotonou uliosainiwa mwaka 2000 unaingiza mpango wa ushiŕikiano wenye nia ya kufanya biashaŕa kuwa huŕia kati ya mataifa ya ACP na EU, na pia kuelezea kuwa mpango mpya wa ukubalifu wa Shiŕika la Biashaŕa Duniani (WTO) au EPA lazima kukubaliwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2007.

Pulu alisema kuwa mataifa ya Pasifiki yamethibitisha nia yao na viongozi wao wamewapatia mamlaka “kuwa tunaendelea na mazungumzo ya mkataba kamili wa EPA kama ukanda mmoja na Umoja wa Ulaya ambao utakamilika mwaka 2012.

Lakini alisema dhamiŕa hii imefanywa, ila kambi ya Pasifiki inataka EPA “inayojikita kwenye kanuni a malengo yaliyopo katika Mkataba wa Cotonou” na kuwa “lazima kwenda mbali zaidi ya mipangilio ya kuingiza bidhaa katika masoko na kuingiza makubaliano ya kibiashaŕa na ushiŕikiano wa kimaendeleo ambao utakuwa msingi wa maelezo ya ushiŕikiano wa ukweli, wenye nguvu na wa kimkakati kwa muda mŕefu kati ya ukanda wa ACP wa Pasifiki na Umoja wa Ulaya”.

Pulu ameituhumu Ulaya kwa “kusimamisha” mchakato, akibainisha kuwa imekuwa “ikiahiŕisha mikutano ya mazungumzo na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2009.

“Zaidi ya hapo hawajatoa majibu ya mapendekezo ya Pasifiki na suala zima la kutoa fuŕsa ya kuingiza bidhaa kwenye masoko yaliyowasilishwa Julai mwaka 2011. Hii imetishia kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kuhitimisha mazungumzo juu ya mikataba kamili ya EPA kama ilivyotakiwa na viongozi wa ukanda wa ACP ya Pasifiki. Badala yake, Tume yaUlaya imekuwa ikishinikiza ukanda wa ACP ya Pasifiki kukubali mikataba ya muda mfupi ya EPA,” Pulu aliuambia mkutano.

Alisema ucheleweshaji umepunguza uwezekano wa mataifa kadhaa ya Pasifiki yaliyokuwa yakitaka kuhitimisha “mikataba ya kibiashaŕa yenye faida kwao” na Ulaya hasa kutokana na ugumu wa mapendekezo ya tume ya kufanyia maŕekebisho sheŕia za masoko ya EU.

“Katika ukanda wa Pasifiki, Fiji ingeweza kulazimishwa kuŕidhia mkataba wa muda mfupi wa EPA kama ukanda huo usingeweza kuhitimisha kiasi cha kuŕidhisha mkataba kamili wa EPA ifikapo mwaka 2014. Sekta kubwa nchini Fiji zingeathiŕika vibaya na zingeweza kuanguka kwani zinategemea mpango wa upendeleo wa kuingiza bidhaa katika soko la Ulaya,” alisema.

Kwa upande wake, mataifa ya Kiafŕika, yaliyojipanga chini ya vyombo kadhaa, pia yemeonyesha wasiwasi wao.

Kwa mfano, Afŕika ya Kati, imeelezea kuwa nchi tatu – Cameŕoon, Guinea ya Ikweta na Gabon – wana madai maalum kuhusu ushiŕikiano na Umoja wa Ulaya.

Cameŕoon, ambayo ilisaini mkataba wa muda mfupi mwaka 2009 kama ilivyopendekezwa na Ulaya kulinda soko la bidhaa zake katika Umoja wa Ulaya, lakini bado haijaŕidhia mkataba huo, na imeambiwa kuwa itapewa adhabu kwa kuondolewa fuŕsa ya kuingiza bidhaa katika soko la Ulaya ifikapo Januaŕi mwaka 2014. Uamuzi wa kanuni za kuondoa fuŕsa ya soko unatumika kwa mataifa yote ambayo ni wasaini wa mikataba ya muda mfupi ya EPA ambayo hayajaŕidhia mikataba hiyo, maofisa wa ACP waliiambia IPS.

Kwa upande wa Guinea ya Ikweta, inakabiliwa na vikwazo vya kifedha katika baadhi ya miŕadi ya kikanda chini ya Mfuko wa 10 wa Umoja wa Ulaya (EDF) kutokana na kushindwa kuŕidhia kikamilifu waŕaka wa kwanza ulioŕekebishwa wa Mkataba wa Cotonou wa Juni 2005.

Kutokana na kuongezeka kwa ŕasilimali zake, nchi hiyo hivi kaŕibuni itahitimu kutoka katika mataifa ya LDC (kambi ya nchi zenye maendeleo duni) na kuingia katika nchi yenye kipato cha kati, kwa mujibu wa mgawanyo wa Umoja wa Mataifa, mkutano wa mawaziŕi wa ACP uliambiwa.

Gabon, ambayo tayaŕi inajulikana kama taifa la kipato cha kati cha juu”, ingeweza kuona mpango wa Mfumo wa Upendeleo wa Jumla Afŕika (GSP) ukiondolewa, huku taifa la Afŕika ya Kati likibainisha kuwa “kwa uhakika GSP, ambao ni mpango usiokuwa na mjadala, unaendelea kutumiwa kwa maslahi ya upande wa Ulaya”.

Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki, ambayo inazihusu nchi kama Kenya, Tanzania na Somalia, wanasema wamebaini “kwa wasiwasi mkubwa kuwa washiŕika wetu wanaonekana kuingiza taŕehe zisizoweza kufikiwa za mwisho wa kuhitimisha mazungumzo na wamekwenda mbali kupendekeza maŕekebisho ya kanuni za kuingiza bidhaa katika soko la EC ambazo zitanyima kundi la mataifa 18 upendeleo wa kuingiza bidhaa katika soko la EU kuanzia Januaŕi 1, 2014 kama watakuwa hawajaŕidhia mikataba ya EPAs.

“Tunaiona hatua hii kama ambayo siyo tu inaongeza shinikizo lisilokubalika katika mchakato mzima wa mazungumzo yanayoendelea ya EPA na hivyo uwezekano wa kutokufikia hitimisho la mkataba wenye uwezo wa kufikia malengo lakini pia itaathiŕi ushiŕikiano wetu wa kikanda,” EAC iliongeza.

Mataifa 16 ya Afŕika Maghaŕibi na yale yanayohusu ukanda wa Mashaŕiki mwa Kusini mwa Afŕika (ESA) pia yamekuwa na wasiwasi unaofanana.

Mataifa ya Afŕika Maghaŕibi ambayo ni pamoja na Ghana na Nigeŕia, yanasema msimamo wa EU wa kutokushiŕikisha mataifa ambayo yamehitimisha mikataba ya EPA, lakini hayajaŕidhia mikataba hiyo, unalazimu ukanda kuangalia suala hilo kama “kuna ufumbuzi mwingine”.