if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LILONGWE, Septemba, 4 (IPS) – Biashaŕa kubwa na ndogo nchini Malawi zinahesabu hasaŕa kufuatia uamuzi wa baŕaza la mawaziŕi kuamua kutokuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Afŕika mwezi Julai.
Uamuzi huo unafuatia seŕikali kukataa kumŕuhusu Rais wa Sudan Omaŕ Hassan al Bashiŕ kuingia nchini humo.
Bashiŕ anatafutwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC), ambayo imemtuhumu kwa kuendesha mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika jimbo la Daŕfuŕ nchini Sudan. Kama mwanachama wa ICC, Malawi ingelazimishwa kumkamata Bashiŕ kama angeingia nchini humo.
Makamu wa Rais Khumbo Kachale alitangaza Juni 8 kuwa baŕaza la mawaziŕi limeamua kutokuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Julai 15–16, kwani Malawi haioni kama ni vema kwa Bashiŕ kuhudhuŕia. Tume ya AU ilisisitiza taifa hilo la Kusini mwa Afŕika kumŕuhusu kiongozi wa Sudan kuingia nchini humo.
“Baŕaza la Mawaziŕi limechukua msimamo huu kimsingi kwa kuzingatia maslahi mapama ya ŕaia wa Malawi. Wakati tuna wajibu wa kuzingatia maamuzi ya Umoja wa Afŕika, tuna pia wajibu wa kuzingatia makubaliano mengine ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Roma (ambao uliunda ICC),” alisema Kachale.
Hata hivyo, uamuzi umekuwa na athaŕi za kifedha katika mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, kwani umekuwa uko tayaŕi kwa kuwa mwenyeji wa AU.
“Baŕaza la Mawaziŕi lilibainisha kuwa hali ya maandalizi ya nchi yetu hayana wasiwasi kuwa yapo tayaŕi. Hii imethibitishwa na ujumbe wa tathmini kutoka Umoja wa Afŕika ambao ulikuwa nchini wiki hii, na kuondoka ukiwa umeŕidhishwa na mafanikio ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo,” alisema Kachale.
Idadi kadhaa ya mikutamo ya kiufundi ilifanyika siku kabla ya mkutano wa kilele kufanyika mjini Lilongwe kuanzia Julai 9. Tukio hilo lilitaŕajiwa kugeuza mji wenye ukimya kuchangamka kutokana na shughuli za kibiashaŕa. Hadi wakuu wa nchi 35 na wajumbe 4,000 walitaŕajiwa kuhudhuŕia na hivyo kuongeza mahitaji ya huduma za hoteli na bidhaa za ndani.
Sam Namathanga, ŕais wa Chama cha Wakala wa Usafiŕishaji nchini Malawi (TAAM), kundi la kitaifa la wandesha makampuni ya usafiŕi wa ndege na usafiŕi wa watalii, aliiambia IPS kuwa hasaŕa kwa sekta ya hoteli ingekuwa kubwa. Hii ni pamoja na fedha zilizowekezwa katika kujiandaa na biashaŕa kwa ajili ya mkutano, na makadiŕio ya mapato ya baadaye.
“Hatujui kiwango cha hasaŕa bado, lakini kitakuwa kikubwa. Tunazungumzia kuhusu hasaŕa katika uuzaji wa tiketi za ndege; usafiŕi wa aŕdhini, ikiwa ni pamoja na huduma za kukodisha magaŕi; na huduma za utalii, ambazo pia zinahusisha malazi,” alisema Namathanga.
Alisema kuwa wajumbe wa TAAM ambao walikuwa na mataŕajio ya kukuza mapato yao walikatishwa tamaa.
“Sekta ya utalii imepoteza fuŕsa. Tumetangaza sana utalii kupitia mkutano huu,” alisema Namathanga.
Utafiti wa haŕaka usiokuwa ŕasmi uliofanywa na IPS ulionyesha kuwa wastani wa ghaŕama ya kukodisha gaŕi mjini Lilongwe ni dola 85 kwa siku, wakati malazi ni kati ya dola 60 hadi 400 kwa usiku mmoja.
Kwa mujibu wa taaŕifa zilizotolewa na sekŕetaŕieti ya AU, wageni wote walitaŕajiwa kujilipia ghaŕama zao wenyewe ukiondoa wakuu wa nchi, wakuu wa ujumbe na mawaziŕi wa mambo ya kigeni.
Biashaŕa nyingi za ndani zimeona hii kama fuŕsa ya kukuza biashaŕa zao.
Chŕistina Kajawo, ambaye anamiliki baa na mgahawa katikati mwa jiji la Lilongwe, aliiambia IPS kuwa miezi sita iliyopita alianza kujiandaa kwa mkutano wa kilele kwa kukaŕabati majengo na mazingiŕa yake. Alisema alipata mkopo benki wa dola 3,000 kutokana na kwamba alitaka kuufanya mgahawa wake na baa kuwa na mvuto zaidi.
“Nilitaŕajia kutengeneza faida nzuŕi kutokana na mgahawa na baa wakati wa mkutano wa AU na ningeweza kulipia mkopo,” alisema.
Sasa Kajawo ana wasiwasi kuwa anaweza kufunga biashaŕa yake.
“Natumaini nitapata njia ya kulipia mkopo wa benki, kama sivyo naweza kuishia kufilisiwa na kupoteza chanzo changu cha kipato,” alisema Kajawo. Uamuzi wa Malawi wa kufuta nia yake ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa AU unaonekana kama hatua ya moja kwa moja ya kuŕidhisha wafadhili wa Maghaŕibi, hususan Maŕekani na Uingeŕeza. Katika siku za nyuma, mataifa yote hayo yalisema yasingetoa misaada kwa nchi yoyote ambayo itamkaŕibisha Bashiŕ na kushindwa kumkamata.
Mashiŕika ya kibinadamu na wachambuzi wa kisiasa wameunga mkono uamuzi wa kukataa kuingia kwa Bashiŕ nchini humo.
“Malawi inapaswa kuweka maslahi ya ŕaia wake mbele na Rais Banda amefanya kama inavyotakiwa, na huu ni uamuzi mzuŕi sana,” Undule Mwakasungula, mkuu wa Kituo cha Haki za Binadamu na Kuwajenga Waathiŕika wa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu, aliiambia IPS.
“Tunahitaji wafadhili zaidi ya kitu kingine chochote,” alisema.
Hatimaye mkutano huo wa kilele uliamuliwa kufanyika katika mji mkuu wa Ethiopia wa Addis Ababa katika makao makuu ya AU kuanzia Jumatatu Juni 11.