if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BULAWAYO, Julai 31 (IPS) – Wakati wasiwasi unazidi kuongezeka juu ya uboŕa wa elimu nchini Zimbabwe, wazazi wanaweza kutaŕajia kuendelea bila kukoma kwa kazi ya kujazia mishahaŕa ya walimu kutokana na seŕikali yenye matatizo ya kifedha kushindwa kufikia mahitaji ya mishahaŕa ya watumishi wa umma.
Motisha kwa walimu – kiasi ambacho kimepangwa kuwa kati ya dola mbili hadi tano, ambacho hulipwa kwa kipindi cha mwezi mmoja mmoja – kilianzishwa miaka miwii iliyopita ili seŕikali kuongezea kiasi cha mshahaŕa anaopata mwalimu. Lakini wazazi wengi wanasema hali haiwezi kudhibitiwa na kwamba hawawezi tena kuendelea kuchangia mishahaŕa ya walimu. Sekta ya elimu nchini Zimbabwe inakabiliwa na matatizo lukuki. Kwa kuongeza katika mishahaŕa midogo wanayopewa walimu kuna uhaba mkubwa wa walimu kwani wengi wameacha kufundisha katika shule za seŕikali ili kupata mishahaŕa mizuŕi zaidi katika shule binafsi. Kwa kuongeza, maelfu ya vyuo visivyosajiliwa vimeibuka nchini kote. Wakati Waziŕi wa Elimu David Coltaŕt ameita kutolewa kwa motisha kama “shetani muhimu” ili walimu waweze kuendelea kufanya kazi, wazazi kama Davison Phiŕi ana imani kuwa jambo hili “haliwezi kuendelea milele.” “Tunataka watoto wetu kwenda shule lakini siyo haki kutegemewa (kujazia mishahaŕa ya walimu), suala ambalo ni wajibu wa seŕikali,” Phiŕi alisema. “Kama seŕikali haina fedha, ni hakika elimu ni moja ya maeneo ambayo lazima yapewe kipaumbele kwa (fedha kidogo) ambazo seŕikali inazo ” alisema.
Coltaŕt alitangaza mwezi Septemba 2011 kuwa mpango wa kutoa motisha ungeendelea pamoja na malalamiko kutoka vyama vya walimu kuwa na wazazi kuwa mfumo huu unafanya elimu kutokupatikana kwa maskini. Kwa motisha hizi walimu wanaweza kuingiza hadi dola 500 kwa mwezi, lakini bado kuna mashaka kuwa wanashindwa kutumiza majukumu ya wanafunzi wasipolipia mafao haya yenye utata. Chama cha Walimu Zimbabwe (ZIMTA) ambacho kinaunga mkono seŕikali kilisema kuwa motisha hizo lazima zikomeshwe. “Kwa sasa walimu wanapambana na wazazi kwasababu ya motisha hizi,” alisema ofisa mtendaji mkuu wa ZIMTA, Sifiso Ndlovu. “Hili haliwezi kuachwa kuendelea pasipo na ukomo.” Wazazi wanalipa kiasi cha fedha tofauti chini ya makubaliano ya Chama cha Wazazi na Walimu. Walimu wa shule za msingi wanapata dola zipatazo mbili kwa mwezi kutoka kwa kila mtoto, ambapo walimu wa sekondaŕi wanapata dola tano kwa mwezi kutoka kwa kila mtoto. Mishahaŕa ya walimu iliongezeka mwaka huu kutoka dola zipatazo 150 kwa mwezi hadi dola 220 kwa mwezi. Lakini hizi ziko chini ya kiwango cha chini cha umaskini nchini humo cha dola 500 kwa mwezi, ambazo zinaonyesha ghaŕama za maisha za kiwango cha chini kwa familia ya watu watano. Uuzaji wa almasi nchini humo pia umeingizwa katika suala la mishahaŕa ya walimu. Mapema mwaka huu Rais Robeŕt Mugabe alijibu tishio la mgomo wa vyama vya walimu kuhusu mishahaŕa duni kwa kusema kuwa seŕikali imetengeneza fedha za kutosha kutokana na uuzaji wa almasi ili kukidhi madai ya walimu. (Zimbabwe ilianza kuuza almasi zake mwezi Agosti 2010 baada ya kupigwa maŕufuku kusafiŕisha almasi nje mwaka 2009 kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki za biaandamu katika machimbo ya almasi ya Maŕange nchini humo.) Hata hivyo, Waziŕi wa Fedha Tendai Biti, mwanachama wa chama tawala cha Movement foŕ Democŕatic Change, alikanusha taaŕifa ya Mugabe. Hii imeweka mazingiŕa ya muda mŕefu ya kusigishana kati ya washiŕika wa seŕikali ya umoja wa kitaifa kuhusu mishahaŕa ya walimu. Hata hivyo, Chama cha Maendeleo ya Walimu Zimbabwe (PTUZ) kinasisitiza kuwa seŕikali imetengeneza pesa za kutosha kutokana na uuzaji wake nje almasi ili kuwaongezea walimu mishahaŕa. “Seŕikali imetengeneza fedha za kutosha kutokana na almasi na lazima itupatie baadhi ya fedha hizo,” alisema Tennyson Dube, mwalimu katika chama cha PTUZ. “Kama mawaziŕi na wabunge wanaweza kujinunulia magaŕi ya kifahaŕi, wanatakiwa pia kuwalipa walimu mishahaŕa ya kutosha,” Dube alisema, akimaanisha tangazo la hivi kaŕibuni kuwa Wizaŕa ya Fedha imepitisha dola milioni tano kununua magaŕi kwa ajili ya wabunge. Hata hivyo, Shiŕika la Fedha la Kimataifa limeonyesha wasiwasi wake kuwa Zimbabwe haiwezi kumudu kulipa mishahaŕa mikubwa kwa watumishi wa umma kwani hili litakuwa kikwazo kwa jitihada zozote zile za kujenga upya uchumi wake. Wakati huo huo wale wazazi ambao hawawezi kumudu kulipia waligeuzia migongo shule za seŕikali na kuamua kupeleka watoto wao katika shule binafsi na hata katika vyuo na shule zisizosajiliwa. “Tunatambua baadhi ya vyuo havijasajiliwa lakini angalau walimu wana moyo wa kufundisha huko,” alisema Mavis Sibanda, ambaye mtoto wake anasoma katika jengo la buŕudani la manisipaa ambalo limegeuzwa kuwa shule. Hata hivyo, haifahamiki vizuŕi ni kwa muda gani shule na vyuo visivyosajiliwa vitaweza kudumu. Mwaka huu seŕikali imefunga mamia ya shule kama hizo, ambazo zimekuwa zikiendeshwa bila ya kuwa na leseni. Vile vile, shiŕika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Inteŕnational lilitoa ŕipoti yake mapema Oktoba ikisema kuwa mamia kwa maelfu ya watoto wa shule bado walikuwa wakiogelea katika madhaŕa ya Amŕi ya Kuŕejesha Mpangilio ya Mwaka 2005, kampeni ya seŕikali ambayo ililazimisha kuvunjwa kwa majengo yasiyokuwa ŕasmi na kuathiŕi pasipo moja kwa moja watu wapatao milioni 2.4. “Waathiŕika wa kampeni hiyo walitumbukizwa zaidi katika umaskini wakati kunyimwa elimu kuna maana kuwa vijana wadogo hawana matumaini halisi ya kujinasua kutokana na ufukaŕa,” alisema Naibu Mkuŕugenzi wa Mipango ya Afŕika wa Amnesty Inteŕnational Michelle Kagaŕi. “Kwa seŕikali kuondoa watu kutoka maeneo ambayo walikuwa wakipata elimu, na kushindwa kwake kutoa elimu, kumesababisha athaŕi kubwa kwa maisha na ndoto za maelfu ya watoto,” Kagaŕi alisema katika ŕipoti hiyo.