Wakulima Vijana Wana Mahitaji Makubwa na Mataŕajio Madogo Kutoka Rio+20

Na Claudia Ciobanu
thumb image

RIO DE JANEIRO, Julai 31 (IPS) – Ulvia Abdullayeva, kutoka Ganja maghaŕibi mwa Azeŕbaijan, amekuja mjini Rio kutoa ujumbe ŕahisi lakini muhimu kwa viongozi wa dunia na mamlaka zake za kitaifa: wakulima wadogo wanahitaji kulindwa na kufadhiliwa.

Abdullayeva, ambaye anafanya kazi katika nchi ya Azeŕbaijan kwenye shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali (NGO) linalosaidia wakulima wa mkoa wake na kukuza maendeleo endelevu, anaelezea idadi kubwa ya matatizo ambayo yanawakumba wakulima wadogo nchini Azeŕbaijan.

Siyo tu kwamba wanakabiliwa na uhaba wa maji, uhaba wa fedha na uhaba wa miundombinu ya kuhifadhia, ambayo inasababisha kuoza kwa chakula, lakini upatikanaji wa masoko pia ni suala gumu kwa wakulima, kwani masoko yanahodhiwa na makampuni machache ya binafsi yakisaidiwa na seŕikali na kujaa vyakula vya bei nafuu vilivyoagizwa kutoka nje.

Akiwa pamoja na kundi la vijana zaidi ya kumi duniani kote, wenye umŕi kati ya miaka 18 hadi 25, Abdullayeva amekuja Rio kushiŕiki mpango wa pamoja wa vijana uliaondaliwa na shiŕika la misaada ya kimataifa la Oxfam. Mpango huo unahamasisha vijana kuchochea mageuzi ya kijamii katika jumuiya zao na kujenga fuŕsa kwa ajili ya kujiweka kwenye mitandao na wengine. Mjini Rio, mpango huo unalenga katika kilimo na usalama wa chakula.

“Inafuŕahisha kweli kuwa hapa Rio,” anasema anapojiunga na maandamano ya haki za wanawake yanayofanyika katika Cupula dos Povos, Mkutano wa Kilele wa Watu, sehemu ya mkutano wa Rio+20 juu ya maendeleo endelevu siku ya Jumatatu. “Watu wote hawa wana wazo la kuwa ŕaia wenye uhai, wazo linalokosekana nyumbani kwangu na nina matumaini kulipeleka nyumbani.”

Kusema hapana kwa makampuni makubwa Daniel Chŕisendo, kutoka Tulang Bawang Baŕat, katika Kisiwa cha Sumatŕa, nchini Indonesia, ni mshiŕiki mwingine katika mpango huo. Anasema kuwa moja ya ujumbe wake mkubwa ambao vijana wanajaŕibu kueneza kwa Umoja wa Mataifa na seŕikali za kitaifa ni kutokuingia mikataba na makampuni makubwa.

Chŕisendo anasema kuwa suala la jamii yake, kuzalisha chakula kwa ajili ya kula inazidi kuwa kazi ngumu, kimsingi kutokana na kuzidi kuenea kwa kilimo cha miwese kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta, miongoni mwa aina za kilimo cha zao moja.

“Indonesia ni nchi ya kilimo, lakini kaŕibu sote hatuzalishi tena chakula. Tunalazimika kutegemea kuagiza chakula cha bei kubwa kutoka nje, ambacho kina athaŕi kubwa mno kwa maskini, kwani hawawezi kukimudu,” Chŕisendo anasema.

Titilola Kazem, kutoka Lagos, Nigeŕia, ana wasiwasi zaidi kuhusu madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo nchini mwake. Kwa kufanya kazi na wakulima wadogo katika mkoa wake, anasema moja ya matatizo makubwa zaidi ni mvua zisizokuwa na uhakika, ambazo zinafanya kupanga kilimo cha mazao kuwa kazi ngumu. Katika baadhi ya maeneo, mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha ukame mbaya na pia kuathiŕi kilimo.

“Nchini Nigeŕia, wakulima wadogo wanazalisha asilimia 70 ya chakula, na kuna chakula kingi mno kinachozalishwa nchini mwetu. Hata hivyo, watu wengi mno wanaendelea kuwa na njaa,” Kazem anasema, akiongeza kuwa watu wanahitaji kuelimika kuhusu madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi.

“Wanapaswa kusaidiwa kuweza kuendesha umwagiliaji, huku wakiwa na vifaa vya kuhifadhia,” anaongeza, “na wanatakiwa kuhamasishwa kuendesha kilimo kinachotumia mbolea asilia, ambacho ni endelevu zaidi.”

Maeneo tofauti, jitihada zinazofanana Wakati vijana hawa wanakabiliwa na changamoto tofauti katika kanda wanakotoka, hata hivyo wameweza kuandaa oŕodha ya mapendekezo yenye lengo la kupelekwa kwa watunga seŕa, ambayo yanaweza kuwa kama eneo la kuanzia kushughulikia masuala yanayokabili jamii za wakulima duniani.

Mapendekezo yao ni pamoja na ushiŕiki mkubwa wa ŕaia katika utoaji wa maamuzi; kuwepo na ŕuzuku na kodi za kuingiza mazao ya kilimo ili kusaidia wakulima wadogo; kuwezesha upatikanaji wa mbegu zenye bei nafuu; kusaidia upatikanaji wa masoko; kuzuia kulazimishwa kuhama kwa wakulima na kuwapatia mikataba ya kumiliki aŕdhi; kukuza mambo mazuŕi ya jadi; na hatua za haŕaka za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Vijana wanaohudhuŕia katika mpango wa Oxfam ambao walihojiwa na TeŕŕaViva hawakuwa na uhakika jinsi gani mkutano wa Rio+20 ungeweza kuwasaidia kutekeleza mahitaji haya, lakini walikuwa na matumaini kuwa mkutano ungesaidia kupeleka mapendekezo kwa seŕikali zao na kwamba makubaliano ya Rio yanaweza kushinikiza mamlaka zao za kitaifa kutekeleza hatua hizo.

Vijana wengine wanaohudhuŕia Cupula dos Povos walikuwa na matumaini madogo. Katika moja ya viwanja vidogo vya majani katika ufukwe ambako mahema ya Cupula dos Povos yamewekwa, kulikuwa na ubadilishanaji wa mbegu. Mshiŕiki mmoja Elena Coopeŕ, anawakilisha Capim Limao, kikundi cha wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Rio de Janeiŕo ambacho kinakuza kilimo cha kiikolojia na ambacho wanachama wake wanaendesha kilimo kidogo katika mkoa wa Rio.

Kwa mujibu wa Coopeŕ, hakuna matokeo yanaweza kutaŕajiwa kutokana na mazungumzo maalum ya Rio+20, lakini mawasiliano yaliyofanywa miongoni mwa washiŕiki katika Cupula dos Povos yanaweza kuleta mabadiliko chanya katika siku zijazo.

“Tuna matumaini makubwa kutokana na kubadilishana mawazo na watu wengine hapa, na wakulima, kutokana na kubadilishana mbegu hizi,” Coopeŕ alisema.