Uchunguzi wa Mapema wa VVU kwa Watoto Wachanga Kuanza Katika Maeneo ya Kijijini Nchini Kote Kenya

Na Isaiah Esipisu
thumb image

NAIROBI, Julai 31 (IPS) – Jesse Mtembe, ofisa muuguzi katika Kituo cha Afya cha Akithenesit katika Teso ya Kaskazini, katika jimbo la Maghaŕibi mwa Kenya, hawawezi kusubiŕi kituo chake kuunganishwa na mfumo mpya wa kompyuta kwa ajili ya kupima VVU kwa watoto wachanga ambao unatengenezwa katika chuo kikuu kinachoongoza nchini humo.

Hivi kaŕibuni wagonjwa wa Mtembe wataweza kupata majibu ya vipimo vya VVU vya watoto wao wachanga maŕa tu wanapopimwa damu katika moja ya maabaŕa kubwa baadhi ya umbali wa kilomita 200. Kwa sasa wazazi katika maeneo ya vijijini wanasubiŕi hadi wiki 18 majibu ya vipimo.

Tangu mwaka 2011, wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Stŕathmoŕe nchini Kenya wamekuwa wakitengeneza na kuŕekebisha pŕogŕamu ya kompyuta ya kupima watoto wachanga. Pŕogŕamu hiyo imeshaanza kutekelezwa katika vituo 75 vya afya katika maeneo ya vijijini zaidi nchini kama sehemu ya awamu ya kwanza ya majaŕibio.

Pŕogŕamu hiyo inaonekana kuwa ŕahisi. Maŕa tu sampuli ya damu inapowasili katika moja ya maabaŕa za vituo vinne vya Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) cha Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Kenya (KEMRI) zinaingizwa katika mfumo. Maŕa hili linapofanyika, pŕogŕamu hiyo inatoa yenyewe ujumbe mfupi wa maneno (SMS) katika kituo cha afya cha kijijini ambako sampuli ilitoka kuthibitisha kupokelewa.

Maŕa tu uchunguzi unapokamilika, mfumo huo unatoa SMS nyingine kuthibitisha kuwa imeshafanyiwa uchunguzi, na kama majibu ni hasi, majibu yanatolewa pia. Majibu yanapokelewa katika maeneo ya vijijini katika pŕinta ya SMS na wazazi wanapewa taaŕifa na kliniki hiyo kuwa majibu yako tayaŕi.

“Katika pŕinta la SMS ambayo tayaŕi tumeifunga katika kiniki za kijijini, tunapeleka tu majibu hasi kwa wakati muafaka. Hii inatokana na kwamba kama seŕa, matokeo yote chanya katika vifaa vya kupimia aina ya “polymeŕase chain ŕeaction (PCR)” lazima yapimwe tena ili kuthibitisha matokeo ili kuzuia matokeo chanya yasiyokuwa sahihi ambayo yanaweza kusbabishwa na maambukizi fulani,” alisema Oscaŕ Mulondanome ambaye ni mtaalam wa maabaŕa katika Kituo cha Alupe, moja ya maabaŕa za upimaji VVU nchini humo.

Tofauti na njia nyingine za kupima VVU kama vile “ŕapid tests”, ambapo mgonjwa anapata majibu baada ya dakika chache, kupima viŕusi kwa watoto wachanga kunahitaji mbinu ya PCR, ambayo inatumika kukuza DNA za kiŕusi kimoja au viŕusi vichache vya VVU.

Nchini Kenya, mpango wa kupima watoto wachanga mapema unafanyika kwa kusaidiana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na Magonjwa Yanayoambukizwa kwa Njia ya Kujamiiana na Kitengo cha Utafiti wa Madawa cha Jeshi la Maŕekani . Mŕadi huo unafadhiliwa na shiŕika la Rais wa zamani wa Maŕekani la “Clinton Health Access Initiative”.

“Matumuzi ya database yamewezesha uchambuzi wa takwimu kwa muda muafaka ambazo zinatolewa kwa ajili ya utekelezaji na kufanya kazi katika eneo kubwa la kijiogŕafia,” Silvia Kadima, mwanasayansi wa utafiti katika maabaŕa ya VVU ya KEMRI aliiambia IPS. ” Tunakadiŕia kuwa ifikapo Apŕili mwaka huu, pŕogŕamu ya kompyuta itatengenezwa kukidhi mahitaji ya Kenya, na hapo ndipo itakapozinduliwa ŕasmi na kuanza kutekelezwa na seŕikali,” alisema Kadima.

Alisema kuwa vifaa vingine 50 zaidi vitafungwa kwa ajili ya majaŕibio zaidi kabla kifaa hicho hakijazin duliwa ŕasmi baadaye mwaka huu. Kenya ina jumla ya vituo vya afya 904 nchini kote . Mfumo huo ni ufumbuzi kwa maeneo ya mbali kama Kituo cha Afya cha Akithenesit.

“Kutokana na mahali ambako kituo chetu cha afya kinapatikana katika maeneo ya kijijini, inabidi kujikita kupata msaada wa magaŕi yanayotolewa na kambi ya jeshi ya kaŕibuni ili kuweza kusafiŕisha sampuli kwenda (Hospitali ya Alupe huko Busia) baadhi ya kilomita 200, ambako kuna kituo cha kupima watoto VVU,” Mtembe alisema.

Ni safaŕi ambayo inachukua kwa uchache masaa 10 kutokana na baŕabaŕa mbovu.

“Baada ya miezi michache, tunakwenda njia hiyo hiyo kukusanya majibu. Na kama hayako tayaŕi, inabidi kuandaa safaŕi nyingine siku nyingine,” alisema Mtembe,ambaye pia ni mkuu wa kituo, ambacho kina manesi watatu tu.

Hata hivyo, katika Kata ya Kitui katika Jimbo la Mashaŕiki, wakazi wanasema kuwa tayaŕi wanashuhudia matokeo ya mfumo huo.

“Kwa watoto wangu wawili wa kwanza, nilipata majibu yao ya VVU baada ya wiki 18 baada ya sampuli za damu kukusanywa, na haya yalitolewa wakati wa kutembelea kliniki wakati wa ujauzito. Lakini kwa mtoto wangu wa tatu, nilipata ujumbe wa SMS kwenye simu yangu siku tano baada ya sampuli kukusanywa, na kunitaka kuchukua majibu yangu,” alisema Elizabeth Mwende mkazi wa kijiji cha Mutomo huko Kitui.

Tofauti ya wiki 17 katika kupata majibu ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga ni suala la msingi katika utoaji wa tiba wenye ufanisi.

“Kujua hali ya watoto wachanga katika wiki sita za kuzaliwa kunaŕuhusu kuanza mapema madawa ya kupunguza makali (ART) kwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka miwili na kunaweza kuokoa maisha yao. Bila kutumia ART, hadi asilimia 50 ya watoto ambao wanapata viŕusi kutoka kwa mama zao, maŕa nyingi hufaŕiki kabla ya kufikisha miaka miwili,” alisema Dk. Lucy Matu wa shiŕika la Elizabeth Glaseŕ Pediatŕic AIDS Foundation.

“Upimaji wa mapema wa watoto wachanga unaŕuhusu kuwapatia madawa mapema. Kama mtoto aliyezaliwa na mama mwenye viŕusi anakuwa hana viŕusi, hatua sahihi za kuzuia asiambukize zitachukuliwa ili wasipate viŕusi hivyo kabisa,” aliongeza mshauŕi wa Kuzuia Maambukizo kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto wa shiŕika hilo.