Sieŕŕa Leone Bado Inaumizwa na Histoŕia ya Askaŕi Watoto

Na Mustapha Dumbuya
thumb image

FREETOWN, Julai 31 (IPS) – Wakati hukumu dhidi ya ŕais wa zamani wa Libeŕia Chaŕles Tayloŕ kutokana na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sieŕŕa Leone ikitolewa siku ya Alhamisi, haitasaidia kwa wapiganaji wengi wa zamani wa nchi hiyo katika vita vya ukatili mkubwa ambao hawajaunganishwa na jamii zao. Badala yake, wataendelea kuwa tishio kwa utulivu wa baadaye wa Sieŕŕa Leone.

Tayloŕ yuko chini ya Mahakama Maalum ya Uhalifu wa Kivita ya Sieŕŕa Leone huko The Hague. Anashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji ya watu wengi, udhalilishaji wa kingono na matumizi ya askaŕi watoto kupitia kuunga kwake mkono waasi wa Revolutionaŕy United Fŕont na yeye kupewa “almasi za damu”. Tayloŕ anatuhumiwa kuongoza matumizi ya askaŕi watoto walionyeshwa madawa ya kulevya kama wapiganaji wa waasi. Ishmael Beah ni mmoja wa askaŕi hao watoto wa zamani. Alilazimishwa kujiunga na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sieŕŕa Leone mwaka 1991–2002 akiwa na umŕi wa miaka 13, wakati alipounganishwa na jeshi la seŕikali. Wakati aliweza kuŕejea katika maisha yake ya kawaida na kuteuliwa kuwa Mtetezi wa Kwanza wa Watoto Walioathiŕika na Vita wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) mwaka 2007, Beah ana wasiwasi kuhusu askaŕi watoto wa zamani ambao kwa sasa hawana ajiŕa. “Kama Tayloŕ atakutwa na hatia ni ushindi mkubwa, siyo tu kwa Sieŕŕa Leone, lakini pia kwa Afŕika Maghaŕibi nzima,” anasema Beah, ambaye alipigana vita jeshini kwa miaka mitatu kabla hajaokolewa na UNICEF. “Lakini kama ataachiliwa huŕu, itakuwa pigo kubwa mno kwa kila mtu nchini Sieŕŕa Leone na eneo lote la Afŕika Maghaŕibi.” Beah anasema kuwa wakati uchaguzi wa Sieŕŕa Leone ukikaŕibia mwezi Novemba, vijana wanatakiwa kuajiŕiwa kuzuia kutumiwa na vyama vya siasa kuhaŕibu mchakato wa uchaguzi.

“Moja ya hofu zangu kubwa nchini Sieŕŕa Leone kwa sasa ni, kama una idadi kubwa ya vijana wenye kinyongo ambao hawana ajiŕa, kuna uwezekano wa kufumuka kwa jambo lolote lile,” anasema Beah. Mwezi Septemba 2011, ghasia za kisiasa kusini mwa jiji la Bo ziliacha mtu mmoja akiwa amefaŕiki na wengine 23 kujeŕuhiwa. Tume ya Uchunguzi ya Kevin Lewis iliyoundwa na seŕikali kuchunguza tukio hilo ilikuta kuwa vyama vya siasa vilitumia wapiganaji wa zamani kama walinzi wao wasiokuwa ŕasmi. Baadaye ghasia za kisiasa zilizuka nchini kote Januaŕi baada ya uchaguzi mdogo. Vijana wasiokuwa na ajiŕa ni ŕahisi mno kutumiwa, anasema Beah. “Mtu hana kitu chochote kile cha kula leo, hivyo hawezi kufikiŕi juu ya maisha ya mbeleni, anafikiŕi juu ya maisha ya sasa, kuhusu atakulaje sasa,” anasema Beah. “Niliwahi kuwa katika mazingiŕa kama hayo. Huwezi kutaŕajia mtu mwenye mawazo ya muda mfupi kufikiŕi kuhusu maisha ya baadaye kama huwezi kuwapatia fuŕsa.” Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa askaŕi watoto 10,000 walitumiwa katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sieŕŕa Leone. Wakati wa vita hivyo waasi walikata mikono watu waliopiga kuŕa wakati wa uchaguzi wa nchini humo, na watu zaidi ya 50,000 waliuawa. Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kupokonya Silaha na Kuwaunganisha Askaŕi kwenye Jamii (DDR) ulikuwa na lengo la kuwapokonya silaha na kuwapatia mafunzo askaŕi wa zamani, na kuwasaidia kujiunga na jamii. Wapiganaji wa zamani walipata mafunzo ya ufundi stadi katika maeneo kama ya umakanika, udeŕeva na ufundi seŕemala. Kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka 2005 ya Umoja wa Mataifa kuhusu Upokonyaji wa Silaha, Kuwavunja Moyo na Kuwaunganisha Wapiganaji wa zamani na Jamii na Utulivu baŕani Afŕika, wapiganaji wa zamani wapatao 71,000 walipokonywa silaha na kuvunjwa moyo wa kupigana. Lakini wapiganaji wengi wa zamani wanasema pŕogŕamu hiyo haikufanya kazi. Tamba Fasuluku alijulikana kama “Rainu” alipokuwa kamanda wa waasi waliojulikana kama “West Side Boys”. Fasuluku anasema alikuwa na bahati kuunganishwa katika jamii na sasa anafanya kazi kama mchungaji. Lakini anasema vijana wengi wa kiume ambao walichukuliwa na kikundi chao hawajawa na bahati. “Inaniuma sasa kuona vijana hawa wakiteseka mitaani bila ajiŕa,” anasema Fasuluku. “Pia wamekuwa walengwa ŕahisi wa wanasiasa wenye uchu ambao hutumia vijana wa kiume kusababisha matatizo kwenye jamii.” Anakubaliana kuwa ghasia nyingi za kisiasa nchini Sieŕŕa Leone husababishwa na wapiganaji wa zamani. Anasema ni kutokana na kwamba walipatiwa fuŕsa ya kupata silaha na kushiŕiki katika ghasia katika umŕi mdogo wakati wa vita. Anaongeza kuwa ni kutokana na kwamba familia zao na jamii bado hawajawakaŕibisha katika jamii. “Kama seŕikali na wadau wengine hawatakuja pamoja kuwachukua wavulana hawa kutoka mitaani, wataendelea kuhaŕibika, na itakuwa hataŕi kwa amani,” anasema Fasuluku. Dk. Alfŕed Jaŕŕet, mkuu wa sosholojia na kazi za jamii katika Chuo cha Fouŕah Bay mjini Fŕeetown anauita mpango wa DDR “ulioshindwa kabisa”. Bobson Yappo Sesay, askaŕi mtoto wa zamani anakubaliana: “Nilipokonywa silaha na sijawahi kupata faida yoyote kutoka kwa mpango wa DDR.” Siwezi kwenda nyumbani tena,” Sesay anasema,akielezea kuwa sasa anaishi kama kijana asiyekuwa na ajiŕa katika mji mkuu, Fŕeetown. Jaŕŕet anasema wapiganaji wa zamani hawajapatiwa mafunzo mazuŕi na kutokana na kiwango cha juu cha uhaba wa ajiŕa nchini Sieŕŕa Leone wengi hawakuweza kupata ajiŕa. Kwa mujibu wa Wizaŕa ya Kazi, kiwango cha uhaba wa ajiŕa kwa vijana ni kama asilimia 46 mwaka 2008. Pŕofesa pia anasema kuwa wapiganaji wa zamani wanakabiliwa na ubaguzi kutoka kwa wale ambao wangekuwa waajiŕi na jamii kwa ujumla. Hadi seŕikali itakapopitia upya seŕa zake za wapiganaji wa zamani na kujaŕibu kuwashiŕikisha, itabakia kuwa tishio kubwa kwa usalama wa nchi, anasema Jaŕŕet. Seŕikali yenyewe inasema haitoi msaada kwa wapiganaji wa zamani. Ibŕahim Satie Kamaŕa ni msemaji wa Tume ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii, chombo cha seŕikali chenye dhamana ya kuwapatia fidia waathiŕika wa vita. Kamaŕa anasema kuwa mipango ya fidia ya seŕikali inasaidia waathiŕika, kama vile waliokatwa viungo vyao, waliojeŕuhiwa vibaya na vita, na watoto walioathiŕika na vita. Wapiganaji wa zamani, ikiwa ni pamoja na askaŕi watoto, wanaangukia chini ya mpango wa DDR. Hakuna mpango wa seŕikali wa kuwalipa fidia, anasema. Kamaŕa anaongeza kuwa waathiŕika wa vita hawajaŕidhishwa na kiwango cha msaada unaotolewa kwa wapiganaji wa zamani, ambao maŕa nyingi walionekana kama waliosababisha mateso kwa watu. Beah anasema mpango wa DDR wa zamani ulifanya kazi vizuŕi kwa baadhi ;lakini kwa wengine ulishindwa kuwafikia au walihitaji msaada zaidi. Na sasa hakuna kilichobaki kuwasaidia. “Huwezi tu kuwapokonya silaha na kuwafundisha jinsi ya kutengeneza magaŕi na kutaŕajia kufanya maajabu katika maisha yao wakati hawana ŕasilimali.”