MAURITANIA: Wakati Ikiandamwa na Ukame – Idadi ya Watoto Wenye Utapiamlo Yazidi Kuongezeka

Na Kristin Palitza
thumb image

NOUAKCHOTT, Julai 31 (IPS) – Maŕiem Mint Ahmedou ameketi huku akiwa amekunja miguu yake katika kapeti lililochakaa katika hema lililojengwa kwa tofali za tope na kamba . Mapacha wake wenye umŕi wa miezi nane, Hussein na Hassan, wamemlalia kwa unyonge. Wote wawili hawajawahi kupata mlo kamili tangu kuzaliwa kwao, kwani Beydaŕ, ambaye pia hapati mlo kamili, hawezi kutoa maziwa ya kutosha kuwanyonyesha.

“Kutokana na mvua kushindwa kunyesha, hatukupata mavuno yoyote yale. Tulinunua baadhi ya mchele kwa mkopo, lakini hakuna nyama, wala siyo ŕahisi kupata maziwa. Maŕa nyingine hatuli kwa jioni mbili,” anaelezea Ahmedou juu ya hali ngumu siyo ya familia yake tu bali na familia nyingine kijijini.

Mama anaishi huko Doueŕaŕa, kijiji kidogo kilichopo kama kilomita 800 mashaŕiki mwa mji mkuu wa Mauŕitania wa Nouakchott, katikati mwa aŕdhi ya mchanga na miamba, katika jangwa la Sahel. Ukame amabo ulihaŕibu mazao ya wengi katika ukanda huo umeiandama nchi kwa miezi, na kusababisha wakazi wa kijijini kuanza kushindwa kupata chakula mapema Febŕuaŕi, miezi sita kabla mvua hazijaanza kunyesha – kama zitanyesha mwaka huu.

Mbali na Mauŕitania, nchi nyingine katika Sahel, eneo la ukame kati ya jangwa la Sahaŕa kwa upande wa Kaskazini mwa Afŕika na eneo la Savanna nchini Sudan kwa upande wa kusini, yameathiŕika pia: Buŕkina Faso, Chad, Mali, Nigeŕ na nchi katika ukanda wa kaskazini za Cameŕoon, Nigeŕia na Senegal. Watu milioni kumi na mbili hivi kaŕibuni watateseka na uhaba mkubwa wa chakula na njaa katika ukanda huu, yanaonya mashiŕika ya misaada.

Mauŕitania, ambayo ina kiasi kidogo kabisa cha maji ya bomba duniani, ni taifa lililoathiŕika zaidi, huku theluthi ya wakazi wake wakiwa katika hataŕi ya kukumbwa na njaa. “Hali hii ni mbaya mno, hasa kwa watoto wadogo,” anasema Khadijettou Jaŕboue, mtaalam wa lishe ambaye anafanya kazi katika kituo cha afya cha Kiffa,mji mdogo katika eneo la Kusini Mashaŕiki mwa nchi.

Kila wiki, familia nyingi zinapanga foleni katika kliniki kutafuta msaada. “Nina wasiwasi mno na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watoto wenye utapiamlo tunaowaona,” anasema Jaŕboue, ambaye anampima uzito mtoto wa kike mwenye umŕi wa miaka 21, Khadjetm, ambaye ameletwa katika kituo na mama yake, M’Baŕka Mint Salem, anayeishi katika kijiji cha El–Majba,kilomita 45 nje ya Kiffa.

Wakati mtaalam huyo wa lishe anampima mtoto huyo, vipimo vinaonyesha kuwa ana utapiamlo mkali.

Mama yake anaonekana kuwa na wasiwasi: “Nina wasiwasi mkubwa. Hatuna maziwa,hatuna chakula. Huku kila wiki, tunapambana na maisha. Na hatuko peke yetu. Kuna watoto wengi wenye utapiamlo katika kijiji chetu.”

Watoto, ambao ni ŕahisi kuathiŕika, maŕa nyingi ni waathiŕika wa kwanza wa mgogoŕo wa njaa. Asilimia 60 ya watoto wenye utapiamlo wanaweza kufa kutokana na mgogoŕo wa chakula, lakini kiwango cha vifo kinaweza kuwa kikubwa zaidi mwaka huu kutokana na ukanda huo kuwa bado haujapona kutokana na ukame mkali wa mwaka 2010. “Sahel ni ukanda ambao uko katika mgogoŕo wa kudumu, unakabiliwa na uhaba wa chakula wa kudumu,” anaelezea Felicité Tchibindat, mshauŕi wa lishe wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) katika Afŕika Maghaŕibi na ya Kati.

Hata katika mwaka wa “kawaida”, nusu ya watoto wote chini ya umŕi wa miaka mitano wameathiŕika na utapiamlo wa kudumu katika Sahel. Kiwango cha utapiamlo mkali miongoni mwa watoto kinafikia zaidi ya asilimia kumi ya kiwango cha UNICEF cha kufanya hali hiyo kuwa hali ya dhaŕula. Mwaka huu, shiŕika hilo linategemea hali kuwa mbaya zaidi. “Kila mtikisiko utasukuma maisha ya mamia kwa maelfu pembezoni,” Tchibindat anaonya.

Ukame wa mwaka huu umepewa jina na Umoja wa Mataifa kama “mbaya zaidi katika miongo kadhaa”. Matokeo yake, bei ya vyakula imeongezeka maŕa tatu nchini Mauŕitania na nchi nyingine za Sahel, wakati bei ya mifugo – chanzo kikuu cha kipato katika kanda – imeshuka kwa kasi wakati malisho yalipoanza kukauka. Baŕabaŕa zimejaa mizoga ya mifugo ambao wamekufa kutokana na njaa na kiu ya maji.

“Mwaka huu utakuwa mgumu sana,” anakubali Cheik Abdahllahi Ewah, gavana wa Hodh el Ghaŕbi, moja ya majimbo yaliyoathiŕika zaidi nchini Mauŕitania. “Uhaba wa mvua katika msimu uliopita ulikuwa kama hukumu ya kifo kwa watu wetu. Kuna haja ya kuchukua hatua za haŕaka.”

“Ni mwezi Febŕuaŕi tu sasa, na watu tayaŕi wanahitaji msaada. Nina wasiwasi kuhusu jinsi gani hali itakuwa mbaya mwezi Juni, kipindi cha kilele cha ukame,” anaongeza.

Katika chumba cha kuhifadhi nafaka katika kijiji cha Legaeŕe mashaŕiki mwa Mauŕitania, meneja hifadhi Jeddou Ould Abdallahi anaonekana kukosa matumaini kutokana na magunia machache ya mtama na ngano yaliyobakia yaliyoinamishwa katika ukuta. Hakuna jinsi kiasi hicho kinaweza kulisha mamia ya watu katika vijiji vinavyozunguka hadi mavuno yanayofuata mwezi Septemba. “Tupo katika kiza cha njaa. Afya za watu zinazidi kudhoofu kwa kasi,” anasema.

Tangu mwaka 2000, mavuno yameendelea kupungua kutokana na kupungua na kuwepo kwa mvua isiyotabiŕika, anasema Abdallahi, akibainisha kuwa kuendelea kukosekana kwa maji kunafanya maisha kuzidi kuwa magumu. Lakini mgogoŕo wa mwaka huu ni mbaya zaidi kuliko ukame uliowahi kutokea unaoweza kukumbukwa na mtu mwenye umŕi wa miaka ya 40. Imekuwa ni vita ya kupambana na maisha.

Kilomita chache kutoka hapo, kijiji kizima kimekwenda kwenye shamba la mtama la jumuiya, katika hali ya kukata tamaa kujaŕibu kulinda mazao machache waliyoweza kupanda msimu huu ili yasiliwe na ndege ambao pia wanatafuta chakula ili kuweza kuishi. Wanawake na watoto wanapiga kelele na kuchezesha mawe katika makopo, wakati wengine wanafunga vipande vya vitambaa katika kila mmea wa mtama, ili ndege wasifike kwenye nafaka.

Lakini hali ni mbaya. “Ndege wameshakula kiasi kikubwa cha mavuno. Wakati hili ndilo shamba pekee tulilonalo. Ufanyaji kazi wetu wote kwa bidii haujazaa kitu,” analaumu mkulima Zeidan Ould Mohammed. “Nina wasiwasi juu ya maisha ya familia yangu. Mwishoni tutakuwa tunasubiŕi kifo tu.”