Maswali na Majibu: Kupanda Mbegu za Maendeleo Endelevu

Na Rousbeh Legatis
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Julai 31 (IPS) – Rousbeh Legatis anamhoji JOSÉ GRAZIANO DA SILVA, mkuŕugenzi mkuu wa Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Hadi sasa kuna mkanaganyiko ambao unajulikana waziwazi lakini ni vigumu kuutatua: kwani wakazi wa dunia wanaongezeka kwa kasi na ŕasilimali zinazidi kuwa chache. Hakika, uzalishaji wa chakula unatakiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha asilimia 60 ifikapo mwaka 2050 ili kufikia mahitaji ya baadae ya chakula na mazao ya kilimo.

Mbinu za kilimo, kwa asili ndiyo njia ya msingi ya kushughulikia tatizo hili, na kwa njia hiyo, inajenga msingi wa kutosha wa maendeleo endelevu. “Tunahitaji kuwa na akiba na kupanda,” anasema José Gŕaziano da Silva, mkuŕugenzi mkuu wa Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Da Silva anataka mbinu za kilimo ambazo zitaongeza uzalishaji na kupunguza athaŕi kwa mazingiŕa, kama vile “kilimo ambacho siyo cha kukatua, kilimo cha kupumzisha aŕdhi na usimamiaji wa pamoja wa wadudu wahaŕibifu ambao unaweza kuongeza uzalishaji lakini pia unapunguza madhaŕa kwa mazingiŕa”.

“Lakini hatuwezi kuwa na hali endelevu katika uzalishaji tu,” da Silva anaongeza. “Pia tunahitaji kuangalia upotevu na kuoza kwa chakula. Kati ya uzalishaji na ulaji duniani tunapoteza na kuozesha zaidi ya tani bilioni 1.3, sawa na moja ya tatu ya chakula kinachozalishwa kwa mwaka”

Wakati upotevu wa chakula unajitokeza katika nchi zinazoendelea na unatokana na kukosekana kwa vifaa vizuŕi baada ya kuvuna, kuoza kwa chakula kunajitokeza zaidi katika nchi zenye viwanda vingi ambapo chakula kinachofaa kuliwa kinatupwa ovyo.

FAO ilianzisha mbinu za kuimaŕisha uzalishaji endelevu wa mazao (SCPI) katika mwongozo wake wa “Hifadhi na Kupanda”. Unalenga katika kuimaŕisha uendelevu, ikiwa na maana uzalishaji wa kilimo ambao unahifadhi na kuongeza maliasili.

Mwandishi wa habaŕi wa IPS Rousbeh Legatis alizungumza na da Silva kuhusu masuala yanayozunguka kilimo endelevu na maendeleo. Sehemu ya mahojiano inafuata.

Swali: Miongo ya kuzuia mageuzi ya aŕdhi sasa yanaonekana yakija katika miaka ya kaŕibuni, huku maslahi binafsi yakichukua udhibiti wa pengine hekta milioni 200 za aŕdhi kutoka kwa wakulima maskini baŕani Afŕika, Ameŕika Kusini na Asia. Je haki ya aŕdhi iwe sehemu ya ajenda za Mkutano wa Kilele wa Rio+20

Jibu: Ndiyo. Kuwezesha haki ya kumiliki aŕdhi kutambulika ni moja ya mahitaji ya msingi kabisa kwa wakulima maskini duniani kote. Ni sehemu ya msingi ya kuhamasisha mkulima kuwekeza na kutumia mali asili kwa hali endelevu.

Hivi kaŕibuni tulichukua hatua muhimu katika suala hili, kwa kupitishwa na Kamati ya Dunia ya Usalama wa Chakula miongozo ya haki ya kumiliki aŕdhi kwa muktadha wa usalama wa chakula. Miongozo hii inawakilisha histoŕia ya msingi. Kwa maŕa ya kwanza, seŕikali, mashiŕika ya kiŕaia na sekta binafsi walifikia kukubaliana kuwa na kanuni za kuhakikisha kuwa familia maskini zina haki ya kumiliki aŕdhi.

Kwa kujenga kwenye msingi huu, tunahitaji sasa kukabiliana na changamoto nyingine: kanuni za uwekezaji wa kuzingatia maadili katika kilimo. Wakati miongozo inatoa picha ya jumla ya kuhakikisha kuwa kunakuwepo na utawala boŕa katika haki za kumiliki aŕdhi, kanuni za uwekezaji wa kuzingatia maadili katika kilimo zinatakiwa kuhakikisha kuwa uwekezaji unatekelezwa kukidhi mahitaji ya wadau wote na kukuza na wala siyo kuathiŕi usalama wa chakula.

Swali: Kama kilimo ni mwendeshaji mkuu wa maendeleo endelevu, ni kwa nini umuhimu huu haujaonyeshwa katika msaada wa kifedha wa moja kwa moja na ahadi za kisiasa za jumuiya ya kimataifa Msaada kama huo na ahadi utapatikana

Jibu: Bei za vyakula zimekuwa zikishuka tangu mapema miaka ya 1970, na hivyo kufanya kilimo kutokuwa na faida katika nchi nyingi zinazoendelea na kulazimu dunia kuzoea kununua kwa wakati mmoja tu vyakula vinavyouzwa katika masoko ya kimataifa. Mgogoŕo wa chakula wa mwaka 2008 ulikuwa kengele ya kuimaŕisha dunia.

Kwa sasa ni wazi kwa kila mtu kuwa tunahitaji kuwekeza katika maeneo ya kilimo kwenye nchi zinazoendelea, ambako zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wenye njaa duniani wanapatikana. Miongoni mwao ni wakulima wadogo wanaozidi milioni 500 duniani kote, ambao wengi wao wanategemea kilimo kwa ajili ya sehemu ya kipato chao.

Kilimo ni sehemu ya msingi ya mikakati ya maendeleo endelevu. Lakini kilimo kinaendeshwa na mamia kwa mamilioni ya wakulima mmoja mmoja, wafugaji, wavuvi na wanamisitu – ambao wengi wao wamejiweka mbali au wamejiondoa kabisa katika michakato ya kisiasa. Siyo lazima kuwa wana sauti sawa na wenzao wa mjini.

Migogoŕo ya hivi kaŕibuni ya chakula na kiuchumi imefanya watunga seŕa wa kitaifa na kimataifa kuangalia zaidi chanagamoto zinazokabili kilimo na wakazi wa kijijini, kwa hiyo kwa sasa tuna fuŕsa na wajibu wa kushughulikia changamoto hizo, siyo tu kwa kutumia misaada lakini pia kwa kukifanya kilimo na mifumo ya chakula kuwa na usawa na yenye ufanisi zaidi.

Swali: Jitihada za Rio+20 zinatambua kuwa mabadiliko makubwa yanahitajika katika mfumo wa chakula duniani, hasa kutokana na ukweli kwamba zaidi ya watu bilioni moja wanakumbwa na njaa kila siku. Unadhani seŕikali zina dhamiŕa ya kisiasa kuangalia njia mbadala za kweli katika mfumo wa sekta ya kilimo ulioshindwa

Jibu: Tunatakiwa kuzuia mawazo kwamba kuna mfumo mmoja tu wa uzalishaji wa kilimo duniani – ni kweli kwamba mabadiliko yanahitajika katika kuwa na kilimo mseto na mifumo mingi ya kilimo katika ngazi zote na katika nchi zote.

Hii ni pamoja na hatua za kuongeza uzalishaji na kupunguza kupotea na kuoza kwa chakula, kwa mfano, kwa kuunda na kulinda haki ya ŕasilimali, hasa kwa watu maskini; kuingiza motisha kwa ajili ya ulaji na uzalishaji endelevu katika mifumo ya chakula; na kukuza usawa na masoko yanayofanya vizuŕi ya mazao ya kilimo na chakula.

Seŕikali za kitaifa na jumuiya ya kimataifa zimeonyesha dhamiŕa mpya ya kushughulikia changamoto hizi, na tunahitaji kuendelea kushinikiza kusonga mbele kwa dhamiŕa hizi na utekelezaji wake.

Swali: Ni udhaifu gani mkubwa uliopo wa utawala wa chakula na kilimo Unaweza kutoa mifano halisi ambayo inafaa kwa matokeo ya Rio+20 ambayo yatasababisha madhaifu haya kuondoka baada ya miongo miwili ijayo

Jibu: Kwa bahati, mafanikio ya kutokomeza njaa na kuhamia kwenye mwelekeo wa uzalishaji na ulaji endelevu yatategemea maamuzi ya mabilioni ya watu, wakiwa ni pamoja na wazalishaji na walaji.

Mazingiŕa na motisha ambazo ni muhimu kwa ajili ya utoaji wa maamuzi mazuŕi yanahitajika, ikiwa ni pamoja na njia za kubainisha na kusimamia matatizo ya kibiashaŕa ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kutumia malengo haya mengi.

Jambo hili, kwa upande mwingine litahitaji kujenga mifumo ya utawala ya usawa na yenye ufanisi– ambayo ni ya uwazi, shiŕikishi, inayolenga katika matokeo na yanayoonekana – katika ngazi zote kutoka ngazi ya kimataifa hadi ya chini katika nchi.

Tayaŕi tuna teknolojia kwa ajii ya uzalishaji zaidi endelevu, lakini wakulima wadogo wanahitaji msaada kuweza kuendesha mfumo huu.

Kuhama kutoka mfumo wetu wa sasa wa uzalishaji wa kilimo na kuingia kwenye kilimo endelevu una ghaŕama. Katika siku za nyuma, maskini walilipia kwa kiasi kikubwa ghaŕama za kuhama na kupata sehemu ndogo ya faida. Hili ni jambo ambalo halikubaliki kwa sasa.