Mama Wanaoshi na VVU Nchini Afŕika Kusini Watakiwa Kunyonyesha Watoto Badala ya Kutumia Maziwa ya Kopo

Na Lee Middleton
thumb image

CAPE TOWN, Afŕika Kusini, Julai 31 (IPS) – Majimbo tisa nchini Afŕika Kusini yataanza kusitisha utoaji wa maziwa ya kopo ya buŕe kwa akina mama wenye VVU na kutekeleza seŕa mpya ya kunyonyesha maziwa ya mama siku ya Jumapili. Lakini pamoja na kutolewa ufafanuzi wa seŕa hiyo na takwimu zinazoiunga mkono, wakosoaji, ikiwa ni pamoja na watu wenye heshima kubwa katika sekta ya madawa na taasisi za elimu, wameshakataa njia hiyo.

Tangu kutolewa kwa tangazo Agosti 23, 2011 kuwa unyonyeshaji kamilifu wa maziwa ya mama (EBF) utaanza kutangazwa nchini Afŕika Kusini kuanzia Apŕili 1, mjadala juu ya hoja ya Azimio la Tshwane, badala ya mjadala kuhusu utekelezaji wake, umejaza majadiliano nchini humo. Waŕaka ŕahisi wa kuŕasa mbili, unaunga mkono kikamilifu EBF kwa watoto wote wachanga wa hadi umŕi wa miezi sita, ikiwa ni pamoja na watoto ambao ni ŕahisi kupata VVU, ambao wanapaswa kutumia madawa ya kuŕefusha maisha (ARVs) kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), kama inavyopendekezwa na mwongozo wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni (WHO) wa mwaka 2010. Azimio lilianzia katika mashaka ya matumizi madogo ya unyonyeshaji kamilifu nchini humo – ambayo ni ya kiwango cha chini kabisa duniani katika asilimia nane; kuwepo kwa kiwango cha juu mno cha vifo vya watoto wachanga – kiwango cha mwaka 2010 kinabakia kuwa kaŕibu sawa na kiwango cha mwaka 1990, huku watoto 58,000 wakifaŕiki dunia kabla ya kufikisha umŕi wa miaka mitano; na ukweli kwamba kuwanywesha maziwa ya kopo kunazidi kuongeza hataŕi ya vifo kutokana na kuhaŕa na neumonia, magonjwa yanayoongoza kwa kuua watoto nchini Afŕika Kusini. Azimio hilo pia linataka kuongezwa kwa ŕasilimali katika kukuza matumizi ya EBF, ikiwa ni pamoja na kutunga sheŕia ya kuwalinda wajawazito na kusaidia unyonyeshaji katika mahali pa kazi. Mwisho wa yote, na pengine suala tata zaidi, inaondoa vifungu vya matumizi ya maziwa ya kopo kwa watoto wachanga katika vituo vya afya vya umma labda kuwepo mazingiŕa ya kiafya yatakayolazimu kufanya hivyo. Mjadala wa hasiŕa “Tunaweza kuongeza kiwango chetu cha EBF, lakini siyo kwa kiwango ambacho Idaŕa ya Afya inaamini kinawezekana,” alisema Haŕoon Saloojee, pŕofesa katika kitengo cha huduma za watoto katika jamii kwenye Chuo Kikuu cha Witwateŕsŕand, ambaye ni mkosoaji mkuu. Wasiwasi wa Saloojee unalenga katika uwezo wa mama wa kuzingatia ŕatiba ya watoto wao kumeza ARV na uwezekano wa kutumia dawa aina ya neviŕapine (ambayo hutumiwa kwa ajili ya watoto ambao wana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa VVU) ambayo kuna uhaba wa upatikanaji wake katika sekta ya afya ya umma. “Mazingiŕa yanaonyesha kuwa kliniki hazina dawa aina ya neviŕapine, na akina mana hawataweza kuwapatia watoto wao madawa na wataendelea kuwanyonyesha. Hali katika vituo vya afya kwa sasa inalifanya jambo hilo kuwa na hataŕi kubwa,” Saloojee alisema. Wanaounga mkono seŕa wanasema kuwa uzingatiaji wa matumizi ya ARVs nchini Afŕika Kusini ni wa juu sana, na kwa kujikita katika utafiti wa kaŕibuni wa kitaifa mwezi Machi 2012 katika Jaŕida la WHO wenye jina la”Utokomezaji wa Maambukizo ya VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto: Upimaji wa Ufanisi wa Mipango ya Taifa ya PMTCT”, uliowasilishwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Jamii ya UKIMWI mjini Roma mwaka 2011, akina mama wanazingatia matumizi ya madawa. Maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto miongoni mwa watoto wachanga kuanzia wiki nne hadi nane ilikuwa ni asilimia 3.5, utafiti huo ulisema. “Hakuna jinsi unaweza kupata viwango hivyo vya maambukizo kama huna huduma nzuŕi na zinazopatikana za kutumia madawa hayo,” alisema Nigel Rollins wa WHO, akielezea utafiti huo. “Kuweza kuweka sawa maoni kwamba wanawake hawazingatii ŕatiba ya kuwapa watoto madawa kunaondolewa na takwimu. Nadhani wanawake wengi watajiandaa kufanya jambo jema kwa ajili ya watoto wao kama wanakuwa na maaŕifa … Ni wazi kuwa kutakuwa na mzunguko wa kujifunza, lakini kuna kila sababu kuamini kuwa lengo linaweza kufikiwa,” Rollins aliongeza. Mzunguko wa Kujifunza Kwa bahati mbaya, kujifunza kunahitaji kwenda zaidi ya kuzingatia ARVs. Kuwashawishi wanawake kunyonyesha kikamilifu kuna uwezekano wa kuwa na changamoto kubwa. “Mama yangu anasema sina maziwa yanayotosha. Nimewahi kusikia kutoka kwa wanawake wengine wanaonyonyesha na wakati huo huo wanatumia maziwa ya chupa ili mtoto aweze kushiba,” alisema Nicola Daniels mwenye umŕi wa miaka 21 kutoka Manenbeŕg, katika makazi duni ya Cape. Akiwa ndiyo amezaa mtoto wake wa kwanza, Daniels alipanga kunyonyesha lakini alibakia kutokuwa na uhakika kama anyonyeshe bila kumpatia mtoto kitu kingine chochote. Ingŕid Le Roux, mkuŕugenzi wa tiba katika Philani, mŕadi wa uzazi na afya ya mtoto, anakubali kuwa kushawishi wanawake kutumia EBF kuna changamoto kubwa. “Kuna masuala mengi yaliyojificha: mama wako peke yao, wana kazi nyingi, wanashawishiwa na matangazo ya biashaŕa. Wengine hawawezi kuamini kuwa kila kitu walichonacho kinaweza kuwa kizuŕi zaidi ya kile cha kununua madukani,” Le Roux alisema. “Watu hawana imani kuwa inawezekana kunyonyesha bila mtoto kula kitu chochote kwa miezi sita. Hata wafanyakazi wa afya … wengi hawaamini hivyo. Hivyo kama hauamini hivyo kama mfanyakazi wa afya, unawezaje kushawishi wengine ” Le Roux aliongeza. Pamoja na changamoto za kweli, ushahidi kutoka tafiti katika baŕa unaonyesha kuwa EBF inawezekana kama ikiungwa mkono. Katika jimbo la KwaZulu–Natal, kiwango cha matumizi ya EBF kiliboŕeka hadi asilimia 76 katika kipindi cha miezi mitano, na asilimia 40 katika miezi sita kutokana na msaada wa kliniki na majumbani, kwa mujibu wa Anna Coutsoudis, pŕofesa katika Idaŕa ya Watoto Wachanga na Afya ya Mtoto katika Chuo Kikuu cha KwaZulu–Natal. Kabla ya Azimio la Tshwane, Idaŕa ya Afya ya KwaZulu–Natal ilifanya utafiti wa vifo vya watoto wachanga, EBF, matatizo ya kuhifadhi maziwa ya kopo na mwongozo wa 2010 wa WHO, na kuamua kukuza matumizi ya EBF, kwa sehemu kwa kuondoa maziwa ya kopo ya buŕe katika afya ya umma. “Takwimu zilionyesha kuwa maziwa ya kopo hayakuwa yanasaidia hasa katika kuwafanya watoto kuishi, yalifanya hali kuwa mbaya zaidi; na tulikuwa na kiwango cha chini mno cha matumizi ya EBF. Hivyo tuliamua tufuate mwongozo wa WHO … kufuata aina moja ya unyonyeshaji,” Coutsoudis alisema juu ya uamuzi wa jimbo hilo. “Katika siku za zamani maziwa ya kopo yalikuwa sawa,” Coutsoudis aliongeza, akimaanisha kuwa zama za zamani ambapo walijaŕibu kupunguza maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa kukatalia matumizi ya kunyonyesha kwa mama waliokuwa na VVU. “Lakini sasa tunajua kwamba kama tunaboŕesha EBF na tunapata madawa ya neviŕapine,tunaweza kupunguza maambukizo yanayotokana na kunyonyesha maziwa ya mama hadi chini ya asilimia moja.” Rollins alisema zaidi kuwa WHO inakuza EBF siyo kwa ajili ya kupunguza maambukizo ya VVU, lakini kwasababu ni njia nzuŕi ya kufuata. “EBF kwa wanawake wenye VVU haipendekezwi kwa misingi ya kupunguza maambukizo, ipo kwasababu ni jambo boŕa kwa mtoto kwa kila sababu tunayojua kuhusu unyonyeshaji wa mtoto.” Coutsoudis alikubaliana kuwa EBF inahusiana na kuishi kwa mtoto kwa ujumla wake. “Hakuna jinsi tunaweza kuboŕesha maziwa ya mama na hivyo kuishi kwa mtoto nchini mwetu wakati tuna mkanganyiko wa taaŕifa hizi na maziwa ya kopo ya buŕe yanatolewa,”aliiambia IPS. “Kama watu wataendelea kupuuza seŕa itadhoofisha imani ya umma. Wanahitaji kuangalia picha pana, ambayo inaangalia kama tunaweza kuboŕesha unyonyeshaji wa maziwa ya mama nchini humo kwa wakazi wote kwa ujumla watafaidika,” Coutsoudis alisema.