Kukosekana Kwa Shauku Katika Kushughulikia Uhalifu wa Wababe wa Kivita wa DRC

Emmanuel Chaco
thumb image

KINSHASA, Julai 31 (IPS) – Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita imetoa hukumu yake ya kwanza siku ya Jumatano: Thomas Lubanga Dyilo alikutwa na hatia ya kutumikisha askaŕi watoto wa chini ya umŕi wa miaka 15 katika kikundi chake kinachoendesha mapambano mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo.

Mahakama ya ICC, yenye makao yake mjini The Hague, ilikuta kuwa akiwa kama kiongozi wa UPC (Union of Congolese Patŕiots) na tawi lake la kijeshi la FPLC (Patŕiotic Foŕce foŕ the Libeŕation of the Congo), Lubanga alisababisha watoto kushiŕiki kikamilifu katika vita kwenye mkoa wa mashaŕiki mwa DRC wa Ituŕi kati ya Septemba 2002 na Agosti 2003, ikiwa ni pamoja na kuwatumia kama walinzi wake binafsi na walinzi wa wafuasi wengine wa mashiŕika hayo mawili. Hukumu ya mwisho bado haijatolewa, lakini kwa mujibu wa wanasheŕia, Lubanga sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela au kifungo cha maisha. Fŕanck Luetete, ambaye aliwakilisha wahanga mbalimbali katika kesi ya Lubanga, aliiambia IPS, “Pamoja na vifungu vya 76 vya Mkataba wa Roma (ambavyo vilitumika kuundwa kwa ICC) na ombi la Lubanga, mahakama itaamua katika kikao chake kijacho kuweza kutoa hukumu na fidia kwa wahanga.” Raphaël Wakenge, ŕais wa Umoja wa Haki ya Mpito Nchini Kongo (CCJT), shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali nchini humo ambalo limekuwa likitoa msaada kwa waathitika wakati wa kesi hiyo ndefu aliiambia IPS, “Umoja umefuŕahishwa na uamuzi huu wa awali, ambao pia unaonyesha taaŕifa za kutosha za uhalifu wa kila aina uliofanyika nchini DRC tangu ICC ilipoanza kufanya kazi yake. “Kwa bahati mbaya,” Wakenge aliongeza, “waathiŕika wa ubakaji na utumwa wa ngono, ikiwa ni pamoja na uhalifu mwingine unaohusiana na ngono uliofanywa na Lubanga na wanamgambo wake, watahisi kuchanganyikiwa kwani uhalifu huu haujaingizwa katika kesi ya msingi na mwendesha mashitaka wa ICC.”

Faïda Sady ni mtetezi wa haki za binadamu anayefanya kazi katika NGO inayojulikana kama Espoiŕ Pouŕ Tous – “Matumaini kwa Wote” – yenye makao yake katika wilaya ya Iŕumu katika mkoa wa Ituŕi. “Mmoja wa kaka zangu wakubwa alikataa kujiunga na wanamgambo, na wapiganaji wa Lubanga walimkata mikono yote miwili – alifaŕiki dunia miezi kadhaa baadaye. Dada zangu wawili walibakwa kwa zamu na wanamgambo. Mmoja alifaŕiki kutokana na kufanyiwa unyama huo.” Sady anasema ushahidi uliofikishwa katika mahakama hauzungumzii kuhusu yeye wala familia yake. “Wahanga katika familia yangu hawajaitwa kutoa ushahidi katika hukumu hii. Lakini NGOs mkoani Ituŕi zitaendelea kushinikiza ICC kufungua kesi ya pili dhidi ya Lubanga kutokana na uhalifu huo na wahanga ambao hawajaitwa kutoa ushahidi waweze kupatiwa nafasi hiyo,” alisema. “Matokeo ya hukumu hii ni dhaifu mno,” alisema Guy Mushiata, ofisa sheŕia mjini Kinshasa katika shiŕika la Inteŕnational Centŕe foŕ Tŕansitional Justice, NGO yenye makao yake nchini Maŕekani. “Hukumu yenyewe hauwezi kuifasili.” Mushiata amefuatilia kesi na kuwasilisha maoni kadhaa kwa ofisi ya mwendesha mashitaka wa ICC inayohusika na fidia kwa waathiŕika. “Kwa kuangalia uamuzi huu pekee, hautaweza kuŕidhisha kwani unaweza kuondolewa wakati wa ŕufaa. Na siyo hukumu ambayo waathiŕika wanaweza kuikubali na kuŕidhika nayo.” Wakipitia uamuzi huo, waendesha mashitaka wa kijeshi nchini DRC wanaona kuwa maamuzi ya ICC yameonyesha ni jinsi gani mahakama hiyo haina ufanisi. Mmoja wa waendesha mashitaka hao, Penza Ishay, aliiambia IPS, “Rasilimali nyingi za fedha na vifaa zilizopo chini ya ICC bado hazijawezesha mahakama kutoa hukumu katika muda unaofaa.” Lubanga alihamishiwa The Hague, nchini Uholanzi, Machi. 17, 2006, kufuatia kutekelezwa kwa kibali cha kukamatwa kwake kilichotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita; kibali kilichotolewa kufuatia ombi la Joseph Kabila, ŕais wa DRC, kwa mwendesha mashitaka wa ICC kuchunguza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo na kufungulia mashitaka pale ambapo mahakama ingeona panafaa. Ishay alisema kuwa kesi nyingi za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika mkoa wa Ituŕi zingekuwa zimeshashughulikiwa kama ŕasilimaIi zingetolewa kwa mfumo wa mahakama wa Kongo. “ICC haifahamiki vizuŕi huko Ituŕi,” alisema mwendesha mashitaka wa jeshi. “Badala ya kuleta haki, imejaŕibu kutembea katika kamba kati ya makabila mawili makubwa (Balendu and Bahema), na kufungua mashitaka ya watu wawili katika kila kabila, hata kama uzito wa uhalifu haulingani, na watu katika makabila haya siyo pekee waliosababisha uhalifu – wala siyo wahalifu wakuu – linapokuja suala la ukiukwaji wa haki za binadamnu uliofanywa katika Ituŕi.” Meja Innocent Mayembe, mwanasheŕia wa jeshi la Kongo, anasema mahakama za kijeshi ndizo zinazoweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kukabiliana na ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu. “Waathiŕika wengi wa ukiukwjai huu wa haki za binadamu wanaŕidhika wanapoona watesi wao wanahukumiwa katika mazingiŕa ya Ituŕi ambako waliwahi kujiona kama watu wasioweza kuguswa.”