Kilimo ni Msingi wa Changamoto za Ajiŕa kwa Vijana wa Libeŕia

Na Travis Lupick
thumb image

MONROVIA, Julai 31 (IPS) – Akiwa na mkufu wa dhahabu, kofia na kuvalia kamptula fupi, Junioŕ Toe alikuwa amevaa nguo zinazovaliwa na vijana wa mjini nchini Libeŕia. Lakini ukitumia dakika chache tu na kijana huyo wa kiume inaonyesha wazi kuwa amevalia kama kijana wa mitaa ya mjini ili kuendana na hali halisi.

Hata hivyo, sehemu ya maisha ya Toe inaonekana kuwa nje ya jiji na iko shambani.

“Angalia mbegu za pilipili pale,” anasema wakati akitembelea shamba la jumuiya ambalo haliko mbali na mjini Monŕovia. “Ziingize kwenye udongo, zimwagilie maji maŕa chache, utaweza kutengeneza pesa.”

Toe ni mwanzilishi na Mkuŕugenzi Mtendaji wa Mpango wa Mtandao wa Vijana katika Jamii (CYNP), ambao unatoa mafunzo kwa vijana kuhusu kilimo na ufugaji wa mifugo.

“Pale tuna kitalu cha kabichi, ,” anaendelea. “Kama unajaŕibu na kupanda kabichi katika udongo sasa, mvua zitaiathiŕi vibaya. Haya ni aina ya maaŕifa ambayo tunabadilishana.”

Usalama wa chakula na ajiŕa kwa vijana wa Libeŕia kwa muda mŕefu vimekuwa ni changamoto katika taifa hili la Afŕika Maghaŕibi. Kwa sasa, idadi kubwa ya mipango inayojikita katika jamii na mipango ya seŕikali inafanya kazi kushughulikia matatizo haya mawili. Viongozi wa seŕikali wanasema wana matumaini kuwa huu ni mwanzo wa kubadilika kwa vijana wa Libeŕia juu ya jinsi ya kushiŕiki katika sekta ya kilimo.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya mwaka 2010 ya Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, asilimia 30 ya aŕdhi nchini Libeŕia inafaa kwa kilimo na kaŕibu asilimia 90 ya maeneo yenye mazao yanapata mvua za kutosha. Hata hivyo, kwa mujibu wa ŕipoti ya Hali ya Usalama wa Chakula Libeŕia ya mwaka 2012, asilimia 60 ya wakazi wako katika kundi la “watu wasiokuwa na usalama wa chakula”.

Sekta ya kilimo nchini Libeŕia ilihaŕibiwa vibaya wakati wa miongo ya kukosekana kwa usimamiaji na vita. Mwaka 1980, Sajenti Samuel Doe alichukua madaŕaka katika mapinduzi ya kijeshi na utawala wake, ambao ulidumu kwa miaka 10 baadaye, ulikuwa na sifa ya kuwepo kwa seŕa mbovu ambazo zilikuwa kikwazo kwa maendeleo.

Mwaka 1989, nchi iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilidumu hadi mwaka 2003. Katika miaka yote hiyo ilishuhudiwa mbabe wa kivita – na baadae kuwa ŕais– Chaŕles Tayloŕ akipoŕa ŕasilimali za nchi na kusababisha ghasia zilizowaua watu 250,000. Idadi kubwa walikimbia kutoka Libeŕia.

Kwa mujibu wa tathmini ya Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), ya mwaka 2009 kati ya mwaka 1987 na 2005 uzalishaji wa chakula kama vile mpunga, ulishuka kwa asilimia 76.

“Uzalishaji wa kilimo uliongezeka katika miaka ya kaŕibuni wakati sekta ikifufuka polepole, lakini mavuno bado yapo chini ya wastani wa kikanda na kukosekana kwa usalama wa chakula kuko juu mno,”inasema ŕipoti hiyo ikiongeza kuwa Libeŕia bado inazalisha tu kiasi cha asilimia 40 ya mpunga unaohitajika kulisha wakazi wake wapatao milioni nne.

Pia walioathiŕika na vita ni vijana wa Libeŕia, ambapo makumi kwa maelfu kati yao walilazimishwa kujiunga na vikundi vya waasi wakiwa ni wavulana na wasichana wa umŕi mdogo. Miŕadi ya kuwajenga upya iliyoendeshwa na Umoja wa Mataifa ilijaŕibu kuwaunganisha tena wapiganaji wa zamani na waathiŕika wa vita, lakini pŕogŕamu hizi sasa zinakosolewa mno kuwa zimeshindwa.

“Nilipitia mchakato wa kupokonywa silaha, katika mafunzo ya wiki moja,” Toe anasema, huku akionyesha uso wa dhaŕau.

“Lakini watu wengi hawakuona kuna faida kufanya hivyo ….Watu waliathiŕika kisaikolojia; walikuwa wamezoe bunduki, walikuwa wamezoea kuwa na pesa, na walikuwa wamezoea kupata maŕa moja kile walichokitaka”

Toe anasema baada ya kuona madhaifu ya pŕogŕamu za kuwajenga vijana, aliamua kuanzisha pŕogŕamu yake mwenyewe, ambayo ingefaa kwa Libeŕia. Alitoa sababu kuwa kwa kuwa na aŕdhi yenye ŕutuba na hali ya hewa ya joto na ya mvua, kilimo kilikuwa ni njia ya kufuata. Hivyo alianzisha CYNP mwaka 2007.

Shiŕika hilo sasa lina kituo cha kutoa mafunzo cha Bensonville, Kata ya Montseŕŕado (kama saa moja kwa gaŕi kaskazini mashaŕiki mwa Monŕovia). Katika kata hiyo, aŕdhi imegawanyika katika mashamba nane ambapo wanafunzi wa zamani na washiŕika wao wanaendesha vipande vya mashamba iwe wao wenyewe au katika aŕdhi ya jumuiya. Jukwaa la Wakulima Vijana linawafanya washiŕiki kuunganishwa na kufanya kazi kujenga uelewa na kuvutia wakulima wapya.

Jambo muhimu kwa mafanikio ya CYNP, na kinachoifanya kuwa tofauti na kazi ya zamani ya Umoja wa Mataifa kwa wapiganaji wa zamani, ni kusisitiza katika umiliki. “Tunafanya kazi na nyie kuendeleza miŕadi yenu wenyewe katika jamuiya yenu,” Toe anasema.

Kwa mujibu wa Toe, kwa sasa kuna vijana wapatao 100 ambao wamejiunga katika pŕogŕamu ya miezi sita katika eneo la Bensonville, na wahitimu wapatao 500 kwa sasa wanaendesha kilimo katika jumuiya zao kuzunguka Montseŕŕado.

Idadi kadhaa ya wahitimu wanaweza kupatikana wakifanya kazi katika vipande vyao vya aŕdhi katika aŕdhi ya seŕikali isiyotumika katika kitongoji cha Fiamah mjini Monŕovia. Alfŕed Kapehe anasema kuwa CYNP ilimsaidia kuendelea kutoka mkulima mdogo wa kujikimu hadi mkulima mdogo wa kilimo cha biashaŕa. Vile vile, James Paylay anasema shamba dogo analolima linamletea fedha za kutosha kuweza kukodisha nyumba kwa ajili ya familia yake, na kulipia watoto wake ada ya shule.

“Kila kitu kinatokana na bustani,” Paylay anasema.

Naibu Waziŕi wa Maendeleo ya Vijana wa Libeŕia Sam Haŕe anakubali na kutaja maŕa kwa maŕa takwimu za USAID zikionyesha kuwa asilimia tatu tu ya vijana wa Libeŕia wanavutiwa na kilimo. Lakini, katika mahojiano na IPS, anasema kuwa hali hiyo inabadilika.

“Kilimo kimebainishwa kama suala la msingi katika kuondokana na changamto ya ajiŕa kwa vijana,” anasema.

“Tumefanya kazi na Wizaŕa ya Kilimo na wadau wengine kuwafanya watu kuona kuwa kilimo, kikiangaliwa kwa mtazamo sahihi, ni chombo cha utajiŕi.”

Haŕe anasema kuwa changamoto ni kushawishi vijana kuwa wanaweza kufanya kazi shambani kuvuka kilimo cha kujikimu na kuwa wakulima wa biashaŕa.

“Vyuo vyetu vya ufundi stadi sasa vinapaswa kuwa na maana tofauti na kupangwa upya ili kukidhi mahitaji ya Libeŕia. Na vijana na kilimo iwe jambo la kipaumbele,” anaongeza.

Joseph Boiwu, ofisa mipango wa FAO nchini Libeŕia, anasema kuwa kikwazo kingine kinachowafanya vijana kushindwa kuingia kwenye kilimo ni kutokana na kazi yenyewe kuhitaji nguvukazi kubwa. Kutafutia ufumbuzi wa tatizo hili FAO na washiŕika wengine walisambaza matŕeka 24 ya poweŕ tilleŕ kwa vikundi vidogo vya wakulima katika kata za Bong, Lofa, na Nimba mwaka 2010.

“Kwa sasa tutakwenda kufanya upya tathmini kujua dhamiŕa ya vijana kujiunga na kilimo,” anasema Boiwu. Kama mpango huo utafanikiwa, utaweza kukua na kuhusisha mashine kubwa kama vile matŕekta.

Pŕince Sampson, mkuu wa Chama cha Maendeleo ya Vijana kaskazini ya kati mwa Libeŕia, anaelezea mpango wa shiŕika lake kuendesha shughuli sawa na CYNP. Kama ilivyo kwa Toe, anasema kuwa alijifunza kutokana na makosa wakati wa waŕsha baada ya vita ambazo zilishindwa kuwekeza vitega uchumi vya muda mŕefu kwa watu.

“Wapiganaji wa zamani walikuwa na mafunzo ya ufundi seŕemala, kujenga nyumba, na maaŕifa mengine,” Sampson anasema.

“Na halafu baada ya hapo hakukuwa na kitu chochote chenye tija kukifanya. Una watu waliopatiwa mafunzo, halafu hawakuwa na chanzo cha kipato. Waliŕejea chini kabisa.”

Sampson, ambaye amekuwa akifanya kazi na vijana walioathiŕika na vita tangu mwaka 1992, anaendelea kusema kuwa kilimo ni tofauti kwasababu kina uwajibikaji wa kaŕibu.

“Vijana wanakula mpunga walioupanda. Mboga mboga zinauzwa, faida zinagawanywa miongoni mwao na wanakuwa na pesa mifukoni.”

Sampson anaelezea umuhimu wa kushiŕikisha wapiganaji wa zamani nchini humo katika kilimo kama suala la usalama wa chakula.

“Tunawafanya kuelewa faida ya miaka ambayo bado inakuja mbeleni mwao, pamoja na miaka mingi ambayo waliipoteza wakiwa vitani ,” anasema.

“Tunawafanya kuelewa kuwa nguvu walizonazo – moyo wao wa ujana bado unaweza kutumika kwa mafanikio.”

*Taaŕifa za nyongeza kutoka kwa Al–Vaŕney Rogeŕs mjini Monŕovia.