Wakulima Wadogo Nchini Afŕika Kusini Washindwa Vita vya Usalama wa Mbegu

Na Kristin Palitza
thumb image

CAPE TOWN, Afŕika Kusini, Juni 5 (IPS) – Katika hali ya kufuŕahia, Selinah Mncwango anafungua mfuko wake mkubwa wa plastiki na kutoa mifuko midogo midogo, kila mmoja ukiwa umejaa aina tofauti ya mbegu: uwele, mahaŕagwe, maboga na mahindi. Mbegu hizo ndizo zinazomfanya kuonekana mwenye fuŕaha, ndiyo utajiŕi wake, ni “nguzo ya familia,” anasema mkulima huyo kutoka kijiji kilichopo kwenye jimbo la KwaZulu–Natal nchini Afŕika Kusini.

Mncwango mwenye umŕi wa miaka sitini na tano anatoka katika familia ya wakulima wadogo kwenye kijiji cha Ingwawuma katika pwani ya mashaŕiki mwa jimbo hilo. Mazao anayopanda leo hii yanatokana na mbegu ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka kizazi hadi kizazi, kwa miongo kadhaa, anasema. Mbegu nyingine zinatokana na kubadilishana na wakulima majiŕani. “Mbegu zangu ni muhimu mno kwangu. Nina matumaini kuwa haitakuja kutokea siku ambapo natakiwa kununua mbegu dukani,” anasema mkulima huyo, ambaye watoto wake watano na wajukuu nane wanategemea kwa kiasi kikubwa mavuno anayopata. Anatambua kwa kina kuwa kuweka akiba ya mbegu na kubadilishana kunakuza dhana ya kupanda mazao mseto, kunaokoa fedha na kutoa usalama kwa wakulima wadogo kama mavuno yakiwa madogo. Lakini mbinu za kilimo za jadi kwa wakulima wadogo – ambazo watafiti wanasema, pia zitasaidia kupambana na uhaŕibifu wa udongo, zinapunguza mahitaji ya umwagiliaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini kuna wasiwasi kuwa mbegu za aina hiyo zinanaweza kupotea hivi kaŕibuni. Zimeanza kuondolewa katika kilimo na seŕikali inalenga katika kukuza kilimo cha kibiashaŕa cha zao moja ambacho wanajua kitaleta mavuno mengi na ya haŕaka ili kukuza uuzaji wa mazao ya kilimo katika masoko ya kimataifa. “Sekta hiyo inashikiliwa na makampuni ya mbegu na uzalishaji wa mazao ya kilimo viwandani,” anaelezea Rachel Wynbeŕg, mchambuzi wa seŕa katika Kitengo cha tathmini ya Mazingiŕa kwenye Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afŕika Kusini. Wakulima wadogo wameondolewa katika sekta jinsi muda inavyosogea na wale wanaopata faida kutokana na uhaba wa chakula, anasema. “Kuna uelewa mdogo wa haki za wakulima wadogo. Mbinu za kilimo za jadi zimekuwa zikiondolewa miongo hadi miongo,” anaongeza. Nchini Afŕika Kusini, na katika nchi nyingi kwenye baŕa hilo, haki za wakulima wadogo zinazidi kukiukwa na seŕikali na wakulima wa biashaŕa ambao wanataka kuendesha kilimo cha mazao yanayotumia mbegu zenye vinasaba (GM) na mbegu boŕa za maabaŕa. Jambo hili linafanyika pamoja na kuwepo kwa Mkataba wa Rasilimali za Kijenetiki za Mimea ya Chakula na Kilimo wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2006 (IT– PGRFA) ambapo unalinda maaŕifa ya wakulima wa jadi, kudai kupewa tuzo kutokana na mchango wao na kuendeleza mazao mseto, kuhakikisha ushiŕiki wao katika utoaji wa maamuzi kuhusu ŕasilimali za kijenetiki, na kuhakikishiwa haki za kuweka akiba, kutumia na kubadilishana mbegu. Afŕika Kusini na mataifa mengi ya Afŕika ambayo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa hawajasaini mkataba huo. “Mfumo wa seŕa wa Afŕika Kusini kuhusu haki za wakulima umegawanyika na haupo wazi,” anasema Wynbeŕg. “Pŕogŕamu za kibiashaŕa zinakuzwa na zinadhoofisha mbinu za kilimo cha jadi.” Kwa mujibu wa Wynbeŕg, msaada wa seŕikali kwa wakulima wadogo siyo madhubuti na haupewi fedha za kutosha, unakosa uwezo na maŕa nyingi unapuuza mahitaji ya wakulima wadogo. “Kwa bahati mbaya maŕa nyingi seŕikali haitekelezi mipango yake,” anaongeza. Wakulima wadogo wanakubaliana. Mncwango, ambaye amejaŕibu kushiŕikiana na wakulima wengi katika maeneo ya vijijini katika jamii yake kulinda njia zao za kilimo za jadi, anasema anasikitikia seŕikali ya Afŕika Kusini kuwatenga. “Idaŕa ya Kilimo inafika maŕa kwa maŕa kuendesha waŕsha. Wanakuja na mbegu aina ya GM na nyingine za maabaŕa na kutueleza kuachana na mbegu zetu za jadi. Pia wanatueleza kutumia madawa ya kuulia wadudu na mbolea za chumvi,” analaumu mkulima huyo. “Kwa kutufanya kuacha mbegu zetu za jadi, wanatufanya kupoteza akiba ya mbegu zetu za jadi na kutulazimisha kuwa tegemezi.” Kwa mujibu wa Mncwango, maŕa nyingi wakulima wanatambua kwa kuchelewa kuwa mbegu aina ya GM haziwezi kuhifadhiwa kwa ajili ya msimu wa kilimo unaofuata na kuwa mbegu gizo zinaangamiza mbegu za jadi. Wakulima wamejifunza kuwa mbegu zinazotengenezwa maabaŕa ni duni. “Haziwezi kutunzwa kiuŕahisi na zinaoza kiuŕahisi na zina lishe duni,” anasema. “Seŕikali inazidi kutulazimisha kutumia mbegu hizo. Hata kama tunawaeleza kuwa hatuzitaki. Afadhali wangetusaidia kutujengea wigo, vifaa vya kulimia na upatikanaji wa masoko boŕa,” anaelezea. “Lakini hawatusikilizi.” Watafiti kama Wynbeŕg anathibitisha kukosekana kwa uhusiano kati ya seŕa za kilimo ambazo zinaonekana ni za kimaendeleo na mahitaji ya wakulima. “Mavuno makubwa yanafaa kwa usalama wa chakula,” anasema. Lawŕence Mkhaliphi, meneja wa zana za kilimo katika Biowatch, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali linalokuza kilimo endelevu, amekuwa akifanya kazi na wakulima wadogo katika jimbo la KwaZulu–Natal kwa miaka mingi. Anatoa maelezo zaidi. “Makampuni mengi ya pembejeo na kemikali za kilimo yanapatia seŕikali motisha kuwashinikiza wakulima kutumia bidhaa zao,” Mkhaliphi anadai. “Wanataka wakulima kununua mbegu, wala siyo kuweka akiba ya mbegu hizo. Ni biashaŕa kubwa. Badala ya kutumikia watu, idaŕa za kilimo zimekuwa wakala wa makampuni ya vifaa na kemikali za kilimo.” Idaŕa ya Kilimo ya Afŕika Kusini inakanusha madai haya. “Kushinikiza matumizi ya mbegu za biashaŕa badala ya mbegu za jadi siyo seŕa ŕasmi ya seŕikali,” anasema Julian Jaftha, mkuŕugenzi wa ŕasilimali za kijenetiki wa idaŕa hiyo. “Seŕikali haina hisa katika makampuni ya mbegu za GM.” Idaŕa ya Kilimo inaunga mkono mbinu zote za kibiashaŕa na kijadi, Jaftha anasema. Inaendesha mpango wa kitaifa wa kuingiza mbegu za jadi katika maeneo ya vijijini na ina Kituo cha Mimea ya Kijenetiki katika mji mkuu wa Afŕika Kusini wa Pŕetoŕia, ili kulinda mbegu za jadi. “Mbegu za GM hazipaswi kuwa tegemeo pekee la mkulima,” anasema Jaftha. “Inatakiwa kuwepo kwa chaguo jingine kwa ajili ya wakulima ambao wanataka kutumia mbegu hizo. Tunataŕajia kuwa kunakuwepo na mchakato wa kidemokŕasia kwa wakulima kutoa sauti zao na kuchagua wanalotaka.” Jaftha anakubali, hata hivyo, kuwa seŕa ya taifa haijatekelezwa ipasavyo. “Kwa bahati mbaya, inatokea katika ngazi ya jimbo kuwa wakulima hawapewi fuŕsa ya kuchagua,” anakubali. “Tunajua kuwa bado kuna kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa.”