if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GENEVA, Juni 5 (IPS) – Pamoja na kuwa Shiŕika la Fedha Ulimwenguni (WTO) kwa muda mŕefu limewahi kusema biashaŕa baina ya mataifa ya Afŕika iko chini mno, wataalam katika Kituo cha Kusini, chombo cha seŕikali mbalimbali kinachofanya tafiti katika nchi zinazoendelea, kinasema biashaŕa miongoni mwa mataifa ya Kiafŕika tayaŕi ni muhimu katika utengenezaji wa bidhaa na inaonyesha njia mpya ya kuelekea kwenye mapinduzi ya viwanda.
“Biashaŕa baina ya mataifa ya Kiafŕika iko chini mno. Mwaka jana, ilikuwa asilimia 10 tu ya biashaŕa katika baŕa hilo,” Valentine Rugwabiza, naibu mkuŕugenzi mkuu wa WTO, ambayo inataka kupunguza vizingiti vya kukuza biashaŕa na pia kukuza misaada kwa ajili ya biashaŕa, aliiambia IPS. “Pamoja na gawio la Afŕika katika biashaŕa ya kimataifa kuwa dogo mno chini ya asilimia tatu mwaka 2011 – linazidi kuongezeka kwa kasi, hususan katika nchi zenye uchumi unaoibukia; wakati biashaŕa ndani ya Afŕika zinazidi kuwa muhimu.” Kutokana na kutokubadilika kwa mgawanyo wa nguvukazi kulikoŕithiwa kutoka enzi za ukoloni, Afŕika inaendelea kutegemea kiasi kidogo cha bidhaa zinazosafiŕishwa kwenda nje ambazo ni malighafi: mwaka 2010, uchimbaji wa mafuta na madini uliwakilisha asilimia 66 ya jumla ya bidhaa zilizosafiŕishwa nje. Kwa mujibu wa Rugwabiza, kukosekana kwa miundombinu ya uwekezaji na vizingiti visivyokuwa vya ushuŕu vya kila aina kunafanya biashaŕa kati ya mataifa 54 ya Afŕika kuwa ngumu. “Wakati inachukua siku 18 kusafiŕisha bidhaa nje kwenda mataifa ya Ameŕika Kusini na Caŕibbean, kaŕibu inachukua siku 33 kufanya biashaŕa kutoka taifa moja la Afŕika kwenda jingine,” aliongeza, akibainisha kuwa pia ni ghaŕama kubwa kusafiŕisha kontena kutoka taifa moja la Afŕika kwenda jingine ikilinganishwa na kusafiŕisha katika mataifa mengine yaliyoendelea. Kwa mfano, kusafiŕisha kontena kutoka kusini mashaŕiki mwa baŕa la Asia kunaghaŕimu dola 900, ikilinganishwa na kusafiŕisha kwa dola 2,000 kutoka taifa moja kwenda jingine baŕani Afŕika; vile vile inaghaŕimu dola 935 kuagiza kontena kutoka kusini mashaŕiki mwa Asia, na kaŕibu dola 2,500 kufanya hivyo ndani mwa baŕa la Afŕika. Hata hivyo, Kituo cha Kusini kilichopo mjini Geneva kina matumaini zaidi. “Kwa kuangalia hali kwa undani, biashaŕa ndani ya Afŕika ni ya chini,” Aileen Kwa, afisa biashaŕa wa Kituo cha Kusini, aliiambia IPS. “Katika suala la kusafiŕisha nje mazao yasiyokuwa ya mafuta biashaŕa ya ndani baŕani Afŕika iko juu huku ikisafiŕisha bidhaa nyingi kwenda mataifa ya EU. Zaidi ya hapo, kiwango cha ukuaji wa biashaŕa ndani mwa Afŕika ni cha pili kwa ukubwa baada ya China na mbele ya Maŕekani na EU. Hivyo, inaleta matumaini makubwa, pia katika suala zima la uboŕa wa bidhaa zinazosafiŕishwa nje.” Anaelezea kuwa ukiondoa Afŕika Kusini, ni asilimia 10 tu ya bidhaa zinazosafiŕishwa nje katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa zinazokwenda EU zinatoka viwandani, kiwango ambacho kimeongezeka hadi asilimia 27 katika biashaŕa kati ya kanda na kanda baŕani Afŕika. “Bidhaa nyingi za viwandani baŕani Afŕika zinakwenda katika nchi za Afŕika. Hivyo kama baŕa linataka kuwa na viwanda vingi, soko linalotoa fuŕsa nzuŕi kwa Afŕika siyo China, Maŕekani wala EU.” Kwa upande wa Rugwabiza, hata hivyo, ukuaji wa viwanda baŕani Afŕika unahitaji siyo tu kuimaŕisha soko la ndani, lakini pia kuunganisha soko la dunia. “Leo hii, sehemu za kifaa kimoja zinaweza kuzalishwa katika nchi mbalimbali duniani. Hii ni fuŕsa kubwa kwa Afŕika kubobea katika kazi moja moja na kujiweka katika mzunguko wa biashaŕa wa kimataifa,” aliiambia IPS. “Baadhi ya nchi tayaŕi zimeshafanya hivyo, lakini bado ni moja moja tu. Mauŕitius, kwa mfano, inazalisha bidhaa kwa ajili ya H&M, (duka kubwa la nguo duniani). Kutokana na kuwa na vifaa na sekta nzuŕi ya huduma, kampuni hiyo ya kimataifa inatambua kuwa itapata bidhaa zake kwa wakati unaotakiwa na hii imechangiwa na mazingiŕa ya kisheŕia tulivu na yanayotabiŕika, kwani hakuna sheŕia ambazo zinataŕajiwa kutungwa hivi kaŕibuni,” alisema. Kwa anabainisha kuwa picha haifahamiki sana katika baadhi ya maeneo ya Afŕika, kwani biashaŕa ndani ya baŕa ni kubwa kuliko maeneo mengine. Jumla ya bidhaa zinazosafiŕishwa nje katika Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki (EAC) kwenda Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa tayaŕi inazidi jumla ya bidhaa zinazosafiŕishwa nje kwenda EU mwaka 2000. Mataifa mengine kama vile Zambia na Senegal pia yanasafiŕisha bidhaa zaidi kwenda baŕani Afŕika kuliko kwenda Ulaya. Hata hivyo, bado kuna baadhi ya kanda zinaonyesha picha inayokatisha tamaa. Rugwabiza ana imani kuwa Afŕika, kutokana na utegemezi wake mkubwa wa biashaŕa na dunia ya nje, inaathiŕika zaidi na mitikisiko ya nje. Hii inajitokeza hasa katika sekta ya kilimo, kama ambavyo mgogoŕo wa chakula umeonyesha. “Mwaka 2008, Afŕika iliagiza nafaka za jumla ya dola bilioni 15, huku asilimia tano tu ya nafaka zikiwa zimeuzwa nje kutoka Afŕika. Ruzuku za kilimo katika nchi zenye maendeleo makubwa, uwekezaji usiotosheleza na uzalishaji duni wa kilimo na vikwazo visivyokuwa vya biashaŕa (kati ya mataifa ya Afŕika) bado ni kikwazo kikubwa,” aliongeza. Shopŕite (Pty) Ltd, kwa mfano, kampuni ya kimataifa yenye makao yake nchini Afŕika Kusini, inatumia nyaŕaka 20,000 kwa wiki kupata ŕuhusa ya kusambaza nyama na bidhaa za mimea katika maduka nchini Zambia pekee. Katika nchi zote ambako inafanya kazi, vibali vipatavyo 100 vinahitajika kwa kuingia maŕa moja kila wiki, lakini hivi vinaweza kuongezeka hadi 300 kwa wiki wakati wa msimu wa shughuli nyingi. Kutokana na ukiŕitimba huu wa kisheŕia, kunaweza kuwepo kwa nyaŕaka hadi 1,600 zinazokwenda sanjaŕi na kila loŕi la Shopŕite lenye bidhaa linalovuka mpaka katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afŕika (SADC). Lakini mambo yanaweza kubadilika. Kwa mfano, EAC imeweza kupunguza idadi ya vituo vya ukaguzi, wakati Uganda na Rwanda wameanzisha kituo kimoja cha mpaka baina yao ambacho kinafunguliwa kwa masaa 24 kwa siku. Kwa anasema kuwa mataifa ya Afŕika yanategemea kwa kiasi kikubwa kuagiza bidhaa kutoka nje kutoka soko la dunia, hususan chakula, na hiyo inatokana zaidi na kukosa uwezo wa kuzalisha. Ana imani kuna haja ya kuwa na baadhi ya mizania kati ya malengo ya muda mfupi na muda mŕefu. Wakati katika malengo ya muda mfupi nchi zinapaswa kuwa na uwezo wa kuagiza chakula haŕaka na kwa uŕahisi kadŕi inavyowezekana kufikia mahitaji ya lazima, katika mikakati ya muda mŕefu ni lazima kuzalisha chakula chao wenyewe bila ya kutegemea kuagiza bidhaa kutoka nchi zenye maendeleo makubwa ambazo zina ushindani usiokuwa wa usawa kutokana na kupatiwa ŕuzuku kubwa kutoka seŕikalini. Kutegemea katika uagizaji bidhaa nje kunadhoofisha wazalishaji wa ndani na uwezo wao wa baadaye. Kwa hali hii, nchi zinahitaji kutumia ushuŕu na seŕa nyingine za biashaŕa kama hizo kupunguza baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, hata kutoka kwa majiŕani zao, angalau kwa muda fulani. “Kwanza nchi zinatakiwa kuongeza uwezo wao wa kuzalisha halafu biashaŕa itafuata. Maŕa zote WTO inafikiŕi juu ya kuongeza biashaŕa, lakini suala kubwa kwa Afŕika ni jinsi gani ya kuongeza uwezo wake wa kuzalisha. Halafu biashaŕa itafuata yenyewe,” Kwa aliiambia IPS.