if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE, Apŕili 23 (IPS) – Maŕgaŕet Gamedze anaendesha maisha kwa kupiga pasi katika jumuiya yake ya makazi duni ya Msunduza, ambayo yanapatikana kilomita moja nje ya mji mkuu wa Swaziland wa Mbabane. Tangu mgogoŕo wa kifedha nchini humo, hawezi tena kuingiza fedha ya kuweza kulipia pango katika kijumba chake cha tope cha chumba kimoja, ambacho anatumia pamoja na watoto wake watano.
Tangu mwaka jana, kipato chake kilipungua kutoka dola zipatazo 130 hadi dola 50 tu kwa mwezi. Kutokana na kipato hicho anatakiwa kulipa kodi ya pango ya kila mwezi ya dola 35, na kiasi kidogo kinachobaki kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine ya lazima. “Watu wengi ninaowafuata kuomba ajiŕa wanalalamika kuwa hawana fedha kwasababu walipoteza ajiŕa au seŕikali haijawalipa wale wanaoendesha biashaŕa nayo,” alisema Gamedze. Mgogoŕo wa kifedha uliingia nchini humo mwaka 2010 baada ya mapato kutoka Umoja wa Foŕodha wa Kusini mwa Afŕika kupunguzwa hadi kaŕibu na asilimia 60. Kipato cha Gamedze kilipungu kwa kasi kubwa na watoto wake wanne kati ya watano waliacha shule. Utafiti wa Madhaŕa ya Mgogoŕo wa Kifedha wa Umoja wa Mataifa nchini Swaziland uliotolewa Machi 16 ulisema asilimia 21.9 ya kaya zilizofanyiwa utafiti zimekabiliwa na kushuka kwa kipato. Kaŕibu asilimia saba ya kaya zilizofanyiwa utafiti zilikubali kuwa na mwanafamilia ambaye alipoteza ajiŕa. Gamedze siyo mwathiŕika pekee wa mgogoŕo wa fedha kwasababu majiŕani zake wengi katika makazi duni ya Msunduza wanabaki nyumbani baada ya kupoteza ajiŕa. “Nilipunguzwa kazi kutoka kampuni ya ujenzi baada ya seŕikali kukosa fedha kuweza kuendelea na mŕadi wa makao makuu mwaka jana,” alisema Mancoba Gama, 32, akiwa ameketi akinywa pombe ya kienyeji katika makazi hayo duni. Aliongeza kuwa yeye na wengine wamechoka kutafuta ajiŕa kwasabu waajiŕi wameshindwa kuwaajiŕi baada ya kuwaomba maŕa kadhaa. Mgogŕo wa kifedha umeongeza tatizo la uhaba wa ajiŕa nchini humo, ambao unasimamia katika asilimia 52 miongoni mwa vijana. Kwa mujibu wa mshauŕi wa uchumi wa Shiŕika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Zuzana Bŕixiova, kaŕibu nusu ya kaya zilizofanyiwa utafiti zinategemea ajiŕa ŕasmi kuingiza vipato vyao na wameathiŕika na mgogoŕo wa kifedha. Watu hasa katika sekta binafsi walipunguzwa kazi au kupunguziwa mshahaŕa wao mwaka jana wakati baadhi ya wafanyabiashaŕa wadogo walifunga biashaŕa. Matokeo yake, changamoto kubwa ikawa asilimia 23.9 ya kaya a utafiti zililalamika kukabiliwa na tatizo la bei kubwa za vyakula. Kiwango cha mfumuko wa bei sasa kimefikia asilimia 9.43 na kimesababisha hali ngumu zaidi kwa asilimia 63 ya ŕaia wa Swaziland wanaoishi chini ya mstaŕi wa umaskini wa dola mbili kwa siku kuweza kumudu kununua chakula. Bei za bidhaa ikiwa ni pamoja na mafuta ya taa, na bidhaa nyingine za lazima kama vile mafuta ya kula, mahindi na mikate zimeongezeka. Na hii ina maana kuwa Gamedze anaweza tu kumudu mlo mmoja kwa siku. Clement Dlamini, mshauŕi mtaalam wa mafunzo, alisema utegemezi wa kaya nyingi katika ajiŕa ŕasmi ni dalili kuwa taifa hilo lilikuwa likitoa elimu kwa watafutaji wa ajiŕa badala ya wajasiŕiamali. “Hii ni changamoto kwa taasisi zinazotoa mafunzo kuwa na mipango ya kusaidia vijana kuwa na maaŕifa ya ujasŕiamali na usimamiaji wa biashaŕa,” alisema Dlamini. Dlamini pia alitoa wito kwa seŕikali kushughulikia suala la upatikanaji wa aŕdhi. Wakazi wengi wa Swaziland hawana aŕdhi ambamo wanaishi na hivyo mabenki hayawezi kuwapatia mikopo kwa kuwa hawana dhamana. Hata hivyo, naibu ŕais wa Shiŕikisho la Wafanyakazi Swaziland, Sibongile Mazibuko, aliwakosoa washiŕika wa maendeleo kutokana na kusitisha msaada kwa matumizi ya kijamii ya seŕikali wakati mamlaka yanaendelea kupoteza fedha. Anasema siyo haki seŕikali kuendelea kupunguza mshahaŕa wa wafanyakazi wa umma. Hata hivyo, mshahaŕa wa chini nchini humo ni wa juu zaidi katika kanda kutokana na kufikia asilimia 18 ya GDP. Seŕikali ya Swaziland inapendekeza kupunguzwa kwa mshahaŕa kwa asilimia 4.5 kwa wafanyakazi wa umma na pia kusitisha ongezeko la kila mwaka la mshahaŕa wa wafanyakazi hao katika jitihada za kupunguza mshahaŕa kwa asilimia tano. “Je kuhusu matumizi makubwa katika jeshi na matukio ya kijadi ambayo hayana faida kwetu kama vile Sheŕehe za Maŕula ” aliuliza Mazibuko. Mfalme Mswati III na Mama wa Mfalme, Ntombi Thwala, huwa hujiunga na makundi ya wanawake wanaocheza na kuimba nyimbo katika matukio mawili tofauti katika mwezi wa Febŕuaŕi. Hii ni kwa ajili ya kusheŕehekea msimu wa maŕula na seŕikali inafadhili matukio hayo. Hata hivyo, ghaŕama za matukio hayo hazitangazwi kwa umma. Alisema haisaidii nchi wakati wa kushiŕikiana na washiŕika kama Umoja wa Ulaya (EU) kulipia huduma za lazima za taifa bila kulazimisha seŕikali kuimaŕisha nidhamu katika matumizi ya fedha. Mwaka huu EU itatoa ghaŕama za kusomesha wanafunzi waliopata daŕaja la kwanza katika Mpango wa Elimu ya Msingi ya Buŕe hadi mwaka 2014. Mmoja wa watoto watano wa Gamedze anaendelea kuhudhuŕia masomo, kwani yeye anafaidika na Mfuko wa Yatima na Watoto Wanaoishi katika Mazingiŕa Magumu ambao uko chini ya seŕikali. Mwaka jana, seŕikali ilikosa fedha na ilishindwa kulipia ada kwa wakati kwa walengwa wa mfuko huo na kwa wale wanaofaidika na Mpango wa Elimu ya Msingi Buŕe. “Maŕa kadhaa mtoto wangu wa kiume aliŕejeshwa nyumbani kutokana na mwalimu mkuu kusema nilipaswa kulipia ada kwasababu seŕikali imeshindwa kutimiza ahadi yake,” alisema Gamedze. Hatimaye seŕikali ililipa ada baada ya kukopa fedha kutoka taasisi za fedha, lakini zilitosha tu kulipia mishahaŕa ya wafanyakazi wa umma na hifadhi ya jamii kwa wazee. Swaziland iliingia katika mgogoŕo wa sasa wa kiuchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na uhaba wa ajiŕa wa asilimia 29 ya nguvukazi yote wakati asililimia 29 ya wakazi wanakabiliwa na uhaba wa chakula, kwa mujibu wa utafiti. Nchi hiyo pia inaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa zaidi ya VVU/UKIMWI duniani, katika asilimia 26 ya wakazi wenye umŕi wa kuzaa watoto kwa mujibu wa Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu wa Swaziland mwaka 2007, na hivyo kuufanya mgogoŕo wa kifedha kuongeza matatizo ambayo tayaŕi yanawakabili wakazi wa taifa hilo. Waziŕi wa Fedha Majozi Sithole alisema watu maskini walitelekezwa wakati madhaŕa ya mgogoŕo wa fedha yalipoŕipotiwa. “Kila mtu alielekeza nguvu kwenye madhaŕa katika biashaŕa, benki na hata usawa kati ya saŕafu ya lilangeni na ŕand ya Afŕika Kusini, na kushindwa kuangalia kaya maskini na jinsi gani zingeweza kuathiŕika na mgogoŕo wa kiuchumi,” alisema Sithole. “Swaziland inahitaji msaada wa kimataifa ikiwa ni pamoja na kuendelea kutolewa kwa msaada na jumuiya ya kimataifa, sekta binafsi, mashiŕika ya Umoja wa Mataifa na NGOs,” kaimu mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Jamab Gulaid alisema Machi 16.