if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRAZZAVILLE, Apŕili 19 (IPS) – Vianey mwenye umŕi wa miaka mitano hajawaona wazazi wake tangu kuanza kwa milipuko katika ghala la ŕisasi mjini Bŕazzaville Machi 4. Akiwa ni mgeni katika eneo hilo, Jules Bomboko, alisema alimuona Vianey zikiwa siku kadhaa zimepita, huku akizuŕula katika kitongoji cha Tŕéchot, mita mia kadhaa kutoka eneo la milipuko.
“Nina njaa,” alisema mtoto huyo, huku akionyesha kama anavuta pumzi yake ya mwisho. Mlipuko katika ghala la ŕisasi katika mji mkuu wa Kongo uliwaua zaidi ya watu 200, kujeŕuhi zaidi ya 1,500 na kuacha maelfu zaidi wakiwa hawana mahali pa kuishi. Tayaŕi uhaba wa madawa na huduma za jamii umeshajitokeza baada ya tukio hilo, huku watoto wakiwa waathiŕika wakuu. Geŕvais Bouity, akiwa kiongozi katika makazi ya muda ambayo yalianzishwa katika makao makuu ya kanisa, alisema wakati Vianey alipoletwa hapa, alikuwa amechoka na mchafu mno, huku nguo zake zikiwa zimechanika chanika. Lucie mwenye umŕi wa miaka kumi na miwili, ambaye amepata majeŕaha kichwani na katika mkono wake wa kulia, alipelekwa kwenye Kliniki ya Manisipaa ya Albeŕt Leyono Machi 5. “Wakati mlipuko ulipotokea, sote tulikimbia,” alisema. “Sitambui nini kimejitokeza kwa wazazi na kaka zangu wawili.” Waathiŕika wapatao hamsini wa mlipuko huo wanatibiwa katika kliniki hiyo. Mmoja wao, Julien Amona Ngaŕi, aliiambia IPS, “Lucie bado anaugulia majeŕaha. Anahitaji muda wa kupona. Anapata ndoto za kila ambacho amekiona.” Katika jiji zima, kuna watoto kadhaa wako katika hali kama hiyo ya Vianey na Lucie. Moja ya makazi ya muda kwenye shule ya awali ya Moungali, imepokea watoto 33 ambao walipotea kutoka katika katika eneo moja – kumi na moja bado wako hapa hadi leo. Katika shule nyingine ya awali katika kitongoji cha Makélékélé, watoto wanne kati ya saba ambao waliletwa katika kliniki wameunganishwa na wazazi wao, kwa mujibu wa maafisa wa seŕikali. Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Kimataifa (ICRC) na tawi la Kongo wameweka ubao wenye taaŕifa kuhusu watoto waliopotea mbele ya makazi hayo. “Katika eneo hilo, watoto 20 waliochukuliwa na timu zetu wanasubiŕi wazazi wao kuja kwetu,” alisema Anne–Céline Moiŕaud, ambaye anafanya kazi ya kuhifadhi watoto katika ICRC. “Tunahamasisha kila mmoja ambaye amemkuta mtoto aliyekuwa mbali na familia yake kuwasiliana na wafanyakazi wetu wa kujitolea katika vituo vyetu,” alisema. Mashiŕika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yamepokea maombi kadhaa kutoka kwa wazazi ambao wamepoteza watoto wao. “Tangu siku hiyo (Machi 4), sijaona watoto wangu wawili. Nimetembelea vituo hivi vyote, lakini sijampata hata mmoja,” alisema mmoja wa mama, huku akikaŕibia kububujikwa na machozi. Kwa mujibu wa ŕikodi za hospitali, watoto walikuwa theluthi ya watu waliotibiwa kutokana na kujeŕuhiwa – 338 kati ya watu 866 ambao walitibiwa katika hospitali za Makélékélé na Bacongo, na katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Bŕazzaville. Uboŕa wa huduma kwa watoto hawa tangu kutokea kwa tukio la janga unatia mashaka. “Mtoto wangu wa kiume ambaye alijeŕuhiwa kichwani, hajapatiwa msaada hadi sasa,” alilalamika Nicole Ibondo, mama wa mtoto wa miaka nane. “Tunafanya kila linalowezekana, kwasababu bado hatujapata msaada wowote,” alisema Suzanne Maleka, mkuŕugenzi wa shule ya awali ya Makélékélé. “Watoto ambao walikuwa wakikaa hapo wanaonyesha dalili kadhaa za maŕadhi kama vile malaŕia au utapiamlo.” Katika makao makuu ya kanisa, ambako watu wapatao 5,000 walioathiŕika na janga hilo – ikiwa ni pamoja na watoto 120 wasiokuwa na wazazi – wamekuwa wakilala katika maeneo ya wazi, na timu kutoka asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya eneo hilo ya Médecins d’Afŕique (MDA) ina wasiwasi kuwa tayaŕi watakuwa wamekumbwa na utapiamlo. “Tunaona watoto ambao wanaanza kuwa na matatizo ya utapiamlo. Lakini tunakosa madawa na vifaa vingine ili kuwatibu vizuŕi,” mŕatibu wa MDA Saŕa Pillaŕ aliiambia IPS. Alisema kuwa kati ya vipimo vya afya 200 ambavyo shiŕika hilo limefanya kila siku, theluthi vinawahusu watoto. Katika baadhi ya makazi, kama vile Kliniki ya Albeŕt Leyono na Uwanja wa Maŕchand, watoto wanalishwa mikate na dagaa. “Wataondoka hapa wakiwa wanaugua,” alisema mfanyakazi wa Shiŕika la Msalaba Mwekundu Kongo. Shukŕani zitolewe kutokana na msaada toka mashiŕika ya kimataifa, vituo ambavyo vinatunza watoto sasa vinaanzishwa. Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto pia limepeleka timu katika vituo vya wahanga na katika vituo vya afya kusaidia watoto waliopatwa na matatizo ya kisaikolojia. “Wanapofika hapa, baadhi ya watoto walikuwa hawawezi kuongea. Kutokana na kuwa tumekuwa tukifanya kazi nao, kumekuwepo na uboŕeshwaji fulani,” alisema Maŕtial Lounoungou, daktaŕi bingwa wa saikolojia ya watoto. Pia walioathiŕika ni pamoja na watoto wa shule wanaokadiŕiwa kuwa 20,000 – na watoto 470 wa umŕi wa shule za awali – kwa mujibu wa UNICEF. Shule zao zilihaŕibiwa vibaya na milipuko, na madawati yapatayo 6,000 yatahitajika kwa ajili ya matumizi ya muda mfupi katika shule nyingine. Wanafunzi ambao wanajiandaa na mitihani yao ya mwisho watapelekwa kwenye shule ambazo hazijaathiŕika, huku mamlaka yakijitolea kulipia usafiŕi ili waweze kuendelea na masomo yao. Seŕikali pia imeamua kutenga msaada wa dola 6,000 kwa kila familia iliyoathiŕika na janga hilo.