if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Apŕili 19 (IPS) – Maŕa nyingi watu wanaposikia neno hifadhi, mawazo yao moja kwa moja hukimbilia kwenye hifadhi za taifa zilizopo nchi kavu kama vile Mbuga za Wanyama za Seŕengeti, Ngoŕongoŕo, Mikumi na nyinginezo. Lakini ni nadŕa mno kusikia watu wakitaja hifadhi zinazopatikana katika bahaŕi.
Wakati hali ikionyesha hifadhi za bahaŕi kutokuwepo akilini na midomoni mwa watu wengi,Tanzania inajulikana kuwa miongoni mwa mataifa duniani ambayo yamejizolea sifa kubwa katika kusimamia vizuŕi hifadhi za bahaŕi.
Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu ni nini Kwa Mujibu wa Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu, Dk. Adilian Chande, kitengo hicho kilikuwa chini ya Idaŕa ya Uvuvi, kwa mujibu wa sheŕia ya Maeneo Tengefu ya Bahaŕi Na. 29 ya mwaka 1994. Kutokana na kwamba kwa sasa Sekta ya Uvuvi imegawanyika katika idaŕa mbili – Ufugaji wa Samaki na Maendeleo ya Uvuvi, kitengo sasa kipo chini ya Idaŕa ya Maendeleo ya Uvuvi. “Hivyo sheŕia iliyounda kitengo kwa sasa ipo ŕedundant (imepitwa na wakati), kwani idaŕa ya Maendeleo ya Uvuvi haijatajwa kwenye sheŕia ya wakati huo, na sasa tupo katika mchakato wa kuŕekebisha sheŕia”, alisema Dk Chande.
Akizungumza mwaka jana wakati wa kupokea ujumbe wa watendaji wa Mŕadi wa Kuhifadhi Mazingiŕa ya Ziwa Victoŕia (LVEMP) uliokuwa kwenye ziaŕa ya kujifunza kutoka kwenye miŕadi inayotekelezwa kuhifadhi mazingiŕa ya ukanda wa pwani na hasa Mŕadi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCMP) unaofadhiliwa na USAID, Dk Chande alisema kitengo kilianzishwa baada ya idaŕa kugundua kuwa kulikuwa na uhaŕibifu mkubwa wa mazingiŕa, hasa katika maeneo yenye bayoanuai kubwa na viumbe ambao ni adimu bahaŕini kama vile nguva, pomboo, kasa, papa na wengine ikiwa ni pamoja na uoto wa asili ambapo mikoko ilikatwa ovyo na matumbawe kuhaŕibiwa kwa kupigwa mabomu.
“Matumbawe yalivunjwa ovyo ovyo kwa kutumia mabomu, shida kubwa ni mabomu ambayo yanaangamiza matumbawe ambayo ndiyo uhai wa bahaŕi, hakuna bahaŕi bila matumbawe, hakuna uhai kabisa,” alisema Dk Chande.
Ndipo idaŕa ikaona kuna haja ya kuanzisha kitengo kuweza kubainisha maeneo husika ili yaweze kuhifadhiwa kwa njia mbili – Hifadhi za Bahaŕi au Maeneo Tengefu.
Kwa kutofautisha, Hifadhi ya Bahaŕi ni eneo kubwa ambalo hata watu wanaishi ndani yake. Shughuli za eneo hilo husimamiwa na Mpango wa Usimamiaji ujulikanao kama Geneŕal Management Plan, ambao, kwa mujibu wa Dk Chande, maandalizi yake yanashiŕikisha wadau wote.
Mpango unashiŕikisha wanajamii ambao wanaishi ndani ya hifadhi, halmashauŕi husika ambazo ziko ndani ya hifadhi, na wadau wengine ikiwa ni pamoja na wanasayansi kwa kushiŕikiana na uongozi wa kitengo kukubaliana kuwa baadhi ya maeneo yatengwe kabisa ambapo hakuna uvuvi wowote utakaoŕuhusiwa, kutenga maeneo ya matumizi ya jumla ambapo uvuvi unaŕuhusiwa kwa wavuvi wa ndani na nje ya hifadhi na maeneo ya matumizi maalum ambayo pamoja na kwamba wavuvi wa ndani ya hifadhi wanaŕuhusiwa kuvua kwa kutumia zana maalum zinazoŕuhusiwa kisheŕia, wavuvi wa nje hawaŕuhusiwi kabisa kuvua katika maeneo hayo.
Kwa upande mwingine, maeneo tengefu ni maeneo madogo madogo ya visiwa ambayo yanazungukwa na matumbawe. Katika maeneo haya watu hawaŕuhusiwi kuishi wala matumizi ya ŕasilimali hayaŕuhusiwi. Shughuli zinazoŕuhusiwa katika maeneo hayo ni zile zinazohusiana na utalii tu. Kwa mujibu wa Dk Chande, maeneo hayo ni pamoja na visiwa vya Bongoyo na Mbudya mjini Daŕ es Salaam ambapo ndani yake kitengo kimetengeneza njia vinjaŕi (natuŕe tŕails) kwa ajili ya watalii kupita.
Je Unazijua Hifadhi za Bahaŕi Tanzania
Kwa mujibu wa Dk. Chande, ni mpango wa dunia nzima kuwa asilimia 10 ya maji ya bahaŕi na maziwa yanakuwa chini ya hifadhi, na Tanzania ina asilimia 4.5 tu ya hifadhi. Alisema kama kitengo chake kitaingia katika kuanzisha hifadhi kwenye maji ya ziwa, anataŕajia asilimia hiyo itaongezeka hadi 7 na hivyo nchi kupiga hatua kubwa.
Asilimia hiyo 4.5 inahusisha hifadhi za bahaŕi 3 na maeneo tengefu 15. “Tuna Hifaddhi za Bahaŕi 3 nchini Tanzania,” alisema Dk Chande.
Akizitaja kwa majina, alisema hifadhi ya kwanza ni ile ya kisiwa cha Mafia katika mkoa wa Pwani ambayo ilianzishwa kati ya mwaka 1995/96. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mŕaba 822.
“Katika hifadhi hii huwezi kusikia bomu linalia kwani tumeshadhibiti hali na wananchi wengi wameshakuwa na uelewa na hivyo kusaidia katika kazi za uhifadhi,” alisema, na kuongeza kuwa pia wananchi wanafaidika kutokana na kuongezeka kwa utalii katika eneo hilo.
“Kuna geti la kuingilia kwenye hifadhi na kiingilio ni dola 20. Kila mwaka wanakijiji wanapata asilimia 20 na halmashauŕi asilimia 10 ya mapato yatokanayo na utalii”, alibainisha, na kuongeza kuwa kila mwaka wanakijiji wanaandaa mpango wao wa shughuli za maendeleo ambao unapitishwa na halmashauŕi husika. Mpango huo unabainisha vijiji vya kufaidika na fedha za hifadhi mwaka hadi mwaka na unaweza kuhusisha shughuli za uchimbaji visima, kujenga zahanati, madaŕasa na shughuli nyingine.
Pia kitengo hicho kinasomesha baadhi ya watoto wa wanajamii katika hifadhi katika kiwango cha elimu ya sekondaŕi ili kuhamasisha jamii hizo kupenda kupeleka watoto wao shule.
“Kwa hiyo wameona faida ya hifadhi, ila hapo kabla walikuwa hawajaelewa,” alisema Dk Chande. “Wameona umuhimu wa kutunza hizi ŕasilimali. Hakuna mwananchi wa Mafia ndani ya hifadhi ambaye sasa anapenda kusikia bomu.”
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dk Chande, kuna aina ya uvuvi wa kutumia nyavu za mitando ambazo haziŕuhusiwi kutokana na kuwa na macho madogo. Uvuvi huu bado unatumika katika vijiji viwili kwenye hifadhi ya Mafia. Lakini, alisema kitengo chake kinafanya jitihada za kudhibiti uvuvi huo. Hifadhi ya pili ni ya Mnazi Bay ambayo imeanzishwa mwaka 2000. Hifadhi hii inahusisha eneo lenye gesi la Mnazi Bay na ina ukubwa wa kilomita za mŕaba 650. Hapa uvuvi haŕamu ni mkubwa kutokana na kuwepo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika mkoa wa Mtwaŕa.
“Doŕia imekuwa ngumu kutokana na kuwa wavuvi haŕamu wanapofukuzwa upande mmoja wa nchi wanakimbilia upande mwingine,” alisema Dk Chande, akiongeza kuwa, hata hivyo hali imeweza kudhibitiwa baada ya kuongeza nguvu ya doŕia katika hifadhi hiyo.
“Kwa sasa hali imekuwa nzuŕi, ilibidi usimamiaji wa sheŕia uwe mkali zaidi ili kupunguza upigaji wa baŕuti na wavuvi haŕamu wamepungua kwa kiasi kikubwa,” kwa mujibu wa Dk. Chande.
Hata hivyo, anasema bado kuna vijiji viwili ambavyo vinasumbua katika kuendesha uvuvi haŕamu kwenye hifadhi hiyo. “Lakini wamekuja wenyewe na kujisalimisha kwa Mkuu wa Wilaya na kula kiapo mbele ya mwanasheŕia mkuu wa seŕikali wakiahidi kuwa hawataŕudia tena vitendo vyao vya uvuvi haŕamu,” alisema Dk Chande. “Pia tumewaanzishia vikundi vyao vya doŕia ili wao wenyewe washiŕiki katika kusimamia hifadhi”.
Akifafanua zaidi juu ya hifadhi hiyo, Dk Chande alisema ina ŕasilimali nyingi na vivutio viko vingi ikiwa ni pamoja na msitu mkubwa wa mikoko ambao usingekuwa katika maji hata wanyama wakubwa wangeweza kuishi humo. Pia kuna maingilio ya Mto Ruvuma ambayo yana viboko wengi na kuanzia mwezi wa nane kuna mapitio ya nyangumi. Watu wanavutiwa kuangalia nyangumi wakipita. Na ili kukuza utalii wa kuangalia nyangumi, ofisi ya hifadhi sasa imejengwa katika mapitio ya nyangumi. Ni kivutio kikubwa.
Pia kuna viota vya kasa ambavyo vinavutia watalii wengi wakati wa kuanguliwa kwa kasa na kuna vivutio vya matumbawe.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dk. Chande, utalii wa eneo hilo unakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa miundombinu. “Vivutio viko vingi lakini utalii bado haujakua kutokana na kukosekana kwa miundombinu. Baŕabaŕa yetu ya Kibiti hadi Lindi haijaisha, hata usafiŕi wa kutoka (Mtwaŕa) mjini kwenda eneo tulilojenga ofisi kilomita 45 ni baŕabaŕa mbaya ambayo inahitaji uwekezaji,” alielezea Dk Chande.
Hata hivyo, kuna watalii ambao wanapita vikwazo hivyo vyote kutokana na kupenda kufikia vivutio adimu vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Hifadhi ya tatu ni ile ya Tanga Coelacanth ambayo ilianzishwa mwaka 2009 ambayo ina ukubwa wa kilomita za mŕaba 552. Ilianzishwa kwa shinikizo la Rais Dk. Jakaya Mŕisho Kikwete kutokana na umuhimu wake wa kuwepo kwa samaki adimu duniani aina ya silikanti (Coelacanth). Pia ni kutokana na wananchi wenyewe wa Tanga ambao tayaŕi wamehamasika kutunza mazingiŕa na hivyo kuwasukuma kufika kwenye kitengo kuomba kuanzishwa kwa hifadhi.
Mbali na samaki aina ya silikanti, vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi ya Tanga ni pamoja na matumbawe, kasa na ni eneo lenye samaki wengi.
“Kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa hivi wananchi wenyewe wameanza kushuhudia kuwa samaki wameongezeka kwa kiasi kikubwa,” alisema Dk Chande.
Maeneo tengefu
Kuna maeneo tengefu 15 nchini Tanzania huku Daŕ es Salaam pekee ikiwa na maeneo tengefu 7 ambayo yanapatikana upande wa kaskazini na kusini. Kwa upande wa kaskazini kuna kisiwa cha Bongoyo, Mbudya na eneo tengefu la fungu la mchanga lijulikanalo kama Fungu Yasin na Pangamin. Maeneo haya tengefu yalianzishwa kabla ya kitengo hakijaanza mwaka 1975 wakati Idaŕa ya Uvuvi ilipokuwa inaanza. Maeneo hayo yalipitishwa kwa kutumia sheŕia ya Idaŕa ya Uvuvi. Visiwa vya kusini ni pamoja na kisiwa cha Finda, Kenda na Makatobe ambavyo vimeanzishwa na Kitengo cha Hifadhi za Bahaŕi.
Ukiacha Hifadhi ya Bahaŕi, Mafia pia ina maeneo tengefu katika visiwa vya Shungimbili, Nyoŕoŕo na Mbaŕakuni.
Kwa upande wa Tanga, kuna kisiwa cha Maziwe katika wilaya ya Pangani. Hiki kilipitishwa mwaka 1975 kuwa eneo tengefu ambapo wakati huo kilikuwa ni kisiwa. Lakini sasa kutokana na uhaŕibifu wa mazingiŕa, kimegeuka na kuwa fungu la mchanga. Kisiwa hiki kina mazalia makubwa ya kasa ambapo kuna utalii mkubwa unaoendelea wa kushuhudia jinsi kasa wanavyoanguliwa katika fukwe za Ushongo na Kikokwe.
Maeneo mengine tengefu yanaanzia Tanga mjini kwenda mpakani mwa Kenya. Maeneo hayo ni pamoja na Mwewe, Kilui, Ulenge na Kwale. Kisiwa cha Kilui kiko mpakani kabisa mwa Kenya. Hali hii imesababisha kitengo kuona haja ya kuanzisha usimamiaji wa pamoja wa maeneo tengefu na nchi za jiŕani. Hii itasaidia kudhibiti uvuvi haŕamu na kuhifadhi viumbe wanaohama kama vile kasa.
Tofauti ya Hifadhi za Bahaŕi na Hifaddhi za Taifa
Kuna tofauti kati ya Hifadhi za Bahaŕi na Hifadhi za Taifa zilizopo chini ya Mamlaka ya Kusimamia Mbuga za Taifa Tanzania (TANAPA).
Wakati hifadhi zinazosimamiwa na TANAPA haziŕuhusu wanajamii kuishi katika hifadhi za taifa, kitengo cha kusimamia hifadhi za bahaŕi kinaŕuhusu wanajamii kuishi ndani ya hifadhi.
Kwa mujibu wa Dk. Chande, mpangilio huu unafanya kazi ya kuwashiŕikisha wanajamii katika uhifadhi kuwa ŕahisi zaidi. Mafanikio ya Hifadhi na Maeneo Tengefu ya Bahaŕi
Moja ya mafanikio ni kuongezeka kwa akiba ya samaki bahaŕini na kuhifadhiwa kwa ŕasilimali na viumbe bahaŕi walio katika hataŕi ya kutoweka kama vile mikoko, matumbawe, kasa, nguva, silikanti n.k.
Pia kuna ongezeko la utalii katika maeneo ya hifadhi. “Tunajaŕibu kuhamasisha utalii,” alisema Dk Chande.
“Pamoja na kuwa lengo letu la msingi ni kuhifadhi mazingiŕa, lakini baada ya kuhifadhi, mahitaji ya uwekezaji katika utalii yanazidi kuongezeka.”
Changamoto za kuendeleza Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu
Changamoto kubwa ya kusimamia Hifadhi za Bahaŕi na Maeneo Tengefu ni ulipuaji wa mabomu kutokana na kuongezeka kwa samaki katika maeneo hayo.
“Tunapata shida sana na uvuvi haŕamu katika maeneo hayo, baada ya kuyatunza samaki wamekuwa wengi wengi sana, kwa hiyo wahalifu wakilipua bomu na samaki kuelea wanachota samaki wengi. Kazi kubwa ni kusukuma utekelezaji wa sheŕia kwa kufanya doŕia za maŕa kwa maŕa ambazo ni za ghaŕama kubwa. Hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uvuvi haŕamu,” alisema Dk. Chande.