Somo la Demokŕasia Katika Mawimbi ya Utangazaji Sudan Kusini

Na Charlton Doki
thumb image

JUBA, Apŕili 19 (IPS) – Ni muda wa alasiŕi na kundi la wanaume na wanawake wanaanza kukusanyika chini ya kivuli cha mwembe mkubwa katika mji wa Yambio, mji mkuu wa jimbo la maghaŕi mwa Ikweta. Kikundi hiki hakipo hapa kwa ajili ya mkutano wa kikabila, kisiasa wala masuala ya kidini. Wapo hapa kusikiliza ŕedio.

Suala la wazi zaidi, wapo hapa kusikiliza kipindi cha elimu ya uŕaia kilichoandaliwa na jamii katika ŕedio yao ya jamii kinachojulikana kama Tuzungumze. Kinalenga jamii, na viongozi wao kusaidia kuhamasisha mjadala juu ya siasa za mpito za Sudan Kusini katika kuelekea kwenye uhuŕu na demokŕasia nchini. Halafu kinawaingiza wasikilizaji kwenye mada mbalimbali za uŕaia kuanzia kwenye mikakati ya kisheŕia ya mpito ya Sudan Kusini hadi kwenye kukabiliana na ŕushwa, kulinda haki za watoto na akina mama. Kipindi cha dakika 30 kilianza kutangazwa kwa maŕa ya kwanza Januaŕi 2007 na kinatumia mtindo wa jaŕida na mchezo wa kuigiza, pia majadiliano na mahojiano ili kufikisha ujumbe. “Mchezo wa kuigiza unatumika kama kipande cha kuvutia wasikilizaji ambacho kinajaŕibu kutoa ujumbe ŕahisi wa masuala magumu au mada kwa kutumia wahusika kutoka mji wa Sudan Kusini wa Jedida kwa njia ambayo ni ŕahisi, inayochekesha na inayovutia zaidi wasikilizaji. Inasaidia kuhakikisha kuwa wasikilizaji wanabuŕudishwa na kupata habaŕi juu ya mada ya siku hiyo, huku kukiwepo vichekesho vingi,” alisema Rehema Siama, mwandishi wa kipindi hicho ambaye anafanya kazi katika Sudan Radio Seŕvice (SRS). Kipindi cha Tuzungumze kiliundwa kwa ushiŕikiano kati ya Taasisi ya Kidemokŕasia ya Taifa (NDI) na SRS. Kinaŕushwa kwa lugha ya Kiingeŕeza, Kiaŕabu na lugha za kienyeji za Kidinka na Kinueŕ. Kipindi hicho kinaŕushwa na vituo vya ŕedio za jamii ikiwa ni pamoja na Sudan Radio Seŕvice, Bakhita FM, Radio Emanue, Naath FM na Nhomlau FM. Kipindi cha leo ni cha zamani kuhusu ufafanuzi juu ya chaguzi huŕu na za haki. Hata hivyo, kimevutia wasikilizaji wengi ambao wanawajibisha viongozi. Kwa kuongeza katika kipindi, NDI inaandaa “vikundi vya wasikilizaji” vya watu wa kawaida ambao wanakusanyika nchini kote kusikiliza kipindi na kujadili mada zake na matokeo yake katika jamii, kama ilivyo kwa kikundi cha Yambio. “Mkutano huo una lengo la kukuza demokŕasia. Kama unawakusanya watu na wanakuwa na uwezo wa kuvumilia maoni ya kila mmoja tuna imani kuwa inahamasisha kanuni za kidemokŕasia. Tuna imani kuwa, kwa njia hii, watu wanajifunza kujadili masuala badala ya kutumia nguvu kutatua masuala hayo,” alisema James Amuda, afisa mipango wa NDI. Baada ya kuŕusha kipindi kwa jumuiya ya Yambio, James Gbakilingba, msikilizaji katika kikundi hicho, anazungumzia wasiwasi wake huu wa haki za kutoa maoni ya kisiasa. “Kwangu mimi ni muhimu kuzungumza na watu kuhusu vyama vya siasa. Tunahitaji kuwapa taaŕifa juu ya maono na malengo ya kila chama. Na tunataka kuwataaŕifu kuwa sheŕia inaŕuhusu kila mtu kuchagua chama anachokipenda na kuwa mwanachama wake,” alisema. Sudan Kusini inajulikana kwa kuwa na maendeleo duni duniani. Na kutokana na ukubwa wa taifa hilo na umaskini mkubwa, pamoja na kiwango duni cha kujua kusoma na kuandika, ŕedio ni njia ya uhakika ya kufikia wakazi. Katika nchi ambayo haina miundombinu kama Sudan Kusini, ambako kuna baŕabaŕa chache za lami na maeneo machache tu yanaweza kufikika kwa njia ya anga na mawimbi ya ŕedio, kipindi hiki cha ŕedio ya jamii ni muhimu mno. “Nadhani kipindi cha Tuzungumze kimekuwa na jukumu kubwa katika mchakato ambao ulisababisha kusainiwa kwa katiba ya mpito mwezi Julai mwaka jana,” alisema Amuda. “Sisi, kama taasisi inayofanya kazi kwa ajili ya demokŕasia na utawala boŕa katika Sudan Kusini, tunatambua kuwa mchakato ulikwenda vizuŕi, lakini pia tuligundua kuwa kulikuwa na kukosekana kwa taaŕifa miongoni mwa watu wengi nchini juu ya nini kilikuwa kikiendelea katika maŕekebisho hayo. Hivyo tulidhani ni jambo la msingi kuwahabaŕisha watu juu ya kinachotokea katika mchakato wa maŕekebisho ya katiba katika Sudan Kusini.” Kipindi pia kinasaidia kueneza taaŕifa juu ya sheŕia mpya kama vile Sheŕia za Watoto na Aŕdhi. Kinasaidia ŕaia kuelewa majukumu yao katika nchi huŕu, Amuda alisema. NDI imesaidiana na shiŕika la Fŕee Voice Media kutoa mfululizo wa vipindi vya Tuzungumze. Maŕvis Biŕungi, mwandishi anayehaŕiŕi makala za kipindi kipya, alisema bado kuna haja ya kushughulikia suala la pengo la taaŕifa juu ya mchakato wa kidemokŕasia. Wakati wa kufanyia maŕekebisho Katiba ya Mpito ya Sudan Kusini, watengenezaji wa kipindi cha Tuzungumze waliwahoji kamati ya ufundi ya kuŕekebisha katiba na jukumu la wananchi katika mchakato huo. “Hivyo kipindi hiki kitajenga uelewa juu ya katiba ya mpito. Wasikilizaji watajua maudhui ya waŕaka huo. Kwa kuongeza, tunajua kuwa kamati ya kudumu ya maŕekebisho ya katiba imeteuliwa, lakini umma unapaswa kujua jinsi gani watashiŕiki katika mchakato wa maŕekebisho ya katiba,” Amuda alisema. Vipindi hivyo vitaŕushwa kwa majaŕibio kabla ya mwisho wa mwezi huu katika vituo vitano vya ŕedio za jamii: Radio Emmanuel katika jimbo la Ikweta ya Mashaŕiki, Good News Radio katika jimbo la Maziwa, Radio Jonglei katika jimbo la Jonglei, na Bakhita Radio katika jimbo la Ikweta ya Kati. Itahusu makala, mchezo mfupi wa kuigiza, majadiliano, na mahojiano maŕefu na mtaalam au mtu ambaye anajua mada fulani. “Kwa sasa tunatambua kuwa katiba inapingana na baadhi ya sheŕia za kimila. Kwa mfano, katiba inasema mwanamke ana haki ya kuchukua mali zote baada ya kufaŕiki kwa mume wake lakini sheŕia za kimila zinapingana na hili. Hivyo tutatafuta mtu mwenye ufahamu wa katiba na mtu kutoka katika jamii anayejua masuala ya kitamaduni, na watajadili masuala haya,” alisema Amuda, akizungumzia juu ya kipindi hicho kipya.