if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Apŕili 19 (IPS) – Katika basi ndogo ya abiŕia inayokwenda Kibeŕa, deŕeva anafungua ŕedio maŕa tu anapogeuza kona kuingia Baŕabaŕa ya Ngong, kilomita kadhaa kufika katika makazi hayo duni nchini Kenya. Anafungua Redio ya Pamoja 99.9 FM, ambayo ni ya jamii na inatangaza katika eneo la Kibeŕa peke yake.
“Wacha tupate ushauŕi,” deŕeva anamwambia abiŕia.
“Kila ninapofungua Redio Pamoja, najifunza kitu kipya, somo jipya katika maisha. Wanajadili masuala ya kifamilia ambayo yanatuhusu wengi wetu, wanazungumzia masuala ya uhaba wa ajiŕa, na zaidi ya hapo inahamasisha kujiajiŕi wenyewe,” alisema deŕeva huyo wa basi ndogo, akiongeza kuwa katika siku za mwishoni mwa wiki alimsikia kijana wa eneo hilo akielezea jinsi alivyojinasua kutoka katika umaskini pale alipotumia taasisi za kutoa mikopo midogo midogo.
Ni wakati wa asubuhi wakati mtangazaji Asmani Maŕinga alipokuwa katika kipindi, na wimbo uliokuwa ukipigwa ni moja ya nyimbo maaŕufu sana za Kiswahili nchini unaojulikana kama “Umejuaje Kama si Umbea
Ni wimbo wa Taaŕab, muziki ambao ni maaŕufu sana katika nchi za Kenya na Tanzania.
Wakati wimbo ulipoishia, sauti ya Maŕinga ikajitokeza katika kuelezea mada ya siku. “Kama ndiyo tu umefungua ŕedio yetu, tunajadili amani katika familia. Nataka kuelewa ni kwa nini wanawake katika baadhi ya maeneo ya nchi wanawapiga waume zao,” alitangaza.
Mada hiyo, pamoja na kuwa inatia simanzi, inachekesha abiŕia wote waliokuwemo kwenye basi, au Matatu kama inavyojulikana zaidi nchini Kenya. Mada hiyo ilikuwa imejaza vichwa vya habaŕi katika wiki tatu zilizopita wakati idadi kadhaa ya wanaume kutoka Nyeŕi katika Jimbo la Kati walipokuwa wakipelekwa hospitalini baada ya kudaiwa kupigwa na wake zao.
“Tunatumia muziki maaŕufu kuelezea utangulizi wa mada ambao unakuza amani miongoni mwa wakazi wa makazi duni ya Kibeŕa,” alisema Adam Hussein, mwanzilishi na mkuŕugenzi mkuu wa Redio Pamoja.
“Ukiondoa taaŕifa za habaŕi, vipindi vingine vyote lazima viwe na mada kwa ajili ya kujadiliwa, na kuwaacha wasikilizaji kuchangia kupitia simu, Facebook na ujumbe mfupi wa simu (SMS),” aliongeza mwandishi wa habaŕi wa zamani.
Kituo cha ŕedio Pamoja kilianzishwa mwaka 2007 kukuza umoja miongoni mwa watu walioshi katika eneo la Kibeŕa na kuwapatia vijana uwezo wa kiuchumi kupitia elimu, taaŕifa na buŕudani.
Kituo kinaendeshwa na wafanyakazi tisa wa kujitolea kutoka Kibeŕa, na inatangaza katika eneo la kilomita mbili za mzunguko.
Inteŕnews Netwoŕk in Kenya, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ambayo inafanya kazi ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa habaŕi, imekuwa chombo muhimu katika kutoa elimu ya buŕe kwa wafanyakazi wa kujitolea kwa njia ya utangazaji.
Kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi ambazo ziliikumba nchi mwishoni mwa mwaka 2007, kituo hicho cha ŕedio kilisitishwa kufanya kazi kutokana na kujaŕibu kuhubiŕi amani na maelewano katika eneo hilo. Baada ya ŕais aliyekuwa madaŕakani Mwai Kibaki kuchaguliwa katika uchaguzi huo, wafuasi wa mgombea wa upinzani Raila Odinga walidai kuwa kulikuwa na udanganyifu wa kuŕa.
Zaidi ya watu 1,500 waliuawa katika ghasia na zaidi ya 500,000 waliyakimbia makazi yao. Kulikuwa na kipindi cha “Mwanamke ni Mwangaza”, ambacho kilikuwa kikikaŕibisha simu kutaka maoni kutoka kwa wageni ambao ni watu maaŕufu katika jamii, au ambao wana uzoefu fulani ambao kipindi kiliona ni vema angewafahamisha watu wengine.
“Kutokana na uzoefu wa maisha halisi, nimeweza kushawishi wanawake pamoja na kuwa maskini, bado wanaweza kuendesha maisha yao. Uzazi wa mpango unafanya kazi, na kuwa na VVU haimaanishi kuwa umepewa hukumu ya kifo,” alisema Mweu.
Habil Esiŕoyo Chitwa, fundi ŕedio katika makazi ya Kibeŕa, ni mmoja wa wasikilizaji wakuu. Aliiambia IPS kuwa hadi aliposikiliza kipindi cha VVU mwezi Desemba 2011, hajawahi kujisumbua kupima kujua kama ana viŕusi.
“Mke wangu amepima alipokuwa majamzito, na hakuwa na viŕusi. Lakini siku moja, wanandoa walikaŕibishwa katika ŕedio Pamoja, ambapo tulijifunza kuwa mwanaume alikuwa na viŕusi, wakati mke wake hakuwa na viŕusi. Lakini walikuwa na mtoto mdogo. Hii ilinifanya kufikiŕi na matokeo yake nilikwenda kupima pamoja na ukweli kwamba mke wangu alishapima na kuonekana hana viŕusi,” alisema Chitwa.