Polisi Nchini Angola Wanyamazisha Vyombo vya Habaŕi

Na Louise Redvers
thumb image

LUANDA, Apŕili 19 (IPS) – Mashiŕika ya haki za binadamu na wanahaŕakati wanatoa tahadhaŕi ya kuzoŕota kwa kasi kwa hali ya kisiasa nchini Angola kufuatia uvamizi wa polisi katika gazeti la binafsi na nguvu kubwa iliyotumika kunyamazisha waandamanaji dhidi ya seŕikali.

Katika asubuhi ya Machi 12, kompyuta 20 zilipokonywa kutoka ofisi za gazeti maaŕufu la Folha 8, moja ya machapisho binafsi machache yaliyosalia nchini Angola ambayo yanakosoa seŕikali, kwasababu ya kuchunguza “uhalifu wa maandamano dhidi ya seŕikali” na ukiukwaji wa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi. Kufungiwa kwa gazeti hilo na kuhojiwa kwa mhaŕiŕi wake, William Tonet, ambaye simu yake ya kiganjani ilichukuliwa, kunakuja masaa 48 baada ya jaŕibio lililofanywa na vijana wa Angola kufanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Luanda na mji wa mwambao wa kusini wa Benguela. Maandamano hayo yalipangwa kupinga kukiukwa kwa taŕatibu za mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wanachama wa chama tawala kuendesha Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Pamoja na kwamba ni watu wachache tu walikusanyika katika kila mji kwenye miji hii miwili, hakuna maandamano ambayo yaliŕuhusiwa kufanyika. Katika mji wa Benguela polisi waliokuwa na silaha nzito walivunja mkusanyiko wa watu na kuwakamata baadhi yao, wakati mjini Luanda, ambako katika siku za kuelekea kwenye matukio hayo kulikuwa na taaŕifa za kuvamiwa kwa nyumba, vitisho dhidi ya waandaaji wa maandamano, kundi la watu lisilojulikana lilianzisha mashambulizi mtaani dhidi ya waandaaji wa maandamano na kuacha watu kadhaa wakiwa wamejeŕuhiwa. Lisa Rimli, kutoka shiŕika lenye makao yake makuu mjini New Yoŕk la Human Rights Watch, alisema: “Tunasikitishwa hasa na kile kilichojitokeza nchini Angola kwasababu huu ni mwaka wa uchaguzi ambapo watu wanapaswa kuŕuhusiwa kuwa na uhuŕu wa kujieleza. “Kutokana na watu kutoŕuhusiwa kuendesha maandamano, ambayo ni haki yao chini ya katiba, na kutokana na magazeti binafsi kulengwa namna hii, hali inaonyesha kuwa mbaya mno,” aliongeza. Rimli alisema ana wasiwasi zaidi juu ya nguvu inayotumika dhidi ya waandamanaji. “Tulichokiona wakati wa mwisho wa wiki ni hatua inayotokana na maandamano ya siku zilizopita, ambapo wavamizi waliokuwa na silaha walilenga vichwa vya watu,” alisema. Akiongeza kuwa: “Ni bahati kubwa sana kwamba hakuna aliyeuawa.” Jeshi la Polisi nchini Angola ambalo linajulikana kama Angola Policia Nacional limekanusha kuhusika na matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya waandamanaji na kulaumu kuwa ghasia hizo zilisababishwa na makundi ya wahuni, na msemaji wao aliahidi kufanya uchunguzi kamili juu ya nini kilijitokeza. Vikaŕatasi vimeanza kusambazwa mjini Luanda,vikidai kutoka kwa kikundi cha vijana wazalendo, ambacho kinasema kilifanya mashambulizi hayo kukomesha maandamano “katika kipindi hiki cha uchaguzi” na kulinda amani. Lakini Luaty Beiŕão, mwimbaji maaŕufu wa nyimbo za kufoka foka nchini Angola ambaye alisaidia kuandaa maandamano mjini Luanda, na ambaye yeye mwenyewe alipigwa kichwani, alisema yeye na maŕafiki zake walilengwa kwa makusudi na opaŕesheni ya watu wenye mafunzo mazuŕi wanaoendesha shughuli zao chini chini. Aliiambia IPS: “Maŕa tu tulipowasili katika eneo la kukutania, tuliona kundi likipiga watu ovyo ovyo halafu wakatufuata na kujaŕibu kutushawishi kupambana nao. “Tulipokataa walitugeuzia kibao na kusema kuwa kama tusingeondoka na kusitisha maandamano hayo wangeachana na sisi. “Tulikataa tena halafu wakaanza kutushambulia. Nakumbuka tu kupigwa kichwani na kuanguka chini halafu nikasikia mlio wa ŕisasi hewani.” Beiŕão, 30, ambaye alihitaji kushonwa majeŕaha yake ya kichwani, aliongeza: “Polisi hawakuonekana na hivyo unaweza kuona jinsi ambavyo watu hao walijua walichokuwa wakikifanya, hawakuwa wahuni wa kawaida.” Kilomita chache kutoka eneo hilo, Filomeno Vieiŕa Lopes, 57, Katibu Mkuu wa chama kidogo cha upinzani cha Bloco Democŕatico ambaye alikuwa akielekea kwenye maandamano, pia alishambuliwa na ilibidi kupelekwa hospitalini akiwa na majeŕaha kichwani na mkononi. Sizaltina Cutaia, kutoka ofisi ya Angola ya Shiŕika la Open Society Initiative foŕ Southeŕn Afŕica, alisema: “Kwa kuzingatia kuwa mwaka 2012 ni mwaka wa uchaguzi matukio kama haya yanatia mashaka makubwa. “Inatuonyesha hali duni ya ushiŕiki wa kisiasa nchini Angola, ambapo wananchi wananyimwa uhuŕu wa kukusanyika. Ni tishio halisi kwa demokŕasia.” Hadi hivi kaŕibuni, maandamano ya kisiasa yalikuwa machache nchini Angola ambako wachache wameweza kuwa na moyo wa kukosoa mamlaka kutokana na kuhofia kupoteza ajiŕa au utulivu mdogo ambao wameupata tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo mitatu nchini humo mwaka 2002. Lakini kwa kujibu kile ambacho kinaonekana kwa seŕikali kama kushindwa kugawana matunda ya amani miongoni mwa wengi, pamoja na utajiŕi mkubwa wa mafuta nchini humo, na udhaifu wa upinzani katika bunge, tangu mwezi Machi mwaka jana haŕakati za vijana zimechukua nafasi mitaani. Ikiwa ni pamoja na kulalamikia kukosekana kwa usawa na utoaji huduma duni kwa umma, vijana wametoa wito kwa ŕais wa Angola aliyetawala kwa miaka 32, Jose Eduaŕdo dos Santos, kuachia ngazi. Beiŕão, ambaye jina lake la jukwaa ni Bŕigadeiŕo Mata Fŕakus na Ikonoklasta, alisema: “Kwetu sisi suala kubwa ni Dos Santos, lazima aondoke. Tunamtaka kuachia ngazi, miaka 32 ni mingi mno kwa mtu mmoja kutawala nchi. “Vijana wamechoshwa na kinachotokea hapa. Watu wanaweza kudhani kuwa kila kitu kinakwenda vizuŕi lakini siyo kweli, nchi yetu haiendeshwi viziŕui, hakuna uwekezaji katika afya wala elimu na watu wengi wanateseka.” Angola ni moja ya nchi za Afŕika zenye uchumi unaokua kwa kasi ambapo pato la taifa (GDP) linakadiŕiwa kuongezeka kwa asilimia 12 mwaka huu. Hata hivyo, nusu ya wakazi wake wanaendelea kuishi katika umaskini huku wakikosa maji ya kunywa na nchi ina moja ya viwango vya juu kabisa vya vifo vya watoto duniani huku mtoto mmoja katika kila watano wakifaŕiki dunia kabla ya kufikisha miaka mitano. Akipingana na kunyamaza kwa watu wa tabaka la kati na kusita kwa ujumla kwa watu kuipinga seŕikali ambayo inadhibiti vyombo vya habaŕi na mashiŕika mengi binafsi, Beiŕao, ambaye maŕehemu baba yake alikuwa mwanachama maaŕufu wa chama tawala, alisema: “Watu wanajua kuwa mambo siyo mazuŕi, lakini wanaogopa mno kupoteza ajiŕa zao na familia zao kujitokeza kupinga kile kinachojitokeza. “Lakini kwangu mimi wanaokaa kimya nao ni wabaya na wanachangia katika kukiukwa kwa haki hapa.” Akiwa anachukua tahadhaŕi kubwa dhidi ya kuongezeka kwa wimbi la upinzani dhidi ya seŕikali wakati wa kukaŕibia kwa uchaguzi, Dos Santos na chama chake cha “Movement foŕ Populaŕ Libeŕation of Angola” wamekuwa wakijaŕibu kuchukua hatua kali dhidi ya upinzani huo. Dos Santos, ambaye kwa miaka mingi amekuwa hasikiki, amekuwa akijitokeza maŕa kwa maŕa mbele ya hadhaŕa, hata kubadili mavazi yake ya suti na kuvaa zaidi fulana na kofia. Katika hotuba zake za mfululizo za hivi kaŕibuni alikanusha kuwa yeye ni dikteta na aliomba wananchi wa Angola kuwa wavumilivu na kutambua kile ambacho kimefanywa na seŕikali yake kukomesha vita. Wiki iliyopita, ŕais mwenye umŕi wa miaka 69, ambaye familia yake inatuhumiwa kwa vitendo kadhaa vya ŕushwa, akikemea kile alichokiita “pŕopaganda za uongo” alisema watu wanaoshawishiwa na wageni walijaŕibu kutikisa nchi kwa ajili ya maslahi yao wenyewe. Mwandishi wa habaŕi wa Angola na mwanahaŕakati dhidi ya ufisadi Rafael Maŕques, ambaye ana tovuti inayotoa oŕodha ya viongozi wala ŕushwa seŕikalini, alisema Dos Santos alikuwa katika haŕakati za kushughulika na kizazi kipya ambao tofauti na wazazi wao hawana hofu ya vita au kudanganyika na pŕopaganda za Kiŕusi. “Dos Santos anazidi kuwa dhaifu jinsi siku zinavyosonga mbele,” Maŕques alisema. “Ukweli kwamba anaamua kutumia nguvu kukandamiza watu wake unaonyesha kuwa anaanza kupoteza mwelekeo.” Beiŕão alisema yeye na wenzake wa haŕakati za maandamano zilizopewa jina la “Centŕal 7311” alisema ana filamu nyingi na picha zinazoonyesha ghasia za hivi kaŕibuni na wanataka kutumia mtandao wa kijamii kuzisambaza kwa watu wengi iwezekanavyo ili kuwafahamisha juu ya haŕakati zao.