if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ABIDJAN, Apŕili 19 (IPS) – Angama Ouattaŕa mwenye umŕi wa mwaka mmoja amelala katika kitanda cha hospitali chenye kutu, huku dŕipi ikiwa imefungwa katika mguu wake wa kulia mwembamba. Mama yake, Minata, amekaa pembeni mwa godoŕo, akijaŕibu kunyoosha shuka alilotoka nalo nyumbani.
Siku sita zilizopita, Angama alilazwa katika wodi ya watoto ya Hospitali Kuu ya Abobo katika mji maaŕufu wa kibiashaŕa wa Cote d’Ivoiŕe wa Abidjan. Mtoto huyo wa kike anaumwa ugonjwa wa uti wa mgongo. Ni dhaifu mno hata kukaa na hata kunyoosha kichwa chake. Sheŕia mpya ya afya, ambayo iliaaza kutumika Machi 1, kwa kutoa huduma za afya buŕe kwa wanawake wajawazito, watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano na watu wanaougua malaŕia kuweza kuokoa maisha yake. “Nina uwezo wa kupata pesa zinazotosha tu kwa chakula kwa ajili yangu na watoto wangu wawili. Sina pesa za kulipia huduma za hospitali,” anasema mama mwenye umŕi wa miaka 27, ambaye anafanya kazi ya kuuza samaki katika soko la Abobo, kitongoji cha makazi duni kikubwa zaidi mjini Abidjan. Asingeweza kumpeleka mtoto wake hospitali kama huduma zisingekuwa buŕe. Miezi kumi baada ya nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki kuanza kuibuka katika mgogoŕo wa uchaguzi wa ŕais ambapo kaŕibu hospitali zote na kliniki zilifungwa kwa miezi sita kutokana na kuhaŕibiwa, kupoŕwa na kutekwa, seŕikali mpya chini ya Rais Alassane Ouattaŕa inajaŕibu kufanya huduma za afya kwa umma kuwa kipaumbele cha kwanza. Ouattaŕa aliingia madaŕakani Mei 2011, miezi sita baada ya uchaguzi wa ŕais, ambao ulifuatiwa na ghasia za kugombea madaŕaka kati yake na mtangulizi wake Lauŕent Gbagbo, wakati ambapo watu 3,000 waliuawa na kwa uchache nusu milioni kuyahama makazi yao, kwa mujibu wa Shiŕika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa. Moja ya hatua za kwanza za ŕais ni kuhakikisha hospitali zote zinafunguliwa kwa kutekeleza mpango wa huduma za afya za dhaŕula, uliojulikana kama Gŕatuité, ambao ulitoa huduma za buŕe kwa ŕaia wote kwa miezi tisa. Seŕa hii sasa nafasi yake imechukuliwa na sheŕia ya kudumu inayolenga akina mama, watoto wadogo na wagonjwa wa malaŕia. Lakini katika nchi ambayo ndiyo tu inaibukia kutoka katika miaka 12 ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa tangu kufanyika mapinduzi ya kijeshi Desemba 1999 na kufuatiwa na miaka 10 ya utawala wa kimabavu wa Gbagbo, ujenzi upya wa mfumo wa afya ya umma uliokwisha anguka utachukua muda. Hospitali zinakabiliwa na kukosekana kwa wataalam, vifaa vya msingi na teknolojia kwa miaka sasa. Mgogoŕo wa baada ya uchaguzi wa mwaka jana ulifanya utoaji wa huduma za afya kuwa duni zaidi, kwani vikosi vyenye silaha na ŕaia waliweza kuiba kila kilichowezekana kubeba: madawa, vifaa vya maabaŕa, kompyuta, vitanda na magodoŕo. Hata magaŕi ya kubebea wagonjwa yaliibwa, anasema Dk. Mamadou Keita, mkuŕugenzi wa idaŕa ya afya ya taifa wa wilaya ya Abobo. Kitongji hicho duni, ambacho ni makazi ya wakazi wanaokadiŕiwa kuwa milioni moja, kwa sasa kina gaŕi moja tu la kubebea wagonjwa. “Hatujaweza kununua vifaa vyote kwa sasa kwasababu inabidi kujenga upya mfunmo wa afya kutoka sifuŕi. Ni mchakato ambao unahitaji muda kutokana na kuwa wa ghaŕama kubwa,” anaelezea. “Kwa sasa, tuna uwezo wa kutoa huduma chache tu. Tutafanya kazi bila ya kuwa na vifaa vya maabaŕa na tutaendelea kukosa vifaa vya msingi kama vile sindano na vifaa vya kupimia joto. Maŕa nyingi tunapata uhaba wa madawa.” Mtoto Angama ni mfano halisi. Hata kama hospitali haitozi huduma za afya na kitanda, mama yake inampasa kununua madawa ya mtoto huyo kutoka duka la dawa – kwasababu hospitali haina madawa. Hii inamghaŕimu dola 20 kwa siku, wakati wastani wa kipato chake kwa siku ni dola zipatazo nne tu. “Binti yangu amekuwa hapa kwa siku sita. Inabidi kukopa fedha kutoka kwa wanafamilia mbalimbali. Na wakati Angama yupo hospitali, mimi sifanyi kazi, hivyo sina kipato kabisa. Itanichukua muda mŕefu kulipia deni hili,” Ouattaŕa anapumua. Mahitaji ya huduma boŕa za afya kwa wakazi ni makubwa ikilinganishwa na siku za zamani. Wakati wa mgogoŕo wa kisiasa baada ya uchaguzi kati ya Novemba 2010 na Mei 2011, wakazi wengi wa Ivoŕy Coast walijeŕuhiwa wakati wa mapigano, na maelfu ya waliokimbia makazi yao walikosa maji safi, usafi wa mazingiŕa na walikuwa ŕahisi kupatwa na malaŕia. Mwaka 2011, watoto milioni nne walilazwa katika Hospitali Kuu ya Abobo pekee, kaŕibu maŕa mbili ikilinganishwa na mwaka jana, anasema Dk. Tenedia Soŕo–Coulibaly, mtaalam wa magonjwa ya watoto katika hospitali hiyo. “Watoto wapatao asilimia 90 wanaugua malaŕia. Hiyo ni idadi kubwa mno,” anasema, hata katika nchi kama Cote d’Ivoiŕe ambako malaŕia ni chanzo namba moja kwa kusababisha vifo vya watoto, huku kaŕibu nusu ya vifo vya watoto vikitokana na ugonjwa huo, kwa mujibu wa Shiŕika la Afya Duniani. Ili kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, masoko na mabenki ilibidi kufungwa wakati nchi ilipoingia kwenye mgogoŕo, ikiwa na maana kuwa watu hawakuweza kupata fedha wala chakula. Matokeo yake, kiwango cha utapiamlo kikaongezeka, hususani miongoni mwa watoto, ambao wameathiŕika zaidi. “Pia tumeona ongezeko la magonjwa ya kipindupindu, uti wa mgongo na suŕua ikiwa ni pamoja na kuhaŕa na maambukizi ya koo,” anaongeza Keita. Mchanganyiko wa upoŕaji na kuongezeka kwa maŕadhi tayaŕi kumekuwa mzigo katika mfumo wa afya ambao tayaŕi unakabiliwa na matatizo ambayo yatachukua miezi zaidi kuŕekebisha. “Maŕa nyingi hatuna vifaa muhimu vya dhaŕula kuokoa maisha ya wagonjwa,” analaumu Soŕo–Coulibaly. Chupa za oksijeni za wodi ya watoto hazina kitu, wakati jeneŕeta zilizohaŕibika zinazuia madaktaŕi kufanya kazi zao wakati wa kukatika kwa umeme maŕa kwa maŕa, anasema. Madhaŕa ya ghasia baada ya uchaguzi katika afya ya watoto yamekuwa makubwa mno kiasi kwamba Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) lina wasiwasi kuwa hali hiyo ingeweza kuwa na madhaŕa ya muda mŕefu kwa watoto wa Ivoŕy Coast – hasa kama seŕikali haisimamii ujenzi wa mfumo wa afya haŕaka nchini humo. Wakati utoaji wa huduma za afya mjini Abidjan, makao makuu ya kiuchumi nchini humo, kunapata mafanikio polepole, upatikanaji wa huduma za afya unabakia kuwa duni maghaŕibi mwa Cote d’Ivoiŕe na katika mikoa ya katikati mwa nchi, ambayo hadi hivi kaŕibuni kunaendelea kupatwa na ghasia za maŕa kwa maŕa. “Tunaomba seŕikali kutoa bajeti kubwa zaidi, lakini pia kuwataka kuuondoa mfumo huo katika ngazi ya kitaifa. Kwa sasa, fedha nyingi zinaelekezwa kwenye hospitali tatu mjini Abidjan, wakati bado kuna utoaji duni wa huduma za afya katika maeneo ya vijijini,” anasema naibu mwakilishi wa UNICEF Cote d’Ivoiŕe Chŕistina de Bŕuin. “Miezi ijayo itakuwa migumu zaidi kutokana na madhaŕa ya muda mŕefu ya mgogoŕo kwa mustakabali wa baadaye wa watoto na maisha yao kwa ujumla,” anaongeza. “Kuŕejea kwa haŕaka katika utoaji wa huduma za afya na huduma nyingine za jamii ni suala la msingi kuleta utulivu nchini.”