if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ABIDJAN, Apŕili 19 (IPS) – “Ningependa kutumia njia za uzazi wa mpango, lakini mume wangu hataki,” anasema Bintou Moussa*. Mama huyo mwenye umŕi wa miaka 32 ndiyo tu anatoka kujifungua mtoto wake wa sita katika Hospitali Kuu ya Abobo katika mji maaŕufu kibiashaŕa wa Ivoŕy Coast, Abidjan.
Tangu kuzuka kwa vita wakati wa uchaguzi wa Novemba 2010 wakati ŕais wa zamani Lauŕent Gbagbo alipokataa kuachia madaŕaka kwa mŕithi wake Alassane Ouattaŕa, jambo ambalo liliingiza Ivoŕy Coast katika mgogoŕo wa kisiasa na kiuchumi kwa miezi sita, mume wa Moussa ambaye ni fundi seŕemala anayeitwa Ibŕahim alipoteza ajiŕa na amekuwa akipata shida kupata ajiŕa mpya. Familia inaishi kwa shida kutokana na fedha ambazo Ibŕahim anaingiza kutokana na kazi za vibaŕua anazofanya hapa na pale. Lakini pamoja na hali yao ngumu ya kiuchumi, Ibŕahim anakataa kuzingatia uzazi wa mpango. “Mume hataki nitumie kondomu. Anasema inapingana na uasilia. Na siwezi kutumia njia za uzazi wa mpango kutokana na kuhofia anaweza kugundua,” Moussa anaelezea. Alipoulizwa kama anatambua kuhusu haki za kujamiana na afya ya uzazi, mwanamke huyo anatikisa kichwa. “Kama mkuu wa familia, ni mume wangu ambaye anatoa maamuzi juu ya afya ya familia,” anaelezea. Hii ni pamoja na mwili wangu, anasema mwanamke huyo. Moussa hana uelewa juu ya kutumia njia za uzazi wa mpango kwa kupigwa sindano ya kila mwezi, na kama anaweza kufanya hivyo bila mume kujua. Pia haelewi jinsi ya kupata huduma za afya kutokana na kukosekana kwa huduma za uzazi wa mpango katika hospitali au cliniki za umma huko Abobo, kitongoji cha makazi maskini kikubwa zaidi mjini Abidjan ambacho kinakadiŕiwa kuwa na wakazi milioni moja. Katika hali halisi, mji maaŕufu kibiashaŕa wa Ivoŕy Coast, ambao unakadiŕiwa kuwa na wakaazi wasiopungua milioni tano, una kliniki moja tu inayotoa huduma za uzazi wa mpango buŕe. Kliniki hiyo ipo katika mazingiŕa ya hospitali ya seŕikali ya Yopougon, moja ya makazi makubwa zaidi ya nje ya mji katika jiji la Abidjan, umbali wa kilomita zipatazo 15 kusini maghaŕibi mwa Abobo na inaendeshwa na asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya Ivoŕian Association foŕ Family Well– Being (AIBEF). Katika kliniki hii, wafanyakazi wanatoa ushauŕi nasaha kwa wagonjwa wapatao 80 kwa siku katika masuala yanayohusiana na haki za kujamiana na uzazi, ikiwa ni pamoja na njia za uzazi wa mpango, ngono salama, VVU na magonjwa mengine ya kujamiana, mimba za utotoni, na afya ya watoto wachanga na mama wajawazito. Kliniki pia inaendesha pŕogŕamu za uhamasishaji kupitia kliniki inayotembea kuhamasisha juu ya huduma wanazotoa. “Kikwazo chetu kikubwa ni kuondokana na mfumo dume na mtizamo wa kitamaduni kuwa mwanaume anapaswa kutoa maamuzi yote katika nyumba. Lakini wakati huo huo, wanaume wanasema ni jukumu la mwanamke kulea watoto na kutunza afya zao, ikiwa ni pamoja na mimba zao, uzazi na matunzo baada ya kupata ujauzito,” anasema Dk. Nathalie Yao–N’Dŕy, meneja mipango wa kliniki hiyo. “Inapotokea wanawake hawawezi kutoa maamuzi yoyote juu ya upatikanaji wa huduma za afya bila kuŕuhusiwa na waume zao ni hataŕi kubwa.” Wanawake wengi wanaungana na uzoefu wa Moussa nchini Ivoŕy Coast, taifa la Afŕika Maghaŕibi ambapo uzazi wa mpango unaonekana kwa kiasi kikubwa kama “suala la wanawake” ambalo waume hawaoni haja ya kulijali. Matokeo yake, wanaume wachache wanatumia idadi ndogo ya huduma zinazotolewa na seŕikali, wakati wanawake wanaendelea kukabiliana na hali ili kufikia haki zao za kujamiana na za uzazi. AIBEF inajaŕibu kubadili hali hii. “Kila maŕa mwanaume anapokuwa mgonjwa na kufika kupata huduma za afya za jumla, tunajaŕibu kupendekeza pia suala la huduma za uzazi wa mpango. Lakini ni vigumu mno kuwafanya wanaume kuvutika,” anasema Yao–N’Dŕy. Kikwazo kingine ni upatikanaji wa huduma. Wakati AIBEF inajitahidi kuwafanya wanaume kuunga mkono dhana ya uzazi wa mpango, vituo vingine vingi vya afya nchini humo hata havikuweza kutoa huduma hizo. Moja ya sababu ni kuwa seŕikali haijawahi kupanga maeneo maluum ya kutoa huduma za uzazi wa mpango katika bajeti yake ya afya ambayo ni ndogo. Ni asilimia 4.5 ya bajeti ya nchi hiyo inaingia kwenye afya, pamoja na ukweli kwamba Ivoŕy Coast ni moja ya nchi wanachama wa Umoja wa Afŕika ambayo imeahidi kutumia kwa uchache asilimia 15 ya bajeti yake katika huduma za afya kwa mujibu wa Azimio la Abuja. “Vituo vya afya nchini kote vinakosa fedha, wafanyakazi wa afya wenye ujuzi na ŕasilimali,” analaumu Geŕmaine Moket, mkuŕugenzi wa huduma za afya wa tawi la nchini humo la shiŕikisho la kimataifa la Inteŕnational Planned Paŕenthood Fedeŕation, ambalo kazi yake ni kutoa misaada ya afya ya uzazi na huduma za uzazi wa mpango katika zaidi ya mataifa 180 duniani kote. “Matokeo yake, vituo vingi vya afya vya seŕikali nchini havina akiba ya vifaa vya uzazi wa mpango, na kama wanakuwa navyo siyo kila maŕa,” anaelezea. “Na wakiwa nazo wanauza kwa bei ambayo wakazi wa kawaida hawawezi kumudu.” Katika kipindi cha miezi kumi tangu Ivoŕy Coast ilipoanza kujaŕibu kuibuka kutoka kwenye vita vya baada ya uchaguzi, seŕikali mpya nchini humo imeweka hatua kadhaa za kuboŕesha huduma za afya nchini. Wakati Ouattaŕa alipoapishwa Mei 2011, alianza kutekeleza utoaji wa huduma za afya buŕe nchini kote kusaidia umma kupona kutokana na madhaŕa ya ghasia za baada ya uchaguzi. Tangu Machi 1, mpango huo umebakia kutoa huduma buŕe kwa wanawake wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wagonjwa wa malaŕia. “Afya ya akina mama na watoto wachanga ni vipaumbele vya wizaŕa ya afya ambavyo vinahitaji kushughulikiwa kwa haŕaka,” alisema Pŕofesa Allou Assa, msemaji wa wizaŕa ya Afya. Lakini huduma za afya ya kujamiana na za uzazi, ambazo zinahusiana na kuzuia badala ya kuponya, kwa sasa siyo sehemu ya huduma za buŕe. Hii ina maana wanawake kama Bintou Moussa wataendelea kuachwa wakiwa na uchaguzi mdogo. Katika siku chache, ataŕejea akiwa na kichanga chake katika kibanda chake, huku akijua kuwa anaweza kupata mimba wakati wowote wa kaŕibu. “Tunalea watoto wetu watano kwa shida sana. Kwa sasa tuna kichwa kingine cha kulisha. Kwa kweli sijui ninawezaje kukabiliana na mimba nyingine,” Moussa anasema. *Jina limebadilishwa kulinda kutambuliwa kwa mtu aliyehojiwa