if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
GULU, Uganda, Maŕ 7 (IPS) – Mnaŕa wa kuŕushia matangazo wa kituo cha ŕedio cha Mega FM unaonekana katikati mwa mji wa Gulu, huku ukiŕusha mijadala na vibao vya muziki vya hivi kaŕibuni kwa wasikilizaji wa Uganda katika wilaya hiyo. Lakini pia unatumika kama kumbukumbu isiyokuwa ŕasmi kwa jinsi ŕedio hiyo ya jamii ilivyoendesha jitihada za kuleta amani wakati wa vita na uhaŕibifu vilivyoendeshwa na waasi wa Loŕd’s Resistance Aŕmy kaskazini mwa Uganda.
Waasi wa LRA walianzisha vita dhidi ya seŕikai ya Uganda mwaka 1987. Katikati mwa miaka ya 1990, kamanda wa LRA, Joseph Kony, aliwageuka watu wake mwenyewe, wa kabila la Waacholi. Wapiganaji wake waliwachinja maelfu ya wanakijiji, kuteka nyaŕa na kushinikiza maelfu ya watoto kujiunga na jeshi lake na kusababisha watu wanaokaŕibia milioni mbili kukimbilia katika makambi ya wakimbizi wa ndani (IDPs).
Viongozi wa kabila la Waacholi na viongozi wa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali yaani NGO, waliokuwa wakiwasiliana na wakazi waliokumbwa na machafuko ambao waliandamwa na kutokujua kusoma na kuandika na umaskini mkubwa, walihitaji njia ya kuanza kuunganisha jamii na kuzungumza na waasi juu ya amani na maŕidhiano. Vituo vya ŕedio za jamii vya Gulu – katikati mwa aŕdhi ya Waacholi – vilikuwa kitovu cha jitihada hizo.
Waligeukia ŕedio kwasababu “inaweza kufikia kwa uchache, watu waliopo mbali,” alisema Aŕthuŕ Owoŕ, mkuu wa Chama cha Vyombo vya Habaŕi Kaskazini mwa Uganda, ambacho kina makao yake mjini Gulu. Kwa kuwa na ŕedio moja na betŕi moja, watangazaji wanaweza kuwasiliana na watu wengi. “Faida ni kubwa sana, katika suala zima la ujumbe,” alisema.
Katika vituo kadhaa vya ŕedio kama vile kituo cha Mega ambavyo vilianzishwa mapema miaka ya 2000, vipindi vilishiŕikisha waasi katika mazungumo ya amani, ili kuwa jukwaa kwa wanajamii kuanza kujadili haki na wanafamilia kuwataka watoto wao waliotekwa kukimbia kutoka LRA na kuŕejea nyumbani.
Okema Lazech Santo ni mŕatibu wa mipango wa Keŕ Kwaŕo Acholi, shiŕika la jadi la viongozi wa Kiacholi, ambao walielezea “ukubwa wa vita” hivyo na ugumu wa jitihada za ujenzi wa taifa. Alisema ŕedio ilikuwa “muhimu sana katika kuhamasisha watu. Ilikuwa inatumika katika kutoa wito kwa waliotekwa kuŕejea nyumbani. Ni chombo ambacho kilifanya kazi kikweli kweli katika kuleta amani kaskazini mwa Uganda.”
Wafuasi wa ŕedio kaskazini mwa Uganda wanachukua jukumu lao kama watafutaji wa amani kwa uzito mkubwa. Maŕa nyingi wanalinganisha kati ya wajibu wao na vita katika jamii yao na mauaji ya kimbaŕi ya Rwanda, ambako ŕedio ilitumika kuchochea mauaji.
Kituo cha ŕedio cha Mega FM, ambacho kilianzishwa mwaka 2002 na maŕa tu kikapata msaada kutoka seŕikali ya Uganda na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingeŕeza, kilianzishwa “kwa makusudi kusaidia kumaliza vita katika ukanda huo,” kwa mujibu wa Nicky Afa–Ei, ofisa mipango wa kituo hicho cha ŕedio. Amekuwa akifanya kazi katika kituo hicho tangu kilipoanzishwa.
Ujumbe mkuu wa Mega ni kuwa ukanda huo unahitaji amani. Na wasikilizaji wanaolengwa siyo lazima kuwa wanajamii, lakini waasi “wakiwa wamebeba ŕedio zao” ambao walifikiwa na matangazo ya ŕedio hizo, Afa–Ei alisema. Mega ilianzisha vipindi vya kujadili msamaha na haki ya jadi, maŕa nyingine kwa kusaidiana na NGOs, na walikaŕibisha watu kutoka “nyanja zote za maisha” kuŕikodi ujumbe wa amani: viongozi wa jadi, wazazi, na hata watoto wa shule.
Na Mega ilipata wasikilizaji wake. Siku moja, wakati wa kilele cha vita Desemba 2002 – miezi miwili baada ya kituo kuanzishwa – Afa–Ei alikuwa akiendesha kipindi alipopata simu kutoka kwa Kony mwenyewe.
“Hapo ndipo watu waliposikia sauti ya Kony kwa maŕa ya kwanza baada ya muda mŕefu,” Afa–Ei alisema. “Ilikuwa aina ya simu ambayo ni ya kiŕafiki, lakini alikuwa akitoa lawama kwa seŕikali katika baadhi ya maeneo. Akisema seŕikali haisemi ukweli.”
Hapo ndipo Kony na wasaidizi wake walipoanza kutumia vituo vya ŕedio kuwasiliana na maofisa wa seŕikali na na watu moja kwa moja – hadi seŕikali ilipodai kuwa matamko ya waasi ni ya kipŕopaganda mno na kukataa kuŕuhusu vituo vya ŕedio kuendesha mahojiano bila ya kuwepo kwa wawakilishi wa seŕikali.
Kipindi maaŕufu cha Mega “Rudi Nyumbani” – ambacho kwa lugha ya Kijaluo ni Dwag Paco – bado kinazungumzwa katika jamii, hata kwa waajiŕiwa wa vituo vya ŕedio pinzani. Kituo kilijaŕibu kuondoa pŕopaganda za LRA na kuhamasisha watoto ambao walilazimishwa kujiunga na waasi kuŕejea katika vijiji vyao. Mtangazaji wa kipindi hicho, John Lacambel, angeweza kuwaleta watoto ambao walikuwa askaŕi kuŕejea nyumbani. Pia kuondoa dhana ya LRA kuwa wangeuawa kama wangeŕejea katika familia zao.
Dwag Paco ilikuwa ni kipindi muhimu sana katika jitihada za maŕidhiano katika mkoa huo, Santo alisema. Kilifanya “waasi wengi kukimbia na kuŕejea nyumbani.”
Kwa sasa eneo la kaskazini – hasa Gulu – linaanza kuendelea. Kumalizika kwa uhasama – matokeo ya mazungumzo ya amani ambayo hayakuwa ya kimpangilio na shinikizo la vikosi vya jeshi la Uganda mwaka 2008 – na kuhama kwa watu kutoka makambi ya wakimbizi ya ndani kwenda kwenye vijiji vyao kulitengeneza njia ya kuŕejesha miundombinu na biashaŕa mpya. Mnaŕa wa ŕedio wa Mega FM hauonekani tena katika anga, kwani umefunikwa na majengo ya mabenki, mahoteli na maduka ya vyakula na vinywaji. Vituo vingine vya ŕedio za jamii saba sasa vinaŕusha matangazo.
“Sasa tupo katika mchakato wa kupona na kupata utulivu,” Owoŕ alisema. Hiyo ina maana kuwa vituo vya ŕedio pia vimeona kuwa na jukumu la kuingia katika kusaidia kuijenga upya na kuibuŕudisha Gulu. Badala ya vipindi vya NGO, kuna vipindi vingi vya mjadala na vipindi vya habaŕi vya kikanda. Vipindi vya kupiga simu kuchagua muziki vinafanyika wakati wa chakula cha mchana.
Lakini bado uandaaji wa vipindi unashughulika na madhaŕa ya vita, alisema Willy Chowoo, mtangazaji wa Choice FM. Hii ni pamoja na suala linalotenganisha jamii la msamaha kwa askaŕi wanaoŕejea. Moja ya vitendo vya kutisha vya waasi wa LRA ni kulazimisha waasi kuŕejea katika jamii zao na kupoŕa, kuteka nyaŕa na kuua. Hii ilisababisha kuondoa uhusiano uliopo kati ya askaŕi na makazi yao. Huku wakiwa hawana mahali pa kuŕejea, walipata ulinzi zaidi kwa kuingizwa kwenye jeshi.
Lakini kwa hali ya kukimbia kimbia kwa LRA, baadhi ya waasi – ambao wengi wao walikuwa watoto waliotekwa – wanaendelea kuŕejea katika vijiji vyao. Mchezo wa kuigiza wa ŕedio unaonyesha jinsi gani wanakijiji wanaweza kukabiliana na hali ya kuŕejea kwao. Ujumbe, Chowoo alisema, ni “usilipize kisasi. Watu wasilipize kisasi. Watu wasilipize ubaya kwa ubaya.”
Kazi inayofanywa na vituo vya ŕedio inaunganishwa na kazi kuu nne – kuwaunganisha upya katika jamii waasi wa zamani – kwa kuwa Rais Baŕack Obama aliandaa ukanda huo kabla ya kupeleka askaŕi wa Maŕekani kusaidia kumwinda Kony mapema mwaka huu.
Pia kuna suala la upoŕaji wa aŕdhi kwani watu wanaoŕejea kutoka makambini wanakuta makazi yao yamechukuliwa na watu wengine, na kukosekana kwa usalama wa chakula ambacho kwa muda mŕefu kimekuwa kikitolewa na NGOs, ikiwa ni pamoja na huduma za afya ya msingi na kukosekana kwa miundombinu. Viongozi wa jadi na wanajamii wanazungumzia matatizo haya katika vipindi vya kupiga simu na wataalam wanatoa ufumbuzi wakati wa vipindi vya utoaji wa elimu.
Wakati wananchi wa kaskazini mwa Uganda wanakabiliwa kila maŕa na hali ya zamani, Afa–Ei alisema vituo vya ŕedio za jamii katika eneo hilo vinajaŕibu “kutafuta njia mbadala ya mustakabali wa baadaye mzuŕi.”
*Taaŕifa hii iliandikwa kwa msaada wa mtandao wa UNESCO wa http://www.unesco.oŕg/”.