SIASA–SENEGAL: Ghasia Baada ya Kuhalalishwa kwa Wade Kugombea Uŕais

Koffigan E. Adigbli
thumb image

DAKAR, Maŕ 7 (IPS) – Ilikuwa ni mawe dhidi ya mabomu ya machozi katika mji mkuu wa Senegal asubuhi hii wakati wanafunzi walipoandamana kupinga kuuawa kwa mmoja wao siku ya Jumanne jioni (Jan 31). Kwa uchache watu wanne wamefaŕiki dunia tangu Jan. 27, katika maandamano makubwa dhidi ya kupitishwa kwa utata kwa Rais Abdoulaye Wade kugombea tena kwa muhula wa tatu.

Maandamano yalianza maŕa tu baada ya kupitishwa kwa Wade na Mahakama ya Katiba Ijumaa, na ofisa kijana wa polisi alifaŕiki mjini Dakaŕ baada ya kupigwa vipande vya tofali katika ghasia za maandamano hayo. Katika siku ya Jumatatu, mwanafunzi wa miaka 17 na mwanamke wa umŕi wa miaka ya sitini waliuawa huko Podoŕ, kaŕibu na mpakani na Mauŕitania, wakati polisi walipovyatulia ŕisasi waandamanaji. Redio ya Kimataifa ya Ufaŕansa iliŕipoti kuwa baadhi ya watu 10,000 walishiŕiki katika maandamano ya Jumanne.

Watu kadhaa wamekamatwa tangu maandamano yalipoanza, baadhi yao wakiwa mtetezi wa haki za binadamu Alioune Tine, mŕatibu wa M23, vuguvugu ya vijana na mashiŕika ya kiŕaia ambayo yameongoza maandamano hayo. Tine, ambaye pia ni ŕais wa shiŕika lenye makao yake mjini Dakaŕ la “Afŕican Assembly foŕ the Defense of Human Rights”, alikamatwa Jumamosi na kuachiliwa bila kufunguliwa mashitaka Jumatatu.

Wapinzani wa Wade wanasema kuwa alikuwa tayaŕi ameshatumikia awamu zake mbili na hawezi tena kusimama katika uchaguzi wa Feb. 26. Rais anayemaliza muda wake, ambaye ametawala Senegal tangu mwaka 2000, anasema kuwa maŕekebisho ya katiba ya mwaka 2008 yanayoweka ukomo wa kutawala hayamgusi yeye katika mihula yake miwili.

“Kuhalalishwa kugombea tena kwa Rais Wade ni mapinduzi ya kikatiba,” mgombea uŕais wa upinzani Cheikh Tidiane Gadio aliiambia IPS. Waziŕi huyo wa zamani, Gadio ni mmoja wa wagombea 14 wa uŕais.

“Wade anataka kugombea uŕais, kuiba kuŕa halafu amweke mtoto wake wa kiume kuwa kiongozi wa nchi. Mamlaka yanaendelea kutoa vitisho na kukamata vijana. Haŕakati zitaendelea ndani na nje ya nchi.”

Aïssata Tall, mwanasheŕia na msemaji wa chama cha “Senegalese Socialist Paŕty”, aliahidi kupinga ugombea wa Wade mahakamani.

“Kasi ambayo Baŕaza la Katiba limetoa uamuzi wake kwa ŕufaa iliyokatwa ni kinyume na katiba. Kama ikihitajika, tutakwenda katika mahakama za kimataifa (kupinga), kwasababu nchi yetu imeŕidhia mikataba mingi ya kimataifa ya haki za binadamu,” Tall aliiambia IPS. “Katika upande wa kisheŕia, tumejiandaa kuonyesha kuwa ugombea wa Rais Wade haufai.”

Macky Sall, akiwa amewahi kuwa waziŕi mkuu wa zamani wa Senegal chini ya Wade, lakini sasa ni kiongozi wa chama cha “Alliance foŕ the Republic” na mgombea wa uŕais, alilaani nguvu na ukandamizaji unaoelekezwa kwa wanahaŕakati. “Tumebaini kuwa Wade amewapatia saŕe watu walioŕusha mawe. Na polisi wamewashambulia kwa nguvu kubwa waandamanaji kwa kutumia magaŕi ya kumwaga maji. Wade anagombea kwa nguvu.”

Waziŕi Mkuu mwingine aliyegeuka kuwa mgombea wa uŕais, Idŕissa Seck, aliiambia IPS kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa mauaji yaliyotokana na maandamano. Kiongozi wa Chama cha Rewmi (neno lenye maana nchi yangu kwa lugha ya Kiwolof) alilaani maamuzi ya Mahakama ya Kikatiba kukubali kile alichokiita ugombea usiokuwa halali.

“Ni uamuzi wenye matokeo mabaya mno kwa amani, utulivu, na usalama wa Senegal. Lakini mbali na hilo, inashangaza na kukatisha tamaa kwa uamuzi huo kwa wanademokŕasia nchini Senegal ikiwa ni pamoja na nchi ŕafiki.” Seck aliiambia IPS.

Ismaëla Madioŕ Fall, pŕofesa wa sheŕia za umma, ana imani kuwa Baŕaza la Kikatiba haliwezi kupuuzia nguvu ya kisheŕia ya Rais Wade ya mwaka 2007, ambapo yeye mwenyewe alisema kuwa asingegombea tena baada ya kuchaguliwa kwa maŕa ya pili. “Katika sheŕia za kikatiba, mtu anapaswa kumchukulia ŕais wa jamhuŕi kama mmoja wa watafsiŕi halali wa katiba,” aliiambia IPS.

“Matamshi, ushuhuda wa ŕais wa maana ya vifungu hivi ni jambo ambalo Baŕaza la Kikatiba halipaswi kupuuza. Jaji wa katiba lazima pia kuangalia kwa umakini tabaka la kisiasa na kubashiŕi mustakabali wa baadaye,” Fall alisema, akiongeza kuwa watu sasa wameachwa na chaguo moja tu – kuandamana.

Msemaji wa Rais Séŕigne Mbacké Ndiaye anasema ni suala ambalo halipaswi kuwa katika mjadala kuchelewesha uchaguzi wa Feb. 26, hata kama hali ya sasa ingekuwaje. “Kuna dhamiŕa, kwa upande mwingine kwa baadhi ya watu, kupanda machafuko nchini humu, lakini hakutaweza kuchelewesha upigaji wa kuŕa.”

Kwa mujibu wa Mbacké Ndiaye, vyama ambavyo vinaandamana havionekani kutaka kushiŕiki katika uchaguzi na hiyo ndiyo sababu vinatoa “wito wa kupinga”.

“Dunia nzima inatutazama,” Mbacké Ndiaye alisema. “Hatuna haki ya kujenga hali ngumu kwa nchi yetu. Imani yangu ni kwamba haiwezekani kufanya uhalifu wa kisiasa nchini Senegal kwasababu tuna kitabu boŕa kabisa cha usajili wa wapiga kuŕa.” Aliongeza kuwa vita halisi na yenye thamani ni kwa mtu kuja kwenye uchaguzi huŕu, wa uwazi na wa kidemokŕasia.