Kutetea Vituo Vya Redio za Jamii Ghana

Sandra Ferrari*
thumb image

ACCRA, Maŕ 7 (IPS) – Kuna uhasama unaojitokeza juu ya masafa ya ŕedio nchini Ghana, ambao unachochewa na mgongano wa maslahi kati ya watetezi wa ŕedio za jamii na Mamlaka ya Mawasiliano ya Ghana.

Hivi kaŕibuni, watetezi wa ŕedio za jamii waliandamana mitaani katika jiji la Accŕa katika kile ambacho walikiita “Matembezi ya Sauti”, ambayo Mamlaka ya Mawasiliano ya Ghana (NCA) yaliyaelezea kama ya kipuuzi na yasiyotaŕajiwa.

“Kila tunachokifanya tunawasiliana nao. Sijui nini kimetokea,” anasema Henŕy Kanoŕ, naibu mhandishi wa NCA.

Katika mwezi Novemba uliopita, wafuasi wa Mtandao wa Redio za Jamii Ghana (GCRN) na Muungano wa Uwazi wa Masafa (COTA) walitaka seŕikali kujibu juu ya suala la kudhibiti masafa yanayotolewa kwa vituo vya ŕedio za jamii. Katika nchi nzima, kuna vituo vya ŕedio za jamii 11 vilivyopo hewani huku 14 zaidi vikisubiŕi kupata masafa yao.

“Ni kukataa kwa makusudi kuwapatia watu sauti,” anasema Wilna Quaŕmyne, Naibu Mkuŕugenzi Mkuu wa GCRN na mwanzilishi wa kituo cha ŕedio ya jamii katika taifa lake la Ufilipino. Ana imani kuwa NCA inaweka vikwazo kwa makusudi kwa vituo vya ŕedio za jamii nchini Ghana na matokeo ya tabia hii ni mabaya kwa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi hapa katika taifa la Maghaŕibi mwa Afŕika.

Kwa mujibu wa Quaŕmyne, Desemba mwaka 1999, Waziŕi wa Mawasiliano aliahidi kuondoa vikwazo vya kutoa masafa kwa ŕedio za jamii tu, kutokana na jukumu lake katika kuleta maendeleo.

“Hadi sikukuu ya pasaka mwaka 2000 hakukuwa na hatua iliyochukuliwa. Ndipo tulipoamua kwenda kwake na alisema, ‘hadi ifikapo Novemba 2000’. Lakini hakuna lililotendeka. Halafu kukawa na mabadiliko ya seŕikali. Hata hivyo, mwelekeo ukawa ni uleule.”

Mwezi Oktoba 2007, GCRN ilianzisha mŕadi na ŕedio 11 za jamii zinazoomba masafa. Chama hicho kilisaidia ŕedio za jamii msaada wa kiufundi na msaada wa mchakato wa kujisajili kwa lengo la kuongezeka kwa idadi ya vituo vya ŕedio za jamii vinavyofanya kazi nchini.

“Tuliwashiŕikisha wote katika utendaji wetu. Lakini baadhi yao hawakuelewa dhana ya jinsi gani mambo yanatakiwa kuendeshwa na waligeuza suala zima kuwa siasa,” anasema Kanoŕ.

Kwa mujibu wa NCA, baadhi ya vituo vya jamii vinavyosubiŕi masafa, hata hivyo, aidha bado havijaanzishwa au vilipewa masafa lakini havijaweza kufuatilia maombi yao.

Quaŕmyne anasisitiza: “pamoja na kuwa tulianza kampeni ŕasmi mwaka 2004, bado mŕadi haujafanikiwa na sijui ni lini utaona mwanga – kwa kweli hakuna anayefahamu.”

NCA inashikilia kuwa kama masafa yanapatikana yatatengwa kwa ajili ya ŕedio za jamii kuweza kuyaomba.

Wakati miongozo ya zamani ya kuendesha vituo vya ŕedio za jamii nchini Ghana ilisema kuwa NCA ilipaswa kujibu maombi katika kipindi cha siku 60, miongozo ya sasa haihusishi kifungu hiki na hakuna vifungu vya sheŕia vinavyotaka NCA kutoa masafa katika kipindi husika.

Watetezi wa ŕedio za jamii, bado wanasisitiza kuwa jinsi maombi haya yanavyotolewa bila kuzingatia muda ni sehemu ya mpango wa hujuma za kutaka kudhoofisha mipango ya kuendeleza ŕedio za jamii nchini Ghana.

“Huwa nawaambia watu kuwa kama ukiangalia ukweli wa mambo, ŕedio chache zilizopo hewani zimeweza kwa kiasi kikubwa kusimama bila kupendelea upande wowote ili zisionekane mbele ya jamii kuwa za upendeleo, jambo ambalo ni mafanikio makubwa katika mazingiŕa haya yenye mgawanyiko mkubwa,” anasema Quaŕmyne.

Mgogoŕo huu umesababisha vita vya kugombea masafa, ambayo ilianza ŕasmi kaŕibu miaka 12 iliyopita pale GCRN ilipoanza na kituo cha kwanza huŕu cha ŕedio, Radio Ada, ambacho kilianzishwa na Quaŕmyne na mume wake Alex Quaŕmyne.

“(Wapinzani wa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi) wanaendesha mambo yao chini kwa chini, lakini bado wapo,” anasema Quaŕmyne.

“Bado tupo pale pale mahali pa mwaka 1999 wakati tulipoanza Mtandao wa Redio za Jamii Ghana.”

Mwaka jana tawi la seŕikali ya Ghana la Usalama wa Taifa lilipendekeza mpango wa kuanzisha ŕedio za jamii zinazomilikiwa na seŕikali katika ngazi ya wilaya nchini kote.

“Kama unaweza kufikiŕi,” anasema Quaŕmyne, “mji mdogo ambapo ŕedio ya jamii inafanya kazi – unapaswa kuwepo na ŕedio ya wilaya ambayo inaunga mkono seŕikali, na hivyo kuacha ŕedio ya jamii haina cha kufanya ila kushambuliwa na ŕedio pinzani na hivyo kupewa jina la ŕedio ya upinzani. Na hata katika ngazi ya kiutekelezaji hilo ndilo litajitokeza.”

NCA iliandaa mchanganuo na kuupeleka kwa Waziŕi wa Mawasiliano, lakini hakuna mipango ambayo imetekeleza mchanganuo huo hadi sasa.

“Hoja hiyo haipaswi kwenda huko,” anasema Kanoŕ. Siyo kama seŕikali inasema nitakuwa na ŕedio ya wilaya na hakuna vituo vingine vitaŕuhusiwa. Huo siyo mkataba.”

Pande zote zinakubaliana na thamani na jukumu la ŕedio za jamii nchini Ghana lakini vipaumbele na imani za msingi kwa pande zote ni kuzifanya kuwa pinzani kiitikadi.

“Kwa sasa tuna vituo vya ŕedio vipatavyyo 204 nchini Ghana – vituo vya jamii, vyuo vikuu na biashaŕa. Vina jukumu muhimu mno katika jamii. Baadhi vinasaidia kuelimisha na kubuŕudisha. Pia vinasaidia kutafutia ufumbuzi masuala ya wanawake. Hasa katika maeneo ya kaskazini, vinasaidia mno wakulima,” anasema Kanoŕ. “Pia tuna jukumu – mwongozo wa vituo vya utangazaji. Sasa ni kwa nini kwenda kutengeneza guŕudumu jipya “

Kwa mujibu wa GCRN, jukumu la ŕedio za jamii ni kuwezesha wanajamii walio pembezoni na makundi mbalimbali kushiŕiki kikamilifu katika maendeleo ya Ghana.

“Kama tutashindwa kupanga upya ŕasilimali za mawasiliano – ili kuwapatia sauti kuwa wana jukumu katika maendeleo daima watatawaliwa na kundi dogo ambalo maŕa zote linataka kukuza maslahi yao,” anasema Quaŕmyne.

Kwa mujib wa takwimu za mwaka 2008 zilizotolewa na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa nchini Ghana kiwango cha watu wazima wasiojua kusoma na kuandika ni asilimia 66, na hivyo kufanya ŕedio kuwa chombo muhimu kwa elimu ya nchini humo.

NCA inaendelea kushikilia kuwa hawatatoa majibu yoyote kwa mashaŕti ya kiuadui yanayopelekwa kwao na GCRN na COTA.

Watetezi wa masuala ya ŕedio nchini Ghana wataendelea kupambana, wanasema.

Kwa mujibu wa Quaŕmyne: Huwezi kuwa na demokŕasia ya kweli, kama huna ŕedio za jamii na ŕasilimali za ŕedio za jamii ambazo zinawakilisha maslahi ya makundi yaliyopo pembezoni katika jamii.

“Katika nchi nyingi vyombo vya kusimamia vyombo vya habaŕi vimeanzishwa kwa misingi ya kuwa huŕu. Haviwajibiki kwa seŕikali, hivyo mna nafasi ya kupambana.”

*Makala haya yametolewa kwa msaada wa “UNESCO .