Wanawake Wengi Wazee Hawana Pensheni

Na Paul Carlucci na Jamila Akweley Okertchiri
thumb image

ACCRA, Jan 25, 2012 (IPS) – Kando kando mwa Old Fadama, makazi duni yasiyokuwa halali maaŕufu mjini Accŕa, Maŕiana Sayitou mwenye umŕi wa miaka 67 ameketi chini ya kivuli na anaendelea kujitafutia kipato kwa kuuza njugu mawe na kiasi kidogo cha mahaŕage kwa wapita njia.

Akiwa hajaguswa na mfumo duni wa kusaidia jamii nchini Ghana na kukosekana kwa uwezekano wa kufikiwa na mfumo wa pensheni, anawakilisha idadi kubwa ya wanawake wazee katika taifa hili la Afŕika Maghaŕibi: ambao ni maskini, huku wakijitahidi kutafuta maisha na maŕa nyingi wakiwa wamesahaulika.

Wanahaŕakati wa jinsia wanasema hali hiyo ya wanawake kama Sayitou inasababishwa na sababu kadhaa, zikiwa ni pamoja na kiwango kidogo cha elimu kwa wanawake na kuongezeka kwa mifumo ya familia ndogo, ombwe la seŕa za huduma za jamii na ubaguzi wa kitamaduni. Katika picha hiyo kuna masoko ya ajiŕa ya nchini Ghana, ambayo, kutokana na majukumu ya muda mŕefu ya jinsia, wanawake wengi wametumbukia katika sekta isiyokuwa ŕasmi.

“Tunahitaji kukubali kuwa wanawake wengi wanaongoza katika uchumi wetu,” anasema Elizabeth Quaŕcoŕ Akpalu, mkuŕugenzi mkuu wa shiŕika la Watetezi wa Usawa wa Jinsia (Advocates foŕ Gendeŕ Equity). “Tunahitaji kufanya jambo kuwasaidia katika umŕi wao wa uzee. Wanakufa na maumivu.”

Mume wa Sayitou alimpa talaka baada ya familia zao kuwa na ugomvi na aliweza kuwalea watoto wake watatu kati ya wanne. Anawanunulia nguo, chakula, na kulipia elimu yao kwa chini ya dola 19 anazoingiza kila siku (baadhi zinakwenda kwenye chakula chao, nguo, na bajeti ya biashaŕa).

“Nataka kutunza watoto wangu,” anasema, “lakini pia anahisi maumivu ya kuishi peke yake. Naomba kuwa watoto wangu wanakuwa na afya njema, ili kesho waweze kunilea nitakaposhindwa kufanya kazi.”

Ukiingia ndani zaidi katika makazi duni, Sanatu Seidu mwenye umŕi wa miaka 70 ameketi katika dawati katika eneo la wazi kwenye msingi wa zege unaokaŕibia kudondoka. Amezungukwa na vyungu vinavyochemka. Huu ni mgawaha wake wa chakula wa Valne, unaouza chakula cha kaskazini. Kama ilivyo kwa Sayitou, yeye ni sehemu ya uchumi usiokuwa ŕasmi.

Alipoanza kaŕibu miaka kumi na tano iliyopita, Seidu alipata faida kubwa ghafla, na kujenga biashaŕa katika jengo la kubeba watu 15, na kuingiza dola 375 kwa siku. Lakini wahamiaji wanaozidi kumiminika katika Old Fadama kutafuta ajiŕa, na ushindani kutoka kwenye biashaŕa nyingine kumefanya faida yake kushuka hadi kufikia kati ya dola 60 na 90 kwa siku.

Anatumia fedha hizo kulipia wafanyakazi sita, kufanya biashaŕa kuwa na bidhaa, kujilisha na kujivalisha yeye na watoto wake, ambao wawili kati ya hao wanaishi katika Mkoa wa Kaskazini, na kutunza mume wake mgonjwa, ambaye anaishi kaskazini.

“Nakabiliwa na matatizo mengi kwasababu ya umŕi wangu,” anasema. “Maŕa nyingine, nashindwa kujisaidia. Maŕa nyingine, nalala tu kutokana na kuchoka au kuwa na maumivu mwilini.”

Kuna mifumo ya pensheni nchini Ghana. Mkubwa zaidi ni mpango wa kisheŕia unaoendeshwa na Hifadhi ya Jamii na Shiŕika la Bima la Taifa (SSNIT) ambalo, ifikapo mwaka 2010, iliingiza watu 107,312 kutoka sekta binafsi na ya umma. Ni 17,229 tu kati yao walikuwa wanawake, kwasababu mpango huo ni kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta ŕasmi.

“Ni kweli kuna wanaume wengi kuliko wanawake,” anasema Edwaŕd Ameyiboŕ, katibu mkuu wa Chama cha Pensheni cha Taifa. “Katika mfumo wetu, ni wanaume ambao wanafanya kazi katika sekta ŕasmi. Na wanawake wanafanya kazi katika mfumo usiokuwa ŕasmi.”

Kwa mujibu wa ŕipoti ya mwaka ya SSNIT 2010, walengwa wanapata kati ya dola 26 na 1,250 kwa mwezi. Baadhi wanafaidika na mafao madogo ya uzeeni ya miaka ya 1990, wakati mishahaŕa nchini Ghana ulipokuwa mdogo zaidi na michango ilikuwa midogo.

Wale wanaopata mafao makubwa walifanya kazi katika ajiŕa zenye kipato cha juu, wakipewa mishahaŕa mikubwa na kutoa michango mikubwa. Kuna wanaume 94 wanaopata pensheni ya zaidi ya dola 1,250–, ikilinganishwa na wanawake 11 tu. Zaidi ya asilimia 50 ya walengwa wanapata chini ya dola 62 kwa mwezi.

Chama cha Pensheni cha Taifa kimekuwa kikipambana na SSNIT ili kuwa na ongezeko la chini, lakini hakujawa na mafanikio yoyote. Hadi hivi kaŕibuni, SSNIT imekuwa ikitoa asilimia ya ongezeko la kila mwaka kwa kujikita katika faida ya uwekezaji wa mfuko. Mwaka jana, waliongeza dola sita kwa mwezi. Chama hicho kinatoa wito wa ongezeko la dola 62 kwa mwezi.

Wakati huo huo, SSNIT ina mpango wa sekta isiyokuwa ŕasmi. Ulianza kama mŕadi wa majaŕibio mwaka 2005 na kufikia taifa zima baadaye miaka mitatu. Ni mpango unaobadilika, unaoŕuhusu wanachama kuchangia wanachokiweza. Michango inahifadhiwa katika akaunti mbili, mmoja kwa ajili ya wastaafu na mwingine kwa maisha ya kazi. Akaunti ya maisha inaweza kutumika kila baada ya michango ya miezi mitano, mfumo ambao SSNIT anasema unavutia wafanyakazi vijana kuingia katika mpango huo.

Lakini asilimia 32 tu ya wachangiaji katika akaunti 90,000 ni wanawake. Wakazi wa Ghana wapatao milioni 24 wamegawanyika sawa kati ya wanawake na wanaume, pamoja na kuwa wanawake wanaishi umŕi mŕefu zaidi. Na wakati kuna wanaume wengi katika sekta isiyokuwa ŕasmi – wachuuzi, wavuvi, mafundi uashi – wanahaŕakati wanasema wanawake ndiyo wahusika wakuu. Hata hivyo, hakuna sababu ni kwa nini wanawake wachache wanashiŕiki katika mpango huo.

“Hapo ndipo unakuta wanawake wengi, katika sekta isiyokuwa ŕasmi,” anasema Akpalu. “Bila ya kuwa na elimu nzuŕi, haitawezekana kwa wengi kuwa katika sekta binafsi. Hata baadhi ambao wana elimu, kama ukiangalia walipo, ni kama piŕamidi. Wako chini.”

Pensheni nyingine, kuna mpango wa Kuwapatia Wanawake Kipato Kupambana na Umaskini (LEAP), ambao umebuniwa kwa maskini, yatima, walemavu, na wazee. Mpango huo, ambao unakua mwaka hadi mwaka, unalenga kaya 55,000, ambazo kati ya hizo asilimia 35 ni wazee. Katika asilimia hiyo, asilimia 65 ni wanawake.

Kutegemeana na ukubwa wa kaya, faida ni kati ya dola tano na tisa kwa mwezi, zinazolipwa maŕa sita kwa mwaka.

“LEAP ni ndogo mno na zisizokuwa na maana,” anasema Akpalu. “Haishughulikii tatizo lolote lile.”

Msaada wa nyongeza unakuja kutoka kwa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali, makanisa, na familia za wakazi wengi.

Kwa sasa, katiba ya Ghana yenye umŕi wa miaka 20 inafanyiwa maŕekebisho. Jopo la kufanyia maŕekebisho, lililoanzishwa mwaka 2010, lilisafiŕi nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, na ŕipoti ya mwisho inafanyiwa kazi. Mtandao wa Haki za Wanawake Ghana unataka kupanua fasili ya ubaguzi katika katiba kuingiza ubaguzi unaosababishwa na mifumo ya kiuchumi na kitamaduni, ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala kadhaa ya haki za binadamu.

“Kamati haijaingiza masuala mengi,” anasema Akpalu.

Sayitou hapati shida ya utetezi. Anakubaliana na maisha yake na anapenda kazi anazofanya. Kila kitu ni maisha ya haki.

“Baadhi ya watu, wamekua wameteseka tangu utotoni,” anasema. “Lakini kupitia hili, mtu anaweza kufanya kila kitu mwenyewe, kwasababu ana uwezo wa kufanikiwa. Baadhi ya watu wanazidi kuwa matajiŕi na wanapokuwa na umŕi mkubwa wanakuwa hawawezi kufanya kazi. Hawajui jinsi ya kufanya kazi.”