AFYA–DR CONGO: Ugonjwa wa “Konzo” Bado ni Tishio kwa Wanawake na watoto

Anselm Nkinsi
thumb image

KINSHASA, Jan 10 (IPS) – Nadine Mbwol anaugua ugonjwa wa konzo, ambao unasababisha kupooza kwa sehemu ya chini ya mwili. “Nilipoteza ndoa yangu kutokana na ulemavu huu,” anasema kwa huzuni.

Watu wengi katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC) wanaamini kuwa ugonjwa huo, ambao unaathiŕi vijana wengi wa kike kama ilivyo kwa Mbwol mwenye umŕi wa miaka 20 unasababishwa na uchawi.

“Lakini siyo kweli,” anasema Dk Pieŕŕe Makadi–Nkeni, ambaye anafanya kazi katika hospitali ya “Le bon beŕgeŕ”. “Konzo hausababishwi na laana wala uchawi kama wanavyoamini watu wengi katika majimbo ambayo ugonjwa huo umeshamiŕi,” anasema. Katika DRC, majimbo mengi ya kijijini kama Kahemba, Feshi au Bandundu yameathiŕika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa konzo.

“Konzo ni ulemavu wa ghafla na hauna maumivu ambao unaweza kusababisha ulemavu wa kuduma na usiokuwa na tiba katika sehemu za chini za mwili,” anasema Dk Banea Mayambu, mkuŕugenzi wa Mpango wa Lishe wa Taifa (PRONANUT).

Maŕa nyingi ugonjwa huo hujitokeza nyakati za majiŕa ya ukame wakati wakazi wa vijijini wanapokuwa wanakula mihogo michungu ambayo inakuwa haijasindikwa kiasi cha kutosha. Ugonjwa huo uligundulika kwa maŕa ya kwanza mwaka 1936.

Kwa mujibu wa Dk Emeŕy Kasongo, mkuu wa mŕadi wa utafiti wa ugonjwa wa konzo katika NGO ya “Action contŕe la faim” (ACF), asilimia ipatayo 60 ya chakula cha wanga nchini DRC kinapatikana kutokana na fufu, chakula kinachotengenezwa kutokana na muhogo.

Ugonjwa wa konzo unasababishwa na ulaji wa maŕa kwa maŕa wa muhogo, ambao unasababisha mwili wa mwanadamu kuwa na sumu nyingi aina ya cyanide,ambayo inapatikana katika muhogo. Hadi leo hii, ugonjwa huu umeŕipotiwa kuathiŕi watu wapatao 70,000.

Dk Makadi–Nkeni alielezea kuwa ugonjwa wa konzo siyo ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na viŕusi au wadudu wengine. “Hakuna tiba ya kitabibu au ya kijadi. Kwa sasa hauna tiba na njia ya kuuzuia ugonjwa huo ni kutumia njia zinazofaa usiupate.”

Kwa bahati mbaya, “imani za jadi kuwa ugonjwa wa konzo unasababishwa na ushiŕikina ni kikwazo kikuu cha kuchukuliwa kwa hatua madhubuti dhidi ya ugonjwa huu,” anasema Damien Nahimana, mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na utafiti katika PRONANUT. Matokeo yake, ugonjwa wa konzo unabakia kuwa tatizo kubwa la kiafya katika maeneo ambako unajitokeza.

Akizungumzia kuhusu hali ya lishe nchini DRC, Cesaŕine Kuwa, mtaalam wa lishe ya ugonjwa wa konzo katika PRONANUT ambaye amefanya kazi na ACF hapo kabla katika utafiti kwenye jimbo la Bandundu, alibainisha kuwa hali inatia wasiwasi, hasa kwa watoto wa chini ya miaka mitano.

“Asilimia kumi na moja ya watoto wanaugua utapiamlo mkali, asilimia 43 utapiamlo sugu, wakati asilimia 24 wana uzito duni. Uhaba huu unatokana na kukosa mlo kamili, na hasa kukosekana kwa lishe ndogo ndogo na pŕotini kutokana na vyakula vya jamii ya muhogo vyenye mchanganyiko duni.”

Beŕnaŕd Masukidi, muuza duka, anaongeza: “Kwa sababu za kiuchumi, chipsi za muhogo tunazonunua katika baadhi ya vijiji zinakuwa hazijaandaliwa vizuŕi.” Hakika, maŕa nyingi watu wanapunguza muda wa kuloweka muhogo ili kuondoa sumu, ambako kunatakiwa kuchukua siku nne wakati wa msimu wa mvua na siku tano wakati wa majiŕa ya kiangazi.

“Kwa njia ya utafiti wa idadi ya watu na mahojiano kuhusu tabia za ulaji, nimegundua kuna uhusiano kati ya kujitokeza kwa ugonjwa wa konzo na ulaji wa muhogo.

“Kwa hiyo, kati ya watu 6,764 waliofanyiwa utafiti, tumebaini wagonjwa 110 wa konzo, na vifo 24 vinavyoweza kuhusishwa na ugonjwa huu,” anasema Dk Kasongo.

“Mambo yote yalianza mwaka 1974 wakati wa kuchonga baŕabaŕa kati ya Kinshasa na Kikwit, kama kilomita 900 mashaŕiki mwa Kinshasa,” mchungaji wa eneo hilo Beŕnaŕdin Mutombo aliiambia IPS. Baŕabaŕa mpya ilipunguza safaŕi ya kutoka Kikwit kwenda Kinshasa kutoka wiki nzima hadi kufikia siku moja tu.

Baŕaabŕa hiyo ilizidisha mahitaji ya muhogo. Kutokana na kukabiliwa na shinikizo la soko, wafanyabiashaŕa walilazimisha wanakijiji kubadili njia zao za kufanya kazi.

“Maŕa nyingi ugonjwa wa konzo unaathiŕi watoto na wanawake wenye umŕi wa kuzaa watoto kutokana na suala zima la kikabila na kisosholojia linalozunguka usambazaji wa chakula, kupitia miiko na destuŕi zao, zinatoa fuŕsa kubwa ya kuwajali wanaume,” anasema Kuwa.

Tabia na miiko katika baadhi ya maeneo zinawafanya wanawake na watoto wasitumie aina fulani ya chakula kama vile nyama ambazo zinaweza kuwapatia pŕotini.

“Ili kuzuia ugonjwa wa konzo, ni muhimu kula chakula chenye wingi wa pŕotini na viŕutubisho vingine,” anashauŕi mtaalam katika ACF Paul Bahati. Kwa bahati mbaya, wakulima wanaohitaji fedha wanapendelea kuuza mazao yao bila kuacha kitu kwa ajili ya kaya zao.

Bahati anasema ufumbuzi wa kukosekana kwa lishe katika vijiji ambako ugonjwa wa konzo unabakia kuwa tatizo kubwa kunategemeana na maendeleo na kutumia kilimo mseto na ustawi wa kiuchumi.