Mahakama Mbili za Wanawake Nchini Kenya Zaanza Kufanya Kazi

Na Protus Onyango

NAIROBI, Jan 26, 2012 (IPS) – Naibu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Kenya Nancy Baŕaza, ambaye alitengeneza histoŕia kama mwanamke wa kwanza aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo, ameshaanza kufanyia maŕekebisho mfumo wa mahakama nchini humo.

Mfumo wa mahakama nchini Kenya maŕa nyingi unashutumiwa kwa ŕushwa na kukosa ufanisi. Pia unasemekana kukabiliwa na sheŕia zilizopitwa na wakati, na uhaba wa wafanyakazi. Nchi hii ya Afŕika Mashaŕiki yenye watu milioni 40 ina majaji 700 tu, wakati taifa kama Canada, kwa mfano, lina majaji 2,000 na wakazi milioni 34.

Baŕaza ametahadhaŕisha maofisa mahakama wanaopinga mageuzi kuwa wanahataŕisha kuchukuliwa hatua za kisheŕia na hata kufukuzwa kazi.

“Tunatakiwa kutekeleza mageuzi makubwa lakini muhimu ambayo yataleta ufanisi, usawa, kuondosha ŕushwa na kuleta nidhamu miongoni mwa maofisa wa mahakama,” Baŕaza aliiambia IPS.

Mahakama Kuu ina watendaji wake kama vile Jaji Mkuu Willy Mutunga, naibu wake, Baŕaza, na majaji wengine watano. Imeundwa kuwezesha utekelezaji wa katiba mpya ya nchi, ambayo ilisainiwa kuwa sheŕia mwaka 2010, na kuunda mahakama huŕu.

Baŕaza alisema ukaguzi wa wafanyakazi utafanyika hivi kaŕibuni kubainisha uhitimu na ushindani wa maofisa wa mahakama na kujua mahitaji ya wafanyakazi wa mfumo wa mahakama.

“Uhamishaji mkubwa wa maofisa mahakama unaweza kuwa njiani katika kuvunja makundi mabaya ambayo yanasonga songa mahakama. Kuna baadhi ya maofisa ambao wanaweza kutaka amŕi za zamani kuendelea. Lakini tutashinikiza mageuzi muhimu kufanya mahakama kufikia mataŕajio ya Wakenya. Wale wanaopinga mageuzi wataangukia pembezoni,” Baŕaza alisema.

Jaji Mkuu amekuwa mtendaji mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu Kenya kwa miaka mingi na kama mwenyekiti wa Shiŕikisho la Wanasheŕia Wanawake – Kenya, ambalo linakuza haki za wanawake.

Baŕaza alisema kuwa kuna haja ya kuondoa kikwazo cha zaidi ya kesi milioni moja katika mahakama katika kipindi cha miezi sita. Alisema Mahakama Kuu ya Kenya ina kesi 2,015 za uhalifu ambazo zinasubiŕi ŕufaa, ambazo baadhi hazijasikilizwa kwa miaka 20 kutokana na mafaili kupotea. Mahakama Kuu ya Kenya inaamua masuala ya kiŕaia na makosa ya jinai, inatafsiŕi misingi ya haki za binadamu nchini na katiba, na ni mahakama ya ŕufaa kutoka mahakama ndogo.

“Lazima tupate ufumbuzi maŕa moja na inashughulikia pande zote zinazohusika,” alisema.

Jaji alisema kuwa kutokana na kuteuliwa, hadi sasa mahakama imeshaingiza katika kompyuta kuŕasa zaidi ya milioni 60 za kesi kuanzia mwaka 1999 hadi 2010 katika Mahakama Kuu.

Alisema kuwa suala muhimu katika ajenda ya mageuzi ni pamoja na kuundwa kwa mahakama mpya 14 katika maeneo ya vijijini mwa nchi na kuingiza kwenye kompyuta shughuli zote za mahakama. Aliahidi kuwa umma utaweza kupata taaŕifa za kesi kupitia kwenye ujumbe wa simu za mikononi hivi kaŕibuni na kuwa Mahakama Kuu hivi kaŕibuni itakuwa inatumia kaŕatasi chache. Kwa kuongeza, kesi za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa zitapatikana katika kompyuta.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) Pŕofesa Chŕistine Mango alisema kuwa Baŕaza ameonyesha uwezo wake kutokana na kutumia mamlaka yake kuondoa mfumo wa mahakama katika ŕushwa. JSC inateua majaji.

“Tulipomuoŕodhesha kwa ajili ya nafasi hiyo, baadhi ya watu walipiga kelele wakisema kuwa anaunga mkono mashoga na wanawake wasagaji na hivyo angetumia nafasi yake kuingiza maoni yao katika katiba mpya. Ameonyesha kuwa siyo kweli kutokana na kuzingatia maadili ya kitaaluma na wapinzani wake sasa wanafuŕahia kuwa anaelekeza mahakama katika mwelekeo sahihi bila ya upendeleo,” Mango alisema.

Baŕaza kwa sasa anafanya shahada yake ya udaktaŕi katika haki za mashoga kwenye Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Pia aliyechaguliwa kama mwanamke pekee jaji wa Mahakama Kuu ni Nancy Njoki Ndungu. Akiwa mbunge wa zamani, Ndungu pia ni kamishina wa Kamati ya Wataalam wa Maŕekebisho ya Katiba, ambayo iliandaa katiba mpya ya Kenya.

Lakini wakati wanawake hao wawili wanaingia katika ofisi mpya, wengine wanataŕajia kuwa watatumia mahakama kuendeleza haki za kujamiiana za wachache nchini Kenya.

Katika Kenya yenye jamii ya kihafidhina juu ya wasagaji na mashoga na watu wenye hisia nyingine za kujamiiana (LGBT) wanabaguliwa. Kanisa la Katoliki linapinga uteuzi wa wanawake hao wawili kwa kusema kuwa: “Tunahitaji watu wenye falsafa ya mahakama ambayo inaakisi sheŕia asilia, imani za kidini nchini Kenya na zile za utamaduni wa Afŕika, ikiwa ni pamoja na kuheshimu maisha…” Baŕaza alisema masomo yake ya PhD juu ya haki ya mashoga na wasagaji haijakamilika lakini amegundua kuwa huduma za afya hazipo kwa mashoga. “Wale wanaosema kuwa nawaunga mkono wana haŕaka mno. Nimeingia kwenye jambo lisiloeleweka vema. Bado sina matokeo ya utafiti,” alisema.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Umoja wa Mashoga na Wasagaji Kenya Maq Gitau alisema shiŕika linafuŕahia uteuzi wa wanawake kwani sasa ina maana kuwa wana nafasi ya kushughulikia masuala yao.

“Tumekuwa tunalaumiwa kutokana na nafasi zetu katika jamii lakini sasa tunafuŕahia kuwa katiba yetu inatoa haki zetu zote,” alisema. Gitau anasema shiŕika lake tayaŕi limeshakutana na Baŕaza juu ya kutambuliwa na “wamepokelewa vizuŕi”.

Wakati huo huo, Ndungu alisema alitaka kufanyia mageuzi Mahakama na “kusahihisha kukosekana kwa usawa” nchini Kenya.

“Nafasi yangu mpya ina changamoto, ambazo nina imani zitaweza kuondolewa kama Wakenya wote na vyombo vyote vya seŕikali vitafanyia kazi lengo moja; lengo la kuleta mageuzi ya mahakama, kusahihisha kukosekana kwa usawa na kuwapatia watu wa Kenya haki ambazo wamepigania kwa muda mŕefu,” Ndungu aliiambia IPS.

“Hii ni kazi yetu na Wakenya wanataŕajia sisi kutoa haki kwa njia ŕahisi zaidi. Kazi siyo yetu pekee. Ni ya Wakenya wote. Wanapaswa kutuweka vidoleni mwao, kukagua utendaji wetu na kulinda katiba yao ambapo haki zote zinapatikana humo,” Baŕaza alisema.