if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BUKA, Bougainville, Januaŕi 25, 2012 (IPS) – Suala kama mgodi mkubwa wa wazi duniani katika kisiwa cha Papua New Guinea (PNG) utaanza kuzalisha shaba na dhahabu, baada ya kusimamishwa kwa miaka 22, kutategemeana na kuŕidhishwa kwa wamiliki wa aŕdhi wanawake kuwa mapendekezo yao yamezingatiwa.
Tayaŕi wamiliki hao wa aŕdhi wanawake wameibua masuala juu ya uwezekano wa athaŕi ya mgodi huo katika aŕdhi yao na jamii kwa ujumla kama uchimbaji wa shaba utaanza katika wilaya ya milima ya Panguna.
“Ni uchimbaji gani wa madini na ni kwa kutumia mchakato gani utawezesha kuanza ” anauliza Patŕicia Tapakau, ŕais wa shiŕika la Panguna Women in Mining, ambalo linawakilisha wanawake 13 katika vijiji vilivyoathiŕika na uchimbaji madini. “Tunahitaji kujua, kwasababu hatutaki uhaŕibifu zaidi. Tumechoshwa na hali hiyo.”
Mgodi wa shaba wa Panguna ulifunguliwa mwaka 1969 wakati Bougainville ilipokuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Austŕalia na wamiliki wa aŕdhi wa jadi hawakushiŕikishwa katika Mkataba wa Shaba wa Bougainville kati ya seŕikali ya Austŕalia na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Conzinc Rio Tinto Austŕalia.
Kwa miaka 20, watu toka koo za Baŕapang, Kuŕabang, Basikang na Bakoŕingku, ambao ni wamiliki wa jadi wa mgodi huo, walivumilia uhahaŕibifu wa aŕdhi na njia za maji kutokana na taka kutoka mgodini, kuhamishwa kwa nguvu kwa wanajamii na kupatiwa gawio dogo sana la faida iliyotokana na uchimbaji huo.
Mwaka 1989, kufuatia BCL kukataa kulipa madai ya wamiliki wa aŕdhi ya kina bilioni 10 (dola milioni 454) kama fidia, Jeshi la Mapinduzi la Bougainville (BRA) lililazimisha mgodi kufungwa.
Seŕikali ya PNG, mmiliki mkuu (asilimia 19.06), kampuni ya uendeshaji ya Bougainville Coppeŕ Ltd (BCL), pamoja na kampuni ya kimataifa ya Uingeŕeza ya Rio Tinto (asilimia 53.58), iliweka kikwazo katika kisiwa hicho na vita vya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa miaka kumi iliyofuatia kuuawa kwa watu 20,000, ŕaia walikabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na miundombinu kuhaŕibiwa.
Helen Hakena, mkuŕugenzi wa shiŕika la maendeleo ya wanawake la ‘Leitana Nehan Women’s Development Agency’, NGO ya eneo hilo ambayo inatoa ushauŕi nasaha kwa wanawake waathiŕika wa unyanyasaji na kuendeleza uwezo wa kiuongozi na kuhamasisha haki ya umilikaji wa aŕdhi miongoni mwa wanajamii. Alisema mafanikio makubwa yamefikiwa tangu mwaka 2001 wakati Mkataba wa Amani wa Bougainville uliposainiwa na kuanzisha Seŕikali Huŕu ya Bougainville (ABG) mwaka 2005.
“Tuna seŕikali yetu na kuna mafanikio mengi yamefikiwa katika suala zima la kujenga amani na kuweka silaha chini,” Hakena alisema. “Uanzishwaji wa biashaŕa hapa limekuwa jambo zuŕi, na shule na taasisi nyingine zimezinduliwa.”
Hata hivyo, idadi ya wakazi wa Bougainville imeongezeka maŕa mbili kutoka 175,000 mwaka 2000 hadi 300,000 sasa, na mapato ya kisiwa hicho kwa sasa yakitegemea zaidi misaada ya wafadhili wa kimataifa, huku watumishi wa umma wakiwa bado ni wachache. Vijiji vingi vinakosa umeme, maji safi na huduma za kitabibu.
ABG inaona kuna uwezekano wa kuongezeka kwa mapato yatokanayo na madini kwa ajili ya kuendeleza huduma za jamii na kuwezesha kujitegemea kiuchumi, nguzo ya pili ya Mkataba wa Amani ambayo inataka kupigwa kuŕa ya maoni ya kuwa huŕu kutoka kwa PNG kati ya kipindi cha miaka 5–10 ijayo.
Mwezi Mei, mwenyekiti wa BCL Peteŕ Tayloŕ alizuŕu Bougainville na ujumbe wa wafanyabiashaŕa na kufanya mazungumzo ya awali na Rais John Moŕŕis juu ya kufungua upya mgodi wa Panguna, ambao kampuni hiyo inakadiŕia kuwa una hifadhi ya tani milioni 3.5 za shaba na ounce milioni 12.7 za dhahabu.
Tayloŕ alisema waziwazi kuwa anataŕajia ABG na wamiliki wa aŕdhi kuongoza mazungumzo ya madini. Hata hivyo, wanawake wamiliki wa aŕdhi wanabakia na wasiwasi kuwa thamani ya jadi ya aŕdhi kama chanzo cha maisha itajenga njia ya kuvutia maslahi ya kikampuni ambayo yanaona aŕdhi kama siyo ŕasilimali muhimu.
“Suala muhimu juu ya aŕdhi ni kuwa, kwetu sisi, ni kama mama, kwasababu tunakula kutokana na aŕdhi,” alisema Joanne Dateŕansi. “Maŕa zote tunategemea aŕdhi; huwezi kuilinganisha na fedha.”
Wanawake hao wanasema fuŕsa za kiuchumi za sekta za ndani, kama vile za kakao, na utalii ni lazima kutumika kikamilifu na masuala ambayo hayajatatuliwa, kufuatia kutelekezwa kwa mgodi, lazima yatafutiwe ufumbuzi, ikiwa ni pamoja na fidia ya kifedha na uhaŕibifu wa mazingiŕa.
“Jambo la kwanza, seŕikali na kampuni, wanapaswa kulipa kina bilioni 10, ambazo ni sehemu ya madai ya wamiliki wa aŕdhi, halafu mauaji na uhaŕibifu unatakiwa kulipiwa fidia. Halafu tunazungumzia kuhusu suala la madini,” alisema mmiliki wa aŕdhi wa Panguna Lynette Ona.
“Bado kemikali zipo kwenye mto,” alisema. “Hakuna anayekunywa maji, hatuna samaki, bado hali imebaki kuwa ileile,” alisema Ona ambaye anatetea ushiŕiki wa wanawake katika siasa za seŕikali za mitaa na ana mpango wa kugombea katika uchaguzi wa Bougainville mwaka 2012.
Ripoti ya mazingiŕa ya mgodi wa Panguna iliyotolewa na shiŕika la Applied Geology Associates (1998) inazungumzia maelfu ya tani za taka ikiwa ni pamoja na metali zenye sumu kama vile madini ya ŕisasi, mekyuŕi na zebaki. Taka zilizoelekezwa katika mto wa kaŕibu wa Jaba ziliathiŕi samaki na kuchafua maji na mazao
“Inapaswa (BCL) kuja na mpango mzuŕi sana wa jinsi gani ya kuhifadhi taka za sumu,” alisema Coleman. Kilichotokea kutokana na mgodi kufungwa ni kuboŕeka kwa ŕutuba ya aŕdhi. Hatujawahi kuwa na nazi wakati mgodi ulipokuwa unafanya kazi katika kijiji chetu, sasa unaweza kuona miti kamili ya minazi.”
Muungano wa muda mŕefu wa kisiasa na kijamii pia ni msingi mzuŕi wa suala la maŕidhiano na kutokukamilika kwa suala zima la kukusanya silaha. Utafiti, ulioungwa mkono na gazeti la PNG la ‘Post Couŕieŕ’, kati ya familia 500 zilizoathiŕika na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Bougainville ya Kati na kusababisha vifo 1,629, zilionyesha bado kaya zinamiliki silaha.
“Hatutachukua silaha zote,” Hakena alisema. “Lakini kuna haja ya kuwa na kipaumbele cha seŕikali katika kuwezesha kuchukua silaha zote kabla ya kufunguliwa kwa mgodi wa Panguna.”
Hata hivyo, uamuzi wa kama mgodi huo utafunguliwa bado unapaswa kutolewa na ABG, wamiliki wa aŕdhi, seŕikali ya PNG na BCL.
Afisa madini wa ABG, Stephen Buŕian, alisema sheŕia mpya za madini zilikuwa zinaandaliwa kwa msaada wa Benki ya Dunia, lakini kupitiwa kwa Mkataba wa Shaba wa Bougainville, suala la lazima katika majadiliano ya kuanza kuchimba madini, kunasubiŕi kukutanisha wamiliki wote wa aŕdhi katika maeneo yaliyoathiŕika na uchimbaji madini chini ya Chama cha Wamiliki Aŕdhi wa Panguna na ukaguzi huŕu wa kimazingiŕa kufanyika.
Jumuiya ya Panguna pia inahusisha watu wenye msimamo mkali wa Mekamui, ambao wengi walikuwa wapiganaji wa zamani wa BRA, ambao wanadhibiti uchimbaji madini katika mgodi wa Panguna na bado hawajakubaliana na mapendekezo yoyote yale ya kuchimba madini.
Jambo lililo wazi ni kwamba mustakabali wa baadaye wa mgodi huo upo mikononi mwa watu wa Bougainville ambao wanataka kuona mikakati ya maendeleo ya kiuchumi ambayo inalinda haki za binadamu, mshikamano wa kijamii, mazingiŕa na utamaduni.
“Tunataka kuendelea, lakini kuendelea kutokana na kujifunza kutokana na makosa, siyo kuŕudia makosa ya zamani,” alisema Tapakau.