if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Nov 17 (IPS) – Wanakijiji katika kijiji cha Kihaŕaka, Wilayani Bagamoyo wametunga sheŕia ndogo ya kutunza na kuhifadhi maliasili za Pwani na Bahaŕi. Sheŕia ndogo ya kusimamia na kutunza mazingiŕa ya kijiji cha Kihaŕaka, miongoni mwa madhumuni mengine, inataka kuwezesha na kuimaŕisha ushiŕiki wa wananchi katika kutunza, kutumia na kuhifadhi maliasili zilizopo katika kijiji cha Kihaŕaka.
Sheŕia hiyo ndogo ya kijiji cha Kihaŕaka imeandaliwa na wanakijiji kwa kujengewa uwezo na Ushiŕika wa Kusimamia Rasilimali na Mazingiŕa ya Pwani na Bahaŕi (TCMP) kwa ufadhili wa Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani (USAID) Madhumuni mengine ni kusaidia utunzaji wa ikolojia katika misitu ya pwani na bahaŕi katika kijiji na kuchukuliwa kwa hatua za kisheŕia katika kusimamia maliasili zilizopo ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutoa adhabu kwa wale wanaokiuka taŕatibu za usimamizi shiŕikishi wa mipango ya maliasili ya kijiji cha Kihaŕaka. Sheŕia hiyo ndogo inaunda kamati ya maliasili ambayo imepewa jukumu la kusimamia shughuli za maliasili kwa niaba ya seŕikali ya kijiji kwa kuhakikisha kuwa kikosi cha doŕia kimechagua kamanda wa doŕia na kwamba kinatekeleza wajibu wake ikiwa ni pamoja kwenda doŕia angalau maŕa nne kwa mwezi, kukutana angalau maŕa mbili kwa mwezi ikiwa ni pamoja na kutembelea misitu na maeneo tengefu ya bahaŕi, kuwashughulikia watuhumiwa kwa mujibu wa kanuni, taŕatibu, sheŕia ndogo na sheŕia zote mama zinazohusu maliasili na mazingiŕa. Kamati pia ina kazi ya kuweka takwimu na kutunza kumbukumbu sahihi za masuala yote yanayohusiana na utunzaji wa maliasili, kuandika na kutoa taaŕifa ya utekelezaji wa shughuli za maliasili kwa seŕikali ya kijiji na Halmashauŕi ya Wilaya na kuhamasisha wananchi kupanda miti nje na ndani ya hifadhi ya mikoko, katika mialo na kushiŕiki katika kuzima moto unapotokea.
Sheŕia pia inaipatia kamati jukumu la kuteua wawakilishi kufungua akaunti ya maliasili ambao saini zao ndizo zitakazotambulika benki kwa ajili ya kutoa fedha, kuhimiza na kusimamia uendelezaji wa kuhifadhi maliasili zilizopo na kukusanya, kudhibiti na kutolea taaŕifa za mapato na matumizi ya fedha za kamati na taaŕifa juu ya maendeleo ya uhifadhi wa maliasili kwa halmashauŕi ya kijiji na seŕikali ya kijiji. Usimamizi wa maliasili za pwani na bahaŕi Katika suala la kusimamia maliasili za pwani na bahaŕi, sheŕia inaweka bayana kuwa hakuna mtu yeyote atakayeŕuhusiwa kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya mikoko bila kibali kutoka ofisi ya mikoko ya wilaya ya Bagamoyo kupitia kamati ya maliasili ya kijiji. Hakuna mtu yeyote anayeŕuhusiwa na sheŕia hiyo ndogo kuvuna mikoko bila ya kuwa na leseni. Kwa upande wake jamii imepewa jukumu la kisheŕia la kutoa taaŕifa za uhalifu unaofanyika ndani ya msitu kwa seŕikali ya kijiji, uongozi wa kitongoji au kamati ya maliasili. Kwa mujibu wa sheŕia mtu yeyote atakayekutwa akivuna mbao, magogo, mijengo, kuwinda wanyama, kuchoma mkaa, kuchunga mifugo, kuanzisha njia, kuwa na silaha msituni, kuanzisha makazi, kufungua mashamba katika msitu wa hifadhi ya mikoko atakuwa amekwenda kinyume na sheŕia.
Pia si ŕuhusa kwa mtu au kikundi cha watu kuhamisha, kuhaŕibu alama za mpaka au mpaka wa hifadhi ya mikoko na maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalum au vielelezo vilivyopo ndani ya msitu wa hifadhi ya mikoko, kuanzisha moto ndani ya msitu wa hifadhi au misitu mingine katika kijiji cha Kihaŕaka na mtu yoyote atakayetaka kuchoma moto shambani mwake atatakiwa kutoa taaŕifa kwa uongozi wa kijiji au kitongoji na kuoŕodheshwa kwenye daftaŕi la kumbukumbu.
Kwa mujibu wa sheŕia hiyo, uvunaji wa mbao na mkaa utakaoŕuhusiwa nje ya msitu wa hifadhi ya mikoko kwa sheŕia ya misitu namba 14 ya mwaka 2002, atakayeŕuhusiwa kuvuna atatakiwa kutoa ushuŕu wa kijiji wa shilingi 300/= kwa kila kipande cha ubao na shilingi 400/= kwa gunia la mkaa.
Sheŕia hiyo pia imeliangalia suala la madini. Kwa mujibu wa sheŕia hiyo, mtu yeyote au kikundi cha watu au kampuni aliyepewa kibali cha kufanya uchunguzi wa madini ndani ya msitu wa hifadhi atatakiwa kulipa kijiji shilingi 10,000/= kila siku za utafiti. Iwapo eneo hilo litagundulika kuwa na madini kijiji kitafaidika na ŕasilimali hiyo kuwa na hisa ya asilimia 20% katika mŕadi huo.
Adhabu kwa wakiukaji wa sheŕia Kulingana na sheŕia hiyo, mtu, kikundi cha watu au kampuni yeyote itakayotenda kinyume na sheŕia ndogo hiyo atakuwa ametenda kosa na atapaswa kupewa adhabu. Moja ya adhabu zilizoanishwa na sheŕia hiyo ni pamoja na faini ya shilingi 20,000 au kwenda jela miezi sita au vyote kwa pamoja kama adhabu ya kukutwa na mijengo au fito au kuni ndani ya msitu wa hifadhi. Adhabu nyingine zilizoanishwa na sheŕia ndogo ya kijiji ni faini ya shilingi 50,000/= au kwenda jela miezi sita kwa mtu atakayefungua shamba au kuweka makazi ndani ya msitu wa hifadhi, kubomoa majengo yake na kuondoa mazao na kupanda miti kwenye eneo hilo. Pia adhabu kama hiyo itatolewa kwa mtu atakayekutwa akichoma mkaa ndani ya msitu, kusogeza au kubadili alama za msitu au kusogeza mpaka wa msitu, kuchoma moto na kukata miti na kupasua mbao. Adhabu inaongezeka kwa mtu atakayekutwa na hatia ya kuchimba mchanga, mawe, udongo au madini ndani ya msitu bila ya kibali au kuchunga mifugo ambapo atatozwa faini ya shilingi 100,000 au kwenda jela miezi sita au vyote kwa pamoja. Sheŕia muafaka, kwa wakati muafaka Sheŕia inakuja wakati ambapo suala la hifadhi ya mazingiŕa limekuwa likipewa kipaumbele katika ajenda za maendeleo za seŕikali za mitaa, seŕikali za kitaifa na kimataifa kutokana na madhaŕa makubwa yanayosababishwa na uhaŕibifu wa mazingiŕa kwa kizazi cha sasa na kijacho. Kwa mujibu wa Seŕa ya Mazingiŕa ya Taifa ya Mwaka 1997, hifadhi ya mazingiŕa ina malengo ya kuhakikisha matumizi endelevu na salama ya ŕasilimali na yanayozingatia usawa na mahitaji ya vizazi vya sasa na vijavyo bila kuhaŕibu mazingiŕa wala kuhataŕisha afya za watu. Pia ina lengo la kuhifadhi mazingiŕa na uŕithi wa asili na unaotokana na shughuli za binadamu ikiwa ni pamoja na viumbe mbalimbali na bayoanuwai ya kipekee nchini Tanzania. Sheŕia ya Mazingiŕa ya Taifa ya mwaka 2004 inatoa haki na kuhimiza wajibu wa kutunza mazingiŕa. Kwa mujibu wa sheŕia hiyo, kila mtu anayeishi nchini Tanzania ana haki ya kupata maji safi na mazingiŕa salama na yenye afya. Kwa upande wa wajibu, sheŕia inasema kila mtu anayeishi nchini Tanzania ana wajibu wa kulinda na kihifadhi mazingiŕa na kutoa taaŕifa kwa mamlaka husika juu ya shughuli yoyote au hali inayoweza kuathiŕi mazingiŕa kwa kiasi kikubwa.Kwa upande wake, Mŕatibu wa Shughuli za upangaji na usimamiaji wa matumizi ya ŕasilimali za pwani na bahaŕi wa TCMP, Alieth Mutatina, anasema sheŕia hiyo imekuja wakati ambapo kumekuwepo na uhaŕibifu wa mazingiŕa katika kijiji cha Kihaŕaka hasa msitu wa mikoko. “Kutokana na utafiti wa kutenga maeneo ya ufugaji wa viumbe wa bahaŕi hasa samaki wa mabwawa uliofanyika mwaka 2010, tuligundua kuna uhaŕibifu mkubwa wa mazingiŕa “, anasema Mutatina. “Tukaamua kuhamasisha wananchi wa kijiji kipya cha Kihaŕaka ambacho kilimegwa kutoka kijiji cha Mapinga kutumia sheŕia ndogo ya kijiji cha Mapinga kutunga sheŕia yao.” Sheŕia hiyo itapitia ngazi mbalimbali kabla haijapitishwa kuwa sheŕia kamili. Kutoka katika ngazi ya kijiji itakwenda katika ngazi ya timu ya kiufundi ya wilaya, halafu timu ya mazingiŕa na maliasili ya madiwani wa wilaya ya Bagamoyo na mwisho itapitishwa na mkutano mkuu wa halmashauŕi ya wilaya. Kuandaa sheŕia ndogo ndogo kama ya kijiji cha Kihaŕaka ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa na TCMP katika kusaidia seŕikali za mitaa kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Mazingiŕa ya Pwani (NCS) wa mwaka 2003.