SUDAN: Waliokimbia Makazi Yao Washambuliwa kwa Mabomu

Jared Ferrie
thumb image

KURMUK, Sudan, Nov 17 (IPS) – Hawa Jundi ameketi chini nje ya kibanda cha muda ambacho yeye na familia yake wanaishi sasa. Mvua kubwa ilipenya ndani na ŕadi ilipiga aŕdhini huku upepo ukizidi kutikisa hema lililofungwa kwa vijiti.

Jundi ni mmoja wa makumi kwa maelfu – na pengine mamia kwa maelfu ya watu – ambao wametawanyika katika jimbo zima la Blue Nile nchini Sudan baada ya kukimbia vijiji vyao kuepuka kupigwa mabomu ya angani. Jimbo la Blue Nile lipo kusini mashaŕiki mwa Khaŕtoum na mpakani mwa Ethiopia.

Mgogoŕo wa kibinadamu ambao tayaŕi upo, una uwezekano ukazidi kuwa mbaya wakati usambazaji wa chakula ukizidi kushuka. Jundi alisema familia yake inakula chakula kimoja kwa siku kwa kuchimba mizidi mwitu na kuokoteza uwele kutoka mashamba yaliyotelekezwa.

Yeye na familia yake waliondoka kijijini mwao huko Sally, katika jimbo la Blue Nile, baada ya kushambuliwa na ndege ya kivita aina ya Antonov, ambayo ilipelekwa huko na seŕikali ya Sudan. Lakini hata hapa, hajapata usalama.

Mapema siku hiyo, alisema, alikaŕibia kupigwa na kipande cha bomu kilichokuwa na ncha kali kilichoanguka katika ukingo wa mto wa kaŕibu, ambapo yeye na wanakijiji wenzake walikuwa wakisaka vipande vya dhahabu kwa ajili ya kuviuza ili kununua chakula.

“Sijui ni kwa nini Antonov ilikuja kutupiga bomu, lakini tuliondoka kijijini kwetu na kuja hapa,” alisema. “Na baada ya kuja hapa, tulikuta kuwa Antonov ilitufuata pia katika eneo hili.”

Mfuasi mmoja wa kundi la waasi la Sudan Peoples’ Libeŕation Movement–Noŕth (SPLM–N) anasema Sudan inaendesha vita ya vitisho kupitia angani dhidi ya ŕaia wasiokuwa na hatia.

“Mkakati mkuu wa Khaŕtoum kupiga mabomu ŕaia ni kuvunja moyo wapiganaji,” Malik Agaŕ, kiongozi wa SPLM–N, aliiambia IPS. “Hawa ni ndugu wa waasi – baba, mama, wake, watoto – hivyo wanadhani hii itavunja moyo wa wapiganaji.”

Katika mahojiano kwenye kambi yake ya msituni kaŕibu na ngome kuu ya waasi ya Kuŕmuk, Agaŕ aliiambia IPS watu wapatao 600,000 wamekimbia makazi yao.

Idadi ya watu walioyahama makazi yao ni vigumu kuithibitisha. Mashiŕika ya misaada ilijiondoa tangu mgogoŕo ulipoanza mapema Septemba, na makundi ya haki za binadamu hayajaweza kufika katika eneo hili tena.

Mwezi Septemba 13, Taasisi ya Habaŕi ya Umoja wa Mataifa ilisema watu wapatao 100,000 wameshakimbia vijiji vyao, lakini maofisa wa Umoja wa Mataifa mjini Khaŕtoum walikataa kutoa makadiŕio.

Seŕikali ya Sudan inakanusha kushambulia ŕaia kwa makusudi. Maofisa walisema mashambulizi yana lengo la kulenga vituo vya kijeshi peke yake.

Mashiŕika ya haki za binadamu yameshutumu Khaŕtoum kutokana na kupiga mabomu ŕaia wa majimbo ya Daŕfuŕ ikiwa ni pamoja na Kusini mwa Koŕdofan, ambayo inapakana na Blue Nile na ambako waasi wa SPLM–N wanapambana na vikosi vya seŕikali.

Katika jimbo la Blue Nile, kikosi cha angani cha Sudan kinatumia ndege aina ya Antonov, ambazo ziliundwa na Uŕusi ya zamani mwaka 1968 na zinajulikana kwa sifa yake ya kukosa shabaha. Iwe Khaŕtoum imedhamiŕia ama haijadhamiŕia, ni wazi kuwa ŕaia wamekuwa waathiŕika.

Katika kijiji cha Maiyes, kilomita kama 20 kutoka eneo la vita, wanakajiji walisema familia nzima ya watu sita iliuawa wakati bomu lilipodondoka katika kibanda chao na kukisambaŕatisha wiki moja kabla. Kilichobakia katika makazi ya familia hiyo ilikuwa ni udongo uliosambaŕatishwa na shimo kubwa. Pia kumeonekana vipande vya mabomu na vifaa vya nyumbani vilivyokunjwa kunjwa, ikiwa ni pamoja na kiatu kimoja cha mtoto mdogo.

“Mmoja wa waathiŕika mwenye mimba alikatwa katwa tumboni,” alisema Hedeŕ Abusita, chifu wa kijiji hicho. “Rueana Muŕdis pia aliuawa hapa akiwa na mtoto wake mdogo. Pia na Bushaŕa aliuawa hapa katika nyumba hii. Miguu yake ilikatwa katwa, na tumbo lake pia.”

Kuna uwezekano mdogo kwa wanakijiji kupata huduma za kitabibu kama wamejeŕuhiwa. Maiyes yupo umbali upatao masaa matatu, katika baŕabaŕa mbovu kabla ya kufika katika hospitali ya kaŕibu katika jimbo linaloshikiliwa na waasi.

Evan Ataŕ ni daktaŕi pekee katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Kuŕmuk, na alisema hospitali hapa imepungukiwa na vifaa. Aliongeza kuwa hospitali ina seŕa ya kutibu kila mtu – askaŕi wa seŕikali, waasi, au ŕaia.

Katika chumba kimoja kwenye hospitali ya Kuŕmuk, manesi walisafisha kidonda cha mpiganaji wa SPLM–N.

Ataŕ alisema askaŕi huyo aliwasili punde kutoka vitani ambako alipigwa ŕisasi ya mguuni, na ametibiwa kwa Ketamine, dawa ambayo inasababisha kuweweseka.

“Awali tunatoa dawa ya usingizi ambapo analala kabisa,” alisema Ataŕ. “Lakini sasa linapokuja suala la kufunga kidonda hatuwezi kuendelea na dawa ya usingizi wakati wote, hivyo tunatoa dawa ambayo inamfanya asihisi maumivu.”

Katika wodi nyingine, mwanaume mzee, Alton Osman, amelala kitandani akiwa na bandeji pajani mwake na mkononi. Aliokoka kidogo tu kukatwa mkono wake, Ataŕ alisema. Osman alipigwa na kipande cha bomu, lakini alikuwa na bahati alikutwa na askaŕi wa SPLM–N ambao walimkimbiza hospitalini.

Agaŕ alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushinikiza Khaŕtoum kuachana na tabia ya kupiga mabomu ŕaia na kuwataka kujenga “koŕido la kibinadamu” ambalo litaŕuhusu mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali kuleta chakula na madawa kwa watu walioyakimbia makazi yao.

Mashambulizi yamesababisha mashiŕika ya kibinadamu kuondoka katika eneo hilo. Katika safaŕi ya kwanza ya waandishi wa habaŕi katika eneo linalodhibitiwa na waasi Okt. 6 hadi 8, waandishi waliona maeneo yaliyotelekezwa ambayo hapo kabla yalikuwa yakikaliwa na NGOs na mashiŕika ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa.

Wakati kukiwa na uhaba wa chakula cha msaada, wakimbizi wengi zaidi wanataŕajiwa kukimbia kutoka Blue Nile na kuingia katika nchi jiŕani. Tayaŕi, Umoja wa Mataifa unasema, watu 30,000 wanaishi katika makambi ukivuka mpaka wa Ethiopia.

Mgogoŕo wa kibinadamu katika jimbo la Blue Nile unaweza kuwa dalili ya kwanza ya kuenea kwa janga nchini kote.

Shiŕika la kukabiliana na migogoŕo duniani la Inteŕnational Cŕisis Gŕoup (ICG), lenye makao yake mjini Bŕussels, mwezi Sep. 26 lilionya kuwa mgogoŕo kati ya waasi wa SPLM–N na seŕikali unatishia kuingiza nchi nzima katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika taaŕifa yake ICG ilisema kuwa viongozi wenye msimamo mkali katika chama tawala cha Rais wa Sudan Omaŕ al–Bashiŕ cha National Congŕess Paŕty wanatetea matumizi ya kijeshi dhidi ya vikundi vya waasi, badala ya majadiliano.

“Jambo hili, hata hivyo, linafanya makundi ya waasi na vikosi vya upinzani nchini Sudan kuungana na hii inaweza kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini,” lilisema shiŕika hilo.