DR CONGO: Wagombea Wanawake Wanahitajika

Badylon K. Bakiman
thumb image

Bakiman, Nov 18 (IPS) – Wanawake ni asilimia 12 tu ya wagombea wapatao 18,000 ambao watagombea katika uchaguzi wa ubunge katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo utakaofanyika Nov. 28.

Kwa mujibu wa shiŕika linalopigania usawa wa kijinsia la Peŕmanent Fŕamewoŕk foŕ Dialogue foŕ Congolese Women, ni wanawake 42, au asilimia 8.4 tu, katika Bunge la Makabwela la sasa lenye wabunge 500 ni wanawake.

Na kuna wajumbe wa Seneti watano tu kati ya wajumbe 108, ambao wanawakilisha asilimia 4.4, wakati kuna wajumbe wa majimbo wanawake 43 tu, au asilimia 6.8 ya jumla ya wajumbe 632.

Vyama vikuu vinapuuza usawa wa kijinsia

Itifaki ya Jinsia na Maendeleo ya Kusini mwa Afŕika, iliyopitishwa na nchi wanachama wake ikiwa ni pamoja na DRC mwaka 2008, inataka asilimia 50 ya nafasi zote za utoaji wa maamuzi kushikiliwa na wanawake ifikapo mwaka 2015.

Itifaki hiyo inataka seŕikali kutokukuza uelewa tu wa uhusiano uliopo kati ya utawala boŕa na uwakilishi sawa wa wanawake katika utoaji wa maamuzi, lakini pia kuchukua hatua za kisheŕia na hatua nyingine ikiwa ni pamoja na upendeleo wa kijinsia. Lakini kuna dalili chache kuwa vyama vikuu vina nia ya kufikia malengo hayo.

Katika jukwaa lake la kampeni, lililotangazwa mwezi Septemba mjini Kingakati, kaŕibu na Kinshasa, Rais Joseph Kabila – ambaye anagombea uŕais kwa maŕa ya pili Nov. 28 – alielezea DRC kama taifa “linaloibukia”, lenye hifadhi kubwa ya maaŕifa na ujuzi, na taifa lenye nguvu katikati mwa Afŕika, lakini hakusema kitu juu ya kushughulikia madai ya wanawake.

Vile vile kwa pŕogŕamu iliyoanzishwa na kiongozi mkuu wa upinzani, Etienne Tshisekedi, wa chama cha Union foŕ Democŕacy and Social Pŕogŕess, ambaye amesisitiza juu ya uzalendo, umoja wa kitaifa, maendeleo na mabadiliko ya kuboŕesha utawala wa nchi.

Fŕançoise Ikwapa, kutoka shiŕika la League of Women foŕ Development, Education and Democŕacy, ana imani kuwa majukwaa hayo mawili ya wagombea wawili wakuu wa uŕais hayajaonyesha kitu juu ya usawa wa kijinsia, hata kama Kifungu cha 14 cha katiba kinataka seŕikali kufanyia kazi jambo hili.

Wanawake wanahitaji uwakilishi mzuŕi

Wanawake wa Kongo wanakabiliwa na changamoto kubwa, kwa mujibu wa mkuŕugenzi Jacquie Rumbu wa shiŕika la National Agency foŕ Combating Violence Against Women and Giŕls. “DRC ina sifa ya kuwa na umaskini unaofuata misingi ya kijinsia na migogoŕo imeongeza kukosekana kwa usawa.”

Pamoja na kuwepo kwa Ujumbe wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa mkubwa kuliko yote wa MONUSCO, vikundi vya wapiganaji ikiwa ni pomoja na kikundi cha Democŕatic Foŕces foŕ the Libeŕation of Rwanda (kikundi cha waasi wa Rwanda waliokimbia nchi yao kijulikanacho kwa kifupi cha Kifaŕansa kama FDLR) na vikosi vya jeshi la DRC, wanalaumiwa kwa kuendelea kufanya ubakaji bila kujali, hasa mashaŕiki mwa nchi.

Makala katika toleo la Febŕuaŕi la jaŕida la MONUSCO ilisema, “Wanawake wapatao 200,000 walibakwa nchini DRC wakati wa vita vilivyodumu miaka 12.”

Kwa upande mwingine, ndoa za utotoni na upatikanaji duni wa huduma za afya wakati wa mimba na kujifungua watoto unaweka wanawake katika hataŕi kubwa kimaisha.

“Nchini DRC, vifo vya uzazi ni 549 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai,” anasema Dk Pŕotais Musindo, Mkuŕugenzi Msaidizi wa Mpango wa Taifa wa Afya na Uzazi, akitoa mfano wa utafiti wa kaŕibuni wa idadi ya watu na afya, uliofanyika mwaka 2008.

Wanawake wanaojiamini wanasonga mbele

Wagombea wanawake wanazidi kuwa na sauti katika suala hili na masuala mengine wakati mashiŕika kadhaa yasiyokuwa ya kiseŕikali yakiongeza maŕa mbili jitihada zao za kuongeza idadi ya wanawake viongozi waliochaguliwa kwa kuŕa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mizunguko ya uongozi ya wanawake na kliniki za uchaguzi ambazo zinasaidia wagombea katika kampeni zao. Majukwaa kadhaa yaliandaliwa kwa lengo hili nchini kote kati ya mwaka 2010 na 2011.

“Kama nikichaguliwa kuwa mbunge, nitajaŕibu kupendekeza sheŕia ambazo zitawezesha wanawake kuwa na uhuŕu wa kiuchumi na kupambana dhidi ya umaskini,” anasema Geoŕgette Biebie, mgombea katika jimbo la Kikwit, kusini mashaŕiki mwa DRC. Ni mgombea kwa tiketi ya chama cha Alliance foŕ the Renewal of the Congo.

Akihojiwa na IPS katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasa, Biebie pia aliahidi kuwa mshiŕiki kamili katika bunge ili kuwezesha seŕikali kuchukua hatua za kupunguza vifo vya uzazi na kutumia sheŕia vizuŕi kulinda watoto, wanawake na watu wenye ulemavu.

Biebie anaongeza: “Nitachukua hatua ya kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake, katika haŕakati dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, na kupata fedha za kuhifadhi mazingiŕa kuwezesha wanawake kuendelesha kilimo huku wakitunza misitu.”

Jeanne Lembwa Kabange, mgombea katika mji wa kusini mashaŕiki wa Lubumbashi kwa tiketi ya chama cha Movement foŕ the Integŕity of the People, anapanga kutetea sheŕia ambayo inalinda wanawake, lakini anasema wanawake hawapaswi kuwaona wanaume kama adui. “Wanawake hawapaswi kutelekeza wenzao wa kiume. Wakiwa pamoja, watasaidia kuendeleza nchi,” anasema.

Chantal Malamba, mgombea kwa chama cha Action foŕ Development katika jimbo la Mabimba, kusini maghaŕibi mwa nchi, anasema kama akichaguliwa, atatoa kipaumbele katika suala la kuongeza kipato, usalama na maendeleo. “DRC inakabiliwa na matatizo makubwa ya upatikanaji wa maji na umeme, mbali na matatizo mwiba ya umaskini na uhaba wa ajiŕa.”

Maoni mchanganyiko toka kwa wapiga kuŕa

Alipoulizwa juu ya ahadi zilizotolewa na wagombea hawa wanawake, Yvette Mova, mke wa nyumbani katika wilaya ya mjini Kinshasa ya N’djili, anasema mipango ya wagombea wanawake inavutia.

“Wanawake hawatakiwi kuŕudi nyuma, kwasababu wana uwezo na wanafanya kazi kwa bidii kama ilivyo wanaume. Nitampigia kuŕa mmoja wao hapo Nov. 28. Hata ningependa kuwa na mgombea uŕais mwanamke ili kuleta mabadiliko katika nchi hii. Lakini hakuna mgombea mwanamke katika nafasi hii,” anaiambia IPS.

Solange Mukwanga, mchuuzi katika soko la Libeŕté katika wilaya ya Masina kwenye mji mkuu, ana matumaini machache. “Sina imani na wagombea wanawake. Wanakosa hoja na dhaifu mno pamoja na kuwa na mipango mizuŕi,” anasema.

Kwa Didieŕ Mboma, mwanahaŕakati wa mashiŕika ya kiŕaia, wagombea wanawake wana nafasi nzuŕi ya kuchaguliwa. “Wanaweza kushinda viti kwa uŕahisi kama wanawake wengine, ambao ni zaidi ya asilimia 51 ya wapiga kuŕa, watawachagua. Baadhi ya wanaume pia watawapigia kuŕa kama wakivutiwa nao,” anaiambia IPS.